Maboresho ya mfumo wa Luku kuanza rasmi July 22,2024
#bmupdate #bmtvtanzania
Profesa Mohamed Janabi Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili na Dkt. Peter Kisenge, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete ni miongoni mwa madaktari bingwa wanaohudumia wananchi wa Arusha kwenye Kambi ya Matibabu inayoendelea kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Kauli hiyo imezungumzwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda leo Jumatatu Juni 24, 2024 wakati wa Kambi maalum ya Matibabu iliyoanza leo mjini Arusha kwenye viwanja vya Sheikh Amri Abeid, akisema madaktari hao wameambatana na mabingwa wengine wa magonjwa mbalimbali.
Mhe. Makonda kadhalika ametumia nafasi hiyo kuwaomba watoa huduma za afya waliopo kwenye kambi hiyo kutanguliza utu na upendo katika kuhudumia wananchi pamoja na kuwa na sikio la ziada na utulivu katika kusikiliza na kuwaelewa wananchi kikamilifu na kuwahudumia.
Paul Christian Makonda Mkuu wa Mkoa wa Arusha amesema "Ndugu zangu asiwaambie Mtu, kwenye suala la afya kuna watu wameuza nyumba zao, kuna Watu wameuza viwanja, Watu wamefilisika biashara zao katika kupambana kuuguza Ndugu zao na kuna nyakati nyingine kuna ndugu zetu walishindwa hata kuchukua miili ya ndugu zao kutokana na madeni ya gharama za matibabu. Neema hii ambayo Mungu ametupa ya kupata matibabu bure tukaitumie vyema na Mikono ya watumishi wa Mungu ikafungue Baraka ili tukaondokane na magonjwa kupitia madaktari wetu bingwa ili tukawe na mchango kwenye ustawi wa uchumi wa Taifa letu."
TUMEPATANA KESHO SAA 4 ASUBUHI MAHOJIANO YAFANYIKE
Kipekee @bmtvtanzania tunamshukuru mno Yusto Onesmo Mtumishi wa Mungu, Mwimbaji wa nyumbo za Injili na Mchungaji, kwa Makaribisho mazuri hapa nyumbani kwake na ameahidi Kufunguka mengi kuhusu Huduma yake.
Kikubwa ametuhakikishia kuwa atatoa namba na Mawasiliano yake binafsi kwa nyote ambao mngependa kuwasiliana naye kwa Habari ya Huduma na Mialiko.
Usikose Kutazama na kutoa maoni yako wakati atakapokuwa anazungumza LIVE kupitia YouTube Channel yetu BM TV TANZANIA
Asante.
Umoja wa Madereva Bajaji Bunju B (UMABABU) umepongeza jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuteua viongozi wenye tija wanaochochea mabadiliko kwa kutoa ushirikiano kwa wananchi iki waweze kufikia malengo yao pamoja na kukuza uchumi wa nchi.
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa umoja huo, Kulwa Msafiri alipokuwa akieleza namna uongozi wa Wilaya ya Kinondoni unavuoendelea kuwashika mkono kwa kuwatafutia fursa mbali mbali. zinazowaletea mafanikio makubwa.
"Rais Samia ametuletea mkuu wa wilaya sahihi kwani amekuwa akituunga mkono sana, pia tumesikia Serikali imeachia mikopo ya asilimia 10 tunaamini na sisi tutakua ni wanufainika," amesema Kulwa.
Katibu Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba akitoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya umeme.
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu akifanya kampeni na kuomba kura kwa lugha ya kwao ya Kinyaturu akiwa katika ziara yake mkoani Singida.
Lissu amekuwa akizunguka Mkoani Singida akishawashi wananchi wa Mkoa huo kumuumga mkono kwenye harakati zake za kutaka uongozi huku akijielekeza zaidi kutumia lugha ya Kinyaturu kitendo ambacho kimeibua sintofahamu kubwa
TANESCO imefanya mapitio kwenye maeneo 1,570 ya mjini yenye sura ya Vijiji - Mhe. Judith Kapinga, Naibu Waziri Nishati, Bungeni Dodoma Juni 07, 2024
SAKATA LA WAKULIMA KULIPIA MAZAO KWA EFD MACHINE
WAKULIMA KULIPIA KODI MAZAO KWA EFD MACHINE, MBUNGE AMBANANISHA MWIGULU NCHEMBA
Mkuu wa Wilaya ya Ubungo, Mhe. Hassan Bomboko ameeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na huduma kwa jamii iliyotekelezwa na Rais Samia katika wilaya hiyo iliyoanzishwa hivi karibuni ndani ya kipindi cha miaka mitatu.
DC Bomboko amesema ndani ya kipindi cha miaka mitatu, Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amewezesha miradi ya takribani bilioni 306 kutekelezwa ndani ya wilaya ya Ubungo huku akitolea mfano baadhi ya miradi kama vile Ujenzi wa Shule ya Bweni ya wasichana (Dar es Salaam Girls Secondary School), Ujenzi wa hospitali ya wilaya, upanuzi wa zahanati ya Makuburi kuwa kituo cha afya na kadhalika.
"Kwa upande wa barabara peke yake, zitajengwa kilomita 52 ambazo tutazigawa katika mitaa 90 ili kumaliza kero kwa wananchi wa Ubungo, haya ni mafanikio makubwa, sisi watu wa Ubungo tunamshukuru sana Rais Samia" - Aliongeza Bomboko
Mwl. Anthonia Francis ambaye ni Makamu Mkuu wa Shule maalum ya bweni ya Wasichana mkoa wa Dar es Salaam (Dar es Salaam Girls Secondary School) ameeleza sifa mbalimbali za shule hiyo yenye uwezo wa kupokea wanafunzi 1000 kwa mpigo iliyojengwa na serikali ya awamu ya sita katika wilaya ya Ubungo jijini Dar es Salaam.
Akielezea miundombinu ya shule hiyo ya kisasa iliyofunguliwa rasmi Agosti 14, 2023, Mwl. Anthonia amesema mbali na madarasa, matundu ya vyoo, bwalo, jengo la utawala na miundombinu mingine ya msingi, shule hiyo ina mabweni nane, maabara nne kwa maana ya maabara ya baiolojia, maabara ya kemia, maabara ya fizikia na maabara ya jografia pamoja na nyumba za kisasa za walimu.
Kamanda wa jeshi la mkoa wa Ruvuma (SACP)Marco Chilya amesema wafanyakazi wa migodi ya makaa ya mawe mkoa wa Ruvuma wanachangamoto kubwa ya kuiba mafuta ya kuendesha mitambi ya kuchimba makaa hayo ambapo wamiliki wa migodi hiyo wamekuwa wakipata hasara kutokana na wizi huo hivyo amewataka wafanya kazi hao kuacha tabia hiyo ambayo itasababisha migodi kufungwa na na ajira za watu kupotea.
Hayo ameyasema alipokuwa anafunga mafunzo ya waendesha mitambo mikubwa na magari makubwa wa migodi mbalimbali iliyopo katika kata ya Ruanda wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda leo Mei 27.2024 amesema hatishiki na kauli zinazotolewa dhidi yake kuhusu kumdhalilisha mwanamke ambaye ni mtumishi wa Serikali wilayani Longido mkoani Arusha.
Kamanda wa Jeshi la zima moto na Uokoaji Mkoani Geita, Kamanda Mratibu Hamis Dawa,amesema kuwa majanga mengi ya moto yanayozuka majumbani hayasababishwi na umeme unaotoka na TANESCO bali nimatumizi holela ya vyombo vya Umeme pamoja Na kutochukua tahadhari ya vifaa
Kamanda Mratibu Hamis Dawa ameyasema hayo Mei 24, 2024 alipotembelea Banda la TANESCO , katika maonesho ya Biashara ,Viwanda na Kilimo yanayoendelea Mkoani Geita.
Aidha amesema kuwa jukumu la TANESCO ni kupeleka Umeme kwa Mteja mpaka kwenye mita lakini suala la Umeme ndani ya nyumba ni suala la Mteja kuhakikisha Nyaya ndani ya nyumba yake zimetandazwa vizuri, na vifaa vyote vilivyotumika vinaubora ikiwemo saketibreka.
“Mkataba wa Ununuzi wa Umeme kati ya TANESCO na SONGAS utafikia ukomo wake tarehe 31 Julai, 2024. Kwa sasa, Serikali imeunda timu ya wataalam iliyoanza majadiliano mwezi Aprili, 2023 na inatarajia kukamilisha majadiliano hayo kabla ya mkataba kuisha. Serikali kuhakikisha maslahi ya Taifa yanazingatiwa kabla ya kuingia makubaliano na Songas," Mhe. Judith Kapinga, Naibu Waziri Nishati. Bungeni Dodoma Mei 27, 2024.
Wananchi wa wilaya ya Kigamboni wamekua wakipata changamoto ya kusafiri umbali mrefu kufuata matibabu, hali ilopelekea kutumia muda mwingi njiani, gharama kuwa kubwa na hata kutokupata huduma za matibabu kwa wakati.
#DiraYaSamia ilipiga story na Mama Flora, aliyeeleza jinsi gani wananchi wa Kigamboni wamenufaika na uwepo wa hospitali hiyo ya wilaya. Wakimshukuru Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhakikisha hospitali hii inapata wataalamu wa kutosha, dawa na vifaa tiba.
Mkuu wa mko wa Arusha Paul Makonda leo Mei 23 akiwa anazungumza na Kusikiliza kero za wananchi wa Longido mkoani Arusha.