#EmTVNews: Mfanyabiashara ambaye pia aliwahi kuwa Mfadhili na Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji amefariki Dunia wakati akiendelea na matibabu Nchini Marekani
Taarifa iliyotolewa na Mtandao wa Mwananchi imeeleza kwa mujibu wa mtoto wa Manji, Mehbub Manji ni kuwa msiba huo umetokea Jumamosi Juni 29, 2024 katika Jimbo la Florida
Manji alikuwa ni Mkurugenzi Mtendaji wa Quality Group Limited (QGL), pia, aliwahi kujihusisha na siasa kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) na kufanikiwa kuwa Diwani wa Kata ya Mbagala Kuu.
#ErastoMashauriUpdates
#EmTVNews: Watu 14 wamepoteza maisha huku wengine 18 wakijeruhiwa katika ajali iliyohusisha magari matatu Jijini Mbeya leo saa saba mchana katika Mlima wa Simike eneo la Mbembela.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Juma Homera amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyohusisha Lori namba T.979 CVV likiwa na Tela namba T.758 BEU Scania likiendeshwa na Ross Mwaikambo (40) likitokea Shamwengo likiwa limepakia kokoto, Toyota Coaster namba T.167 DLF na Toyota Harries namba T.120 DER.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga amesemna Lori hilo liliendelea kugonga guta namba MC 660 BCR na kisha kugonga pikipiki namba MC 889 CKX huku akibainisha kuwa chanzo cha ajali ni uzembe wa Dereva wa lori namba T979CVV/T758 BEU kushindwa kulimudu gari kwenye mteremko.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linamshikilia Dereva wa gari hilo ambaye anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya akiwa chini ya ulinzi.
#ErastoMashauriUpdates
#EmTVNews: Rais wa Iran Ebrahim Rais amefariki Dunia pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Hossein Amirabdollahian na Viongozi wengine ambao walikuwa wakisafiri pamoja kwenye Helikopta ambayo imeanguka Kaskazini Magharibi mwa Iran wakati Rais huyo na Timu yake wakitokea kwenye shughuli ya kikazi mpakani mwa Nchi hiyo na Azerbaijan ambapo hakuna aliyenusurika kwenye ajali hiyo.
Chombo cha Habari cha Serikali ya Iran kiitwacho IRNA kimethibitisha vifo hivyo na kusema tayari Baraza la Mawaziri la Serikali ya Nchi hiyo limekutana kwa dharura, AFP na Reuters wamethibitisha pia vifo hivyo.
Taarifa za vifo hivyo zimethibitishwa baada ya zoezi la kuisaka ilipoangukia Helikopta hiyo kufanyika kwa saa kadhaa hadi usiku wa kuamkia leo na baadaye mabaki ya Helikopta yamepatikana katika mazingira ambayo yameashiria hakuna aliyepona katika ajali.
#ErastoMashauriUpdates
#EmTVNews: TANZIA: Aliyekuwa Mtayarishaji wa Video za Muziki wa Bongo Flava Nchini, Khalfani Khalimandro amefariki Dunia
Director Khalfani alilazwa katika Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) akiwa na tatizo la Damu kuvilia kwenye Ubongo lililomsababishia kupata Kiharusi (Stroke) upande wake wa kulia
Enzi za Uhai wake alijipatia umaarufu kwa kuongoza Video za Wasanii kama Christian Bella, Baby Madaha, Aslay nk. #RIPKhalfan
#ErastoMashauriUpdates
#EmTVNews: TANZIA: Aliyekuwa Mtangazaji mahiri Nchini, Gardner G. Habash maarufu 'Captain' amefariki Dunia, leo Aprili 20, 2024
Hadi umauti unamkuta Gardner alikuwa amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar es Salaam kutokana na changamoto ya Shinikizo la Damu
Kabla ya Kifo, Gadner alijipatia umaarufu kutokana aina ya utangazaji wake wa ucheshi kupitia vipindi vya jioni ambapo alianzia katika Kituo cha Redio cha Clouds FM baadaye Times FM, E-FM na kisha kurejea Clouds FM
#ErastoMashauriUpdates
#EmTVNews: Msanii wa vichekesho, Umar Iahbedi Issa maarufu โMzee wa Mjegejeโ amefariki dunia leo alfajiri katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala, Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.
Meneja wa msanii huyo, Real Jimmy amethibitisha taarifa hizo.
#erastomashauriupdates
#EmTVNews: TANZIA: Rais wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi amefariki Dunia, leo Februari 29, 2024 akiwa na Miaka 98
Taarifa imetolewa usiku huu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Huku Chanzo cha Kifo chake kikitajwa Kuwa Ni Saratani Ya Mapafu.
#ErastoMashauriUpdates
#EmTVNews: Watu 15 wamefariki Dunia katika ajali iliyohusisha Lori la Mizigo (Semi Trailer) na magari madogo matatu iliyotokea katika eneo la Ngaramtoni, Wilayani Arumeru, Februari 24, 2024, ambapo Jeshi la Polisi limesema chanzo cha ajali bado hakijafahamika lakini taarifa za awali zinaonesha Lori lilipoteza uelekeo
Kwa mujibuwa taarifa za mashuhuda, Lori hilo aina ya Scania lenye namba za Usajili ZF 6778 lilikuwa likionesha ishara Taa za Hatari likiwa katika mwendo mkali na baadaye kuyagonga magari matatu ambayo ni Basi dogo la Abiria (Hiace), Basi la Shule ya New Vision lililokuwa na Watumishi wa Shule na Gari lingine dogo
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, SACP Justine Masejo amesema kuna majeruhi kadhaa ambao wapo katika hali mbaya, pia amewataka Wananchi kufika Hospitali ya Rufaa ya Mount Meru kutambua Miili ya waliofariki pamoja na majeruhi katika ajali hiyo
#ErastoMashauriUpdates
#EmTVNews: Rais wa Kongo DRC Felix Tshisekedi ameridhia Barua ya Kujiuzulu ya Waziri Mkuu, Jean-Michel Sama Lukonde ikiwa ni Miaka Mitatu toka ateuliwe, hivyo kusababisha kuvunjwa kwa Baraza la Mawaziri
Taarifa kutoka Ikulu ambayo haikuweka wazi sababu za Waziri huyo kujiuzulu imesema Rais ameagiza Serikali iliyovunjwa kuendelea na majukumu hadi pale Serikali mpya itakapoundwa
Lukonde aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu Februari 2021, akichukua Madaraka kutoka kwa Sylvestre Ilunga Ilunkamba, aliyejiuzulu baada ya Wabunge kupiga kura ya kutokuwa na imani naye na Serikali yake.
#ErastoMashauriUpdates
#EmTVNews: Msafara wa Katibu wa Itikadi Uenezi na Mafunzo wa @ccmtanzania @baba_keagan umepata ajali eneo la Masasi mkoani Mtwara.
Ajali hiyo iliyotokea saa 9:00 Alasiri leo Februari 11, 2024, imehusisha zaidi ya magari 7 yaliyokuwepo katika msafara wa Makonda uliokuwa unatoka mkoani Ruvuma kuelekea Jijini Dar es salaam.
Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza watu wasiopungua wawili wamejeruhiwa na kukimbizwa katika hospital ya mkoa wa Mtwara na huku kukiwa hakuna kifo chochote.
Afya ya Katibu wa NEC Itikadi ,Uenezi na Mafunzo Paul Makonda ipo salama.
#ErastoMashauriUpdates
#EmTVNews: Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 'Dk.Philip Mpangp' amethibitisha taarifa za kifo cha Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa kilichotokea leo saa Nane mchana katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete.
Kufuatia kifo hicho Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametangaza siku tano za maombolezo ambapo bendera zitapepea nusu mlingoti kuanzia leo.
#ErastoMashauriUpdates