Kwani huyu mama mlimkosea nini hadi aingie kwenye himaya yetu😳😂???
KUNA UKWELI JUU YA MANENO YA DADA HUYU??
Viumbe watakao tawala dunia.
Basi kampuni ya mwekezaji kutoka China, New Force/Golden Deer imepata ajali na kuua watu kadhaa.
Wakati ajali hiyo inatokea ndani ya mwezi huu itakuwa ajali ya 3 kwa kampuni hiyo baada ya last week kupata pia ajali maeneo ya Morogoro.
Chanzo ni mwendo wa mashindano.
======
Kamanda wa Polisi, Kamishna Msaidizi wa Polisi, ACP John Makuri amethibitisha tukio la ajali mbaya iliyotokea katika Eneo la Igando Wilaya ya Waging'ombe ikihusisha basi la NewForce lililokuwa linatoka Dar kwenda Sumbawanga.
Kwa mujibu wa Kamanda Makuri, Idadi ya vifo vi 5 na Majeruhi kadhaa wakipelekwa Hospitali ya Kanisa ya Ilembula
SERIKALI: HATUJASIMAMISHA ZOEZI LA KUHAMISHA WANANCHI NGORONGORO
Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Omary Mchengerwa amesema “Zoezi la kuhamishia Wananchi Msomera Mkoani #Tanga kutoka Hifadhi ya Ngorongoro linaendelea na halijasimamishwa kama inavyosema hasa na majirani zetu.”
Amesema Wananchi wanaojiandikisha na kuhamia Msomela wanapata haki zao za kibinadamu ikiwemo Shule, Nyumba na kufanya Biashara tofauti na walivyokuwa wakiishi kwa mashaka
#ZAMBIA: MTANGAZAJI ASITISHA TAARIFA YA HABARI NA KUTAJA KERO YA KUTOLIPWA MSHAHARA
Kalimina Kabinda wa KBN alilalamikia kutolipwa mshahara mubashara katika taarifa ya habari
> Mkuu wa Kituo amesema Kabinda alilewa, hakujibu madai ya malipo
Class part . Mtoto aja na keki shuleni yenye suma .
Apatiwa na mama wakambo aliyekua akiishi nae .
Wazazi muwape watoto vyakula vya kutosha kuepusha kutamani cha mwenzake mashuleni.
IDADI ya watu waliouawa kwa mashambulizi Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza imefikia 132, ambapo 32 kati yao ni watoto na 21 ni wanawake, huku Israel ikipoteza watu tisa tangu mapigano kuanza siku ya Jumatatu.
Siku ya Jumamosi (Mei 15), madaktari katika Ukanda wa Gaza walisema watu saba walikuwa wameuawa kufuatia mashambulizi ya anga ya jeshi la Israel katika eneo la kaskazini la Ukanda huo.
Wakazi wa huko waliripoti pia taarifa za jeshi la wanamaji la Israel kurusha makombora kutokea Bahari ya Mediterenia.
Katika mitaa ya Ukingo wa Magharibi, wanajeshi wa Israel waliwauwa waandamanaji saba wa Kipalestina siku ya Ijumaa (Mei 14), wakati ghasia zikizuka katika maeneo mbalimbali ya Israel, ambako raia wa Kiyahudi na Kiarabu wanapambana.
Milio ya ving’ora vya tahadhari ilisikika kwenye miji mikubwa miwili ya kusini mwa Israel asubuhi ya Jumamosi, baada ya Hamas kurusha makombora mengine kutokea Gaza.
Tangu mapigano kuanza siku ya Jumatatu, zaidi ya makombora 2,000 yamesharushwa kutokea Gaza kuelekea Israel, yakiwauwa watu tisa, mmoja mtoto mdogo na mwanajeshi mmoja na kujeruhi watu 560.
Chanzo Dw
#2skys_updates