27/02/2024
Tanzania Yavunja Rekodi Mwaka 2023: Mapinduzi Katika Sekta Ya Utalii Yalivyoimarisha Uchumi
Mwaka 2023 umekuwa mwaka wa kipekee kwa sekta ya utalii katika uchumi wa Tanzania ambapo hivi karibuni Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilitoa ripoti inayofurahisha, ikiwa na maelezo ya ongezeko la kiasi cha watalii — kufikia watalii milioni 1.8 mwaka 2023, wakizalisha mapato ya zaidi ya dola za Marekani bilioni 3.37, kutoka dola za Marekani bilioni 2.527 mwaka 2022.
Ukuaji huu wa kustaajabisha si tu unaonyesha mvuto wa Tanzania k**a kivutio cha juu cha utalii bali pia unathibitisha hadhi yake k**a chanzo kikuu cha mapato ya kigeni cha nchi kwa mwaka 2023.
Haikuishia hapo, katika utambuzi wa kimataifa ripoti ya utalii ya umoja wa mataifa kupitia World Tourism Barometer katika kipindi cha January hadi December 2023 imeiweka Tanzania katika nafasi ya pili kwa nchi za Afrika kwa ukuaji wa utendaji katika sekta ya utalii ikiwa na ongezeko la 20% nyuma ya nchi ya Ethiopia.
Mafanikio haya yanachangiwa na sababu mbalimbali muhimu zikiwemo zifuatazo:
🔊Juhudi Endelevu Za Kutangaza Utalii Wa Tanzania
🏖️ Wingi Wa Vivutio Vya Utalii Nchini Tanzania
✈️ Ndege Za Moja Kwa Moja Kutoka Mataifa Mbalimbali Kuja Tanzania
✈️ Mfumo Imara Wa Ndege Za Ndani
📖 Sera Imara Zenye Kuvutia Uwekezaji Katika Sekta Ya Utalii Nchini Tanzania
Tunapoadhimisha mafanikio haya, ni dhahiri kuwa sekta ya utalii ya Tanzania inaelekea juu zaidi, ikiendeshwa na mipango mikakati na dhamira thabiti ya kuonyesha ubora zaidi wa nchi yetu kwa ushirikiano imara kati ya serikali na wadau wote katika sekta ya utalii.