BrightSpear Studios

BrightSpear Studios Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from BrightSpear Studios, Digital creator, Earth, Dar es Salaam.

KARIBU KATIKA ULIMWENGU🌍 WA BURUDANI 🎼,
MITINDO 💃,
ELIMU 📚,
MICHEZO ⚽,
STYLE ZA MAISHA🧬
UWANJA WA SIMULIZI📰

"FOLLOW" KUPATA KILA TAARIFA🗞️ NA KUWA MIONGONI MWA WANAFAMILIA👨‍👩‍👧‍👦 YETU...

ASALI HAITIWI KIDOLESEHEMU YA KWANZAMTUNZI: EDGAR MBOGOWHATSAPP: 0673873840TAHADHARI: Hadithi hii ya   .inayo somwa na m...
22/10/2024

ASALI HAITIWI KIDOLE
SEHEMU YA KWANZA
MTUNZI: EDGAR MBOGO
WHATSAPP: 0673873840
TAHADHARI: Hadithi hii ya .inayo somwa na mtu mwenye umri wa kuanzia miaka 18 na kuendelea, ni hadithi yenye kisa chenye ubunifu kwa hasilimia mia moja, sehemu, mitaa na majina yaliyo tumika, siyo harisi, ni ya kufikirika, na ayausiani na kisa hiki.

K**a kuna tukio au kitu chochote kitafanana katika hadithi hii, na tukio la kweli, basi aikuwa dhamira ya mwandishi, k**a utakuwa na maoni ushauri au lolote wasiliana na mwandishi wa hadithi hii, si luksa kunakiri au kubadiri hadithi hii kwa lolote, katika matumizi yoyote, pasipo kibari cha mwandishi kupitia whatsapp namba 0675873840.

Naaaaaaam!, hadithi yetu inaanzia kisiwani Zanzibar, ilikuwa ni jumanne yenye shamla shamla za sikuu za eid ya mfungo mosi, hii ni eid Ahl hadji, moja kati ya kuku kubwa sana kisiwani hapa.

K**a ilivyo kawaida, kwa wakazi wa kisiwa hiki, siku ya leo ilikuwa na pilika nyingi sana, toka asubuhi walionekana wake kwa waume wakitoka msikitini, huku wamependeza kwa mavazi mazuri mpya yenye kuvutia, huku wanawake wakiongoza kwa kupendeza, wakifwatiwa na watoto.

Hakika leo ni siku ambayo, hasilimia kubwa ya watu, walionekana wakiwa wenye nyuso za furaha, arufu nzuri ya vyakula ilizagaa mitaani, na kushibisha pua za kila wapita njia na wakazi, sambamba na sauti za music wa kasiwida, zilizokuwa zinasikika toka kwenye nyumba za watu, kila kona ya mitaa, na sehemu mbali mbali za biashara, zikizidi kuing’alisha siku kuu hii, ambayo kwa huku kisiwani uwa inasherehekewa kwa muda wa siku mbili, mpaka nne.

Mida ya saa saba za mchana, tupo mtaa wa jang’ombe kwa Soudi, ni mtaa wapili, toka kituo cha Mchina mwanzo, barabara kuu ya kiembe samaki, kupitia uwanja wa Amani.

Mtaa umechangamka sana k**a mitaa mingine ya kiswahili, wanaonekana watu wengi wa lika mbali mbali, yani watoto vijana na wazee, wakike kwa wakiume, waliokuwa wamevalia nguo nzuri na mpya za kupendeza, huku wanawake wakiwa wamejipamba zaidi kwa kuchora mikono yao mauwa mazuri kwa kutumia wino wa ina.

Pia wanawake wananukia vyema utuli wa udi, wameficha miili yao kwenye magauni mazuri aina ya baibuhi na habaya, huku vichwani mwao wakificha nywele zao kwa hijab, za rangi mbali mbali, zilizoendana na nguo walizovaa.

Lakini tofauti ilikuwa nyumbani kwa mzee Abeid Ally Makame, ambapo kwanza kabisa, tuna mwona mzee Abeid mwenyewe anatoka nyumbani, akiwa ameongozana na wake zake wawili, yani mke mkubwa, akiwa mwenye hasiri ya Africa bila chembe chembe yoyote ya uchotara, huku bi mdogo akionekana kwenye dalili ya mbali ya uchotara.

Wake wote wawili wa Abeid Makame, wakiwa wamevalia vizuri, magauni yao mapya na hijab zao, zilizo zidi kuwapendezesha, pamoja na viatu vyao vizuri vya mikanda, k**a ilivyokuwa kwa mume wao, ambae ni mwalimu wa shule ya sekondari ya mwanakwelekwe A, alie valia kanzu yake nyeupe mpya, na baraghashia nzuri yenye rangi ya kanzu yake.

Chini alivalia makubanzi, (sendo) za kisasa, ya rangi nyeusi, huku hasiri ya mzee huyu akiwa ni mwafrika hasiria bila chembe chembe yoyote ya mshanganyiko wa hasiri ya taifa au kabila jingine toka nje ya bara la africa.

Lakini ukiwatazama vyema watu awa watatu, utagundua utofauti kati yao, asa katika mwonekano wa hali ya nyuso zao, maana wakati mzee Abeid akiwa katika hali ya kawaida, mke mdogo alionekana kuwa katika hali ya kukosa furaha, kwa kiasi flani, huku mke mkubwa akiwa mwingi wa tabasamu.

Wakati huo huo, kwenye kibaraza cha nyumba ya mwalimu Abeid Makame, wanaonekana watu watatu, wote wakiwa na hasiri ya uchotara japo ulikuwa umefifia, lakini uliwapendezesha, kati yao alikuwepo binti mdogo wakike mwenye umri wa kati ya miaka kumi adi kumi na moja, pia wakiume mwenye umri wa miaka kati ya kumi sita adi kumi na saba.

Walikuwa na dada yao, ambae umri wake, ni mkadilio wa miaka kati ya ishilini sita au ishilini na tano, aliekuwa anawasindikiza kwa macho baba na mama zake, huku uso wake ukiwa umenyongea kwa mawazo, nae pia k**a wale watoto, alikuwa na hasiri ya uchotara, ambao licha ya kuwa ulio fifia, lakini uzuri wake ulionekana wazi wazi, kuanzia sura adi mwili wake, ata uzuni aliyonayo usoni mwake ilishindwa kuondoa uzuri wake wa hasiri.

Tofauti na wadogo zake ni kwamba, yeye alikuwa amevalia mavazi ya kawaida, ambayo japo yalikuwa ni masafi, na unaweza kuvalia popote katika siku za kawaida, pengine ata leo ndiyo aliyovaa msikitini, lakini ni wazi yalikuwa ya zamani, tunaweza kusema yalisha maliza eid moja au mbili kabla ya leo.

Ila pia licha mwonekano wa uzuri wake huo, akuwa amejipamba kwa chochote, k**a wanawake wengine wahuko mtaani, ni k**a wale watoto wawili, ambao mavazi yao licha ya kuwa masafi, ila pia yalionekana ayakuwa mapya, huku wote wakiwa wamekaa kibarazani, nyuso zao zimekata tamaa, macho yao yakitazama kushoto na kulia, yani kwenye barabara ya mtaa, ni wazi walitarajia kumwona mtu flani.

“kaka Mu, mbona rafiki yako mwenyewe aji sasa?” aliuliza yule mschana mdogo, wa miaka kumi na moja, huku anamtazama yule kijana wamiaka kumi na saba, ambae akujibu kitu zaidi ya kutazama kushoto na kulia, huku uso wake ukionyesha wasi wasi na kukata tamaa.

Dada mkubwa anawatazama wadogo zake, huku anawaona jinsi walivyo sawajika nyuso zao, “dada Radhia, mpigie kwanza umuulize mbona aji” anasema yule mschana mdogo, ambae ni k**a alisha kata tamaa, au aliona anacheleweshwa jambo flani.

“Jamani Zahara, uwe mvumilivu kidogo, kwani na yeye binadamu eti, lazima ale akoge ndio aje” anasema yule mwanamke mkubwa, kwa sauti tulivu iliyolemewa na uchungu flani, ambae kwa matazamo wa kawaida, ni mzuri wa sura umbo na rangi ya ngozi yake, “alisema anakuja mchana, lakini mpaka sasa ajaja” alilalamika Zahara.

Zilisha pita dakika kumi, toka mzee Abeid na mke wake waondoke, sasa mlango mkubwa wa mbele unafunguliwa, wanatokea watu watano, yani wanawake wawili wakubwa, mmoja akiwa na umri wa miaka 24 na mwenzie akiwa na umri wa miaka 21, wakiwa na watoto watatu, wakike wawili na wakiume mmoja, ambao umri wao aukuzidi miaka sita, mdogo kabisa akiwa na mkadilio wa miaka mitatu.

Wote walikuwa wenye hasiri ya weusi, lakini awa dada wawili walikuwa wamejipamba wakapambika, na kufanya ule msemo wa usichague mke ngomani utimie, maana licha ya kuwa walikuwa ni wazuri kiasiri, na wenye kuvutia lakini siyo k**a Radhia, huyu alie kaa hapa kibarazani, ila walizidi kupendeza kwa mapambo walivyo jiweka. ITAENDELEA,pia UNAWEZA kuisoma full Whatsapp namba text chap 0675873840
like share follow

ASALI HAITIWI KIDOLE

SEHEMU YA PILI

MTUNZI: Mbogo Edgar

WHATSAPP: 0675873840
ILIPOISHIA SEHEMU YA KWANZA: Wote walikuwa wenye hasiri ya weusi, lakini awa dada wawili walikuwa wamejipamba wakapambika, na kufanya ule msemo wa usichague mke ngomani utimie, maana licha ya kuwa walikuwa ni wazuri kiasiri, na wenye kuvutia lakini siyo k**a Radhia, huyu alie kaa hapa kibarazani, ila walizidi kupendeza kwa mapambo walivyo jiweka, SASA ENDELEA….

Yote kwa yote wote watano, walikuwa wamepeza kwa mavazi yao maalumu kwaajili ya siku kuu, wanakuja na kusimama kibarazani, “Hadija,mwage shangazi mwambie tunaenda kutembea” alisema mmoja wao, yani yule wa miaka ishilini na moja, huku akimwambia binti mdogo wa miaka mitatu, ambae aliishia kujitabasamulisha bila kuongea lolote.

Hii inamfanya Radhia ahisi k**a ni dhihaka, maana licha ya kujuwa anasemwa yeye, lakini niwazi iliwaumiza sana wadogo zake, anashindwa kusema lolote, anaishia kutabasamu, lakini moyoni mwake anahisi uchungu mkubwa sana.

“yani da Mariam ulivyopendeza, Mahamud akikuona anaweza kukusahau” alisema mwanamke wa miaka 21, yani yule mdogo, kwa sauti utani, “anaanzaje kusahau mali yake bwana, ebu achana utani, mwenzio ananijuwa nje ndani” alijibu yule alie itwa Mariam, kwa sauti iliyojaa nyodo, wakati huo huo simu yake inaita.

Mariam anatazama jina mpigaji, anaona ni Mahamud, “huyooo mume anapiga simu” anasema Mariam, huku anaachia tabasamu pana, kisha anapokea simu kwa mbwembwe akimkata jicho la pembeni dada yake mkubwa, “niambie mume wangu, mpo wapi?” anauliza Mariam kwa shahuku, na wakati huo huo kwambali wanatokea vijana wawili, walio valia suruali zao za jinsi na matishert ya rangi tofauti mmoja likiwa jeusi na mwingine likiwa jekundu.

Awa walikuwa na umri wa miaka kati ya ishilini na mbili mpaka ishilini na tano, ambao wanaonekana wakinyoosha mkono kwambali, “waleeeee” anasema yule wa miaka ishilini na moja, kwa sauti yenye shahuku, huku anashuka kwenye ngazi, akiwa amemshika yule mtoto mdogo, kuliko wote, yani Khadija, na kuanza kuongoza kule waliko wale vijana, akifwatiwa na wale wengine wawili, “ok!, tunakuja” alisema Mariam, huku na yeye anashuka kwenye ngazi za kibaraza, akiwa nyuma ya wenzake.

“sasa Da! Radhia, sisi tunaingia zetu forodhani, tuta kukuta jioni” alisema Mariam, huku anatembea kwa kunyata, k**a anavuka eneo lenye tope, ni kutokana na kuto taka viatu vyake vipya vichafuke.

Radhia ajibu chochote, zaidi anazidi kuumia moyoni, maana kila alicho ambiwa aliona kuwa ni kebehi zidi yake, na nimaumivu kwa wadogo zake, maana hayo ni maisha ambayo, amekuwa akiishi na ndugu zake, watoto wa mke mkubwa wa baba yake.

Hii ni tangu alipo arudi toka michenzani tobo la pili, alikokuwa anaishi na mume wake zamani, bwana Issa Kiparago, alie mtariki kwa taraka tatu, mwaka mmoja ulio pita.********

Familia ya mzee Abeid Ally Makame, ni familia ya wake wawili, k**a nilivyokudokeza hapo mwanzo, mmoja mwenye asiri ya Africa hasiria, na mwingine alikuwa na hasiri ya mbali ya uchotara, namaanisha kuwa, toka alipozaliwa chotara wakwanza, sasa vilisha pita vizazi zaidi ya vinne, mpaka mama yake Radhia.

Mzee Abeid amejaliwa kupata watoto saba kwa wake zake wote wawili, wakati bimkubwa akiwa amezaa watoto wanne, mmoja Himid akiwa ndie kwanza, na sasa anaishi Oman, anakofanyia kazi, yeye na mke wake, huku watoto wake wawili wakiwa hapa kwa baba yake.

Pia wanawake watatu kwa mke mkubwa, yani Siwema, ambae ndie dada mkubwa, anae kaa kwa mume wake, kule Marindi, ambae pia kwa sasa mume wake yupo Oman anakofanyia kazi, ambayo inasemekana ni kazi ya kutunza bustani ya kwenye nyumba ya mtu binafsi.

Siwema nae anamtoto moja ndie huyu Khadija, ambae yupo na mama zake wadogo, yani Mariam na Zuhura, ambao ni wapenzi na shabiki wa mitandao ya kijamii, mida mwingi ushinda pamoja, huku wakishindana kujilemba, na kupiga picha, ambazo uzipost mitandaoni, huku wakichati na marafiki zao wakiume.

Kwa upande wa mke mdogo, yeye alikuwa na watoto watatu tu! Hakuwa na mjukuu wala kitukuu, mtoto mdogo kabisa alikuwa ni huyu Zahara, aliekuwa anasoma darasa la tatu shule msingi Jang’ombe, kaka yake Mukhsin, yeye alikuwa anasoma kidato cha tatu shule ya sekondari ya Nyuki, pia alikuwa mchezaji mzuri wa mpira wakikapu, yani basket Ball, ushiriki mazoezi kwenye viwanja vya maisala au kule nyuki, karibu na kambi la jeshi la Idd Ba Vuai Camp.

Mtoto mkubwa kabisa alikuwa ni huyu Radhia, ambae aliolewa mapema kuliko ata dada yake Siwema, lakini maisha yake yaliingia kwenye shida kubwa, mala baada ya kupewa taraka na mume wake, tuangalie ilikuwaje.

MWAKA MMOJA NYUMA: Kipindi hicho tayari Radhia alikuwa amekaa kwenye ndoa yake kwa muda wa miaka miwili, maana aliolewa akiwa na miaka ishilini nambili tu, ilikuwa ni mala tu baada ya kumaliza shule ya sekondari, kidato cha nne, na kupata matokeo ya division 3.

Akiwa k**a mwanamke ambae, alie lelewa katika maadiri mazuri, na kuwa binti mwenye nidhamu na heshima kubwa, kiasi cha kila mmoja kutoa sifa ya kuwa, Radhia alikuwa ni mwamke wa mfano, na kumtamani kwa namna tofauti tofauti, ikiwa wanawake wenzake walitamani kuwa k**a Radhia, au kuwa karibu nae k**a rafiki, pengine ingewaongezea thamani yao.

Huku wanaume wakitamani angarau na mke k**a Radhia, k**a siyo dada au binamu, ilimladi kila mmoja alitamani kitu toka kwa mwanamke huyu, ambae ukiachilia uzuri wa umbo lake, sura, sauti na rangi ya ngozi yake, pia alikuwa na tabia nje, mtaratibu na mpole, asie na majivuno wa kiburi.

Lakini yote kwa yote, bahati ikamdondokea bwana Issa Kiparago, ambae anamkuta mwanamke huyu akiwa bikira, kwa maana akuwai kushiriki tendo la ndoa mpaka pale walipofunga nae ndoa, ni zama ambazo zinaanza kusahaulika kwa sasa, kiasi kwamba ukibahatika kumkuta mwanamke wahivyo unajiona shujaa.

Mwanzo maisha yalikuwa mazuri, akiwa mke wa pili wa mume wake Issa kiparago, mkazi wa mtaa wa michenzani tobo la pili, ambae tayari alikuwa na watoto wawili kwa mke wake wa kwanza.

Lakini mambo yalianza kuwa tofauti kidogo, baada ya mwaka mmoja kupita, bila dalili ya Radhia kushika ujauzito, mume wake akianza kwa kupunguziwa fedha za matumizi, asa zile za mahitajio yake binafsi, pamoja na kunyimwa huduma za ziada, k**a vile pesa ya nguo mpya, fedha za vipodose na manukato.

Pia hapakuwa na mtembezi ya siyo ya lazima, yani k**a ilivyokuwa mwanzo yani matembezi ya pamoja na mume wake, kwenda sehemu mbali mbali, asa siku za siku kuu, na ata ikitokea Radhia akaumwa, basi angeenda mwenyewe hospital, na siyo kupelekwa na mumewe, k**a ilivyokuwa kwa mke mkubwa, ambae aliendelea kupata kila kitu, na mapenzi moto moto k**a zamani.

Siku zilivyo sogea ndivyo visa zaidi vilijitokeza, na sasa alikuwa akifake sana, k**a angefanya kosa dogo, angeambiwa, “k**a ujazaa uwezi kuwa na akili za kiutu uzima ata siku moja” hakika kauri hii, ilimfanya Radhia, ajione mwenye mapungufu makubwa sana, lakini aliendelea kuvumilia.ENDELEA…. KUFATILIA HADITHI HII YA , HAPAHAPA pia usisahau kusoma simulizi Whatsapp namba 0675873840 Iike share follow

ASALI HAITIWI KIDOLE

SEHEMU YA TATU

MTUNZI: Mbogo Edgar
WHATSAPP: 0675873840
ILIPOISHIA SEHEMU YA PILI: Siku zilivyo sogea ndivyo visa zaidi vilijitokeza, na sasa alikuwa akifake sana, k**a angefanya kosa dogo, angeambiwa, “k**a ujazaa uwezi kuwa na akili za kiutu uzima ata siku moja” hakika kauri hii, ilimfanya Radhia, ajione mwenye mapungufu makubwa sana, lakini aliendelea kuvumilia.ENDELEA….

Japo akuwai kufurahia tendo la ndoa kwa mume wake, ambae siku zote alicho kujuwa kwenye mapenzi ni kuchukuwa na kuipachika, kicha nje ndani mala kadhaa na kushusha wazungu, kisha mchezo umekwisha, akimwacha Radhia ndio kwanza anaanza kuita dudu, lakini ilimuuma sana, siku ambayo ilikuwa zamu yake ya kulala na mume wao, lakini mume wake akaenda kwa mke mkubwa.

Siku ya pili Radhia alimfwata mume wake na kuongea nae kistaarabu kabisa, “samahani mume wangu, jana ilikuwa zamu yangu, naona ulipitiwa kidogo, ukaenda kwa mke mkubwa, basi leo naomba ufidie zamu yangu….” Akupewa nafasi ya kumaliza kauri yake, “wala sikupitiwa, na kuanzia sasa nitaendelea kulala kwa mke mkubwa, maana kwa sasa tunatafuta mtoto mwingine, we endelea kulala peke yako” alisema Issa Kiparago, na akusubiri mke wake aseme lolote, akaondoka zake.

Ilimuuma sana Radhia, ambae kiukweli alijifungia chumbani na kulia sana, akuishia hapo akaenda kumweleza mama yake, ambae alimsihi avumilie maana ata yeye ilikuwa hivyo, wakati alipoolewa, maana alichelewa sana kupata mtoto wa kwanza, ambae ndie huyu Radhia.

Radhia alirudi kwa mume wake, na kuendelea na maisha yale mapya, yaliyoitaji uvumilivu, japo baadae mambo yalizidi kuwa mbaya zaidi, pale mke mkubwa alipoanza kumsema wazi wazi, kuwa Radhia amekuja kumaliza fedha zao, na kubana nafasi ya watoto kujiachia, maana akuwa na faida yoyote katika familia ile.

Mwaka wapili ulifika bila dalili yoyote ya ujauzito, angalau ingetokea moja iliyo aribika, angejuwa anauwezo wa kushika mimba, lakini hapakuwa na ata dalili ya kukosa siku zake za mwezi, alikuwa anazipata kwa muda mwafaka kabisa.

Hapo mume wake bwana Issa Kiparago, ambae akutaka kujiangaisha kwenda hospital, kuangalia tatizo la mke wake ni lipi, akaamua kumpatia taraka tatu, ikiwa ni ushauri wa mke wake, pamoja na marafiki zake.

Taraka tatu zikatolewa, na mwanadada huyu, akarudi nyumbani kwao, ambako sasa alikutana na masimango makubwa sana, kuanzia kwa mama yake mkubwa, dada yake mkubwa, ambae ni mtoto wa mama mkubwa, yani mke wakwanza wa bwana Abeid Makame, ambae kwa wakati huo tayari alikuwa amesha olewa, na alisha pata mtoto.

Aikuwa hao peke yao, sasa hadi Mariam na Zuhura, nao waliacha kumheshimu dada yao, na alipo watahadharisha walimjibu vibaya, “k**a ungekuwa na busara ndoa yako isingekushinda” hiyo kauri ilitamkwa mala nyingi sana, na wakina Zuhura na mwenzie Mariam.

Sasa hakuna alie mwelekeza kwa jina lake, wengi walimtambulisha k**a dada mjane, kwamaana kule visiwani, mwanamke alie achika uitwa mjane, majirani nao baadhi yao walimesimanga Radhia, kwa kuachika kwake, na ukichukilia wakati ule alionekana kuwa ndie mwanamke mwenye kuongoza kwa uzuri wa sura tabia na umbo, katika mtaa mzima wa Jang’ombe kwa Soud.

Kuna kipindi majirani na ndugu zake wa damu, yani watoto wa mke mkubwa, waliende mbali zaidi, na kumwambia kuwa alikuwa na lahana ya kulithi kwa mama yake, iliyotokana na kupenda kuolewa na waume za watu, kauri hii ilimuumiza sana Radhia, ambae akutaka masahibu yake, yamwingize mama yake katika tuhuma nzito k**a hii.

Unaweza kuwakuta wadogo zake yani Mariam na Zuhura wamekaa wanaongea na kucheka, huku wakimsimanga kwa mafumbo, “yani mimi niolewe alafu mume wangu aniolee mke mwingine, pata chimbika” ilo angeliongea Mariam, huku Zuhura akiongea la kwake, “kwanza mimi mwenyewe siwezi kuolewa mke wapili, nitakaa mchana kweupe, yanini kuchangia dudu, wakati zimejaa tele” hakika ilimuuma sana Radhia, ambae alishindwa kuwakemea wadogo zake, ambao walikuwa na kauri chafu, k**a fagio la chooni.

Kuna wakati wakina Mariam na Radhia, wakiwa wanatoka kwenda wa marafiki zao wa kiume, yani wapenzi wao, ungesikia wanasemezana kimafumbo, “wacha tuka liwazwe sie wenye waume wetu, kuna wajane wanatamani nafasi k**a hizi, wanazikosa” k**a nilivyo kudokeza, neno mjane ni mwanamke alie tarikiwa.

Pia Mariam na Zuhura, wakirudi toka kwenye matembezi yao, wangebeba p**i na biscuit, au urojo kwenye vimifuko vya prastick, kisha kuwagea wadogo zao, watoto wa dada yao na wakaka yao, kisha wao kula urojo mbele ya Radhia, ili kumrusha roho, “raha ya kuwa na mtu anaekupenda” angesema mmoja wao wakati wanakula, na hayo yote waliyafanya k**a baba yao hayupo karibu, maana akuwa anapenda mambo ya kipuuzi.

Katika vitu vilivyo wai kumuuma, ni siku moja ambayo, dada yake Siwema, alikuja pale nyumbani, mida ya saa tano asubuhi, akitokea kazini, alikokuwa amelala tokajana, japo hakuna mwenye uhakika k**a alikuwa amelala kazini, maana alikuja jana kumleta mtoto, kidai kuwa kesho analala kazini, aliwaachia maagizo yote wakina Mariam na Zuhura.

Sasa slipofika nyumbani alimkuta Khadija amechafuka vibaya sana, Mariam na Zuhura walikuwa chumbani kwao, wanatazama video za ngono kwenye simu zao, Radhia alikuwa chumbani anashona moja ya nguo yake kushindia, mala akasikia sauti ya dada yake Siwema toka nje.

“ebu tokeni nje haraka” ilikuwa sauti kali yenye hasira, Radhia akatoka nje haraka, akamwona Siwema akiwa amesimama mbele ya Khadija aliekuwa amekaa chini anachezea vumbi, “dada kuna nini?” kuna nini, nini umwoni mtoto alivyo chafuka kweli nawaachia mtoto alafu nyie mnamwacha hivi” alibwata Siwema, ambae kwa mtazamo wa haraka, nik**a akuwa sawa, yani alikuwa na dalili ya ulevi.

Radhia anamtazama Khadija, anamwona kweli amechafuka, “samahani dada, ila alikuwa na wakina Mariam…” alisema Radhia huku anataka amchukuwe Khadija akamwongeshe, lakini akupewa nafasi, “tena wewe usimguse mwanangu kabisaaa, k**a ujazaa uwezi kuwa na uchungu wa mtoto, yani unashindwa kumwongesha mtoto, alafu unawasingizia wakina Mariam, kwani wewe uwezi kumwogesha mtoto, alafu unaniona mimi ndio unajifanya samahani” anaongea Siwema akimaliza kwa minya pua.

Wakati huo tayari wakina Mariam walikuwa wamesha fika pale kibaradhani, na kushuhudia lile timbwili, ambalo liliwapa burudani mionyoni mwao, Radhia akiishia kufuta macho, maana kitendo cha kukosa mtoto, kilikuwa fimbo kwa watu, kwaajili ya kumchapia. ENDELEA…. KUFATILIA HADITHI HII YA , HAPAHAPA KWA HADITHI ZA MBOGO EDGAR pia usisahau unaweza kuisoma Whatsapp namba 0675873840 like share follow

MGENI njoo🧌MWENYEJI apone😎
11/10/2024

MGENI njoo🧌
MWENYEJI apone😎

  WAMTIA P.DIDDY MATATANI BAADA YAKUMPA UMAARUFU.Msanii mkongwe na maarufu duniani KANYE WEST anasema kwamba yanayofichu...
10/10/2024

WAMTIA P.DIDDY MATATANI BAADA YAKUMPA UMAARUFU.

Msanii mkongwe na maarufu duniani KANYE WEST anasema kwamba yanayofichuka kwasasa kuhusu rapa P-DIDDY alishawahi kuyasema miaka miwili iliyopita ila watu walimuona chizi. Amesema aliyokua anafanya P-DIDDY yanatokana na masharti ya illuminati inayomuongoza.

"Mfano wao ni raisi tu, kwanza wanakupa nguvu ili waweze kuku-control na pale watakaposhindwa kuku-control wanakupoteza na kukunyang'anya kila kitu"
KANYE WEST ametaja pia baadhi ya mastaa wanaongozwa na illuminati akiwemo MEEKMILL, DIDDY, JAY-Z, BEYONCE, DR-DRE na wengine.

(Illuminati) Wana hasira juu yangu kwasababu wameshindwa Kuni control wanawaweza kum-control JAY-Z NA BEYONCE, DIDDY Na kila mtu lakini sio mimi, wanataka mimi niwe KANYE WEST lakini mimi ni mtu pekee anayeweza kuni-control na kunivunjia heshima k**a akitaka ni MUNGU TU.
Mama yangu leo hii hayupo kwasababu walimtoa kafara, MICHEL JORDAN alimtoa kafara baba yake, DR-DRE alimtoa kafara mtoto wake wa kiume
K**a ukiwa Hollywood, unatoa kafara nyingi ili tu wakupe nguvu, umaarufu na pesa halafu Wana ku-control unakuwa chini yao. MUNGU ananipenda na ndio maana nilimrudia na kuwa MKRISTO.

Nilipokuwa chini yao hawakuwa na chochote cha kutumia dhidi yangu na badala yake walichukua kilakitu nilichonacho ikiwemo dili la ADIDAS, baada ya kuchukua kila kitu, Jarida la Forbes lenye chuki dhidi yangu lilikuwa la kwanza kuchapisha taarifa kuwa (utajiri wa KANYE WEST ni dolla milioni 400) na niliishia kucheka tu kwasababu mimi bado ni bilionea. YESU ni mfalme na MUNGU ananipenda.

Hivyo nasema ukweli huu ikiwa mungu yupo upande wangu basi hakuna kitu kitanitokea " - KANYE WEST

Wasanii wetu, umaarufu mzuri ni ule anao kupa Mungu alie juu mbinguni, sio kikundi cha watu wenye malengo ya upotofu. ✍️

Work of Art❤️Uyu Jamaa anajua sana🙌🙌
09/10/2024

Work of Art❤️
Uyu Jamaa anajua sana🙌🙌

MUNGU ATUPE NINI SISI   🙏🙏Bado sijaona timu ya kumzuia   🏆NA MWAKA HUU   TUNAONDOKA NALO BY POWER💪🏿 BY FORCE🧌           ...
07/10/2024

MUNGU ATUPE NINI SISI 🙏🙏
Bado sijaona timu ya kumzuia 🏆
NA MWAKA HUU TUNAONDOKA NALO BY POWER💪🏿 BY FORCE🧌
💛💚🇹🇿🇹🇿🇹🇿💚💛




MAKUNDI CAF CONFEDERATION CUP🔥🔥MAKOLO🦁 MSHINDWE WENYEWE KUBEBA 🏆🏆🏆
07/10/2024

MAKUNDI CAF CONFEDERATION CUP🔥🔥

MAKOLO🦁 MSHINDWE WENYEWE KUBEBA 🏆🏆🏆

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Mieiam Annet, Simon Josepg, Muneer Benjamin, Seleman Kl, ...
05/10/2024

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Mieiam Annet, Simon Josepg, Muneer Benjamin, Seleman Kl, Erasto Urio, Issaz Abdallah, Zenice Mosha, Martin Willson, Modelly Minah, Sarah Jidiku, Petronell Peter, Priska Jackson, Nyangasa Shamsa, Jamilla Nurdin, Rahma Abubakarii, Balick Balick, Kvoo Mayanjika, Mtiba James, Seifh HR, Neva Kiongoz, Severine Shedrack, Yasr Mtoro, Rama Kapapala, Rashidi Hamiss, Anny Nziwa, Meena Ally, Lbenn't Albert, Adeeh Anderson, Anax Audax, Joshua Kadu, Stephano Gipson, S Tumbo Sasama, Zawadi Mwinuka, Omary Rajabu, Micky A Msumari, Gizho Giselle, Ndevile Ndevile

22/09/2024

Unaweza kuta uyu ndo mwenyewe🎃🎃
Amekuja duniani kuchukua watu wake 🤣🤣🤣

22/09/2024

Hapa kaka yangu ameyabananga😏
Mwenzake kapata yeye kapata 🤮
gani hii

Nipe sifa 3 za awa Mademu alafu toka nduki🏃🏿🏃🏿🤣Comment ziwe
16/09/2024

Nipe sifa 3 za awa Mademu alafu toka nduki🏃🏿🏃🏿🤣

Comment ziwe

SAY SOMETHING PLEASE 😂
15/08/2024

SAY SOMETHING PLEASE 😂

Dear Ladies 💃 Ivi   ni kitu cha kumnyima mtu kweli🤔
14/08/2024

Dear Ladies 💃 Ivi ni kitu cha kumnyima mtu kweli🤔

ILA WANAWAKE 🤣🤣
14/08/2024

ILA WANAWAKE 🤣🤣

Hi! ❤️ Leo Tusalimiane kwa MAKABILA 😀Naanza mimi: Ulimhola 😂
14/08/2024

Hi! ❤️ Leo Tusalimiane kwa MAKABILA 😀

Naanza mimi: Ulimhola 😂

HAPPY BIRTHDAY TO ME🎉🎂I'M THE YOUNGEST C.E.O IN🇹🇿FOLLOW ME AS MY BIRTHDAY GIFT🎁
01/08/2024

HAPPY BIRTHDAY TO ME🎉🎂
I'M THE YOUNGEST C.E.O IN🇹🇿

FOLLOW ME AS MY BIRTHDAY GIFT🎁

Address

Earth
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when BrightSpear Studios posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Videos

Share