24/08/2024
POLISI YATOA TAARIFA YA MATUKIO MATATU YA WATU KUTEKWA NA KUKUTWA WAKIWA WAMEUAWA.
Jeshi la Polisi lingependa kutoa taarifa ya matukio matatu ya watu kutekwa/kutoweka katika mazingira ya kutatanisha na kukutwa wakiwa wameuawa.
Tukio la kwanza ni tukio la kijana mmoja aitwaye Samwaja Sifael Said, miaka 22 mkazi wa Kijiji cha Chalunyangu Mkoani Singida kutoweka tangu Agosti 8, 2024 katika mazingira ya kutatanisha na Agosti 23,2024 mwili wake kukutwa umefukiwa kwenye shimo huku sehemu zake za siri zikiwa zimekatwa.
Tukio la kutoweka kwake liliripotiwa katika Kituo cha Polisi Makuro na lilifunguliwa jalada na uchunguzi kuanza.
Baada ya ufuatiliaji wa kina wa Polisi zilipatikana taarifa kwa kijana ambaye walikwenda
kutizama mpira na Samwaja Sifael Said (marehemu) na baada ya mpira kumalizika
walipokuwa wakirejea nyumbani walikutana na vijana wawili waliomwambia twende tukanywe pombe na walipoondoka pamoja hakurejea nyumbani na ndipo ndugu zake wakafika Polisi kutoa taarifa.
Polisi walifanikiwa kuwak**ata vijana hao wawili na baada ya mahojiano walieleza ni kweli walikwenda kunywa pombe na marehemu na walipokuwa wanarejea walimuua kwa kumnyonga kisha kukata sehemu zake za siri na kuufukia mwili wake kwenye shimo.
Watuhumiwa hao pia walieleza walifanya hivyo baada ya kuelezwa na Mganga wa kienyeji kuwa, wakipata sehemu za siri za binadamu watakuwa matajiri. Polisi walifanikiwa kumk**ata mganga huyo.
Walieleza wapo tayari kwenda kuonyesha walipoufukia mwili wa marehemu.
Aidha, baada ya taratibu kufuatwa, Agosti 23,2024 watuhumiwa hao walikwenda kuonyesha. walipofukia mwili wa marehemu na ufukuaji ulipofanyika mwili huo ulitambuliwa ni wa Samwaja Sifael Said aliyetoweka toka Agosti 8,2024.
Hata hivyo, baada ya wananchi kushuhudia mwili wa marehemu na kubaini watuhumiwa waliohusika waliamua kwenda nyumbani kwa mganga huyo kwa nia ya kuchoma nyumbani yake moto.
Jeshi la Polisi lilifanikiwa kutuliza vurugu hizo na kurejesha hali ya amani. Watuhumiwa wanaotuhumiwa kuhusika katika tukio hilo na wanaendelea kushikiliwa ni Selemani Shabani Nyandalu@Hango, miaka 24. Mkazi wa Chalunyangu, Saidi Haji Msanghaa , miaka 24, Mkazi wa Kijiji cha Migungu na Kamba Kasubi, miaka 34, Mganga wa Kienyeji mkazi wa kijiji cha Migungu Mtinko.
Tukio la pili ni tukio lilitokea Jijini Dar es Salaam ambalo liliripotiwa Agosti 19,2024 kuwa, Mwanamke aitwaye Ezenia Stanley Kamana, miaka 36 Mkazi wa Tandika Maghorofani Temeke ametoweka/ametekwa.
Jeshi la Polisi kulingana na taratibu lilifungua jalada na kuanza uchunguzi. Katika uchunguzi zilipatikana taarifa kuwa mwanamke huyo alikuwa na rafiki yake wa kiume aitwaye Abdallah Miraji @ M***a, miaka 42 Mkazi wa Sinza kwa Remmy na walikuwa na mgogoro.
Alik**atwa na alipohojiwa alikataa kuwa hafahamu alipo huyo rafiki yake. Agosti 22,2024 zilipokelewa taarifa kuwa, huko katika eneo la Silversand barabara ya mtaa wa Freedom Kunduchi kumeonekana mifuko ambayo ina viungo ambavyo vinadhaniwa ni vya binadamu.
Polisi walifika eneo hilo na kukuta mifuko minne ya sulfleti (viroba) na waliichunguza na kukuta viungo vya binadamu ambavyo ni paja moja, vipande vya mikono miwili, eneo la kifua, tako, matumbo na nguo.
Baada ya kupata viungo hivyo na mtuhumiwa kuelezwa aliamua kueleza ukweli kuwa, alimuua mpenzi wake huyo na kutenganisha mwili wake katika vipande na kwenda kuvitupa maeneo tofauti.
Agosti 23,2024 aliwaongoza askari hadi eneo la Tegeta Block D na kuwaonyesha alipotupa miguu na baadaye aliwaonyesha eneo ambalo alitupa kichwa.
Tukio la tatu lilitokea huko Jijini Tanga ambapo mtoto aitwaye Elia Elifaza Mchome wa miaka 3 mkazi wa kitongoji cha Kwedijava Wilayani Handeni Mkoa wa Tanga alitoweka katika mazingira yasiyoeleweka toka Agosti 19,2024 alipokuwa anacheza nje ya nyumba yao.
Taarifa ilitolewa Polisi na Uchunguzi ulianza na ukafanikisha kuk**atwa Jackson Elisante @ Maeda, miaka 23, mkazi wa Kwedijava eneo linalochimbwa madini aina ya dhahabu.
Baada ya kuk**atwa na kuhojiwa alikubali kumchukuwa mtoto huyo na kwamba alimkabidhi Mama yake mkubwa ambaye ameenda naye Babati Mkoa wa Manyara. Askari waliambatana naye hadi Babati lakini alibadili kauli na kueleza mtoto huyo yupo Kwedijava Handeni amemfukia ndani ya chumba anachoishi.
Walirejea Handeni na akaonyesha chini ya kitanda kwenye chumba anachoishi alikokuwa amemfukia mtoto huyo baada ya kumuua. Watuhumiwa wengine ambao wanashikiliwa kutokana na tukio hili kwa ajili ya uchunguzi zaidi ni pamoja na Sadick Lugendo, Mahiza Gumbo, Maligo Juma, Ally Mashaka, Juma Bakari, Abdulrahman Selemani na Bahati Daudi.
Jeshi la Polisi lingependa kutoa onyo kwa baadhi ya watu kuacha tabia hizi ambazo zinatokea ndani ya jamii zinazosababisha watu kudaiwa kupotea/kutekwa ambazo ni pamoja na wivu wa mapenzi, imani za kishirikina, tamaa za mali/fedha na kulipiza kisasi.
Aidha, tunatoa angalizo kwa baadhi ya watu wanaozungumzia matukio ya aina hii watumie majukwaa yao kwa ungalifu kwani sababu wanazotoa ni kutaka kubadilisha ukweli ya yanayoendelea ndani ya jamii ili kuleta taharuki na kujenga uhasama.
Tunatoa rai kwa Viongozi wa Dini, Wazee wa Kimila, Wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla kuona matatizo haya yanayotokea ndani ya jamii hivyo waendelee kujenga misingi bora ya kuyazuia kuanzia ngazi ya familia.
Aidha, Jeshi la Polisi ningependa kutoa taarifa juu ya Afisa wa Polisi anayetajwa kwa jina la Fatuma Kigondo kwamba uchunguzi wa kina ulishafanyika ikiwa ni pamoja na kupata maelezo ya watu mbalimbali pamoja na ya kwake na jalada limepelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka.
Jambo lingine, Jeshi la Polisi lingependa kutoa onyo kali kwa baadhi ya wananchi ambao wamekuwa na tabia ya kujichukulia sheria mikononi badala ya kufuata taratibu zilizopo za kuwasilisha malalamiko ili yapatiwe ufumbuzi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo. Wakumbuke malalamiko au kero hata siku moja hayatatuliwi kwa njia ya kujichukulia sheria mikononi kwani kwa kufanya hivyo ni kosa kisheria ambapo husababisha madhara kwa maisha ya watu na mali zao.
Mfano tukio la baadhi ya wananchi la kujichukulia sheria mikononi huko Lamadi Mkoani Simiyu Agosti 22,2024 na kwenda kuvamia kituo cha Polisi na kuharibu mali wakumbuke ni kosa la jinai na imesababisha madhara kwa binadamu, mali na kuzuia shughuli za maendeleo kuendelea.
Jeshi la Polisi linatoa onyo kwa wenye tabia k**a hizo na yeyote mwenye mawazo ya kuendelea kufanya uhalifu k**a huo, Jeshi la Polisi lipo imara kwani litachukuwa hatua kwa nguvu ile ile ambayo watu wa aina hiyo wanatumia katika kutekeleza uhalifu wa kujichukulia sheria mikononi.
Imetolewa na:
David A. Misime - DCP
Msemaji wa Jeshi la Polisi
Makao Makuu ya Polisi
Dodoma, Tanzania.