Baesadigital

Baesadigital Informing, Educating and Entertaining Knowledge for all.

Hongera kwa kuongeza mwaka mwanafamilia wa Baesa Media
10/01/2025

Hongera kwa kuongeza mwaka mwanafamilia wa Baesa Media

Kampeni ya Mama Samia kuwa mwarobaini wa Migogoro ya wakulima na wafugaji Kilosa. Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. D...
15/12/2024

Kampeni ya Mama Samia kuwa mwarobaini wa Migogoro ya wakulima na wafugaji Kilosa.

Waziri wa Katiba na Sheria Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amesema Wilaya ya Kilosa imekuwa ikikabiliwa na migogoro mingi ikiwemo ya  wakulima na wafugaji na kwamba imekuwa makao makuu ya migogoro ambayo mwarobaini wake ni Kampeni ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia - Mama Samia legal Aid Campaign.

Waziri Ndumbaro amebainisha hayo Disemba 15, Mwaka huu wakati akizindua kampeni ya msaada wa kisheria ya Mama Samia katika kata ya Magomeni Wilayani Kilosa Mkoani humo ikiwa ni siku ya pili baada ya kampeni hiyo kuzinduliwa Kimkoa Disemba 13, 2024.

Akifafanua zaidi, Waziri huyo amesema migogoro inayowakabili wananchi wa Kilosa kumeifanya Wizara ya Uvuvi na Mifugo kuteua Kilosa kuwa makao makuu ya migogoro ya wakulima na wafugaji, hivyo ameitaka timu ya wanasheria wa kampeni hiyo kuandaa ripoti itakayoonesha migogoro iliyotatuliwa na ambayo haijatatuliwa ili  ambayo haijatatuliwa ifanyiwe operesheni maalum ya siku kumi kuhakikisha inaisha.

"...Na mimi niseme sasa baada ya siku hizi kumi itaandaliwa ripoti yenye kuainisha migogoro ipi imekwisha na ipi imesalia ile ambayo imesalia tutakuja na operesheni maalum kumaliza migogoro hiyo..."

Sambamba na hayo, amewataka wananchi wa Mkoa wa Morogoro kujitokeza kwa wingi kwenye kampeni hiyo mara itakapofika katika maeneo yao kwa lengo la kupata usaidizi wa kisheria ili kusuruhisha migogoro yao kwa kufuata misingi ya sheria ili haki ipatikane bila kumuonea mwingine.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amemuomba Waziri wa Katiba na Sheria kuongezewa muda wa kampeni hiyo kwani amesema Wilaya hiyo ni kubwa ambapo Kata 10 na Vijiji 30 pekee vilivyobainishwa kufanyika kampeni hiyo haitakidhi haja ya wananchi wengi wa Wilaya hiyo kufikiwa na Kampeni hiyo.

Amesema, Wilaya hiyo inakabiliwa na migogoro mingi hususan ya wakulima na Wafugaji, migogoro ya kijamii ikiwemo ukatili wa jinsia ya wanawake na watoto, mirathi na ardhi, hivyo kufika kwa msaada huo wa kisheria Kutatatua kero nyingi za kijamii Wilayani na Mkoa kwa ujumla.

Mradi wa TMCHIP kwenda kuboresha afya ya Mama na mtoto. Mradi wa mpango wa uwekezaji wa huduma ya Mama na mtoto (TMCHIP)...
12/12/2024

Mradi wa TMCHIP kwenda kuboresha afya ya Mama na mtoto.

Mradi wa mpango wa uwekezaji wa huduma ya Mama na mtoto (TMCHIP) umelenga  kuboresha afya ya Mama na mtoto pamoja na wananchi wote kwa kuboresha miundombinu yakiwemo majengo, ajira, uboreshaji wa huduma za rufaa na kununua vifaa na vifaa tiba ili kuwa na huduma za uhakika hususan za kundi hilo hapa nchini.

Hayo yamebainishwa Disemba 12, Mwaka huu na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nchi, ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya Dkt. Grace Magembe wakati akifungua mafunzo ya utekelezaji wa mradi wa TMCHIP katika ukumbi wa hoteli ya Cherry iliopo Mkoani Morogoro yakiwa na lengo la kuwajengea uwezo na kuongeza uelewa wa watendaji na wataalam wa sekta ya afya.

Akifafanua zaidi Naibu katibu huyo, amesema mradi huo unaogharimu zaidi ya Tsh. Bil 16 unalenga kupunguza vifo vya Mama na mtoto ambapo hadi sasa imepunguza kutoka vifo 556 kwa kila vizazi hai 100,000 mpaka 104 kwa kila vizazi hai 100,000  ikiwa ni zaidi ya 80%, hivyo mradi huo una malengo mahsusi ya kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi.

"...Mradi huu ambao tunaongelea hapa ni mradi ambao umejikita kuboresha afya ya Mama na mtoto lakini sio afya ya Mama na mtoto pekee bali na afya ya wanannchi wote..." amesema Dkt. Grace Magembe

Aidha, Dkt. Grace amesema mradi huo umepanga kutoa ajira kwa watumishi 1000
ambapo mpaka sasa mradi huo wameajiriwa watumishi 700 na ajira 300 kutangazwa hivi karibuni.

Katika hatua nyingine, Dkt. Magembe amewataka wataalam na wasimamizi hao kusimamia vema miundombinu inayojengwa na mradi huo kwa kutekeleza kwa ufanisi na kuzingatia thamani ya fedha kuendana na ubora wa mradi (Value for money) ili kuwa na miundombinu bora itakayotumika kizazi cha sasa na kijacho.

Sambamba na hayo Dkt. Magembe amewasisitiza kuwa, katika kutekeleza miradi hiyo waepuke uharibifu wa mazingira ili kumuunga Mkono Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kupiga vita uharibifu wa mazingira huku akiwataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuhakikisha maeneo yanayopendekezwa kutekeleza miradi husika yawena hati ili kuepuka migogoro baada ya mradi kuanza kutekelezwa.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi Ya Rais TAMISEMI Dkt. Grace Magembe amepokea Magari sita yaliyotolewa na Amref Health Africa kwa...
12/12/2024

Naibu Katibu Mkuu Ofisi Ya Rais TAMISEMI Dkt. Grace Magembe amepokea Magari sita yaliyotolewa na Amref Health Africa kwaajili ya usimamizi shirikishi wa shughuli za Afya katika Mikoa ya Mara na simiyu.

Magari hayo yamekabidhiwa kwa Mikoa hiyo ikiwa ni awamu ya pili ambapo awali magari mawili yalikabidhiwa Kwa Mkoa wa Simiyu na sasa Amref imetoa Magari manne ambapo matatu yataenda Mkoa wa Mara na moja Simiyu na kufanya jumla ya Magari matatu Kwa Mkoa wa Mara na Simiyu.

ADHA YA MAJI YAISHA MANGAE,  MHE. MKUCHIKA AISHUKURU HALMASHAURI KWA USIMAMIZI BORAWaziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikuku ...
27/10/2024

ADHA YA MAJI YAISHA MANGAE, MHE. MKUCHIKA AISHUKURU HALMASHAURI KWA USIMAMIZI BORA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikuku (kazi Maalum) Captain Mstaafu Mhe. George Mkuchika (MB) ameishukuru na kuipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro kwa usimamizi na ufuatiliaji mzuri wa fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kutekeleza miradi ya maendeleo ili kutatua changamoto zinazowakabili wananchi.

Mhe. Mkuchika amebainisha hayo Oktoba 27, 2024 wakati akizindua mradi wa maji wa Mangae ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake ya kikazi Mkoani Morogoro ya kukagua, kutembelea na kuzindua miradi mbalimbali inayotekelezwa ndani ya Mkoa huo.

Mhe. Mkuchika amesema nia ya Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kuendelea kutoa fedha na kutekeleza miradi ya maji hapa nchini ili kumtua mama ndoo kichwani na kuwashukuru watendaji wa Halmashauri hiyo kwa usimamizi bora wa fedha na kuweza kutekeleza miradi kwa kiwango cha juu.

"...Naishukuru Halmashauri kwa kusimamia vizuri matumizi ya fedha hizi hamkuruhusu mchwa kula noti za hapa..." amesema Mhe. George Mkuchika.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amemshukuru Mhe. Rais kwa niaba ya wanamorogoro kwa kuwajali na kuwaletea miradi mbalimbali hususan ya maji ambapo hapo awali kipindi cha kiangazi idadi ya mifugo hupungua kwa sababu ya uhaba wa maji ya kutosha ya kunywesha mifugo.

Pia amesema uwekezaji wa ujenzi wa tenki la maji katika kijiji cha Mangae utaondoa kero ya upatikanaji wa maji ambapo amemuomba Mhe. Rais kuendelea kutoa fedha katika Mkoa huo ili kuweza kutokomeza adha ya maji.

Naye, Meneja wa RUWASA wa Wilaya ya Mvomero Mhandisi Mlenge Nasib akisoma taarifa ya mradi huo wa maji wa Kijiji hicho amesema mradi huo umegharimu jumla ya shilingi Milioni 643.7 hadi sasa fedha zilizotumika ni shilingi Milioni 388.8 ambapo mradi huo umefikia asilimia 85% kukamilika ambpo utahudumia wakazi 4049 na kuweza kuondoa changamoto ya upatikanaji wa huduma ya maji katika kijiji cha Mangae.

Tumieni Fursa hii ya kuonana na madaktari bingwa - Dr. NkunguMganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro D...
10/10/2024

Tumieni Fursa hii ya kuonana na madaktari bingwa - Dr. Nkungu

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro Dkt. Daniel Nkungu amewataka wananchi wa Mkoa wa huo kutumia fursa iliyotolewa sasa kujitokeza kwa wingi katika hopsitali hiyo kwa ajili ya kuonana na madaktari bingwa kutoka Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI).

Dkt. Nkungu amebainisha hayo Oktoba 10, 2024 wakati akiongea na waandishi wa habari kwa lengo la kutoa taarifa ya uwepo wa madaktari hao bingwa Mkoani Morogoro na hiyo itaanza kutolewa kuanzia Oktoba 15 hadi 19, 2024 katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Morogoro ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya kifo cha Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Dkt. Nkungu amesema matibabu hayo yataongozwa na madaktari bingwa kutoka MOI wakishirikiana na madaktari bingwa wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na kwamba huduma ya kumuona daktari itatolewa bila malipo
Kwa sababu hiyo amewataka wananchi wa Mkoa wa Morogoro na Mikoa ya jirani kutumia fursa hiyo kufika na kuonana na madaktari hao bingwa ili kupata tiba za kibingwa.

".. niwaombe na kuwashauri wananchi wote wa Mkoa wa Morogoro na Mikoa jirani kutumia fursa hii adhimu kuonana na madaktari bingwa na wabobezi kwa ajili ya kupata matibabu..." amesisitiza Dkt. Daniel Nkungu.

Aidha Dkt. Nkungu amebainisha magonjwa ambayo yatatibiwa kuwa ni ni pamoja na watu wenye matatizo ya mivunjiko ya mifupa, matatizo ya nyonga, magoti, mgongo, kiharusi, ubongo, mishipa ya fahamu, watoto wenye ulemavu na mguu kifundo, kibiongo, mgongo wazi na vichwa vikubwa.

Kambii hii ya madaktari bingwa na wabobezi ni utekelezaji wa agizo la Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kusogeza huduma za kibingwa na kibobezi karibu na wananchi.

MWISHO.

RC MOROGORO ATOA WITO, UTUNZAJI WA MAZINGIRA.Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amewataka wadau wa mazing...
04/10/2024

RC MOROGORO ATOA WITO, UTUNZAJI WA MAZINGIRA.

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amewataka wadau wa mazingira na misitu hapa nchini kupiga vita vyanzo vya uharibifu wa misitu ikiwemo uchomaji moto na ukataji holela wa miti na kusababisha uharibifu mkubwa wa mazingira na mabadiliko ya tabia nchi.

Mhe. Malima amesema hayo Oktoba 3, 2024 wakati wa hafla fupi ya kufunga Jubilei ya miaka 50 ya mafunzo ya misitu hapa nchini iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) kilichopo mkoani Morogoro.

Mhe. Kighoma Malima amewataka wataalam wa utafiti wa misitu pamoja na maandiko mbalimbali wahayoandika amesema, bado kuna haja ya wao kwenda kutekeleza kwa vitendo yale waliyoyaandika kwani amesema uharibifu wa mazingira umeendelea kuwa mkubwa jambo ambalo linaongeza mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo ukame, mvua zisizo na uhakika, mafuriko na uharibifu wa mazingira.

" Nitoe wito kwa wadau wa misitu, kuhusu Suala la utunzaji wa Mazingira, tuondokane na tamadumi ya kuchoma misitu hovyo, tunachoma hadi sehemu zenye uoto wa asili, .." amesisitiza Mhe. Adam Malima.

Aidha, amekemea wale wote wanaoendelea kufanya shughulisha za kibinadamu pembezoni mwa mito na vyanzo vya maji k**a kilimo, ufugaji na kufyeka misitu kuacha mara moja tabia hiyo kwani inaongeza uharibifu wa mazingira na akawataka watendaji wa Kata na Tarafa kutoa elimu kwa jamii juu ya utunzaji wa misitu.

Hata hivyo, Mkuu huyo wa Mkoa amemshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuja na mkakati wa matumizi mbadala wa nishati safi ya kupikia utakaosaidia kudhibiti uharibifu wa mazingira kwa kutokata miti hovyo kwa lengo la kuandaa mashamba na kupata mkaa na matumizi mengine ya kibinadamu.

Katika hatua nyingine, Mhe. Malima ameziagiza Halmshauri za Wilaya za Mkoa wa Morogoro kila moja kuwa na vitalu vya miche ya miti na kutenga ekari 200 kwa ajili ya kupanda miti ili wataalamu kutoka Chuo cha SUA kwenda katika maeneo hayo na kufanya utafiti wa aina ya miti inayostahili kupandwa.

Kamati ya Siasa Morogoro haijaridhishwa na utekelezaji wa mradi wa Barabara ya Mbingu.Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu...
01/10/2024

Kamati ya Siasa Morogoro haijaridhishwa na utekelezaji wa mradi wa Barabara ya Mbingu.

Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Morogoro imesema haijaridhishwa na mwenendo wa ujenzi wa barabara ya Ifakara - Mbingu Wilayani Kilombero uliotakiwa kuanza rasmi kutekelezwa Disemba 8, 2023 lakini hadi sasa bado unasuasua.

Kauli hiyo imetolewa Septemba 29, 2024 na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhandisi Joseph Masunga kwa niaba ya wajumbe wenzake baada ya kutembelea mradi huo ikiwa ni mwendelezo wa ziara yao ya siku tano kukagua utekelezaji wa Ilani ya chama hicho mkoani humo.

"...nieleze masikitiko yangu kutokana na mradi huu kususasua... barabara ndio kero kubwa katika maeneo ya huku..." amesema Mhandisi Joseph Masunga.

Kwa mujibu wa maelezo yaliyotolewa imeelezwa kuwa changamoto kubwa ya mradi huo ni mkandarasi wa ujenzi wa barabara hiyo kutolipwa malipo ya awali (Advance Payment) ambayo kimsingi ni haki yake kwa mujibu wa mkataba huo.

Kwa sababu hiyo, Mhandisi Masunga ameiagiza Serikali ngazi ya Wilaya na Mkoa kufuatilia kwa karibu changamoto hiyo na ili mkandarasi huyo alipwe na kuanza mara moja kwani amesema adha kubwa ya wananchi wa Mlimba ni uwepo wa ubovu wa barabara hususan wakati wa masika.

Hata hivyo, Mhandisi Masunga ameipongeza Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa alioufanya kwenye sekta ya afya ikiwa ni pamoja na ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mlimba na kutumia fursa hiyo kuwapongeza watendaji wote wa serikali ngazi ya Mkoa, Wilaya na ngazi nyingine kwa kusimamia maono ya Rais.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam Kighoma Malima, amesema mradi wa Barabara ya Ifakara - Mbingu uko mikononi mwa TANROADS Makao Makuu na Mkoa hivyo ametaka kujipanga zaidi ili kuhakikisha mradi huo unaanza kutekelezwa mapema kwa manufaa ya taifa na usafirishaji wa mazao ya wananchi.

Naye Kaimu Meneja wa TANROADS Mkoa wa Morogoro Bw. Geofrey Mtakubwa amesema, mpaka sasa kazi zilizofanyika katika mradi huo ni upimaji, ujenzi wa kambi ya mkandarasi na kuleta vifaa 57 kati ya 137 ambapo ni sawa na 41.6% pamoja na kuleta wataalamu 7 kati ya 9 wanaohitajika.

SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUSOGEZA HUDUMA ZA KIJAMII KWA WANANCHISerikali ya awamu ya sita inayoongozwa  na Dkt. Samia ...
30/09/2024

SERIKALI YAAHIDI KUENDELEA KUSOGEZA HUDUMA ZA KIJAMII KWA WANANCHI

Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan imesema imejipanga kuendelea kuwasogezea karibu huduma za kijamii ikiwemo sekta ya Afya wananchi walio maeneo ya pembezoni ili kurahisisha kutofuata huduma hizo kwa umbali mrefu hivyo kuchochea maendeleo yao na ya Taifa kwa ujumla.

Kauli hiyo imebainishwa Septemba 29, 2024 na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro Mhandisi Joseph Masunga wakati wa ziara yake pamoja na wajumbe wa k**ati ya siasa ya Halmashauri kuu ya Mkoa huo kwa lengo la kutembelea miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Mkoa huo, na leo ni siku ya tatu wakiwa Wilayani Ulanga.

Mhandisi Masunga amesema, ilani ya CCM inaitaka serikali kuhakikisha inasogeza huduma za kijamii zikiwemo huduma za Afya, Elimu, Maji, miundombinu ya Barabara na umeme na sekta nyingine kwani amesema huduma hizo ndio msingi mkubwa wa maendeleo ya wananchi.

"… serikali inatakiwa kuhakikisha kwamba inapeleka huduma za kijamii karibu zaidi na wananchi na moja ya huduma ya msingi sana ni huduma ya afya…" amesema Mhandisi Joseph Masunga

Akiwa katika mradi wa Daraja la Chigandugandu lililopo Wilayani Ulanga, Mhandisi Joseph amewataka wananchi kulinda miundombinu ya umma likiwemo Daraja hilo huku akiwashauri kupanda miti ama mazao k**a michikichi, mianzi na Migomba pembezoni mwa mto ili kulinda Daraja hilo ambalo hadi kukamilika kwake litagharimu Tsh. Mil. 107.

Mwenyekiti huyo ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wananchi kujiandikisha kkwenye daftari la kudumu la kupiga kura ili kujihakikishia kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopangwa kufanyika Novemba 27, 2024 kwani, amesema, hiyo ni haki ya kila mtanzania kupiga kura, kuchaguliwa kuwa kiongozi au kuchagua viongozi bora watakaowaletea maendeleo.

Kwa upande wake, Mjumbe wa k**ati ya siasa ya Mkoa huo Bw. Deogratius Mzelu amewapongeza wananchi wa Wilaya ya Ulanga kwa kushirikiana na serikali katika kutekeleza miradi ya maendeleo baada ya wananchi hao kuchangia zaidi ya Tsh. Mil. 12 kwenye ujenzi wa shule ya Sekondari ya Lukande.

M/KITI MASUNGA AIAGIZA RUWASA KUKAMILISHA MRADI WA MAJI WA IGAWA.Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Morogoro Mhan...
29/09/2024

M/KITI MASUNGA AIAGIZA RUWASA KUKAMILISHA MRADI WA MAJI WA IGAWA.

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Morogoro Mhandisi Joseph Masunga amewaagiza Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Malinyi kukamilisha ujenzi wa mradi wa maji wa kata ya Igawa ifikapo oktoba 30 mwaka huu.

Mhandisi Masunga ametoa agiza hilo septemba 28, mwaka huu wakati wa ziara ya wajumbe wa k**ati ya siasa ya Mkoa huo kutembelea baadhi ya miradi ya maendeleo inayotekelezwa ndani ya Mkoa leo wakiwa Wilayani Malinyi ili kujionea hatua ya miradi ilipofikia na ubora wake.

Akitoa agizo hilo, Mwenyekiti huyo amesema mradi huo wenye thamani ya Tsh. Milioni 855 ulipaswa kukamilika Julai 7, 2022 hivyo, amewataka watendaji wa RUWASA kukamilisha mradi huo haraka ili kutatua kero ya upatikanaji wa maji kwa wakazi 18674 waliopo katika vijiji vitatu vya Igawa, Lugala na Kiwale.

"… unatakiwa ukamilishe mradi kwa wakati k**a ulivyoahidi hapa, wananchi waanze kupata maji katika kata ya Igawa…" amesema Mhandisi Joseph Masunga.

Katika hatua nyingine, Mhandisi Joseph Masunga amewataka wahandisi wa ujenzi wa barabara ya Itete Njiwa hadi Ipera itakayogharimu Tsh. Mil. 266 kukamilisha mradi huo kwa wakati huku akimtaka msimamizi wa mradi huo uliofikia 65% amlipe kwa wakati mkandarasi ili aweze kutekeleza vema mkataba wake na maagizo anayopewa.

Sambambana hayo, Mwenyekiti Masunga ameipongeza serikali ya awamu ya sita ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji thabiti katika sekta ya elimu ukiwemo ujenzi wa shule ya msingi wa Misegese na kuwapongeza wasimamizi wa mradi huo kwa kusimamia maono ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Kwa upande wake, Meneja wa RUWASA Wilaya ya Malinyi Mhandisi Marco Chogero amebainisha kazi zinazoendelea kufanyika ni ujenzi wa fensi eneo la tanki, uchimbaji na ulazaji wa mabomba na ujenzi wa vituo vya kuchota maji huku akiahidi kazi hizo zote kukamilika kabla au ifikapo Oktoba 30, 2024 k**a ilivyoagizwa.

Naye Diwani wa Kata ya Igawa Mhe. Gegalius Kamguna amesema amefurahishwa na ujio wa k**ati ya siasa wilayani humo kwani amesema inaongeza kasi ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kupitia maelekezo yanayotolewa na Kamati hiyo.

MWISHO.

KINGA NI BORA KULIKO TIBA - DKT. M***A Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Dkt. M***a Ali M***a amelishauri Shirika la German...
28/09/2024

KINGA NI BORA KULIKO TIBA - DKT. M***A

Katibu Tawala Mkoa wa Morogoro Dkt. M***a Ali M***a amelishauri Shirika la Germany TB and Leprosy Relief Association ( GLRA) linalojishughulisha na ugonjwa wa ukoma, kujikita katika kutoa elimu ya namna ya kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo ili kuzuia maambukiza mapya ya ukoma kwa jamii, kwa kuwa amesema KINGA NI BORA KULIKO TIBA.

Dkt. M***a amesema hayo Septemba 26, 2024 wakati akizindua mpango wa kutokomeza ugonjwa wa Ukoma Mkoa wa Morogoro, uzinduzi uliofanyika katika Hoteli ya Morena iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro.

Amesema, programu mbalimbali zinazoanzishwa huwa hazizungumzii sana suala la kuzuia bali huzungumzia masuala ya kutibu hivyo amewataka wataalamu hao kuwa na mpango mkakati wa kuzuia kuenea kwa Ugonjwa huo wa ukoma.

".. kuna haja kwa sisi wataalamu tuendelee kusisitiza kutafuta mbinu ya namna gani ya kuweza kufanya Prevention ya haya maradhi.."Amesisitiza Dkt. M***a

Aidha Dkt. M***a amesema Mikoa ya Morogoro, Mtwara, Lindi, Tanga na visiwa vya Unguja ndio inasemekana ina visa vingi vya ugonjwa huo, hivyo amelitaka shirika hilo kuweka mkazo katika maeneo hayo ili kusaidia kujua chanzo cha kuenea kwa Ugonjwa huo.

Sambamba na hayo amelitaka Shirika hilo la GLRA kuwatumia wataalamu wa Afya walioko ngazi ya chini kwa lengo la kutoa elimu ya jinsi ya kujikinga dhidi ya maambukizi ya ugonjwa wenyewe hivyo kusaidia kutoenea katika ngazi za chini.

Kwa upande wake Meneja wa Mpango wa Taifa wa TB na Ukoma Dkt. Liberate Mleoh amesema programu hiyo ni mahususi kwa ajili ya kutokomeza ugonjwa wa Ukoma lengo ni kwamba ifikapo 2023 kusiwe na maambukizi ya Ukoma.

Aidha, katika kikao hicho imebainishwa kuwa programu hiyo kwa Mkoa wa Morogoro inatekelezwa katika Wilaya tatu za Halmashauri ya Mlimba, Ifakara Mji na Manispaa ya Morogoro, huku wito ukitolewa kwa Wananchi kutoa taarifa kwa wataalamu wa afya pindi mtu atapojihisi ana ugonjwa huo.

Naye Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mlimba Dkt. Deodati Jumanne akiongea kwa niaba ya waganga wa Halmashauri za Ifakara Mji na Halmashauri ya Manispaa amesema, mpango huo wameupokea na wapo tayari kuutekeleza ili kuzuia kuenea zaidi kwa ugonjwa huo.

MWISHO.

KAMATI YA SIASA MOROGORO YARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA SERIKALI, YATOA MAAGIZOKamati ya siasa ya Halmashauri kuu ya Ch...
28/09/2024

KAMATI YA SIASA MOROGORO YARIDHISHWA NA UTENDAJI KAZI WA SERIKALI, YATOA MAAGIZO

Kamati ya siasa ya Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro imeridhishwa na utendaji kazi wa Serikari ndani ya Mkoa huo katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa Mkoani humo.

Hayo yamebainishwa Septemba 27, mwaka huu na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro Bw. Joseph Masunga wakati wa ziara ya Kamati hiyo ya siku tano yenye lengo la kufanya tathmini ili kuona ubora wa miradi hiyo na hatua iliyofikiwa ukilinganisha na fedha zilizopokelewa (value for money).

Aidha, Bw. Masunga amesema, Serikali Kuu imefanya uwekezaji mkubwa kwa wananchi katika kutoa suluhisho la kiuchumi kwa kurahisisha usafiri na usafirishaji wa bidhaa na mazao, kupata maji na matibabu kwa urahisi kazi hiyo inafanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka wananchi kulinda miundombinu ya umma ili idumu kwa muda mrefu likiwemo daraja la Luhembe Wilayani Kilosa.

"… niwaombe sana mshapata Daraja hili, naamini shughuli zenu zitaenda vizuri lakini mna hitaji kulitunza ili liweze kutumika kwa muda mrefu zaidi kwa kuzingatia uhifadhi wa mazingira hususan yanayozunguka Daraja …" amesema Bw. Joseph Masunga

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo amewataka wananchi kujitokeza kujiandikisha katika daftari la kudumu la mpiga kura ili kuwa na haki ya kupiga kura katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliopangwa kufanyika Novemba 27, 2024 kwani amesema ni haki ya kila mtanzania kupiga kura ili kupata viongozi walio bora na watakaowaletea maendeleo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima amewataka wananchi kuacha kulima katika vyanzo vya maji kwani kufanya hivyo kunasababisha mito kubadili njia zao asilia, kuharibu miundombinu ikiwemo madaraja na Barabara badala yake amewataka kila mmoja kupanda miti ikiwemo min**i ili kuzuia mmomonyoko wa udongo na kujipatia n**i kwa matumizi ya nyumbani.

Sambamba na hayo, Mhe. Malima amekemea vikali wakulima wenye tabia ya kuchoma miwa kwa makusudi ili kupewa kipaumbele katika kuuza miwa hiyo na kusisitiza kushirikiana kuwafichua wakulima wenye tabia hiyo ili wachukuliwe hatua

06/09/2024
ULAJI DUNI NA MILA POTOFU NI SABABU ZA KUWA NA LISHE DUNI MOROGORO Imeelezwa kuwa ulaji usiofaa wa vyakula na Mila potof...
22/08/2024

ULAJI DUNI NA MILA POTOFU NI SABABU ZA KUWA NA LISHE DUNI MOROGORO

Imeelezwa kuwa ulaji usiofaa wa vyakula na Mila potofu ni moja ya sababu zinazopelekea Mkoa wa Morogoro kuwa na hali duni ya lishe japo Mkoa huo ni miongoni mwa Mikoa inayozalisha chakula kwa wingi.

Hayo yamebainishwa Agosti 21, 2024 na Afisa Lishe wa Mkoa wa Morogoro Bi. Salome Magembe wakati wa kikao cha Tathmini cha Utekelezaji wa Mkataba wa Lishe kilichofanyika katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.

Katika kikao hicho kilichokuwa na ajenda tatu muhim, kusoma taarifa na Maazimio ya kikao cha tarehe 25/7/2023, kuwasilisha mada kuhusu Utapiamlo na athari zake na kuwasilisha taarifa ya Tathmini ya Mkataba wa Lishe kwa mwaka wa Fedha 2023-2024 kilihusisha Wakuu wa Wilaya zote za Mkoa huo, Makatibu Tawala wa Wilaya, Wajumbe wa Sekretarieti ya Mkoa, Wakurugenzi wa Halmashauri, Wenyeviti wa Halmashauri, Maafisa Lishe pamoja na wajumbe wengine kutoka Halmashauri.

Taarifa iliyotolewa ilieleza hali halisi ya lishe ya Mkoa huo ikiwemo taarifa ya kiwango cha udumavu kwa watoto waliochini ya miaka mitano kuwa ni 30.6%, kiwango cha uzito pungufu kwa watoto waliochini ya miaka mitano kufikia 3.9%, pamoja na upungufu wa damu kwa watoto chini ya miaka mitano kuwa ni 68.1% hali iliyoibua baadhi ya wajumbe kutaka kujua sababu zinazopelekea hali hiyo.

Akibainisha sababu hizo Afisa Afya Mkoa wa Morogoro Bi. Salome Magembe amesema hali hiyo inatokana na sababu nyingi zikiwemo wakazi wa Mkoa huo kutozingatia ulaji wa vyakula mchanganyiko pamoja na kuendelea kufuata mila potofu ikiwemo ya baadhi ya wazazi kukatazwa kula baadhi ya vyakula hasa vyakula vya jamii ya wanyama.

”pamoja na kwamba Morogoro kuna mboga za majiani nyingi na matunda kwa kila msimu lakini bado jamii haina kasumba ya kutumia mboga za majani na matunda” amesema Bi Salome.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Adam Kighoma Malima ambaye alikuwa mwenyekiti wa Kikao hicho pamoja na mambo mengine alijikita kwenye utekelezaji wa Mkataba wa Lishe ambapo aliwaagiza Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Mkoa huo kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza afua za lishe kwa kila robo ya mwaka wa fedha badala ya kutoa fedha hizo.

19/08/2024

Watch, follow, and discover more trending content.

RAS Morogoro awataka wakulima kutunza teknolojia ya KilimoKatibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt. M***a Ali M***a amewata...
17/08/2024

RAS Morogoro awataka wakulima kutunza teknolojia ya Kilimo

Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Dkt. M***a Ali M***a amewataka wakulima kutunza na kuendeleza teknolojia walizojifunza na kuzitumia katika maeneo yao kwa ajili ya maslahi mapana kwa jamii na Taifa Zima.

Dkt. M***a amesema hayo Julai 29, 2023 wakati wa hafla ndogo ya mavuno katika kijiji cha Mtego wa Simba kwa kushirikiana na Chuo kikuu cha kilimo cha China ikiwa na lengo la kusherehekea mafanikio ya mradi wa kilimo cha soya.

akifafanua zaidi Dkt. M***a amesema Jamii inapaswa kutambua mchango wa Chuo hicho katika sekta ya kilimo na kuwataka wakulima Kutumia rasilimali zilizopo yakiwemo maeneo yao madogo kupata mazao mengi kulingana na teknolojia walizojifunza.

"...kwa hii teknolojia mliojifunza mnatakiwa kuitunza na kuendeleza kwa manufaa yenu kwa kutumia rasilimali zilizopo..." amesema Dkt. M***a Ali M***a.

Sambamba na hilo, Dkt. M***a amesema mradi wa soya una mafunzo makubwa sana na inatakiwa kuendeleza kwa ajili ya kupata manufaa zaidi katika jamii zetu.

katika hatua nyingine, Katibu Tawala huyo amesema Mkoa wa Morogoro ni Mkoa tajiri katika mazao mengi likiwemo zao la ndizi kwani migomba ni mali kuliko ndizi ambayo hutengeza nyuzi ngumu kufuma mikoba, mikeka, mazulia na pedi za k**e.

Kwa upande wake, Prof. Tang Lixia wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha China amesema wana mpango wa kuanzisha mradi wa lishe ya soya shule za Kijiji hicho kwani watoto ni nguvu kazi ya Taifa la kesho, hivyo kukabiliana na tatizo la lishe ni muhimu kwa jamii na Taifa Zima.

Naye, Dkt. Rozalia Rwegasira Katibu Tawala msaidizi sehemu ya uchumi na uzalishaji Mkoa wa Morogoro amesema mradi huo umekuwa na Maendeleo makubwa hasa katika kuwapatia kipato na kujikwamua kiuchumi.

mwisho.

31/07/2024

Address

Kisasa
Dodoma

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Baesadigital posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Baesadigital:

Videos

Share