Ahadun Ahad Studio

Ahadun Ahad Studio Ni media, iliodhamiria kukuletea elimu juu ya Imani yako, ukumbusho, mawaidha, pamoja na upambanuzi juu ya Uislam na waislam. Baki hapa ili ufaidike.

media hii ipo kwa ajili ya kukufahamisha Uislam nje, ndani.. Ahadun Ahad Studio,
Onja Ladha Ya Imaan.

Sadaka humpandisha mtoaji wake daraja la juu zaidi Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, amesema:  “Maisha haya ya dunia ...
08/09/2024

Sadaka humpandisha mtoaji wake daraja la juu zaidi

Mtume, swallallahu alayhi wa sallam, amesema:

“Maisha haya ya dunia ni ya makundi manne ya watu: mtu ambaye Allah amempa mali na elimu, basi akamcha Mola wake Mlezi, akaweka mafungamano mazuri na ndugu zake kwa mali hii, na anazijua haki za Allah juu yake, hakika huyu ndiye katika kiwango bora…”

[At-Tirmithi]

Assalam alaykum warahmatullah..U hali gani ndugu?Huenda wewe ni miongoni mwa watu wanao struggle kuamka kusali Tahajjud....
30/08/2024

Assalam alaykum warahmatullah..

U hali gani ndugu?

Huenda wewe ni miongoni mwa watu wanao struggle kuamka kusali Tahajjud..

Umeset alarm, lakini wapi..🤦🏽‍♂️
Umejitahid ulale mapema, wapi wee..🤦🏽‍♂️
Ukamuomba hadi mtu akuamshe, ase kwan uliamka basi..😄

Ikiwa huyu ni wewe basi shuka nami nikueleze mambo 5 ya kufanya ili uweze kuamka usiku na kumuomba Allah..

1. Lala ukiwa twahara (wudhu), na utakapolala ukiwa na wudhu utapata Faida ya kuomba na malaika pindi utapopatwa na usingiz hadi utakapoamka na kutokana na hilo itakuwa rahisi kwako kuamka..

2. Weka Nia ya kuamka usiku kuswali, Na hakika penye Nia, Pana njia. Utakapokusudia kuamka usiku, itakuwa vyepesi kwako kuamka usiku na pia hata usipoamka utalipwa na Allah kwa Nia yako ya kuamka

3. Jitahidi Usile Sana usiku, Usile hadi ukashiba. Kumbuka shibe ni mwana malevya😄. Ukishiba sana utalewa na utashindwa kuamka usiku kuswali..

4. Ikiwa utapata nafasi mchana, pumzika kidogo lala. Ili kuupa mwili nguvu ya kuamka usiku..

5. Jiepushe na maradhi ya Moyo k**a vile chuki, hasadi, unafiki, kusengenya watu katika moyo wako, kuwadhania watu vibaya moyoni mwako, kuwasema watu vibaya moyoni mwako n.k.

Kwan ukiwa na tabia hizo moyo wako utakuwa mzito na utashindwa kuamka kuswali Tahajjud.

By the way, ikiwa unahitaji kujifunza zaidi na kupata ukumbusho na mawaidha kutoka kwangu kwa njia ya WhatsApp bonyeza hapo

https://bit.ly/3Mx7IPH

Al Akh. Mubaarak

يوم الجمعة Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira kuwa Mtume wa Allah (ﷺ) amesema: Aliyetawadha vizuri kisha akaja kwenye Swal...
29/08/2024

يوم الجمعة

Imepokewa kutoka kwa Abu Huraira kuwa Mtume wa Allah (ﷺ) amesema:

Aliyetawadha vizuri kisha akaja kwenye Swalah ya Ijumaa, akasikiliza (mahubiri), akanyamaza, (madhambi yake) yote baina ya muda huo na Ijumaa ijayo yatasamehewa kwa ziada ya siku tatu.

[Sahih Muslim 857]

゚ ゚viralシ

Tetea heshima ya kaka/dada yako Muislamu: Amesema Mtume ﷺ: "Mwenye kulinda utukufu wa ndugu yake ALLAH atauepusha moto u...
24/08/2024

Tetea heshima ya kaka/dada yako Muislamu:

Amesema Mtume ﷺ:

"Mwenye kulinda utukufu wa ndugu yake ALLAH atauepusha moto usoni mwake Siku ya Kiyama."

[Sahih At-Tirmidhiy #1931]

Papaa Sedute Mpenda Amani, Hamisi Matimbwa, Azhad Said, Mwanaidy Hamadi, Emanuel Msafiri

✒ Allah Harudishi Mikono Iliyoinuliwa Mtupu 🤲🏻 Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: إن ا...
12/08/2024

✒ Allah Harudishi Mikono Iliyoinuliwa Mtupu 🤲🏻

Mtume Muhammad (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

إن الله رحيم حيي كريم يستحي من عبده أن يرفع إليه يديه ثم لا يضع فيهما خيرا

“Hakika Allaah ni Mwingi wa Rehema, Mwenye haya, Mkarimu, Anafedheheka kwa mja Wake kunyanyua mikono yake Kwake kisha Haweki chochote cha Khayr (wema).”

● [مختصر صحيح الجامع الصغير ١٧٦٨ ، صححه الألباني]

✒ Malipo ya Maswahabah 50 (Allah Awawiye Radhi) Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Kw...
09/08/2024

✒ Malipo ya Maswahabah 50 (Allah Awawiye Radhi)

Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“Kwa hakika mbele yenu zipo siku za subira ambazo ndani yake kuifuata dini kikweli kweli itakuwa k**a KUSHIKA KAA LA MOTO, mwenye kutenda haki katika kipindi hicho atapata thawabu k**a WANAUME HAMSINI watendao k**a yeye.”

Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) aliulizwa na Swahaba: “Ewe Mtume wa Allah ujira wa watu hamsini miongoni mwetu au wao?”, akajibu: “Bali malipo ya watu hamsini miongoni mwenu.”

● [صحيح الترغيب والترهيب ٣١٧٢ ، صححه الألباني]

Moja ya Hadiyth ninazozipenda sana kusoma ninapopitia majaribio ni hii..Na ni kwa sababu kuisoma pekee huleta furaha.  B...
06/08/2024

Moja ya Hadiyth ninazozipenda sana kusoma ninapopitia majaribio ni hii..

Na ni kwa sababu kuisoma pekee huleta furaha.

Baki daima kuwa mtiifu kwa Allah pekee na uwe na subira unapojaribiwa, kwani unafuu utakuja kwa njia ambazo hukuzitarajia.

Imepokewa kutoka kwa Abu Razin kuwa Mtume wa Allah ﷺ amesema:

“Allah anatabasamu kwa Yale mazito anayopitia mja wake na huzuni ya mja wake, kwakuwa hivi karibuni atamsaidia.” Nikasema, “Ewe Mtume wa Allah, je, Mola wetu anatabasamu? Mtume ﷺ akasema, “Ndio”. Nikasema,

"Hatutanyimwa wema na Mola anayetabasamu(juu yetu)?!"

[Chanzo: Sunan Ibn Majah 181 Daraja: Hasan (haki) kwa mujibu wa Al-Albani]

Mwanangu, unapokuwa na khofu ya Allah, utayaona mema yote. Mtu anayemcha Mola wake kwa hakika hajali (yale) wengine (wat...
26/07/2024

Mwanangu, unapokuwa na khofu ya Allah, utayaona mema yote.

Mtu anayemcha Mola wake kwa hakika hajali (yale) wengine (watakayofikiri au kusema juu yake)

na hajiweki katika hali ambayo mwenendo wa dini yake uko hatarini.

Mwenye kuchunga mipaka ya Allah basi Naye atachungwa..

[Ibn al-Jawzi’s (rahimahullah) advice to his son: Sincere Counsel to the Seekers of Sacred Knowledge, pg. 72]
•┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•

03/07/2024

Hakika Allah atawasaidia..

Imepokewa kutoka kwa Abu Hurayrah kuwa Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“Kuna aina tatu za watu ambao Allah atawasaidia..

Mujaahid (mpiganaji) katika Njia ya Allah;

Mukaatab (mtumwa ambaye ana hati ya maandishi ya kujikomboa kwa malipo ya kiasi fulani cha kulipa kwa awamu kwa bwana wake) ambaye anataka uhuru;

na anayetaka kuoa kwaajili ya kutafuta usafi(wa uchafu wa zinaa)"

[At-Tirmidhi na An-Nasaa’iy]

02/07/2024

✒ Ukitaka Kujua Hali Yako Kwa Allah Angalia Taqwa Yako

Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

“Mwenye kutaka kujua y
alivyo kwa Allaah (kwa daraja na cheo) basi na atazame aliyo nayo kwa Allaah pamoja naye (katika utiifu na khofu ya Mola wake).

● [مختصر صحيح الجامع الصغير برقم ٦٠٠٦ , حسنه الألباني]

30/06/2024

✒ Njia Bora ya Kuhifadhi ʿIlm

Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema:

‎قيدوا العلم بالكتاب

"Nasa maarifa kwa kuyaandika.."

‎● [مختصر صحيح الجامع الصغير برقم ٤٤٣٤ , صححه الألباني]

19/06/2024

📌 AINA ZA UPENDO

🔹 Mapenzi Kwa Allah Pekee:

• Huu ndio msingi wa eeman na tahweed.

🔹 Kupenda Kwa Ajili Ya Allah:

• Kuwapenda Manabii wa Allaah na Mitume na wafuasi wao, na kupenda yale matendo, nyakati, sehemu anazozipenda Allaah.

• Na haya yanafuata kutokana na mapenzi ya mtu kwa Allaah na ni ukamilifu wake (kumpenda Allah).

🔹 Kupenda Pamoja Na Allah:

• Mapenzi waliyonayo washirikina kwa miungu na washirika wao - iwe miti, mawe, wanadamu, malaika au vinginevyo.

• Huu ndio msingi wa shirki na mzizi wake.

🔹 Upendo Wa Asili:

• Yale ambayo hayana lawama kwa mja na ni yale anayojisikia kwa chakula, kinywaji, jimai, mavazi, uswahaba n.k.

[Chanzo: al-Qawl al-Sadeed Sharh Kitab al-Tawhiyd (uk.128, sura ya 31) na Imam as-Sa’di]

‘Aisha, Allah amuwiye radhi: “Hakuna siku katika mwaka ninayopenda kufunga zaidi ya siku ya ‘Arafah.  ● [Sahih, Ibn al-J...
15/06/2024

‘Aisha, Allah amuwiye radhi: “Hakuna siku katika mwaka ninayopenda kufunga zaidi ya siku ya ‘Arafah.

● [Sahih, Ibn al-Ja’d 512]

Amesema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kuhusu kufunga siku ya Arafa kwa wale wasiohiji:

❝Inafuta dhambi za mwaka uliopita na mwaka unaofuata.❞

● [Imeripotiwa na Muslim, (Na. 1250)]

Du’a ya ‘Aliy siku ya ‘Arafah:

“Ee Allaah!” Niokoe na moto, na unizidishie riziki zangu za halali, na uwaweke mbali na majini waasi na wanadamu.”

‎● [Lataif al-Ma'rif, uk.

✒ Ni Du'a Gani Ya Kusoma Siku Ya 'Arafah | Rudia Hii Sana

Amesema Mtume wa Allah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam): Dua iliyo bora zaidi ni dua ya Siku ya Arafa, na iliyo bora kuliko yote niliyosema mimi na Mitume kabla yangu: Hapana mungu ila Mwenyezi Mungu peke yake. hakuna mshirika wake.

Mtume wa Allah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: “Dua iliyo bora zaidi ni dua siku ya ‘Arafah na bora zaidi ni ninayosema na Mitume wa kabla yangu walisema;

'Laa Ilaaha Illallaahu Wahdahoo Laa Shareeka Lahoo, Lahul Mulku Walahul Hamdu Wahuwa 'Alaa Kulli Shayin Qadeer'

(Hapana apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu, na Yeye yuko peke yake, hana mshirika, ni Kwake Mwenye ufalme na sifa njema, na Yeye ni Muweza wa kila kitu).

Imepokewa na Al-Tirmidhiy 3585, nayo ni hasan kwa mujibu wa wengine, k**a alivyosema Al-Albani, Mwenyezi Mungu amrehemu.]

Imaam An-Nawawiy [Allah amrehemu] amesema:

❝Imetufikia kutoka kwa Saalim bin ‘Abdillaah bin ‘Umar [Radhiya Allaahu ‘anhu] kwamba alimuona muombaji akiwauliza watu siku ya ‘Arafah, akasema: ‘Ewe mnyonge! Siku hii ni kuulizwa asiyekuwa Allaah, Mwenye nguvu na utukufu?’❞

● [Al-Adhkaar, (Ukurasa: 210)]

✨تكبيرات✨ ♦️الله اكبر الله اكبر الله اكبر لااله الا الله والله اكبر الله اكبر ولله الحمد♦️ Inapendekezwa Kwa Wanaume Kup...
13/06/2024

✨تكبيرات✨

♦️الله اكبر الله اكبر الله اكبر لااله الا الله والله اكبر الله اكبر ولله الحمد♦️

Inapendekezwa Kwa Wanaume Kupaza Sauti Zao Wakati Wa Kusema Takbir Katika Siku Kumi Za Kwanza Za Dhū al-Hijjah.

Imamu al-Bukhaariy رحمه الله amesema: "Ibn 'Umar رضي الله عنه na Abu Hurayrah رضي الله عنه walikuwa wakitoka kwenda sokoni siku kumi za Dhul-Hijjah wakisema takbir. Watu walipokuwa wakiwasikia wakafanya vivyo hivyo. ."

● [صحيح البخاري ٣٢٩/١]

Nilitamani sana niwe miongoni mwa Mahujaji, kila nikiangalia walivovaa na wanavomsabihi Allah, napatwa na hamu ya kuwepo...
12/06/2024

Nilitamani sana niwe miongoni mwa Mahujaji, kila nikiangalia walivovaa na wanavomsabihi Allah, napatwa na hamu ya kuwepo na Mimi katika Alkaaba..

Niizunguke al Kaaba huku nikisema "Labaikallahumma Labaik..".

Lakini bado sijaruzukiwa uwezo wa kwenda huko. Najiskia vibaya.

Leo, baada ya kuswali swala ya Ishaa, likanijia wazo, kwamba "hivi kweli hamna a'amali maalumu nitazozifanya katika Mwez huu wa Dhul Hijja ili na Mimi nipate barka zake?"

Nikawaza, lakini siku hizi elimu ipo kiganjani, huenda nikapata hata mwanga, hivo nikazama kwenye Google, nikitafuta mawaidha yanayohusu mwez huu wa Dhul Hijja..

Ndipo nikapita, nikakutana na hii makala, kwamba "Jins ya KuHiji bila Kutumia Hata Senti",

nilishangaa. Nikatamani kujua kivipi...

Nilipofungua, nilipata mwanga na elimu pia Alhamdulillah..

Ikiwa na wewe unataman ujue a'amal za kufanya katika mwez huu wa Dhul Hijja, zitakazokufanya uwe sawa na Hujaji..

Basi soma hapa..

Unatamani kwenda Hija, lakini pesa ndo kipengele?, Si ndio? , Usijali, Shuka nami nikupe njia za kwenda Hija bila kupoteza hata senti.. (100% Proved)

06/06/2024

Al-Haafidh bin Hajar al-'Asqalaani رحمه الله ameandika kuhusu sifa kubwa ya siku hizi 10 za mwanzo wa mwezi huu wa Dhul Hijjah kwa kusema:

Kinachodhihirika ni kwamba sababu ya kupambanuliwa kwa siku kumi (za kwanza) za Dhu'l-Hijjah ni kutokana na jukumu lake la kukusanya 'mama' wa ibada humo - ambayo ni al-Swalaat, al-siyaam. , sadaka, na Hajj - na hii haitokei wakati mwingine wowote.

💡Fath al-Baari 2/534

Ibn al-Qayyim رحمه الله amesema: “Ikiwa unataka kuona ukubwa wa Iman yako basi angalia jinsi ulivyo faragha. Kwani hakik...
03/06/2024

Ibn al-Qayyim رحمه الله amesema:

“Ikiwa unataka kuona ukubwa wa Iman yako basi angalia jinsi ulivyo faragha.

Kwani hakika Iman haionyeshi kiwango chake cha kweli katika rakaa mbili za swala au katika kufunga mchana.

Lakini inadhihiri katika kupigana dhidi ya nafsi yako na matamanio yako.”

[Madārij As-Sālikīn | 164/82]

👍 *Wema ni nini katika Uislamu?* Hii ndiyo Hadith sahihi kabisa ninayoifahamu kuhusu kile ambacho Uislamu unatufundisha ...
24/04/2024

👍 *Wema ni nini katika Uislamu?*

Hii ndiyo Hadith sahihi kabisa ninayoifahamu kuhusu kile ambacho Uislamu unatufundisha kuhusu "wema".

Jabir bin Sulaym amesimulia:

"Nilikuja Madina na kukutana na Mtume wa Allah(s a w) katika uchochoro fulani. Wakati huo, Mtume (s.a.w.w.) alikuwa amevaa vazi lisiloburura chini lililotengenezwa kwa pamba, na ncha zake zikiwa zimepindwa(kwa chini).

Nikasema: “Ewe Mtume wa Allah Alaika As-Salam (amani iwe juu yako)!” Akasema: “ Alaika salaam hio ni salamu ya wafu! Sema AsSalam Alaikum (amani iwe juu yako)!

Kisha nikauliza: “Vazi langu kwa chini linapaswa kuwa la urefu kadiri gani?” Hivyo Mtume (saww) akaufunua mguu wake na kuukandamiza mfupa wa ugoko wake na akasema: “Shusha nguo yako kwa chini mpaka hapa. Ikiwa huwezi kufanya hivyo, kisha Shusha chini yake kidogo. Ikiwa bado hauwezi kufanya hivyo, basi Ishushe juu ya vifundo vyako vya mguu. Ikiwa bado hamwezi kufanya hivi, basi Allah hawapendi wadanganyika na wenye kiburi.”

Kisha nikamwomba aniusie juu ya suala la wema, kwa hiyo akasema:

“Usidharau wema wowote unaofanywa, iwe ni kutoa kipande cha kamba, kutoa kamba ya kiatu, kumwaga maji kutoka kwenye ndoo yako kwenye chombo mtu mwenye kiu, akiondoa kitu katika njia ambayo inaweza kuwadhuru wengine, kukutana na ndugu yako Mwislamu kwa uso uliochangamka, kumsalimia ndugu yako Mwislamu kwa salamu za amani, na kufanya urafiki na kuonyesha mapenzi kwa wale wanaoonekana kuwa wageni katika ardhi.

Ikiwa mtu anakusema vibaya kutokana na jambo analolijua juu yako ambalo ni la kibinafsi kwako, basi usimsemee vibaya ikiwa una ujuzi wa jambo ambalo ni la kibinafsi kwake, kwani hii itakuwa chanzo cha malipo kwako, na chanzo cha uharibifu kwake.

Na tendeni yale ambayo masikio yenu yanapenda kusikia, na jiepusheni na yale ambayo masikio yenu yanachukia kuyasikia.”

📝[Musnad Ahmad 15955, As-Sahihah 3422; Sahih]

_______

Karibu katika group yetu kwa Faida zaidi
https://chat.whatsapp.com/FoeLN2YEfr0CLgwXvTEySQ

𝐐𝐮𝐫'𝐚̄𝐧 Ibn al-Qayyim رحمه الله amesema: Lau watu wangejua utamu, na manufaa ya kuitafakari Qur'ani wakati wa kuisoma, w...
24/04/2024

𝐐𝐮𝐫'𝐚̄𝐧

Ibn al-Qayyim رحمه الله amesema:

Lau watu wangejua utamu, na manufaa ya kuitafakari Qur'ani wakati wa kuisoma, wangejishughulisha na kuitakari Qur'ani tu.

Kwani kusoma na kutafakari Aya moja ni bora kuliko ḵẖatma (kukamilisha Qur-aan nzima kwa kusoma tu) bila ya kutafakari wala kuelewa.

Pia ina faida zaidi kwa moyo, inapata Iman na inamfanya mtu aonje utamu wa Qur'an.

[Miftāḥ Dar al-Saadah | 553/1]

_________________

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ahadun Ahad Studio posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Videos

Share

Nearby media companies