Taarifa ZOTE

Taarifa ZOTE Hapa utapata habari za kila saa.Ila huruhusiwi kutupatia habari za Matusi.

Pia unaruhusiwa kutangaza biashara yako.Anayekiuka masharti ataondolewa kwenye kundi Karibuni sana ila vigezo na Masharti kuzingatiwa.

11/09/2022

Bondia Mtanzania amesema begi lake ambalo lilipotea Airport, Amsterdam likiwa na viatu vyake na vifaa vingine, limepatikana, itakumbukwa usiku wa Septemba 3, 2022 Mwakinyo katika pambano dhidi ya Muingereza Liam Smith lililochezwa Liverpool, England alipoteza kwa TKO round ya 4 katika pambano la round 12 ambalo hata hivyo lilikuwa gumzo kutokana na jinsi lilivyomalizika kwa utata.

Baada ya pambano hilo Mwakinyo akasema “Hujuma ambayo imetokea juzi wakati nafika Airport Watu wote walipata mabegi Mimi langu sikulipata karibu masaa matatu nimelisubiri baadaye wakaniambia begi langu limesahauliwa Amsterdam kwahiyo nikae pale masaa matano walilete au nitoe anuani ya napokaa watalituma baada ya siku mbili"

"Niliwasiliana na Promota akaniambia njoo uendelee na mambo mengine sisi tutashughulikia masuala ya begi lako, begi halijakuja juzi, jana na leo siku ya pambano wamenipa vifaa vingine vyao, viatu ambavyo nimevaa sijawahi kuvaa kupigania kuna muda nilipiga goti nikamwambia Refa nimepata ankle akaniambia unaweza kuendelea nikasema naweza kuendelea"

"Mara ya pili nikasikia ankle inakuja tena, nikatema mouth guard chini, sheria ukitema mouth guard Refa anatakiwa amrudishe nyuma Boxer unayepigana nae akuulize kuna tatizo gani au akuhesabia nikamwambia nina ankle ak**aliza pambano"

Bondia Mtanzania Mwakinyo amesema kutokana na Refa wa pambano hilo kuwa ‘unfair’ kwake, Promota Benjamin Shalom amekubali pambano hilo lirudiwe January 2023 vs Liam Smith.

11/09/2022

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa ziarani katika Wilaya ya Uyui Mkoani Tabora amekagua ujenzi wa Chuo kipya cha Ufundi Stadi VETA ambapo ameonesha kutoridhishwa na gharama za ujenzi wa kibanda cha mlinzi ambacho gharama za ujenzi wake zimetajwa kuwa ni Tsh. Milioni 11.

Waziri Mkuu ameiagiza TAKUKURU Mkoa wa Tabora kuingilia kati na kuchunguza gharama za ujenzi wa kibanda hicho.

11/09/2022

Mahak**a ya Hakimu Mkazi Kiteto Mkoani Manyara imemuhukumu kifungo cha miaka 30 Jela, Yerenia Chidaka, Mkazi wa Kijiji cha Dongo Wilayani Kiteto, baada ya kufanya ngono na kumtia mimba Mtoto wake wa miaka 16.

Mtuhumiwa amekiri kosa hilo mbele ya Hakimu Mkazi Mosi Sasy, na kusema hataki kuisumbua Mahak**a na kusema aliamua kumpa mimba Mtoto wake huyo ili asiolewe na Mwanaume wa Kabila la Wakamba.

Imeelezwa kuwa Baba huyo alipomuuliza Mke wake juu ya suala la kutotaka Mtoto wao aolewe na Wakamba, Mkewe alimjibu kwa dhihaka kwamba k**a hataki aolewe basi amuoe yeye na ndipo alipoamua kumpa ujauzito.

Alipotakiwa kujitetea, Mtuhumiwa aliiomba Mahak**a impunguzie adhabu kwakuwa shetani alimpitia kutenda kosa hilo, huku Mwendesha Mashtaka wa Polisi Mahak**ani hapo Inspekta Wilfred Mollel, akisema Jeshi la Polisi halina taarifa k**a Mtuhumiwa aliwahi kufanya kosa zaidi ya hilo na kumwomba Hakimu kumpa adhabu inayostahiki.

11/09/2022

Malkia wa Uingereza Elizabeth II amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 96, Kasiri la Buckingham limethibitisha kifo chake na kusema amefariki akiwa chini ya uangalizi wa matibabu huko Balmoral baada ya Madaktari kuwa na wasiwasi juu ya afya yake.

11/09/2022

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. John Dodoma, Winfrida Michael (24), aliyekuwa anasoma Diploma ya Medical Laboratory amefariki dunia baada ya kushambuliwa kwa kuchomwa kisu na Mpenzi wake, Julius Gervas (26), RPC Dodoma Martin Otieno amethibitisha .

Winfrida alifariki wakati anapelekwa Hospitali baada ya kuwa amevuja damu nyingi na Julius baada ya kufanya tukio hilo alijaribu kujichoma kisu tumboni lakini Watu walimuwahi na kumchukua kisha kumpeleka Hospitalini ambako anaendelea na matibabu chini ya ulinzi.

Inaelezwa kuwa Winfrida alikuwa amepanga nje ya Chuo na alikuwa na mahusiano na Kijana huyo kwa muda fulani lakini walikuwa wameachana na Kijana alikuwa anamsumbua Msichama hivyo alimuahidi kuwa akimaliza mtihani atamjulisha.

Juzi Msichana alikuwa amemaliza mtihani wake wa mwisho na kwa mujibu wa Mama mwenye nyumba walikutana wakaongea sana pale ndani na ilipofika saa nne na nusu walitoka nje akawa anamsindikiza ndio lilipotokea tukio la kuchomwa kisu na akawa anaomba msaada na walimchukua na kumpeleka Hospitali lakini akawa amefariki, mwili wa Marehemu umeagwa na kusafirishwa kwenda Ukerewe kwa mazishi.

11/09/2022
11/09/2022

Namungo FC 'Wauwaji wa Kusini' leo watashuka kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Majaliwa ambao ulikuwa unafanyiwa marekebisho msimu uliopita kucheza dhidi ya Ruvu Shooting saa 1:00 usiku huku uzinduzi wake ukinogeshwa na msanii nyota Harmonize 'Konde Boy' na mgeni rasmi ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa



11/09/2022

Over 500 pieces will be returned under the deal. The artifacts were looted by British soldiers in the 1800s and sold all over Europe.

11/09/2022
11/09/2022
11/09/2022
11/09/2022

A mural in Ukraine

23/08/2022
23/08/2022
23/08/2022
22/08/2022

Mgombea Mwenza wa Raila Odinga, Martha Karua amesema “Ngoma haijaisha, mpaka iwe imekwisha kabisa”

Cristiano Ronaldo apata virusi vya coronahttps://bbc.in/372KBJC
14/10/2020

Cristiano Ronaldo apata virusi vya corona
https://bbc.in/372KBJC

Mchezaji wa Ureno na Juventus Cristiano Ronaldo apata virusi vya corona

10/05/2020

Bwana Yesu asifiwe! Tumsifu Yesu Kristo! Mwanakondoo ameshinda...Karibu sana katika Siku ya Ebenezer ya TBC Taifa tumuabudu Mungu katika roho na kweli! Mungu atimize haja ya Moyo wako hapo ulipo.

19/02/2020

:Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki limepokea muswada wa matumizi na mapato ya nyongeza ya dola za kimarekani milioni 4.8, huku baadhi ya wabunge wakizungumzia maandalizi ya mkutano wa wakuu wa nchi za jumuiya hiyo unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.

11/02/2020

Mamia ya wakaazi mjini Mombasa hii leo wamepata fursa ya kusafiri kuelekea jijini Nairobi kuhudhuria hafla ya maombi ya hayati Daniel Arap Moi itakayofanyika katika uwanja wa Nyayo.
Wakaazi hao waliabiri mabasi katika makao makuu ya kaunti ya Mombasa na kufululiza kwenda Nairobi kupitia mpango wa serikali kuu

10/02/2020

Habarini

 :Mwanamume Aishi juu ya Mti kwa siku 7 ashindia matunda na ndizi 'mbichi'/ asimulia 'Sitaki kuona nguo ya Kijani'Soma z...
08/02/2020

:Mwanamume Aishi juu ya Mti kwa siku 7 ashindia matunda na ndizi 'mbichi'/ asimulia 'Sitaki kuona nguo ya Kijani'Soma zaidi->https://bit.ly/2HiFMOh

George Mokoro mkazi wa kitongoji cha Genteme kijiji cha Buchanchari wilaya ya Serengeti mkoa wa Mara ameeleza namna alivyoishi juu ya mti kwa muda wa siku saba ndani ya bonde la mto mara baada ya kuzingirwa na maji akiwa ameenda kuvuna mazao yake.

08/02/2020

:Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta awasili katika majengo ya Bunge nchini humo kuongoza Wakenya kutoa heshima zao za mwisho kwa aliyekuwa Rais wa pili wa nchi hiyo, Daniel Arap Moi, Siku ya jumatatu Wakenya watapewa siku tatu kwa ajili ya kuanga Mwili wa Moi.

07/02/2020

pata habari za uhakika

Pichani ni Purity Soinato Oiyie, ambaye anatoka katika jamii ya wamaasai, nchini  . Alikuwa msichana wa kwanza aliyekata...
06/02/2020

Pichani ni Purity Soinato Oiyie, ambaye anatoka katika jamii ya wamaasai, nchini . Alikuwa msichana wa kwanza aliyekataa ukeketaji kijijini mwake na msichana wa kwanza pia kupata shahada ya elimu.

Sasa anatetea haki za wanawake, akihamasisha wasichana wenzake kuhusu athari za ukeketaji na umuhimu wa kupata elimu.

"Nilikuwa na umri wa miaka 11 tu wakati baba yangu aliamua kwamba napaswa kufanyiwa ukeketaji. Niliongea na mwalimu wangu na akamtaarifu afisa wa polisi. Saa mbili tu kabla ya utaratibu wa ukeketaji, polisi walikuja kuniokoa. Sasa mimi ni mwanaharakati wa haki za wanawake. Naenda vijijini kuongea na wamaasai kwenye lugha yetu. Tunachohitaji ni elimu bure kwa wasichana. Wazazi wengi ni wafugaji na hawana pesa ya kuwapeleka wasichana wao shuleni."

Leo ni Siku ya Kutokomeza Ukeketaji Duniani. http://bit.ly/1sjZ0CU

📷: UN Women/Ryan Brown

Female ge***al mutilation (FGM) is a practice that involves altering or injuring the female ge***alia for non-medical reasons, and it is internationally recognized as a human rights violation. Globally, it is estimated that some 200 million girls and women alive today have undergone some form of FGM...

Rais wa Malawi Peter Mutharika kutetea nafasi yake kwa rufaa Mahak**a Kuuhttps://bbc.in/2H2vrpa
06/02/2020

Rais wa Malawi Peter Mutharika kutetea nafasi yake kwa rufaa Mahak**a Kuu
https://bbc.in/2H2vrpa

Rais wa Malawi, Peter Mutharika kukata rufaa uamuzi wa Mahak**a, aeleza kuwa Mahak**a.

06/02/2020

:Baraza la seneti mjini Washington limemuondolea hatia rais Donald Trump, katika kesi ambayo alikuwa akishutumiwa na wabunge wa chama cha Democratic, kutumia vibaya madaraka yake na kutatiza kazi za Baraza la Wawakilishi.

Kura za bunge la seneti zamsafisha Trump dhidi ya mashtaka ya matumizi mabaya ya madarakahttps://bbc.in/2UtCO0R
06/02/2020

Kura za bunge la seneti zamsafisha Trump dhidi ya mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka
https://bbc.in/2UtCO0R

Rais Donald Trump ameondolewa mashtaka yaliyokuwa yanamkabili na kumaliza mchakato wa kumuondoa madarakani mchakato ambao uliigawanya vikali Marekani.

Address

Usa River

Telephone

+255752243648

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Taarifa ZOTE posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Nearby media companies


Other Media/News Companies in Usa River

Show All

You may also like