Usikose kusikiliza kipindi Cha Darubini ya Utalii kutoka hapa @kilimanjarorevivalradio siku ya Jumatatu saa 1:00 Jioni hadi saa 1:30 Jioni
Host @naomifred_
📹 @nuhu_suleimantz
Kuna upepo wamafundisho potofu unao pinga watu kuomba na kufunga eti nikujisumbua kwasababu sisi tumeokolewa kwa neema.
Maombi ya kufunga ni njia muhimu katika maisha ya kiroho ya Mkristo, na yana faida nyingi ambazo zinaweza kusaidia mtu katika kutafuta uhusiano wa karibu na Mungu. Hapa kuna faida saba za maombi ya kufunga:
FAIDA 7 ZAKUFUNGA NAKUOMBA.
1. Kuongeza Imani Maombi ya kufunga yanaweza kusaidia kuimarisha imani yako. Katika Mathayo 17:21, Yesu anasema kwamba baadhi ya mambo hayawezi kufanyika isipokuwa kwa kusali na kufunga. Hii inaonyesha kuwa imani inaweza kuongezeka kupitia matokeo ya maombi ya kufunga.
2. Kufumbua Macho ya Ndani Kufunga na kuomba kunaweza kusaidia kufumbua macho yako ya ndani ili uweze kuona mambo mengi ambayo hujui. Zaburi 119:18 inasema, “Unifumbue macho yangu niyatazame maajabu yatokayo katika sheria yako.” Hii ina maana kwamba kuna uelewa wa kiroho ambao unaweza kupatikana kupitia maombi ya kufunga.
3. Kutiisha Mwili Kufunga husaidia kutiisha mwili wako dhidi ya tamaa mbaya na dhambi. Wakolosai 3:5 inatufundisha kuhusu umuhimu wa kuishi maisha matakatifu, na maombi ya kufunga yanatoa nguvu zaidi katika kutimiza hili.
4. Kupokea Majibu kutoka kwa Mungu Maombi ya kufunga yanaweza kuongeza uwezekano wa kupokea majibu kutoka kwa Mungu. Yeremia 29:13 inasema, “Nanyi mtanitafuta na kuniona, mtakaponitafuta kwa moyo wenu wote.” Hii inaonyesha kwamba Mungu anataka tuwasiliane naye kwa dhati.
5. Kuimarisha Uhusiano Wako na Mungu Kufunga ni njia moja wapo inayoweza kusaidia kuimarisha uhusiano wako na Mungu. Wakati unafunga, unajitenga na vitu vya kidunia ili uweze kumtafuta Mungu kwa ukaribu zaidi.
6. Kuwezesha Mabadiliko Kiroho Wakati unapofunga, unaweza kupata mabadiliko makubwa katika maisha yako ya kiroho. Maombi haya yanaweza kukusaidia kushinda vikwazo ambavyo umekuwa ukikabiliana navyo.
7. Kuleta Amani na Utulivu Kufunga mara nyingi huleta hali ya amani na utulivu ndani yako, kwani unajitenga kutoka kwa shughuli z
Karibu utangaze nasi! Mwaka 2025 ni mwaka wako wa kufanya kweli na Mungu akabariki juhudi na mawazo yako.
@kilimanjarorevivalradio itakushika mkono kwa Kila hatua ya kutangaza baishara na huduma yako nasi.
Tafiti juu ya Uhusiano kati ya IQ na Matendo ya Kijamii:
Ukisoma katika kitabu cha Mwandishi Nyborg H cha mwaka 2003 cha "Utafiti wa kisayansi kuhusu akili nyingi"
(The scientific study of general Intelliegence)
Kitabu hiki kinachambua uhusiano kati ya IQ na tabia mbalimbali za kijamii.
Hata ingawa si kipengele cha moja kwa moja, inaonyesha jinsi watu wenye IQ kubwa wanaweza kuzingatia zaidi masuala ya kiakili na kupuuza baadhi ya mambo ya kijamii au kibinafsi.
IQ (Intelligence Quotient) ni kipimo kinachotumika kupima kiwango cha uwezo wa kiakili wa mtu, hasa katika nyanja za ufahamu, ufanisi wa kutatua matatizo, na uwezo wa kujifunza.
Kipimo hiki hutumia maswali ya mitihani inayojumuisha vipengele kama vile mantiki, kumbukumbu, ufanisi wa nadharia, na uwezo wa kuona uhusiano kati ya vitu.
HOST @Floramacha1
🎥cc @nuhu_suleimantz
MAMBO YA KUOMBEA SIKU YA KWANZA
Toba binafsi, Familia (Zab 51:1-13; 1Yoh 1:9;…)
1. Mungu atusamehe pale tulipokosea kwa namna yoyote.
2. Mungu atusamehe kama familia kwa kutokutii sauti ya Mungu,kushindwa kusimamia kusudi la Mungu kwa kiwango cha kutosha n.k
3. Kushughulika na roho ya uasi, ukaidi, ubinafsi, kutokutii kwa namna
zote na mambo yote yanayotubomoa. Tuombe rehema.
Wanawake walioathirika na Ugonjwa wa saratani ya mlango wa kizazi na hatimaye kupatiwa matibabu na kupelekea kurudi katika hali zao za kawaida,wameaswa kuendelea kufuatilia vipimo kulingana na muda aliopangiwa na Daktari ,kwani kumekuwepo na baadhi ya waliopona kutokurudi tena hospitali na kupelekea ugonjwa huo kurudi upya.
Jamii imeshauriwa kuzingatia umuhimu wa kufika katika vituo vya afya na hospitali kupima magonjwa mbalimbali hasa Saratani ya mlango wa kizazi ili kufahamu afya zao.
Hayo yameelezwa na Daktari wa magonjwa ya akina mama na uzazi Dkt. Maria Mussa kutoka hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini @kcmc1971 (KCMC) Wakati akitoa elimu kwa umma kupitia @kilimanjarorevivalradio kwenye kipindi cha Mwanamke na maono.
Amesema kuwa saratani ya shingo ya kizazi husababishwa na virusi vinavyojulikana kama HPV ambavyo wanawake hupata kupitia kwa mwanaume.
#sarataniyashingoyakizazi
#sarataniyamatitiinatibika
#saratani
Meneja wa mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) [@tcra_tanzania ] kanda ya kaskazini Mhandisi Francis Mihayo amewataka Watumiaji wa mitandao ya simu wakataouziwa vocha kwa bei isiyo husika kutoa taarifa.
Ameyasema hayo leo January 10, 2025 wakati akizungumza na Kilimanjaro Revival Radio kupitia kipindi cha SUNSET DRIVE.
Hosts: Peter Abdalah & @Flora Machi
🎥 @nuhu_suleimantz
🅴🅽🅳🅴🅻🅴🅰 🅺🆄🆃🆄🅵🆄🅰🆃🅸🅻🅸🅰
@instagram @kilimanjarorevivalradio
@facebook Kilimanjaro revival fm
#Tusikilize : www.kilimanjarorevivalfm.or.tz
#KilimanjaroRevivalRadio
#PowerOfRevival
Kutokana na wimbi la kuwepo kwa Matapeli katika mitandao ya simu za mkononi, Meneja wa mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) kanda ya kaskazini Mhandisi Francis Mihayo amewataka Watumiaji wa mitandao ya simu kutambua kuwa watoa huduma wa mitandao hiyo wanatumia namba ya huduma ambayo ni 100 kuwasiliana na Wateja wao.
Ameyasema hayo leo January 10, 2025 wakati akizungumza na Kilimanjaro Revival Radio kupitia kipindi cha SUNSET DRIVE.
🅴🅽🅳🅴🅻🅴🅰 🅺🆄🆃🆄🅵🆄🅰🆃🅸🅻🅸🅰
@instagram @kilimanjarorevivalradio
@facebook Kilimanjaro revival fm
#Tusikilize : www.kilimanjarorevivalfm.or.tz
#KilimanjaroRevivalRadio
#PowerOfRevival
Miongoni mwa watu maarufu waliopoteza nyumba zao kutokana na Moto unaoendelea Nchini Marekani katika Mji wa Los Angeles ni pamoja na nyumba ya Leighton Meester na Adam Brody, walioshiriki tu tuzo za Golden Globe siku chache zilizopita, pamoja na Paris Hilton.
Sekta ya bima inahofia kuwa huu unaweza kuwa mmoja wa milipuko mikubwa ya moto katika historia ya Marekani, na hasara za bima zinatarajiwa kuwa zaidi ya dola bilioni 8 (pesa za Uingereza £6.5 bilioni) kutokana na thamani kubwa ya mali kuteketezwa na moto huo wa nyika.
Hata hivyo, kuna tumaini kidogo kwa wazima moto, kwani hali ya hewa ya moto katika kusini mwa California imeshushwa kutoka "yenye hatari sana" hadi "yenye hatari".
Lakini mtaalamu wa hali ya hewa wa BBC, Sarah Keith-Lucas, anasema hakuna mvua inayotarajiwa katika eneo hilo kwa angalau wiki moja ijayo, hivyo hali inabakia kuwa huenda moto ukaendelea.
Mafuta ya umeme yamekatwa katika maeneo mengi ya jiji, na msongamano wa magari umeongezeka.
Kwa kuongeza, baadhi ya shule na Chuo Kikuu cha California, Los Angeles (UCLA) vimefungwa.
Zaburi 104:28
Wewe huwapa,
Wao wanakiokota;
Wewe waukunjua mkono wako,
Wao wanashiba mema;
Tunapandisha 🎚️🎛️ ya @kilimanjarorevivalradio na wewe una tusikiliza 🎫🎧 ili kupata uamsho wa Kiroho na kimwili kupitia Injili ya kweli , habari za kisiasa,kijamii,kiuchumi ,michezo na utamaduni ndio sehemu yake.
TUSIKILIZE kupitia tovuti ya www.kilimanjarorevivalfm.or.tz