๐€๐๐ซ๐ข๐š๐ง ๐€๐ฎ๐๐š๐ฑ

  • Home
  • Tanzania
  • Mwanza
  • ๐€๐๐ซ๐ข๐š๐ง ๐€๐ฎ๐๐š๐ฑ

๐€๐๐ซ๐ข๐š๐ง ๐€๐ฎ๐๐š๐ฑ ๐‰๐จ๐ฎ๐ซ๐ง๐š๐ฅ๐ข๐ฌ๐ญ ๐™ฑ๐™ฐ ๐š’๐š— ๐™ผ๐šŠ๐šœ๐šœ ๐™ฒ๐š˜๐š–๐š–๐šž๐š—๐š’๐šŒ๐šŠ๐š๐š’๐š˜๐š— ๐šŠ๐š—๐š ๐™น๐š˜๐š›๐š—๐šŠ๐š•๐š’๐šœ๐š–

Famili๐Ÿค
31/08/2024

Famili๐Ÿค

We are happy to wish birthday among of our groups and pages Admin Sonbella Classic  May God grant you more blessings in ...
17/07/2024

We are happy to wish birthday among of our groups and pages Admin Sonbella Classic

May God grant you more blessings in your life
Our multi- talented boy, etc

Hapoy birthday ๐ŸŽ‚๐ŸŽ‚

Miaka 12 iliyopita UNESCO waliona kuna umuhimu wa kuwa na siku ya redio duniani, ikapitisha na kila ifikapo Februari 13,...
13/02/2024

Miaka 12 iliyopita UNESCO waliona kuna umuhimu wa kuwa na siku ya redio duniani, ikapitisha na kila ifikapo Februari 13, siku hii uazimisha kwa aina yake kila nchi.

Redio ni njia ya mawasiliano ambayo kila mtu anaweza kuitumia bila kujali kipato ukilinganisha na njia zingne k**a mazageti na Televisheni.

Mimi k**a mdau, mwanahabari na mtu mwenye taaluma ya habari nasherekea karne ya kuburudisha, kuelimisha na kufundisha.

Kwa sababu ya kutokuwa tayari, kuna watu wengi tayari umewapoteza kwenye maisha yako na sasa kila ukiwatazama unaishia k...
06/02/2024

Kwa sababu ya kutokuwa tayari,
kuna watu wengi tayari umewapoteza kwenye maisha yako na sasa kila ukiwatazama unaishia kujuta tu.

Maisha ndivyo yalivyo, mshukuru mungu kwa kila jambo, lbd ungeng'ang'ania ungewachelewesha kufukila pale wanapohitaji.

Big up kwa wale wote niliowapoteza na sasa, mmekuwa sababu ya mimi kujiona kwenye maisha yangu nilikutana na watu walio bora zaidi,

Neno moja la faraja ni kwamba:
Tumeumbwa kukutana na watu ambao sio sahihi kabla ya kukutana na watu sahihi ili tujifunze kwa sababu kwenye ndoa hamna uwanja wa mazoezi, ni FAINALI

I found a place to repose your mind,๐Ÿ™†
03/02/2024

I found a place to repose your mind,๐Ÿ™†

Dear 2023Tumekuwa pamoja kwa takriban miezi 12 yote na kamwe hamna siku nimeacha kuwa pamoja nawe nilitembelea mule mule...
11/12/2023

Dear 2023
Tumekuwa pamoja kwa takriban miezi 12 yote na kamwe hamna siku nimeacha kuwa pamoja nawe nilitembelea mule mule.

K**a unakumbuka kwenye diary yangu, kila nilivyoandika kumbukumbu zangu muhimu mwishoni nilikutaja kabsa 2023 si unakumbuka.

nakushukuru kwa sababu uliniweka mazingira salama na kipindi chote hicho nilikuwa mwenye nguvu, na afya njema kiukweli kabla sijaenda kwa mdogo wako 2024 sitalisahau ilo.

Nisamehe sana kwa sababu ahadi zangu nyingi nilizema nitatekeleza nimedhindwa kuzitimiza, ilo kabsa nakili mbele yako.

Ila niamin sitakuwa hivyo hivyo kwa mdogo wako 2024, nitahakikisha narekebisha makosa yote na kila kitu kitaenda sawa,

Wewe ukiwa shaidi, nimewapoteza wapendwa wangu, kwa ajali, ugonjwa na wengine kwa sababu ya uzee, ila kwa sababu ya neema za mungu bado nipo wewe mpaka sasa

Sambamba na ilo kuna watu nimewakwaza na pengine nimedriki kuvunja moyo ya baadhi ya watu walioniamin na kumiweka karibu nao.

Kwa hizi siku 19 zilizobaki, nitazifanya k**a toba kwa ajili ya makosa niliyoyafanya.

Na wewe sasa nikutakie maandalizi mame ya mapumziko ya kudumu japo, umemaliza vibaya na kumbukumbu ya mafuriko uko Kateshi Manyara. kamwe huu mwaka hautafutika kwenye fikra sa watanzania.

Mwaka jana nadhan ilikuwa mwezi Desember, nilikutana na jamaa mmoja (Baba wa Familia) ambaye alisema aliamua kuanzisha f...
08/12/2023

Mwaka jana nadhan ilikuwa mwezi Desember, nilikutana na jamaa mmoja (Baba wa Familia) ambaye alisema aliamua kuanzisha familia nyingi kwa sababu ya changamoto ya mawasiliano ya simu.

Familia yake ya kwanza ilikua katika mtaa wa Chababara kata ya Kaisho, Wilayani Kyerwa Mkoani Kagera,

Huko mawasiliano ya simu ilikuwa changamoto kwake, na mishe mishe nyingi zilikuwa zinategemea mawasiliano ya simu na kwenye hayo maneo hamna minara ya simu,

Ukifka uko laini zote zinasoma Emergency, hamna kupiga simu, kupigiwa wala kutuma ujumbe mfupi.

Basi mwamba akaona aoe mke wa pili na akaweka makazi yake kwenye mtaa wa Nyakajwenge kata hiyo hiyo ya kaisho, ambapo mawasiliano ya simu yako vizuri.

Uo ni mfano tu wa mtu mmoja, naamin kuna mamia ya watu wameamua kupakimbia kutokana na changamoto hiyo, na kupunguza nguvukazi.

Juzi niliona taarifa kutoka kwenye ukurasa rasmi wa Mbunge wa jimbo la Kyerwa Innocent Bilakwate, Ofisi ya Mbunge wa Kyerwa kwamba serikali imetenga bajeti ya kuboresha mawasiliano maeneo mbalimbali ya wilaya ya Kyerwa kidogo moyo wangu ulifarijika sana.

Kuna taarifa hiyo fungua link hii
https://m.facebook.com/story.php?story_fbid=759808379519363&id=100064706239246&mibextid=Nif5oz

Namaini k**a ikitekelezwa kuna fursa nyingi ambazo wananchi wa mkoa ule walikuwa wakizikosa na rasmi wataanza kuzitumia ipasavyo.

Sambamba na hilo pia itaisaidia serikali kuendesha mifumo yao ya kidigitali katika maeneo hayo, iliwa ni sambamba na mfumo mpya wa kuboresha daftari la kudumu la wapiga kula, tunapoelekea kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka ujao na uchaguzi mkuu 2025.

K**a mbunge atafanikisha hili ila mawasiliano, akahakikisha baadhi ya kata watu wanafikishiwa huduma ya umeme, miradi ya maji safi ikaboresha, na barabara pia, njia itakuwa nyeupe 2025 ila kwa sasa mmmh.

Siku moja nilipata ndoto tamu sana na sikutamani niamke, na ata k**a ningeamka basi nilitamani nikute sio ndoto ila ni k...
16/11/2023

Siku moja nilipata ndoto tamu sana na sikutamani niamke, na ata k**a ningeamka basi nilitamani nikute sio ndoto ila ni kitu cha uhalisia.

Nikarejea kwenye tafiti za baadhi ya wanazuoni ambao wanasema usingizi ni nusu ya kifo,

Ni katika usingizi tunaweza kuona yaliyopita na yajayo, kiasi kwamba unaweza kuota umepanda Ndege, umesafri kutoka Tanzania kwenda Marekani na umerudi,

Taswira ambayo unaiona kwenye ndege ndotoni ni ndege yenyewe kabsa, wakati huo unakuta hujawahi kuona ndege live, hii sayansi ya mungu bado inanichanganya.

Jana usiku kuna ndoto nimeota, yani nipo nasali lila dakika kuomba hilo balaa lisije nitokea kweli, maana kuna baadhi ya ndoto nyingi sana huwa naota na zinatokea

Siku 462 ya Profesa J, hakika ilikuwa vita kati ya uhai na kifo, ila mwishowe uhai umeushinda umautiKuna wakati mtu anaw...
08/11/2023

Siku 462 ya Profesa J, hakika ilikuwa vita kati ya uhai na kifo, ila mwishowe uhai umeushinda umauti

Kuna wakati mtu anaweza pitia mgumu mgumu na mgumu kupitiliza ila mwisho akasimama tena na kurudi k**a mwanzo,

Kwa fununu zilizokuwepo kipindi hicho kutokana na hali yake ya kiafya, hakika hamna aliyetegemea k**a leo angerudi tena studio na kusimulia mkasa huku..

Ikiwa bado upo hai, ishi k**a vile hutakuwepo kesho

Upendo ukianza 0% na ukaongezeka kidogo kidogo mpaka 100% utadumu kwa mda mrefu.Ila k**a ukianza 100% lazima ushuke mpak...
20/10/2023

Upendo ukianza 0% na ukaongezeka kidogo kidogo mpaka 100% utadumu kwa mda mrefu.

Ila k**a ukianza 100% lazima ushuke mpaka 0%, na hapo kinachofata unakifahamu.

Namaanisha kwamba mapenzi yangu na mpira wa miguu yalianza kidogo kidogo, sasa hivi nakaribia kuchukua kadi ya shabiki miwe nalipa kiasi kadhaa kwa mwezi

Kila la heri Simba SC Tanzania kwenye mchezo wako wa Ufunguzi AFL, ila uvune tu ulichopanda basi.

Tangu nizaliwe npaka saaa hivi, sijawahi kuangalia televisheni nikakosa Tangazo la Vodacom au Cocacola, licha ya kujulik...
08/10/2023

Tangu nizaliwe npaka saaa hivi, sijawahi kuangalia televisheni nikakosa Tangazo la Vodacom au Cocacola, licha ya kujulikana lakini bado wanaamini wana nafasi ya kujitangaza

Jina kutengeneza jina, kusikia maskioni mwa watu kila mda imekuwa ndoto ya kila mtu mwenye cheo, mamlaka au kipaji.

Huku Wilaya ya Kyerwa mkoani Kagera, ni wilaya changa kimaendeleo inajijenga na inahitaji viongozi wenye maono, uzalendo wa kuweza kuitengeneza na kusimama angalau ata miaka 10 ijayo ifikie hadhi ya miji au ata manispaa, hii sio ndoto

Nafasi ya wanawake katika uongozi kwa sasa sio story tena, wamepata nafasi na kazi yao inaonekana...

Hii ni hadithi ya Anatropia mbunge wa viti maalumu, leo kawauunganisha wananchi wote wa wilayani hii kimchezo kupitia michezo ANATROPIA CUP

Na leo ni fainali, Nimpongeze kwa hicho alichokifanya na naamini matumda yake atayaona baadae,

Weekend yangu ntakuwa nashuhudia Anatropia CUP fainali viwanja vya Isingro
Anatropia theonest
Anatropia Theonest
Kyerwa District Council

Huwa naionea wivu Misiri, Algeria na Morocco kwa jinsi ambavyo club zao zinafanya vizuri kwenye mashindano ya Afrika.Jan...
16/09/2023

Huwa naionea wivu Misiri, Algeria na Morocco kwa jinsi ambavyo club zao zinafanya vizuri kwenye mashindano ya Afrika.

Jana timu ya USM Alger ambaye ni bingwa wa kombe la shirikisho ameibuka kidedea baada ya kumchapa Bingwa wa Club bingwa Afrika Al Ahal ya Misiri

Ushindi huu unatupa taswira kwamba Msimu uliopita Club ya Yanga Africans ilitafuna mfupa mzito, ni vile tu ukomavu wa meno yao katika hayo mashindano yaliamua matokeo.

Leo club zetu pendwa za Tanzania Simba na Yanga zinarusha karata yake ya kwanza kwenye mechi ya kwanza ya kufuzu hatua ya makundi ya mashindano ya Club bingwa barani Afrika.

Bila kujali ushabiki, furaha yangu ni kuona Simba na Yanga zinafanya vizuri na kuwa tishio barani Afrika na kuipa heshima taifa letu, k**a ilivyo kwa Mataifa ya Kaskazini na kufanya ligi yetu iendelee kuwa bora.

Yanga atakuwa nchi Rwanda kumenyana na Club ya Al-Merrkh ya Sudani, huku Power Dynamo ya Nchini zambia ikiwakaribia Club ya Simba kutoka Tanzania

Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki Simba, Mungu ibariki Yanga Africans

TAJIRI WA MISEMO BONGO MOVIE, Watu hucheza games kwenye simu na playstation, ili kurefresh mind ila kwangu mimi hivyo vy...
12/09/2023

TAJIRI WA MISEMO BONGO MOVIE,
Watu hucheza games kwenye simu na playstation, ili kurefresh mind ila kwangu mimi hivyo vyote vilipita pembeni kabsaa.

Ukitaka kumiweza, niwekee season ya kikorea za ufalme, au ata majambazi na polisi, ntaangali ata siku nzima bila kula.

In short niko adicted sana na series especially za kikorea, Kichini, Tailand, na Hindi na Uturuki kidogo.

Kwa bongo kidogo zilikuwa hazinikoshi kwa sababu nyingi ni single movies, saa moja tu movie imeisha.

Ila nowdays wamekuja kwa kasi kwenye kuandaa series pia hapa naona k**a soon ntaanza kugusa na bongo movies.

Ila licha ya hizo kuna mwamba anaitwa huyu mwamba ata nkipita sehemu nikakuta movie yake inaonyeshwa, lazima misimame kdg k**a sina haraka ntaangalia mpaka iishe, k**a nina haraka ntaangalia jina la movie afu badae naishaka kwa njia yoyote.

Kwenye movies zake zote, ni fundi wa kutumia maneno, uhalisia wake kiasi kwamba unahisi k**a vile upo eneo la tukio.

Kwa mara ya kwanza nilivutiwa na series yake ya , badae nikakutana na da! Tanzania tuna watu wenye vipaji na ujuzi..

Movies zake kwangu ni darasa la maisha, na lugha pia, misemo yake sasa da

Ziko wapi zile enzi tunacheza mchezo wa baba na mama, tunatumia viungo ambavyo kwa wakati huo hatukujua ata kazi yake???...
06/09/2023

Ziko wapi zile enzi tunacheza mchezo wa baba na mama, tunatumia viungo ambavyo kwa wakati huo hatukujua ata kazi yake???

Enzi ukimwambia mtu unampenda, k**a sio kwa mwalimu basi atakusema nyumbani kwenu na utembezewe kichapo kikali na uone k**a vile kupenda ni kosa kubwa.

Leo upendo unakuwa na why nyingi mpaka zina kera, pesa, mali, umaarufu kimekuwa kipaumbele na maslahi kibao tu,

Miaka ijayo, mapenzi yatakuwa biashara k**a biashara nyingine, neno hisia litakufa kabsa.

Ile midoli ilozinduliwa na mmiliki cjui wa twitter ( ร—) cjui wa Meta zitakuja kureplace mambo mengi sana

SHIKAMOO KIFO ๐Ÿ˜ญ, WEWE NDO TATIZO PEKEE AMBALO PESA HAIWEZI KULISOLVEMziki wa Bongofleva umempoteza Mrembo, mwenye kipaji...
02/09/2023

SHIKAMOO KIFO ๐Ÿ˜ญ, WEWE NDO TATIZO PEKEE AMBALO PESA HAIWEZI KULISOLVE

Mziki wa Bongofleva umempoteza Mrembo, mwenye kipaji na sauti nzuri ambaye amefariki dunia siku ya Ijumaa Septemba 01 2023

Kwa mara ya kwanza nimemfaham msanii huyu kupitia wimbo wake wa ***oy aliomshirikisha

Katika wimbo huu, alimuongelee mwanamke ambaye ametokea kuzama kwenye dimbwi la mapenzi na mvulana ambaye hajatulia yaani eat and run ( Pl***oy).

Moja ya mstari wake anasema, anaamini uyo mwanaume lazima ashangae k**a akisikia kuwa kuwa anamuwaza

Pumzika kwa amani ๐Ÿ˜ญ๐Ÿ˜ญ ๐Ÿ•ฏ๏ธ

UNASHEREHEKEA NA NANI MAFANIKIO YAKO??Harakati zote anazozifanya mtu, taasisi binafsi na za uma, ni kwa ajili ya kusonga...
31/08/2023

UNASHEREHEKEA NA NANI MAFANIKIO YAKO??

Harakati zote anazozifanya mtu, taasisi binafsi na za uma, ni kwa ajili ya kusonga mbele na kuleta ustawi miongo mwa taasisi husika au mtu mwenyewe.

Kwenye kupambania mafanikio, taasisi kwa taasisi zinaombeana njaa, kutokana na ushindani, kila mmoja anatamani kuwa juu ya mwenzake,

Kwa mfano mafanikio ya Club ya Mpira ya Yanga, ni k**a dholuba kwa vilabu vingine vinavyotamani kuwa juu pia.

Hawapati usingizi kwa sababu ya mafanikio yao, wanataman yawe upande wao na wako radhi kutumia njia zozote kuvuruga mipango yote

Hii ni vita ya mafanikio,

Je wewe mafanikio yako unayafurahia na nani?

Marafiki wanakuzunguka, ndugu zako au familia yako yote?

Ukweli ni kwamba ata mimi sijui mafanikio yako unaweza kuyafurahia na nan .... Labda ntafahamu kupitia uwanja wa comments

MADARAKA YANAVYOTUTAFUNA Mwezi huu Agosti 24, kumefanyika uchaguzi wa kumpata mkuu wa maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la ...
28/08/2023

MADARAKA YANAVYOTUTAFUNA
Mwezi huu Agosti 24, kumefanyika uchaguzi wa kumpata mkuu wa maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri la Tanzania (KKKT)
Arusha;

Lakini uchaguzi huo umekumbwa na utata juu ya dhuluma zilizofanyika kwa baadhi ya maaskofu kukatwa majina yako akiwemo Askofu Dkt. Benson Bagonza, Mkuu wa
KKKT - Dayosisi ya Karagwe.

Na Bagonza alipewa nafasi kubwa ya kuibuka mshindi lakini jina lake likakatwa mapema sana,

Jana Agosti 27 majumuisho ya kula katika uchaguzi mkuu Nchini Zimbabwe na Rais Emmerson Mnangagwa akafanikiwa kutetea kiti chake cha Urais kwa ushindi wa 52.2%.

Ata hivyo Mpinzani wake kutoka chama cha
Citizens' Coalition for Change (CCC) Nelson Chamisa, bado hajakubaliana na matokeo hayo huku akidai kuwa " matokeo yoyote yaliokusanywa kwa haraka pasi kuhakikiwa.

Mantiki yangu katika hili ni kwamba, kadri siku zinavyozidi kusogea uchu wa madaraka na vyeo unazidi kutawala katika taasisi za Serikali na Dini huku hamna anayekubali kushindwa jambo ambalo sio afya kwa ustawi wa demokrasia.

Kilichotokea kwenye Kanisa la KKKT kitajenga taswira gani kwa hao viongozi ( Maaskofu wa ngazi za juu) baada ya kuonyesha uhasama miongoni mwao, na vipi kuhusu waamin wanaomfuata Askofu Bagonza

NO TIME FOR MIND VOCATIONK**a unadhani kuna mtu akili yake inaweza enda break kabsa asiwe na stress yoyote nikutie moyo ...
26/08/2023

NO TIME FOR MIND VOCATION
K**a unadhani kuna mtu akili yake inaweza enda break kabsa asiwe na stress yoyote nikutie moyo tu, that things never hapen.

Wanamichezo kila siku wanawaza ni vipi timu yake itakuwa namba one ipiku teamu zote kwenye idara zote na ibebe kila kombe,

Watu wa dini, huko ndo usiseme, kila mda muumini anataman ashukiwe na yule anayemwabudu kila siku angalau ampe go on maana dini zimekuwa nyingi ( pumba na mchele umo umo).

Viongozi wa siasa wanawaza kuwa bora kwa wanaowaongoza, huku bado wamegubikwa na upinzani mkali sana,

Nadhan wewe na kuwa na maisha duni ila unapata usingizi mnono kuliko your President...

Tajiri kila mda anawaza kuongeza utajiri, na kupata kila anachohitaji maishani, ila atakosa usingizi kwa kuhofia ulinzi wake,
Matajiri wanawindwa sana nyie ndio maana wako na guards kila kona.

Sasa mimi ni nani akili yangu itulie nisiwaze, sina ela YES, sipendwi YES, ila ata vyote nikipata bado nyawaza namna ya kuvilinda.

Ila ni bora kupitia changamoto ukiwa macho kulilo kupitia changamoto za bila kuwa nacho.

NIMEACHIA Bwana๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€๐Ÿ˜€

DINI INABISHA HODI KWENYE MLANGO WA SIASAWakoloni  walitumia dini kwa asilimia kubwa ili kiteka akili ya Watanganyika mi...
20/08/2023

DINI INABISHA HODI KWENYE MLANGO WA SIASA

Wakoloni walitumia dini kwa asilimia kubwa ili kiteka akili ya Watanganyika miaka hiyo na wakafanikiwa kuitawala na kunyonya rasilimali zao.

Yani unaambiwa katika mahubiri yao, walikuwa wakipenyeza agenda zao, na hivyo kwa sababu waamini walikuwa tayari wamewaamini na wana imani ilikuwa ni vigumu kupinga.

Katika mataifa ya kiislamu ambayo yamejaa mapigano na kesi za kujilipua mara kwa mara, hutumia kigezo cha dini na wakati mwingine wakiwaaminisha kuwa wakishafanya hivyo basi itakuwa rahisi kifika mbinguni.

Nadhani wengi wenu mtakuwa mmetazama kwenye movies mnaweza kuwa mashahidi katika hilo.

Nachotaka kumaanisha ni kwamba, imani ya kidini ina nguvu kubwa katika kubadilisha akili ya binadamu na wakati mwingine kuamua kumfanya unavyotaka wewe.

Leo katikati makanisa yote ya kikristo nchini Tanzania wamewasomea waamini wote walaka wa Baraza la maaskofu Tanzania kukataa uwekezaji wa bandari nchini.

Tukumbuke kuwa Askofu ni kiongozi wa ngazi ya juu katika dini ya kikristo nchini.
hivyo hii ina maana kuwa wanahitaji au wanatamani uwe mtazamo wa waamini wote wa kikristo nchini...

Makanisa ni platform kubwa yenye uwezo wa kuwafikia watu wengi kwa mda mfupi sana, tunavyoongea sasa hivi, kila aliyehudhuria ibada leo katika makanisa ya Roman Catholic tayari hii habari ameisikia.

Kwa wengine haikuwa jambo geni, ila kwa wale ambao hawana uwezo wa kutumia internet, hawana TV wala redio leo taarifa hiyo imewafikia na bahati mbaya katika upande mmoja wa shilingi.

Na ikumbukwe kuwa Mahak**a tayari imetupilia mbali kesi ya kukataa uwekezaji, Bunge tayari limepitisha, na Serikali ya Chama cha Mapinduzi inatumia jitihada zake kufanya wananchi wakubaliane na uamuzi uo wakiamini utaleta tija kubwa nchini.

Endelea kufuatilia page hii,

16/08/2023

Trust me, hamna mtu anaamin k**a kuna urafiki kati ya msichana/ mwanamke na mvulana ( mwanaume), labda tu wao wenyewe waopo kwenye uo urafk ndo uamin,

Mapenzi ni namna tu unavyomchukulia mtu moyoni,

KAHAWA ZINAVYOWAACHA WAKULIMA MACHO KODOBado siku chache kuelekea kufungulia kwa msimu wa kuuza na kununua zao la kahawa...
15/05/2023

KAHAWA ZINAVYOWAACHA WAKULIMA MACHO KODO

Bado siku chache kuelekea kufungulia kwa msimu wa kuuza na kununua zao la kahawa katika mkoa wa Kagera,

Bila shaka unakumbuka kuwa kilimo cha kahawa ndio kilimo pekee cha biashara kinacho tengemewa na wakulima wa mkoa wa Kagera na wilaya zake zote.

Kipindi hiki kila mwenye kahawa anakuwa na mategemeo makubwa ya kutimiza melengo yake ya kiuchumi baada tu ya mauzo.

Mategemeo yao huzimishwa ghafla na bei za kahawa zisizoridhisha kutoka kwa vyama vya msingi huku wanachama wakiwekewa katazo la kuhakikisha kahawa zote zinauzwa kwenye vyama vya msingi na sio vinginevyo.

Kabla ya msimu kuanza kuna mambo kadaha yanaandama wakulima ambayo wenda yakachangia kuleta migogoro katika zao ilo.

1: Baadhi ya wakulima tayari wameanza kuuza kahawa zao rejereja na wengine tayari wameuza ata kabla ya kahawa kuvunywa,

2: Wizi uliokithiri wa kahawa mashambani.

3: Katazo la kutovuna kahawa mpaka kutoa taarifa kwa mwenyekiti wa kijiji au mtaa.

4: Baadhi ya wakulima kutaifishwa kahawa zao kutokana na kuvuma bila vibali.

5: Wanunuzi wa rejereja kunyang'anywa kahawa na kutaifishwa, japo bado zinanunuliwa kwa uficho sana.

Je wewe k**a mkulima una mtazamo gani juu ya matukio haya na unadhani nini kifanyike ile kuondokana na kadhia hii,

Je ni sahihi serikali kujitokeza kwa wakati wa mavuno ilihali haimshiki mkulia mkono wakati wa kupata pembejeo bora na mbolea..

Katika maisha kuwa na washauri (mentor ) ni vizuri zaidi  kuliko washindani (competitor).Mara nyingi tunakosea kuwafanya...
06/03/2023

Katika maisha kuwa na washauri (mentor ) ni vizuri zaidi kuliko washindani (competitor).

Mara nyingi tunakosea kuwafanya watu waliotuzidi mafanikio k**a washindani wetu. Tunatumia nguvu kubwa kutaka kushindana nao badala ya kuwatumia kutufundisha namna ya kufanya vizuri angalau tuwakaribie wao k**a sio kulingana nao kabsa,

Mtu aliyekuzidi maendeleo anafaa kuwa mshauri wako na sio mshindani wako.

Ingali bado upo hai, umejaliwa kukutana na watu wa kila aina, wapo watakao kuona shujaa, mshindi, kiongozi, msaada na we...
19/11/2022

Ingali bado upo hai, umejaliwa kukutana na watu wa kila aina, wapo watakao kuona shujaa, mshindi, kiongozi, msaada na wengine watakutumia k**a mfano kwao.

Vile vile kuna wale watakao kuchukia sio kwa sababu utawafanyia makosa, hapana watakuchukia kwa jinsi tu ulivyo.

Katika kila hatua jifunze kubalance, maaana ata kwa utamu wa sukari lakini ikizidi uharibu kinywaji.

Kuna wakati unaweza kudhani upo sahihi kwa namna unavyoishi na watu kumbe haupo sahihi, na wanaokuunga mkono wanakunafikia,

vile vile na hao ambao unadhani wanakuchukia ndio wanakutaka ubadilike na uwe katika mstari.

Katika maisha kila mtu ni mhumu, ila umuhimu wake uonekane kwa wakati sahihi, kabla wakati haujafika huwezi kuona umuhimu wake, tuwe na subira tuwavumilie,

Jifunze kusikiliza na kufanyia kazi ushauri wa watu, pia akili ya kuambiwa changanya na yako.

Weekend ndio hii, watumie vizuri wale ambao unapenda kusikiliza chochote kitu kutoka kwao ili upate faraja na furaha, na k**a wewe ukigundua ni sehemu ya furaha ya mtu mwingine basi mpe ushirikiano japo kidogo,

Maisha ni kubebana, ile upo chini kesho utakuwa juu, na aliyepojuu leo kesho anaweza kuwa chini.

Credit to , njia yako ya utafutaji, imenipa wepesi wa kupeleka mkono kinywani

16/11/2022

Kabla hujakutana naye kimwili,
Moyo humchanganua na kumpa kila sifa ambazo kihisia unataman mtu wako awe nazo,

kila kitu kinakuwa moto moto, ukipiga hatua moja mbele na yeye anapiga hatua nyingine kuifata njia yako,

Changamoto huanza baada ya kukutana kimwili na kugundua imekuwa tofauti na matarajio yako, kila kitu hubadilika na hatua zilizokuwa zikipigwa kwenda mbele, badala yake huanza kurudi nyuma.

Binafsi huwa napenda kusema Mapenzi huanza pale watu wanapokutana na kujuana, na hapo ndio mtu huchagua kuwa anamudu udhaifu wa mwenzie na ataweza kuvumilia,

Lakini kabla ya hapo, watu wengi tunadanganywa na macho na kujikuta tunapoteza muda mwingi kusubiri mtu ambaye huna uhakika naye na hujaprove k**a anaweza kukidhi mahitaji ya hisia zako

Tupende ila tutupunguze kuwa na mategemeo makubwa kwa watu, ili tusivunjike moyo.

Kwa sasa unaweza fanya utakavyo kuutesa mwili wako, lakini kuna wakati utafika mwili huo huo utakufanya ujute na kujiona...
25/10/2022

Kwa sasa unaweza fanya utakavyo kuutesa mwili wako, lakini kuna wakati utafika mwili huo huo utakufanya ujute na kujiona sio chochote katika sayali hii,

Ukitaka kuamini muulize binti aliyetoa mimba mara kadhaa na sasa yupo kwenye ndoa na anateseka kwa sababu ameshindwa kumpatia mumewe mtoto,

Au muulize mwanaume ambaye ametumia mwili wake kujichua na sasa ana hofu kubwa sana katika ndoa yake kwa sababu anadolora katika tendo,

Utandawazi umedondosha dhoruba ambayo ni kilio kwa kizazi hiki na kijacho.
Kila upatapo nafasi, Mwambie kijana kuwa uvumilivu na kujinyima kwa sasa kutakufanya uishi k**a mfalme siku zijazo

Kuna wakati ndugu hukosana nyumbani, lakini siku zote vita kati ya ndugu na mtu mwingine wa nje, lazima ukae upande wa n...
08/10/2022

Kuna wakati ndugu hukosana nyumbani, lakini siku zote vita kati ya ndugu na mtu mwingine wa nje, lazima ukae upande wa ndugu yako na huu ndio ubinadamu.

Yes kwa sababu wako ndani ya nyumba moja na wanagombania kitu kimoja, mikwaruzano lazima itakuwepo ila kwa sasa kila mmoja ana vita yake na ushindi katika vita hiyo, ni heshima kwa familia yetu kwa ujumla.

Simba, and Azam zote ni damu ya baba mmoja Tanzania, na katika vita hii ya nje basi tuwaombee ili walete heshima katika familia yetu,

Funika kombe mwanaharamu apite,.
All the best
Simba SC Tanzania
YANGA African Sports CLUB
Azam FC

Pengine k**a tungetaka kuandika mahitaji ya msingi ya ili dunia iwe kamili, tusingesahau kuandika Mapenzi,K**a ilivyo se...
08/10/2022

Pengine k**a tungetaka kuandika mahitaji ya msingi ya ili dunia iwe kamili, tusingesahau kuandika Mapenzi,

K**a ilivyo sekta ya siasa, michezo, uchumi na burudani, mapenzi yanachukua taswira pana sana katika dunia ya sasa na pengine yanazungumziwa sana kuliko ata uchumi wa nchi.

Sijui, labda inabidi iwe hivyo, kwa jamii ambazo bado zinafundisha Jando na Unyago nadhani kwa sasa wana kibarua kizito ili kupambana na kirusi cha wivu wa kimapenzi na usaliti kinachoandama ndoa nyingi nchini.

Sasa hivi ndio naelewa kwa nini Tanga wanaweka nguvu kubwa kuwanoa mabinti ili kukabiliana na misukosuko ya mahusiano kuliko kuwaonyesha fursa za kibiashara..

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mhe. Fรฉlix Antoine Tshise...
18/08/2022

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Mhe. Fรฉlix Antoine Tshisekedi alipokua akitambulishwa kwa viongozi mbalimbali wa DRC alipowasili katika Ikulu ya Kinshasa kwa ajili ya kuanza ziara rasmi ya siku moja Agosti 18, 2022.

23/07/2022

Singida big stars msimu ujao itakuwa k**a yanga B๐Ÿ˜†๐Ÿ˜‚

Wachezaji wake wengi wamepita yanga

MANARA AFUNGIWA MIAKA 2 NA FAINI MILIONI 20...Haji Manara [Msemaji/Mhamasishaji wa Yanga] anadaiwa Kumtishia na kumdhali...
21/07/2022

MANARA AFUNGIWA MIAKA 2 NA FAINI MILIONI 20...

Haji Manara [Msemaji/Mhamasishaji wa Yanga] anadaiwa Kumtishia na kumdhalilisha Rais wa TFF Ndg. Walles Karia siku ya Jumamosi Julai 2, 2022 kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha wakati wa mechi ya Fainali kati ya Yanga dhidi ya Coastal Union.

โ€œWewe unanifatafata sana, hii ni mara ya tatu, sikuogopi kwa lolote,kwa chochote na huwezi kunifanya chochote. Nina uwezo wa kukufanya chochote na huna cha kunifanya.โ€

K**ati ya maadili ya (TFF) imefafanua vitu vifuatavyo kuhusu hukumu aliyopewa Haji Manara kutokujihusisha na soka kwa miaka miwili nje na ndani ya Nchi.

1. Anaruhusiwa kwenda viwanjani kutazama michezo mbalimbali.

2. Adhabu haihusu mitandao yake ya kijamii. Anaruhusiwa kupost.

3. Amepewa siku (21) kukata rufaa.

Address

Nyamagana
Mwanza

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when ๐€๐๐ซ๐ข๐š๐ง ๐€๐ฎ๐๐š๐ฑ posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to ๐€๐๐ซ๐ข๐š๐ง ๐€๐ฎ๐๐š๐ฑ:

Videos

Share

Nearby media companies


Other Social Media Agencies in Mwanza

Show All

You may also like