27/10/2024
UKWELI KUHUSU MAHALI PA KAZI
-Bosi wako si rafiki yako, bila kujali ukaribu wenu, jifunze kuweka mipaka ya kikazi uwapo kazini.
-Kuta zina masikio, kuwa mwangalifu unamwamini nani kazini, sikio linalosikiliza linaweza pia kuwa mdomo wa kuongea ovyo.
-Mwajiri wako anajali MATOKEO tu na sio tantalila zako, Jinsi unavyofanya kazi na jinsi ananufaika na utendaji kazi wako.
Kuna wakati anakuwepo mtu mmoja au kikundi cha watu wanaomlisha bosi habari za ofisini, Jiongoze mwenyewe.
-Unapotolewa kwenye project au bosi anaanza kukufatilia au unaposhushwa cheo bila sababu za msingi, hiyo inaweza kuwa ishara kwamba hivi karibuni utaonyeshwa mlango wa kutoka.
-Kadri uwezavyo, weka maisha yako ya kibinafsi mbali na wenzako hapo kazini. Unaweza kuwa unachunguzwa maisha yako binafsi bila hata kujua.
-Wafanyakazi wenzako huenda hawakupendi, kwasababu ya jinsi unavyoonekana, kuvaa, kuzungumza, uwezo wako, mafanikio yako kazini, aura yako au kwa sababu za ajabu na hilo ni sawa. Si kila mtu anaweza kukupenda, kwa hiyo ukubali tu hilo na usonge mbele.
-Zingatia lugha ya mwili, sauti, mdundo na kasi ya sauti kutoka kwa wenzako, wenzako wa kazini au bosi wako.
Utafiti umeonyesha kuwa hisia, mapenzi na chuki huwasilishwa kupitia 92% ya lugha isiyo ya maneno, ni asilimia 7 tu ndiyo huwasilishwa kupitia mawasiliano ya maneno.
-Kazini huwa kunakuwa na "mfanyakazi wa ajabu" ambaye anafanya kazi kwa bidii, anapata kutambuliwa na pongezi nyingi.
Usiruhusu hisia ya kudharau, chuki dhidi yake iingie ndani yako,
Angalia kile mtu huyo anafanya tofauti, jinsi anavyofanya na jifunze, utakuwa mtu bora zaidi. Kuwa muwazi unapotaka kujifunza, sio roho ikuvimbe ukimbilie kuroga au kufanya fitina, hapo utakuwa unajiweka mbali na baraka za Mungu maishani mwako.
-Ingawa mahali pa kazi tunapaswa kukuza uhusiano mzuri na wenzetu, usisahau kuwa lengo lako kuu ni kufanya kazi na kurudi nyumbani.
Usisahau hilo.
Na Princess Swabra Mbisu
share ujumbe huu