Nguvu ya Msalaba/Tafsiri ya ndoto kibiblia

Nguvu ya Msalaba/Tafsiri ya ndoto  kibiblia NENO LA MUNGU /NDOTO NA TAFSIRI ZAKE. https://chat.whatsapp.com/IH95NnA8yeoBfiAQJLdzff

12/09/2024

*UPENDO WA MUNGU*

Upendo wa Mungu kwetu ni wa kipekee sana,

Mungu kuacha vyote kuja kwetu k**a mwana pekee wa Mungu,

Yohana 1:16
[16]Kwa kuwa katika utimilifu wake sisi sote tulipokea, na neema juu ya neema.

Hii ni neema kubwa ,Mungu alitupenda Bure ,Sina maana kwamba sasa hatupendi hapana alitupenda na bado anatupenda

Yohana 3:16
[16]Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.

Kila amwaminiye asipotee Bali awe na uzima wa milele,

Msitari huo inazungumza kwamba asipotee ni wakati uliopo ,Yesu aliishi kwetu miaka 2024 iliopita ila pendo lake linaishi mpaka Leo ,

Kila amwaminiye asipotee Bali awe na uzima wa milele,inazungumzia wakati iliopo,halleluya.

Maandiko yanasema kila amwaminiye asipotee Bali awe na uzima wa milele,

Kila amwaminiye asipotee ,kumbe Kuna waliopotea

Ni kweli alitupenda sote pasipo masharti ila Kuna waliopotea ,

Hawapo zizini,

KUMBE Kuna pendo unalikosa kwa yule alitepotea zizini

Asiye zizini Kuna pendo la Yesu analikosa kwa sababu moja tu upotevu ,kutokuwa zizini pendo la Yesu umelipoteza

Kutokuwa zizini umepoteza thamani ya pendo la Yesu,

Kuto kuwa zizini umepoteza thamani ya kuitwa mwana wa Mungu ,

Wafilipi 2:15
[15]mpate kuwa wana wa Mungu wasio na lawama, wala udanganyifu, wasio na ila kati ya kizazi chenye ukaidi, kilichopotoka; ambao kati ya hao mnaonekana kuwa k**a mianga katika ulimwengu,

Wagalatia 3:26
[26]Kwa kuwa ninyi nyote mmekuwa wana wa Mungu kwa njia ya imani katika Kristo Yesu.

Kuto kuwa zizini umepoteza thamani Kuishi milele

Kutokuwa kuwa zizini umepoteza thamani ya kuziishi ahadi za Mungu ulizokusudiwa,

Kutokuwa kuwa zizini umepoteza haki ukuhani wa kifalme

1 Petro 2:9
[9]Bali ninyi ni mzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;

UPENDO WA MUNGU KWETU HUPIMIKA

Pamoja na Mungu kutupenda sisi pasipo masharti ,

Upendo wake kwetu hupimika ,

Mapenzi ya Mungu kwetu haulingani kati ya Mtu na Mtu,

Kiwango chako Cha Mahusiano Yako na Mungu ndio hututofautisha,

Mahusiano Yako ndio huamua kiwango Cha kupendwa na Mungu,

MSINGI wa mahusiano Yako na Mungu ni mawasiliano,

Hakuna mahusiano yaliokosa mawasiliano,

Marafiki wawili mawasiliano yakikosekana tunasema mahusiano yamekosekana,

Ili upendo wa Mungu kwako uongezeke imarisha mawasiliano,

Mawasiliano yakiongezeka mahusiano yataimarika,

Ngoja tuone kwenye maandiko upendo wa Mungu kwetu namna unavyotutofautisha,

Warumi 8:28
[28]Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake.

Wale wampendao katika kiwapatia Mema,

KUMBE hapa tunaanza kutenganishwa au kujitenganisha na upendo wa Mungu

Anawapatia Mema wale tu wampendao ,

3 Yohana 1:2
[2]Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, k**a vile roho yako ifanikiwavyo.

Hapa Maandiko yanasema Mpenzi ,huyu Mpenzi ni yupi anaelengwa hapa?

3 Yohana 1:3
[3]Maana nalifurahi mno walipokuja ndugu na kuishuhudia kweli yako, k**a uendavyo katika kweli.

KUMBE Mpenzi ni yule aendae katika kweli ya Mungu ,

Nehemia 1:5
[5]nikasema, Nakusihi, Ee BWANA, Mungu wa mbinguni, Mungu mkuu, mwenye kuogofya, mwenye kutimiza agano lake na rehema zake kwa hao wampendao na kuzishika amri zake;

KUMBE Mungu hutimiza agano kwa wale tu wampendao na kuzishika amri zake,

Zaburi 1:3
[3]Naye atakuwa k**a mti uliopandwa
Kandokando ya vijito vya maji,
Uzaao matunda yake kwa majira yake,
Wala jani lake halinyauki;
Na kila alitendalo litafanikiwa.

Atakuwa k**a mti uliopandwa kando ya vijito ,

Huyu ni yupi anaezungumzwa hapa?

Zaburi 1:1-2
[1]Heri mtu yule asiyekwenda
Katika shauri la wasio haki;
Wala hakusimama katika njia ya wakosaji;
Wala hakuketi barazani pa wenye mizaha.
[2]Bali sheria ya BWANA ndiyo impendezayo,
Na sheria yake huitafakari mchana na usiku.

KUMBE anae zungumzwa hapa ni asiye kwenda katika shauri la wasio haki

Bali sheria ya Bwana ndio impendezayo na sheria yake huitafakari mchana na ucku halleluya.

Zaburi 145:18-19
[18]BWANA yu karibu na wote wamwitao,
Wote wamwitao kwa uaminifu.
[19]Atawafanyia wamchao matakwa yao,
Naye atakisikia kilio chao na kuwaokoa.

BWANA yu karibu na Wote wamwitao ,ishu si kumwita tu Bali kumwita kwa UAMINIFU ,

Hivyo msisitizo wa SoMo kukuhimiza kumtafuta Mungu wako,

Mungu YUPO TAYARI KUJIFUNUA KWAKO tu utakapokuwa tayari kuipokea neema ya UWOKOVU ,

UWOKOVU ninapo zungumzia ni kukubali kuacha yote yasio mpendeza Mungu ,Uwe tayari kujitoa Kwa ajili ya Mungu ,haupotezi ila unawekeza kwa Mungu,

Mwili wetu ni mdanganyifu hakuna siku umewai kuridhika na ukakushukuru ukasema umenipendezesha,

Haya nawatakia siku njema na Mungu awabariki sana

Join group letu la wasap

30/08/2024

[8/21, 11:53 PM] jongo: *HATIA YA MJI*

Kuna kitu kinaitwa hatia ya MJI,

MJI wako unaweza ukaingia kwenye hatia tu kwa makosa ya watu,au mtu mmoja,

Kwa kukosa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni,

Warumi 5:12
[12]Kwa hiyo, k**a kwa mtu mmoja dhambi iliingia ulimwenguni, na kwa dhambi hiyo mauti; na hivyo mauti ikawafikia watu wote kwa sababu wote wamefanya dhambi;

Dhambi iliingia kwa kukosa mtu mmoja na Mauti ikawafikia wote ,adhabu ya dhambi ulimwengu mzima ulikabiliwa ,

Kuna mambo yanafanyika ndani ya MJI wako yanapelekea wote mwingine kwenye hatia ,

Kuna baadhi ya miji mnajikuta mnaitumikia adhabu kwa kwa hatia MJI ,

Unajua hatuna utaratibu wa KUMULIZA Mungu pale unapotaka kwenda Kuishi mahali,

Huwa tunajiendea tu ,haya ni mambo ya msingi sana kuyajua,

Nimeenda mahali Rea wameweka umeme kila nyumba wameweka nguzo mlangoni lakini hakuna aliechukua umeme,

Umeme wakati huo kuchukua ni 27000,

Uchumi wao wakulima wa viazi,

Sasa naomba tafakari umeme mlangoni Kijiji chote kila mmoja nguzo mlangoni lakini hakuna aliefanikiwa kuingiza umeme,

Umeme umeingizwa shuleni na nyumba ya MWALIMU basi,

Kuna mahari flani vijana wakifikisha umri flani wanakufa ,miaka 35 hawavuki hapo ,

MJI wamebaki wazee,kufanya utafiti walimzika chifu na kijana na kijana ,

MJI ukapokea hatia ya kumwaga Damu,

Vizazi vilivyo faata vikaendelea kumtumikia adhabu ya hatia,

Ni mambo mengi tunakumbana nayo yana chanzo chake,

Kuna miji ambayo wenyewe ni ulevi tu ,

Vijana wadogo unakuta wameharibika ishu ni pombe ,unaanza kukemea pepo kumbe pombe Ina uhalali,

Kuna sehemu zingine Roho ya uzinzi ,unaanza kuwalaumu vijana kumbe hio Roho Ina uhalali,

Wakazi wa njia mnajikuta watoto wenu wanaitumikia adhabu hio kumbe ni hatia ya MJI ,

Pata mda Muulize Mungu mambo Gani yalifanyika hapo zamani kilicho pelekea MJI uingie kwenye hatia,

Wewe ni Nuru mpendwa sisi ndio tunapaswa kubadili ulimwengu huu,,
Sisi tu mawakili wa kristo,

Lazima tufanyike Nuru,changamoto tumekosa umoja,

Baada ya kujisema Mimi WAKILI wa kristo ,

Tunapaswa kukaa katika nafasi,

Ombea MJI wako,Ombea mkoa wako,Ombea inchi Yako,

Lakini ni vema Muombe Mungu akufunulie MJI wako unatumikia adhabu Gani? Naamini ufunuo utakupa na mlango wa kutokea hapo,

Bila ufunuo ni vigumu kushughulikia na jambo usilo lijua ,

Mwanzo 13:13
[13]Lakini watu wa Sodoma walikuwa wabaya, wenye kufanya dhambi nyingi sana juu ya BWANA.

Hapo inazungumzwa sodoma,maandiko yanasema watu wa sodoma walikuwa wabaya wenye kufanya dhambi nyingi,

Miji k**a sodoma hapa Tanzania haipo,

Kuna maeneo mengi uovu umekithiri,ishu ni neema tu inatufunika,

Je tunachukua hatua Gani wananuru wa eneo Hilo ,

Chukua hatua k**a Danieli ,

NAOMBA kila mmoja apate nafasi ya KUMULIZA Mungu hatia ILIYOMO kwenye eneo unalo ishi,eneo la kazi ,eneo la ibada ,

Unahangaika kutafuta upako kumbe eneo mlilo Jenga kanisa

Ilikuwa NGOME ya wachawi ,ilikuwa madhabahu,je mmeshilikisha Mungu kuziangusha madhabahu ya baali ,bila Mungu hapo usitegemee K**a Kuna mambo ya kiroho yatasogea hapo hakuna,

Ustawi wa uchumi,wa inchi hutegemea wanachi kiwango chako Cha utii juu ya Mungu,hakuna ustawi wa uchumi KIBIBLIA kinyume na utii wa kanuni na Taratibu za kiungu,

Hakuna kulaumi uchumi ,uchumi Ili ustawi kibiblia lazima wananchi wake wafundishwe utii juu ya Mungu na kutoa ,mafanikio mengine kinyume na biblia Mimi hayo hayanihusu,

Nasema Ili jamii ustawi kiuchumi lazima ifundishwe utii juu ya Mungu , ifundishwe kumtolea Mungu ,hakuna mafanikio kinyume na hapo KIBIBLIA,yapo mafanikio au ustawi wa uchumi kinyume na biblia upo ,Mimi nasema ustawi wa uchumi wa inchi kiblia,

Ifike mahali viongozi ,washika nafasi za juu ,tupate wenye hofu ya Mungu,ambao watawafundisha wanachi wao Kuishi maisha ya utii,watawafundisha maisha ya kufanikiwa kiblia,

Wanachi wakifanikiwa ichi imefanikiwa,

Hatukai kwenye nafasi Ili kuombea inchi zetu,tupate viongozi walio kusudiwa ,niwakati wa majira ya uchaguzi sasa Muombe Mungu atupe viongozi alio wakusudia ,

HATIA ya MJI mara nyingi inaweza ikatokana na kiongozi,

Kiongozi anae waongoza inategemea yupo chini ya Mungu yupi?

roho chini ya mungu wa kiongozi alie madarakani ndio zinawaongoza,

AHSANTE Yesu neema ya Mungu imetufunika Tanzania ,Kuna Siri kubwa mno hapo sio SoMo lake Huko,
Kumbukumbu la Torati 32:7
[7]Kumbuka siku za kale,
Tafakari miaka ya vizazi vingi;
Mwulize baba yako, naye atakuonyesha;
Wazee wako, nao watakuambia.

Kuna mambo mengi sana

Naomba tuishie hapo Mungu atusaidie na utuwezeshe Amen
[8/31, 1:08 AM] jongo: KUMSIKIA MUNGU

1 Samweli 3:4-10
[4]basi, wakati huo BWANA akamwita Samweli; naye akasema, Mimi hapa.
[5]Akamwendea Eli kwa haraka, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akasema, Sikukuita; kalale tena. Naye akaenda, akalala tena.
[6]BWANA akaita mara ya pili, Samweli! Samweli! Akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Akajibu, Sikukuita, mwanangu; kalale tena.
[7]Basi Samweli alikuwa hamjui BWANA bado, na neno la BWANA lilikuwa bado halijafunuliwa kwake.
[8]BWANA akamwita Samweli mara ya tatu. Naye akaondoka akamwendea Eli, akasema, Mimi hapa; kwa maana uliniita. Ndipo Eli akatambua ya kuwa BWANA ndiye aliyemwita yule mtoto.
[9]Kwa hivyo Eli akamwambia Samweli, Enenda, kalale; itakuwa, akikuita, utasema, Nena, BWANA; kwa kuwa mtumishi wako anasikia. Basi Samweli akaenda akalala mahali pake.
[10]BWANA akaja, akasimama, akaita vile vile k**a kwanza, Samweli! Samweli! Ndipo Samweli akasema, Nena, BWANA; kwa kuwa mtumishi wako anasikia.

Hapa tunajifunza habari ya samweli juu ya kumsikia Mungu ,

Samweli alikuwa akiitwa na Mungu lakini kiwango chake Cha kumsikia Mungu kilikuwa kidogo ,hakuwa na ufahamu wa kutosha wa kuweza kumsikia Mungu ,

Maandiko yanasema

1 Samweli 3:9
[9]Kwa hivyo Eli akamwambia Samweli, Enenda, kalale; itakuwa, akikuita, utasema, Nena, BWANA; kwa kuwa mtumishi wako anasikia. Basi Samweli akaenda akalala mahali pake.

KUMBE kumsikia Mungu kunafundishika,

Je upo tayari kufundishika? Je umemuomba Mungu akupe Eli wako?

1 Samweli 3:10-11
[10]BWANA akaja, akasimama, akaita vile vile k**a kwanza, Samweli! Samweli! Ndipo Samweli akasema, Nena, BWANA; kwa kuwa mtumishi wako anasikia.
[11]BWANA akamwambia Samweli, Angalia, nitatenda tendo katika Israeli, ambalo kila atakayelisikia masikio yake yatamwasha.

Kiwango chetu Cha ufahamu ni KIZUIZI Cha kumsikia Mungu,

Kiwango chetu Cha ujazo wa neno wa Neno ni KIZUIZI kumsikia Mungu

1 Samweli 3:7
[7]Basi Samweli alikuwa hamjui BWANA bado, na neno la BWANA lilikuwa bado halijafunuliwa kwake.

Tunapaswa tuwe na ujazo wa kutosha wa Neno Ili tumsikie Mungu ,

Ndani ya Neno Kuna uhai na uzima,

Ndani ya Neno Kuna Kweli na Kweli inatuweka huru,

Ndani ya Neno Nuru na Nuru inatuangaza kila tupitapo

Ndani ya Neno Kuna sauti ya Mungu,

Neno la Mungu ni mawazo ya Mungu,

Ndani ya Neno Kuna Maisha ,

Kiwango chako Cha ujazo wa Neno ni sawa na kiwango Chako Cha Mungu Kujifunua kwako,

Hautaweza kumsikia Mungu zaidi ya kiwango chako Cha ujazo wa Neno ,

Neno Ndilo linalo funua Siri za Mungu,

Neno ni mawazo ya Mungu,

Ufahamu wako juu ya Mungu HAKUTAKUWA zaidi ya kiwango Cha ujazo wa Neno ndani Yako ,

Kiwango Cha ujazo wa Neno ndani Yako ni ukuta wa kiwango Cha ufahamu wako,

Kiwango Cha ujazo wa Neno ni kizuizi Cha kumsikia Mungu

Ili uvuke ukuta wa kiwango chako Cha ufahamu lazima kiwango Cha ujazo wa Neno kiongezeke,

Kiwango Cha ujazo wa Neno kikiongezeka ,kiwango Cha ufahamu juu ya Mungu kitaongezeka pamoja na kiwango Cha kumsikia Mungu kitaongezeka ,kwani Neno la Mungu ndani Kuna sauti.

NAWATAKIA USIKU MWEMA

MUNGU AWABARIKI

19/08/2024

*JENGA MAHUSIANO YAKO NA MUNGU ILI SADAKA ZAKO ZIPATE KIBALI*

Mwanzo 4:4
[4]Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. BWANA akamtakabali Habili na sadaka yake;

Hapo tulikuwa tunaangalia sadaka ya Kaini na habili ,sadaka ya habili Ili pata kibali mbele za Mungu,

Kulikuwa na sadaka za aina mbili tofauti,

Kaini alikuwa ni mkulima ,na abili alikuwa mfugaji ,

Maandiko yanasema Kaini alileta mazao sadaka kwa BWANA ,

Habili alileta wanyama wa kwanza na sehemu zilizo Nona sadaka kwa BWANA ,hapo ni sadaka mbili tofauti,inaonekana Kaini hakuzingatia ,nini amtolee Bwana ,

Kaini alileta sadaka k**a kutimiza wajibu,hakutoa k**a anamtolea Mungu ,

Unajua Kuna tofauti ya kutoa na kutimiza wajibu kutoa,

Anamtolea Mungu mandalizi huanzia nyumbani ,anaetimiza wajibu ukifika mda wa kutoa anavuta wallet anangalia mfukoni ILIOPO anatoa,

Nasema unapo panda mbegu ya maharage,

Unapo enda kununua unathamani kubwa kuliko maharage ya kula,

Lakini pia mbegu hio ukifika unaanza kuchambua tena kutoa mbegu zenye mashaka unaziondoa kwenye kundi la kupanda ,

Ukimaliza unayaanika hapo tayari kwa kupanda,

Baada ya hapo unatarajia matokeo mazuri,

Matokeo mazuri ya maharage Yako yalefungwa katika mandalizi mazuri ya mbegu,

Nasema matokeo ya sadaka yamefungwa katika mandalizi mazuri ya nini unatoa,
Usitegemee matokeo mazuri pasipo mandalizi mazuri ya nini unapanda,

Usitegemee matokeo mazuri kwenye eneo la sadaka pasipo maandlizi mazuri ya nini unaemtolea Mungu,

K**a unatoa k**a Kaini usimdai Mungu matokeo ,

Utoaji wenye matokeo lazima uzingztie kanuni za utoaji,

Vingiginevyo utabaki katika eneo moja huwezi kusogea,

Nilitaka tujenge msingi hapo,

Maandiko yanasema Bwana akamtakabali habili+sadaka yake,

KUMBE alimtakabali habili kwanza +sadaka yake,

MSINGI wetu wa SoMo haupo hapo,

Ili sadaka iwe na matokea pamoja na KUZINGATIA kanuni za kutoa k**a tulivyo tizama hapo juu,

Muhusiano ni kitu Muhimu ,

Ukazingatia kuchambua mbegu Yako vizuri utapata matokeo mazuri,ukazingatia kuandaa sadaka Yako vizuri utapata matokeo mazuri

28/06/2024

NDOTO INAYO HUSU NYOKA

Ndoto inayo husu nyoka inatafsiri nyingi ila inahitaji kuto puuza ndani Kuna ujumbe ambao k**a utapuuzia inaweza ikakugharimu,

Kuna shuhuda nilitoa mtu ambae alikuwa anasimamia madhabahu za kishetani namna ambavyo alitaka kuviringishwa na nyoka mwenye vichwa vinne na namna ambavyo Mungu alimshindia kwa kuachilia miale kwenye vichwa vya huyo nyoka ,baada ya hapo akaachiwa na ndio akawa anapata wito wa kutumika kwenye ufalme wa Mungu,

Hapo nyoka amewakilisha ufalme au utawala ambao alikuwa anausimamia ,

Lakini pia Unaweza ukaenda mahali mara nyingi Mungu Huwa hutuonesha utawala wa eneo Hilo kwa picha ya nyoka mkubwa,hio tahadhari Mungu huitoa kuwa mahali ulipo kaa ni penye kiti Cha enzi Cha shetani,

Pia unaweza ukaota pia nyoka amekung'ata hio taarifa ndugu yangu nyoka wa kichawi tayari amekudhuru,
Inawezekana mpaka mwilini akaona alipo kung'ata alama ya me'no ,

Anza kuomba Toba ,Mwaga Damu ya Yesu eneo lililodhulika,ondo sumu iliyo achiliwa,ondoa pando lolote lililo kuwa limepandwa,Kili uzima kwa Damu ya Yesu ,

Warumi 10.10

Funga mlango wowote ambao alipata nafasi kuingia.

Ndoto nyoka ndo anaingia tumboni kupitia mdomo wako ,

Chunguza inawezekana kunaroho ya kishetani unzingiziwa au umeingiziziwa inawezekana kupitia unzchosikiliza ,chunguza umesikia nini,unacho kisikia ni Roho kamili ,Linda sana moyo wako kuliko vyote uvilindavyo

Mithali 4:23
[23]Linda moyo wako kuliko yote uyalindayo;
Maana ndiko zitokako chemchemi za uzima.

Kumbukumbu la Torati 6:6
[6]Na maneno haya ninayokuamuru leo, yatakuwa katika moyo wako;

Kupitia masikio unaweza ukaingiziwa Roho ya udanganyifu,

Chukua hatua ,omba Toba,Ondoa hio Roho katika Jina la Yesu ,Kunywa Damu ya Yesu isafishe hekalu lako la ndani,ondoa madhara yoyote yaliotokea kwa uwepo wa huyo nyoka ndani Yako,ondoa mbegu yoyote iliyo pandwa,omba nguvu ujazo wa Nguvu za Mungu ndani Yako,uwepo wa nyoka ndani ni ishara tosha Kuna upungufu wa Nguvu za Mungu ,omba ujazo ,Ombea masikio yasikie kile chenye faida kwako,Ombea moyo wako Ili Mungu aweke ulinzi na kuifadhi chenye faida tu,

Nyoka kuingia ndani,ni ishara ya adui kuingia kwenye nyumba Yako,ongeza nguvu ya maombi,na funga mlango ambao upo wazi,

Nyoka tayari yupo ndani ,chunguza ndani Yako Kuna adui unae ,unaishi nae ,Muombe Mungu akufunulie na akupe maarifa ya kutoka hapo,

Nyoka dukani,Ombea uchumi wako ,

Nyoka mlango wa nyumba kijijini kwenu ,

Taarifa ya matatizo yanayo kukabili yana uhusiano na madhabahu za nyumbani kwenu ,

Nyoka shambani bado ni ishara ya kuwepo kwa upinzani wa adui kwenye mafanikio Yako,

Ongeza nguvu ya maombi na mahusiano na Mungu ,nikaribieni Mimi shetani nae atawakimbia,

Nyoka kwenye gari unalosafiria,

Safari Yako ya uokovu inakabiliwa na upinza wa adui ,omba Mungu neema yake ikuifunike,

Hivyo Kuna tafsiri nyingi za ndoto inayo husu nyoka hizo ni baadhi tu

Mungu awabariki sana

22/06/2024

NDOTO NA TAFSIRI ZAKE

Tulijaribu kidogo kuangalia kidogo ndoto na tafsiri za ndoto chache naomba tusogee mbele kidogo tena kwa neema ya Mungu ,

1. Ndoto inayo husu Mtihani

➡️ Ni taarifa ya ujio wa msimu mpya ambao unaweza msimu huo usiwe na ufahamu wa kutosha wa msimu huo ,inawezekana ukakupeleka ukafika njia panda,

Omba Mungu akupe maarifa ya kuvuka katika msimu huo mpya

Mara nyingi watu huota mtihani rahisi mda hautoshi ,Omba Mungu akupe uwepesi katika matumizi ya Mda (Time management)tulisha soma

Mtihani mgumu ni ujio wa majira usiyo na ufahamu wa kutosha nayo ,Muombe Mungu akupe Maarifa

2.Ndoto inayo husu kurudi shule ulio ambayo ulisha soma na uk**aliza

Kuna mambo ya nyuma yanaweza yakawa sehemu ya mambo yanayo kumkwamisha (vikwazo kwako)

Muombe Mungu akupe Maarifa ya kutoka hapo ulipo kwama

3 Onaota ndoto unakabidhiwa ufunguo

Ufunguo ni mamlaka wewe unaamua kufunga au kufungua

4.Onaota ndoto upo nyumbani uliko zaliwa

Nyumbani kwenu Kuna sehemu kubwa ya kukwama kwako aidha kiroho au kimwili

Omba Mungu akupe Maarifa namna ya kuvuka hapo

5.Unaota ndoto unashauri watu ,viongozi wa Dini au serikari

Ndani Yako Kuna Roho ya ushauri

Omba Mungu akuongoze kuufikia wito wako zaburi 32.8

6. Ukiota unaimba/unaombea watu

Mungu anatambulisha wito wako ,Muombe Mungu akuongoze kuufikia wito wako sawa na zaburi 32.8

7. Ndoto inayo kuonyesha unavuka maji machafu ,K**a ya ataka 'ukusomba

Huo ni utawala wa Giza,na nguvu zako ni ndogo

Mkaribieni Mungu shetani atawakimbia,
Mtafute Mungu ndio chanzo Cha Nguvu.

8.Kuota ndoto mbwa anakufuatilia,au unaona mbwa

Roho ya uasherati/uzinzi inakufuatilia ambayo inaweza ikakukwamisha safari Yako ya kiroho.

9.unaota unaona nyoka

Huo ni utawala wa Giza ,unafahamishwa mahali ulipo punguza kulala tumia mda huo kuomba.

10. Unaota ndoto unatokewa na ndugu walio kufa

roho ya mizimu inakufuatilia,na ni sehemu ya kikwazo kwa safari yako na Mungu.

Omba Mungu akupe Maarifa kutoka Huko.

Naomba niishie hapo Mungu

22/06/2024

NDOTO NA TAFSIRI ZAKE

NDOTO NA TAFSIRI ZAKE

Tulijaribu kidogo kuangalia kidogo ndoto na tafsiri za ndoto chache naomba tusogee mbele kidogo tena kwa neema ya Mungu ,

1. Ndoto inayo husu Mtihani

➡️ Ni taarifa ya ujio wa msimu mpya ambao unaweza msimu huo usiwe na ufahamu wa kutosha wa msimu huo ,inawezekana ukakupeleka ukafika njia panda,

Omba Mungu akupe maarifa ya kuvuka katika msimu huo mpya

Mara nyingi watu huota mtihani rahisi mda hautoshi ,Omba Mungu akupe uwepesi katika matumizi ya Mda (Time management)tulisha soma

Mtihani mgumu ni ujio wa majira usiyo na ufahamu wa kutosha nayo ,Muombe Mungu akupe Maarifa

2.Ndoto inayo husu kurudi shule ulio ambayo ulisha soma na uk**aliza

Kuna mambo ya nyuma yanaweza yakawa sehemu ya mambo yanayo kumkwamisha (vikwazo kwako)

Muombe Mungu akupe Maarifa ya kutoka hapo ulipo kwama

3 Onaota ndoto unakabidhiwa ufunguo

Ufunguo ni mamlaka wewe unaamua kufunga au kufungua

4.Onaota ndoto upo nyumbani uliko zaliwa

Nyumbani kwenu Kuna sehemu kubwa ya kukwama kwako aidha kiroho au kimwili

Omba Mungu akupe Maarifa namna ya kuvuka hapo

5.Unaota ndoto unashauri watu ,viongozi wa Dini au serikari

Ndani Yako Kuna Roho ya ushauri

Omba Mungu akuongoze kuufikia wito wako zaburi 32.8

6. Ukiota unaimba/unaombea watu

Mungu anatambulisha wito wako ,Muombe Mungu akuongoze kuufikia wito wako sawa na zaburi 32.8

7. Ndoto inayo kuonyesha unavuka maji machafu ,K**a ya ataka 'ukusomba

Huo ni utawala wa Giza,na nguvu zako ni ndogo

Mkaribieni Mungu shetani atawakimbia,
Mtafute Mungu ndio chanzo Cha Nguvu.

8.Kuota ndoto mbwa anakufuatilia,au unaona mbwa

Roho ya uasherati/uzinzi inakufuatilia ambayo inaweza ikakukwamisha safari Yako ya kiroho.

9.unaota unaona nyoka

Huo ni utawala wa Giza ,unafahamishwa mahali ulipo punguza kulala tumia mda huo kuomba.

10. Unaota ndoto unatokewa na ndugu walio kufa

roho ya mizimu inakufuatilia,na ni sehemu ya kikwazo kwa safari yako na Mungu.

Omba Mungu akupe Maarifa kutoka Huko.

16/06/2024

NDOTO INAYO HUSU KUKABIDHIWA FUNGUO

Ndoto inayo husu funguo,ni Mungu anakupa tarifa juu ya kukabidhiwa mamlaka,wewe ndio utakuwa na mamlaka ya kuruhusu au kutokuruhu nani aingie au atoke

30/04/2024

*KUMTEGEMEA MUNGU KATIKA NYAKATI NGUMU*

Ni rahisi sana kumtegemea Mungu nyakati ambazo mambo yote yapo shwari,lakini ni ngumu sana kumtegemea Mungu mambo yakiwa yameharibika,mambo hayaendi,ada inatakiwa,ndani Kuna mgonjwa ,kwenye viko ba unadaiwa ,

Ni mfano tu wa baadhi ya nyakati ambazo unakuta tunapitia ,kuna majira ambayo unaona Mungu k**a hakuoni kabisa ,lakini ukimuliza Mungu mbona mambo yangu yapo hivi anasema naona ,

Isaya 43:2
[2]Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.

Ni rahisi kuhisi Mungu hayupo,hakuoni ,amekuacha lakini wakati mwingi nyakati ngumu hutumika kutuimarisha,au kutufanya kuwa Bora zaidi,

Nyakati ngumu ,ndio wakati Ambao Mungu hukutazama namna unavyo mtegemea,kiwango chako Cha Imani kwa Mungu hupimwa nyakati hizo,

Nyuma ya nyakati ngumu Kuna upako ambao Mungu huachilia kwako baada ya kupita katika Moto au chekeche.

Ukiwatazama watumishi wengi wakubwa saizi wanahudumu kwa upako mkubwa wote ukisoma maisha yao ya hatua ya utumishi wao ,unakuta wote wamepita katika mazingira magumu ambayo ndio yaliyo waimarisha au kuwatengeneza kuwa watu wengine,

Huo ndio utaratibu wa kiroho,mbegu Ili iote lazima ioze ,ikichipua ndio tunarajia kupata matunda Bora zaidi .

Kuna kijana mmoja ni mdogo tu anapatikana eneo linalo itwa Busisya ,kijana huyo saizi ni mganga wa kienyeji,lakini historia yake ya uganga alichukua kamba alijitundika kwenye mti akitaka kujiua baada ya mda wakamuokoa,alicho SEMA mnaniokoa wakati Mimi nachukua uganga?

Mpaka leo mganga wa kienyeji

Ukipata nafasi ya kuwasililiza wachawi mpaka wanafika hatua ya kutusumbua kijijini sio rahisi wengine utasikia nililala ndani ya chupa siku kadhaa,wengine utasikia nilichemshwa ndani ya p**a la maji,wengine walilazimika kufanya hata ambayo ni aibu kuyasema hapa,sasa tunajifunza kuwa Ili uwe bora zaidi lazima upite katika magumu Ili utengenezwe,,magumu ndio yanayo kutengeneza kuwa mtu mwingine,

Mimi sijui unapita,au utapita katika magumu Gani ila ni nyakati ambazo Mungu anakutazama kuliko nyakati nyingine zote ,sio kwamba wakati mwingine hakutazami hapana ,kumbuka upo kwenye mtihani hivyo uangalizi wako ni kipekee kwani kila hatua unayo ichukua hupitishwa katika viwango vya Mungu ,na kupewa maksi.

Ukifanikiwa kuvuka ,kunafaida kubwa sana unapata mbele za Mungu ,kikubwa Mungu hutizama uaminifu wakati wa magumu yako,unaweza usielewe ukaona nyakati za kawaida lakini kumbe upo kupimwa aone k**a unastahili kuliendea jukumu ulilo kusudiwa?

Lakini pia unapo mtegemea Mungu kwenye nyakati ngumu zako uwe na uhakika kuwa kuwa Mungu yupo pamoja nawewe kwani Mungu hataki tupate shida ,hapendi sisi tuwe na maumivu ,anapenda tuishi maisha ya Furaha

3 Yohana 1:2
[2]Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote na kuwa na afya yako, k**a vile roho yako ifanikiwavyo.

Yeye anapenda tufanikiwe ,katika mambo yote hivyo unapo pita amini unapita na Mungu hapo hajakuacha,

Ebu kumbuka Daniel kutupwa katika tundu la Simba nini kilitokea k**a si kufungwa kinywa Simba,

Danieli 6:20-22
[20]Naye alipolikaribia lile tundu, akamlilia Danieli kwa sauti ya huzuni; mfalme akanena; akamwambia Danieli, Ee Danieli, mtumishi wa Mungu aliye hai, je! Mungu wako, unayemtumikia daima, aweza kukuponya na simba hawa?
[21]Ndipo Danieli akamwambia mfalme, Ee mfalme, uishi milele.
[22]Mungu wangu amemtuma malaika wake, naye ameyafumba makanwa ya simba, nao hawakunidhuru; kwa kuwa mbele zake mimi nalionekana kuwa sina hatia; tena, mbele yako, Ee mfalme, sikukosa neno.

Danieli 3:26
[26]Kisha Nebukadreza akaukaribia mdomo wa ile tanuru iliyokuwa inawaka moto. Akanena, akasema, Enyi Shadraka, na Meshaki, na Abednego, watumishi wa Mungu Aliye juu, tokeni, mje huku. Ndipo Shadraka, na Meshaki, na Abednego, wakatoka katika ule moto.

Matendo ya Mitume 16:25-26
[25]Lakini panapo usiku wa manane Paulo na Sila walikuwa wakimwomba Mungu na kumwimbia nyimbo za kumsifu, na wafungwa wengine walikuwa wakiwasikiliza.
[26]Ghafula pakawa tetemeko kuu la nchi, hata misingi ya gereza ikatikisika, na mara hiyo milango ikafunguka, vifungo vya wote vikalegezwa.

Matendo ya Mitume 12:7-8
[7]Mara malaika wa Bwana akasimama karibu naye, nuru ikamulika mle chumbani, akampiga Petro ubavuni, akamwamsha, akisema, Ondoka upesi. Minyororo yake ikamwanguka mikononi.
[8]Malaika akamwambia, Jifunge, kavae viatu vyako. Akafanya hivyo. Kisha akamwambia, Jivike nguo yako, ukanifuate

Nadhani umeona watumishi waliopita kwenye magumu lakini Mungu akajifunua kwao ,mpaka sasa Mungu hujifunua kwetu pale tunapoendelea kumtegemea yeye kwenye magumu yetu ,nakushauri k**a unapita endelea kuwa mwaminifu kuendelea kumtegemea Mungu mpendwa hajakuacha yupo pamoja na wewe endelea kumtumainia yeye.

Yeremia 29:11
[11]Maana nayajua mawazo ninayowawazia ninyi, asema BWANA, ni mawazo ya amani wala si ya mabaya, kuwapa ninyi tumaini siku zenu za mwisho.

Luka 1:37
[37]kwa kuwa hakuna neno lisilowezekana kwa Mungu.

Zaburi 55:22
[22]Umtwike BWANA mzigo wako naye atakutegemeza,
Hatamwacha mwenye haki aondoshwe milele.

Zaburi 56:3
[3]Siku ya hofu yangu nitakutumaini Wewe;

Nimejaribu kutoa mistari ya kutosha ambayo inatuhuisha Pale tulipozimia ,nakutia moyo usithubutu kumuacha Mungu tu kwa sababu jaribu limekulemea endelea kumtegemea Mungu ,hayo unayopitia ni ya mda tu ,Mungu hajakuacha mpendwa ,

Naomba nishie hapo ila nasema endelea kumtegemea Mungu kwenye nyakati ngumu.

MUNGU AWABARIKI SANA.

Karibu kwenye group letu la wasap Ili ukue kiroho

22/04/2024

*BAADHI YA SABABU AMBAZO PEPOKAHABA ZINAMPA UHALALI WA KUWA KING'ANG'ANIZI NDANI YA MTU*

Huyu kahaba sio kazi rahisi mtu kumuachia,mara nyingi sio safari iliyo rahisi ,unakuta unakazana kuomba lakini unakuja changamoto kana kwamba hakuna unacho fanya wanaopitia haya wanakubaliana na Mimi.

Hizi ni baadhi ya sababu zinazo mpa uhalali ,

1.Maisha ya huyu mtu ni kivutio Cha huyu pepo Kuishi nae,

Hii ni sababu kubwa ya huyu pepo kuwa kuwa kazi ngumu kumuondoa ndani ya mtu,hatuna elimu ya kutosha namna ya Kuishi na kuenenda k**a wakristo ,

Wakristo maisha Yetu lazima yawe tofauti na watu wa mataifa bila ivyo Kuna mahali hatuwezi kuvuka ,

Mavazi yetu tunayo vaa yana nafasi kubwa sana kumvuta huyu pepo,kwani kila unacho fanya chini ya jua nyuma yake Kuna Roho inayo kusukuma kufanya hivyo ,hakuna kisicho na Roho ,unavaa nguo fupi jiulize kinacho kusukuma nyuma yake Kuna Roho ipi? Ukijiuliza utapata jibu ,uwe unauhakika Kuna roho ndani Yako ,chunguza vizuri maisha Yako kilavazi mwenendo wako unapenda kuangalia tv vipindi Gani,unavutiwa na tamthiliya Gani,kwenye simu unapenda kuangalia vitu Gani hivyo ndivyo vina nafasi kubwa kumvuta huyu roho kuendelea kumiliki maisha Yako ,ujue hapo haujatoka inahitaji msaada ni ngumu sana kunielewa ila bila kupona hapo huvuki mpendwa,nasisitiza kila ufanyacho nyuma Kuna roho ,chunguza mwenendo wako wote jiulize nyuma Kuna roho gani?

Sasa unamkemea huyu pepo atoke anatazama anakuja wewe mbona bado ni Rafiki kwenye mwenendo wako wa siku zote?

Ili umfukuze mbu wa mararia epukana na madimbwi ya maji ambayo yanaweza kutengeneza mazalia ya mbu ,zui mazalia sio kujifunika neti sio suluhisho mpendwa,

2, Toba ya dhambi hio ya uzinzi baada ya kuokoka mpaka Mungu akukubali.

Ni sentensi ngumu sana kunielewa hio ila naomba Mungu akupe neema ya kuelewa naomba Mimi naeleza kwa sehemu naomba akalithibitishe neno lake kwako zaidi ya hapa nilipo fika kukufungua ufahamu,

Nisema Mungu wetu ni mwenye neema nyingi anatuvumilia sana unajua unaweza ukawa umeokoka sio kwamba ndio Mungu amekukubali hapana,kuokoka ni suala moja na kukubaliwa na Mungu ni suala lingine .

Malaki 3:10
[10]Leteni zaka kamili ghalani, ili kiwemo chakula katika nyumba yangu, mkanijaribu kwa njia hiyo, asema BWANA wa majeshi; mjue k**a sitawafungulia madirisha ya mbinguni, na kuwamwagieni baraka, hata isiwepo nafasi ya kutosha, au la.

Mjaribu uone k**a hatakufungulia madilisha ya Mbinguni ,ok kumbe Kuna watu hawajafunguliwa madilisha ya Mbinguni.

Haya twende turudi kwenye Maada yetu

1 Wakorintho 6:12-13
[12]Vitu vyote ni halali kwangu, lakini si vyote vifaavyo; vitu vyote ni halali kwangu, lakini mimi sitatiwa chini ya uwezo wa kitu cho chote.
[13]Vyakula ni kwa tumbo, na tumbo ni kwa vyakula; lakini Mungu atavitowesha vyote viwili, tumbo na vyakula. Lakini mwili si kwa zinaa, bali ni kwa Bwana, naye Bwana ni kwa mwili.

1 Wakorintho 6:15-16
[15]Je! Hamjui ya kuwa miili yenu ni viungo vya Kristo? Basi nivitwae viungo vya Kristo na kuvifanya viungo vya kahaba? Hasha!
[16]Au hamjui ya kuwa yeye aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja naye? Maana asema, Wale wawili watakuwa mwili mmoja.

Haya itazaame hio sentensi hio aliye ungwa na kahaba ni mwili mmoja nae,Hilo ni agano unakuwa umeingia,unapo funga ndoa Kuna agano lingine ambalo mchungaji anakufunamanisha nalo linasema hao sio wawili tena Bali ni mwili mmoja sasa hili agano Lina kutana na agano la mwanzo aliyeungwa na kahaba ni mwili mmoja nae ,agano la mchungaji linabaki hewani,kwani linamkuta huyu mtu anaagano lingine ambalo ni ALIYE UNGWA NA KAHABA NI MWILI MMOJA NAE ,

Agano la mchungaji linalo Baki hewani ni hili HAWA SI WAWILI TENA NI MWILI MMOJA.hili linabaki hewani ,ni mambo ya ajabu kidogo hata Mimi nilipo kuwa nafundishwa na Mungu hili lilinipa shida sana ,

Agano la kwanza kuliondoa ni hatua lazima uzichukue sio kilahisi tu unasema yakale yamepita sasa yamekuwa mapya,huo ni hatua ya uchanga ,kwa mtu aliye kuwa kiroho Ili Mungu amtumie kwa viwango itakulazimu kupita katika hatua hizi mpendwa,

Muulize Mungu ni eneo Gani ambalo nilikutenda dhambi ambalo mpaka sasa linanikwamisha safari yangu na wewe?kaa katika swali Hilo mpaka uone Matokeo Kuna siku utakuja kushuhudia hapa mpendwa

Wengi baada ya SoMo hili kujifunza na walioingia kufanyia kazi hua wanashuhudia kuwa wameota wanafunga ndoa na waume zao ,kwanini hili linatokea mwanzo bado ndoa Rohoni ila haikufungwa mwilini
Ilifungwa sasa ndo inafungwa baada ya agano la kwanza kuliondoa.

SoMo hili ni la ndani kidogo ni chakula Cha watu wazima hiki ikiwa Mtoto ni ngumu kuelewa hapa.

Sasa k**a Ili eneo halijafanyiwa kazi pepo kahaba ni ngumu kumtoa kwani unauhalali kwako.

Naomba Mungu akusaidie kikufunulia hili.

Naomba tuishie hapa Mungu awabariki k**a hujaelewa niulize inbox au nipigie nikueleweshe,(usiogope) sawa na neema itendayo kazi ndani yangu.

Mungu awabariki sana.

Address

Mbeya

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Nguvu ya Msalaba/Tafsiri ya ndoto kibiblia posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Nguvu ya Msalaba/Tafsiri ya ndoto kibiblia:

Share

Nearby media companies