Kyela Fm Radio

Kyela Fm Radio Kyela Fm Radio Official Facebook Account
96.1 MHZ 📻
Sauti Yako, Mafanikio Yako.

Tuambie Ukweli X-Mass ya mwaka huu Imekukuta Ukiwa Wapi!?
24/12/2024

Tuambie Ukweli X-Mass ya mwaka huu Imekukuta Ukiwa Wapi!?


Jeshi la Polisi Nchini limetoa onyo na kupiga marufuku maandamano yaliyotangazwa na Viongozi wa CHADEMA September 23,202...
13/09/2024

Jeshi la Polisi Nchini limetoa onyo na kupiga marufuku maandamano yaliyotangazwa na Viongozi wa CHADEMA September 23,2024 na kusema Mtu yeyote atakayeingia barabarani atakabiliwa vilivyo kwa mujibu wa sheria za Nchi.

Akiongea Mjini Moshi leo September 13,2024, Msemaji wa Polisi, David Misime amesema “September 11,2024 kupitia Vyombo vya Habari na Mitandao ya Kijamii walisikika Viongozi wa CHADEMA akiwemo Mwenvyekiti wa Chama hicho (Freeman Mbowe), akiwahamasisha Viongozi wa Dar es salaam kuingia barabarani kuanzia September 23,2024, Viongozi hao waliendelea kuhamasisha Wananchi wa Kanda mbalimbali Nchini kukutana Dar es salaam ili kuungana na Wakazi wa Dar es salaam kuingia barabarani”

“Hatua hiyo waliyofikia tunajiuliza na tunaendelea kufuatilia na kuchunguza kwanini wanataka kututoa kwenye reli ya hatua za kiupelelezi zinazoendelea baada ya Rais Samia kuviagiza Vyombo vya Uchunguzi vifanye uchungizi kisha wawasilishe uchunguzi kwake”

“Ikumbukwe mara kadhaa Viongozi na Wafuasi wa Chama hicho wamekuwa wakipanga, kuratibu mikakati mbalimbali na kutoa matamshi yenye lengo la kuleta vurugu Nchini ili kuharibu amani ya Nchi yetu kwasababu wanazozijua wenyewe”

“Jeshi la Polisi linatoa onyo kwa Viongozi wa Chama hicho kuacha kuendelea kuhamasisha Wananchi kujihusisha katika uhalifu huo na yoyote atakayeingia barabarani atakabiliwa vilivyo kwa mujibu wa sheria za Nchi, kwa maana hiyo maandamano hayo yamepigwa marufuku, naomba kurudia kwa maana hiyo maandamano hayo yamepigwa marufuku”

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema vitendo vya utekaji na mauaji vinavyoendelea nch...
13/09/2024

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema vitendo vya utekaji na mauaji vinavyoendelea nchini havikubaliki na yeyote na kuongeza kuwa vitendo hivyo vinafanywa na watu aliowaita ‘genge’ la wasioitakia mema nchi.

Dkt. Nchimbi amesema kutokana na hilo, CCM na vyama vya upinzani vinapaswa kuungana pamoja kupinga vitendo hivyo.
"...tunao wajibu mkubwa sana wa kuhakikisha kwamba tunaacha kunyoosheana vidole tunahakikisha kwamba uchunguzi wa kweli na wa kina unafanyika..."Emmanuel Nchimbi - Katibu Mkuu CCM

Idadi ya vifo hadi sasa nchini Vietnam vimefikia watu 152, maelfu ya watu wamehama kutoka makazi yao ya jiji, Wilaya 10 ...
13/09/2024

Idadi ya vifo hadi sasa nchini Vietnam vimefikia watu 152, maelfu ya watu wamehama kutoka makazi yao ya jiji, Wilaya 10 kati ya 30 ziko kwenye tahadhari ya mafuriko, vyombo vya habari vya serikali nchini Vietnam vimeripoti.

“Kuanzia Jumatatu [Septemba 23] sisi tutaingia barabarani kudai tunachoona ni uhai wa watu wetu waliopotezwa, vinginevyo...
13/09/2024

“Kuanzia Jumatatu [Septemba 23] sisi tutaingia barabarani kudai tunachoona ni uhai wa watu wetu waliopotezwa, vinginevyo serikali imechukua hatua za haraka na za makusudi kuwarejesha, watu kujiuzulu, na watu wote kuwajibika.” - Freeman Mbowe, Mwenyekiti CHADEMA

LATRA imesitisha Leseni ya kusafirisha abiria kwa kampuni ya mabasi ya KATARAMA Luxury kutokana na kuchezea kifaa cha ku...
13/09/2024

LATRA imesitisha Leseni ya kusafirisha abiria kwa kampuni ya mabasi ya KATARAMA Luxury kutokana na kuchezea kifaa cha kufuatilia mwenendo wa magari (VTD) kwa kuondoa kifaa kilichofungwa katika mabasi yake na kufunga kifaa kingine kilichosababisha utumaji wa taarifa potofu katika mfumo wa VTS.

Kosa hilo, lilibainika baada ya wataalamu kufanya uchunguzi na kubaini kuwa kosa hilo haliwezi kuvumilika na linahitaji uchunguzi Zaidi kufanyika na watuhumiwa kufikishwa Mahakamani kwa mujibu wa sheria.

Kampuni ya Katarama imekuwa ikiendelea na makosa hayo hata baada ya kusitishiwa leseni na kurejeshewa kwa mara kadhaa.

Kufuatia kikao hicho, Mamlaka imetoa onyo kali kwa makampuni ya usafirishaji ya ABOOD Bus Service, BM Coach na SUPER FEO na kuwataka wazingatie Sheria, Kanuni na taratibu zilizowekwa.

Kikao hicho kimefanyika Ofisi ya LATRA Dar es Salaam, Septemba na kuhudhuriwa wadau mbalimbali wakiwemo Chama cha wamiliki wa mabasi Tanzania (TABOA), Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, pamoja na Wamiliki na Wawakilishi wa Makampuni hayo.

Kilio na simanzi Vimetawala katika msiba wa mtoto Ufunuo Mwamlima aliyekuwa Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule...
13/09/2024

Kilio na simanzi Vimetawala katika msiba wa mtoto Ufunuo Mwamlima aliyekuwa Mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Mpakani A iliyopo Halmashauri ya Mji Tunduma Mkoani Songwe ambaye amefariki baada ya kujichoma na kisu tumboni usiku wa kuamkia septemba 10 nyumbani kwao Mtaa wa Chapwa A.

Baba mkubwa wa Marehemu Fadhiri Mwamlima akizungumza kwa niaba ya Familia amesema kuwa usiku wa septemba 10 ,2024 wazazi walimuita kijana wao kumhoji juu ya matukio ya wizi wa hela kwenye kibanda chao ndipo kijana alikiri kuwa na chenji alizodai anaenda kuzichukua ili awaletee na baadaye walisikia kelele kutoka jikoni ambapo walipotoka walikuta kijana huyo amejichoma kisu na utumbo uko nje na alifariki wakati wakiwa njiani wakimpeleka hospitali kwaajili ya Matibabu.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Chapwa A Steven Minga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku Diwani wa kata hiyo Chapwa A, Amos Siame ametoa rai kwa wazazi na walezi kuendelea kuwa karibu na watoto wao ikiwemo kuwazuia kuangalia filamu ambazo zina maudhui ya kujiua ili kuwaondoa na dhana ya kufanya hivyo.

Mkuu wa jeshi la polisi nchi |GP Camillius Wambura amesema hali ya nchini ni shwari kutokana na umahiri wa jeshi la poli...
13/09/2024

Mkuu wa jeshi la polisi nchi |GP Camillius Wambura amesema hali ya nchini ni shwari kutokana na umahiri wa jeshi la polisi katika kupambana na uhalifu kwa kushirikiana na raia wema.

Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa maofisa wakuu waandamizi wa jeshi la polisi uliofanyika katika shule ya polisi Moshi wenye lengo la kujadili na kutathmini mikakati ya jeshi hilo.

Kwa upande wake naibu waziri wa mambo ya ndani, Daniel Sillo amelipongeza jeshi la polisi kwa kulinda na kuhakikisha amani inaendelea kuimarika, huku akiwataka waendelee kuwa karibu na jamii katika kupata ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao.

Catch the one  live ndani ya mjengo tukitambulisha ngoma yake mpya inayoitwa   em jerry rebiam
12/09/2024

Catch the one live ndani ya mjengo tukitambulisha ngoma yake mpya inayoitwa


em jerry rebiam


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 11,2024 amemuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano ...
11/09/2024

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 11,2024 amemuwakilisha Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Nane wa Mawaziri wa Umoja wa Nchi za Afrika, Karibian na Pasifiki (OACPS) wanaohusika na masuala ya Uvuvi, Bahari, Maziwa na Mito, kwenye Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Malengo ya mkutano huo ni kuimarisha utekelezaji wa Makubaliano yaliyofikiwa, kuimarisha utekelezaji wa vipaumbele vya kimkakati vya umoja,kubadilishana uzoefu, kuweka mikakati ya pamoja na kuimarisha ushirikiano na washirika ili kuboresha usimamizi wa bahari, uchumi wa buluu, na maendeleo endelevu ya uvuvi.

Aidha, Mkutano huo unatarajiwa kutoa mwongozo wa kimkakati kwenye vikao vya juu vya maamuzi vya Umoja wa Nchi za Afrika, Karibian na Pasifiki ili kuboresha usimamizi wa bahari, uvuvi na ufugaji wa samaki endelevu.

Wagombea wa nafasi ya Urais wa Marekani Kamala Harris (Democrat) na Donald Trump (Republican) wamekabiliana vikali katik...
11/09/2024

Wagombea wa nafasi ya Urais wa Marekani Kamala Harris (Democrat) na Donald Trump (Republican) wamekabiliana vikali katika mdahalo wa Urais uliofanyika nchini Marekani leo, Jumatano Septemba 11.2024

Wagombea hao wawili (2) wameonekana wakishutumiana kwa kila mmoja wao kusema uwongo katika masuala kadhaa ya msingi, kwa mfano katika suala la uchumi Makamu wa Rais wa sasa wa Marekani Kamala Harris ambaye pia ni mgombea wa chama cha Democrat amejibu kwa kumshambulia Trump akielekeza lawama kwa utawala wake wakati alipoongoza Taifa hilo

“Donald Trump alituacha na ukosefu mbaya Zaidi wa ajira tangu kutokea kwa mdororo mkubwa wa kiuchumi nchini Marekani, tulichofanya ni kusafisha uchafu wa Donald Trump" -Harris

Kwa upande wake Trump amejibu tuhuma hizo kwa kusema kuwa Maprofesa wa uchumi wameuchukuliwa mpango wake wa kiuchumi kuwa ‘wa kipekee’ na ‘mzuri Zaidi’, huku katika suala la uhamiaji Trump ametoa madai yasiyo na msingi kwamba wahamiaji wanakula wanyama katika eneo la Springfield, Ohio, "wanakula mbwa, wanakula wanyama wa nyumbani wa watu wanaoishi huko"

Taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa shirika la habari la kimataifa la Uingereza (BBC) baada ya kukamilika kwa mdahalo huo imesema muongozaji wa mdahalo huo David Muir amebainisha kuwa Meneja wa jiji la Springfield amekanusha madai hayo kwa kueleza kuwa hakuna ushahidi wa dai hilo.

Watu 26 wamefariki dunia, baada ya mashua iliyokuwa imebeba wahamiaji kupinduka katika Pwani ya Senegal, ambapo zaidi ya...
11/09/2024

Watu 26 wamefariki dunia, baada ya mashua iliyokuwa imebeba wahamiaji kupinduka katika Pwani ya Senegal, ambapo zaidi ya watu 100 walikuwa kwenye mashua hiyo ya mbao, wakati ilipozama kilomita 4 tu tangu kuanza safari yake.

Mpaka sasa watu wanne wameokolewa na juhudi za kuwatafuta wale ambao hawajulikani walipo bado zinaendelea.

Inaelezwa kuwa vijana wengi wanaokimbia migogoro, umaskini, na ukosefu wa ajira, wanajaribu njia hatari ya Atlantiki kuelekea Visiwa vya Uhispania, huku karibu watu 30,000 wakirekodiwa kufika eneo hilo mwaka huu.

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Hamad Masauni ameliagiza jeshi la polisi nchini kuendelea kulinda kiapo chake kwa kufan...
11/09/2024

Waziri wa mambo ya ndani ya nchi Hamad Masauni ameliagiza jeshi la polisi nchini kuendelea kulinda kiapo chake kwa kufanya kazi kwa weledi huku wakiishi falsafa ya Rais Samia Suluhu Hassan ya Maridhiano,Mabadiliko, Ustahimilivu na Kujenga Upya.

Waziri Masauni ametoa kauli hiyo wilayani Lushoto Mkoani Tanga wakati akifungua kituo kipya cha polisi kilichojengwa na serikali kwa gharama ya zaidi ya shilingi Milioni 400.

Amesema moja kati ya kazi kubwa za jeshi la polisi ni kulinda usalama wa raia na mali zao,hivyo kufanya kazi kwa weledi na kuwa karibu na wananchi kutaifanya jamii iendelea kuongeza ushirikiano.

Nao baadhi ya wananchi wa eneo hilo wamesema wana imani kubwa na jeshi la polisi na wako tayari kuliunga mkono pindi watakapowahitaji kwa maslahi mapana ya Taifa.

Leo kwenye   tunawaza kwa pamoja alafu tuna pata majibu kwa pamoja pia,Upewe mpenzi mwaminifu au elfu tano mpaka decembe...
11/09/2024

Leo kwenye tunawaza kwa pamoja alafu tuna pata majibu kwa pamoja pia,Upewe mpenzi mwaminifu au elfu tano mpaka december..? tusanue kwenye comment hapo chini alafu

AfternoonBeat Gang watapita nayo live kwenye code za 96.1


em jerry rebiam


gang

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa, amesema suala la uhifadhi wa mazingira liwe ajenda ya Kitaifa na jukumu la kila mmoja k...
11/09/2024

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa, amesema suala la uhifadhi wa mazingira liwe ajenda ya Kitaifa na jukumu la kila mmoja kuanzia ngazi ya familia mpaka Taifa.

"Na tunapokwenda kuhifadhi mazingira lazima tuanze na ngazi ya familia na tunapopanda juu tupanue wigo hadi kwa wadau mbalimbali.

Viongozi wa dini mnayo nafasi kubwa na hii lazima iwe ajenda maalum, iwe ni ofisi za umma, za binafsi au kwenye taasisi"-Mhe.Majaliwa Ametoa kauli hiyo, wakati akifunga mkutano maalum wa viongozi na wadau wa mazingira ulioitishwa ili kujadili mwenendo wa mazingira nchini. Mkutano huo ulifanyika kwenye Kituo cha Mikutano cha Jakaya Kikwete, jijini Dodoma.

Amesema kitendo hicho kitakuwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan za kuendelea kuimarisha uhifadhi na Usimamizi wa mazingira nchini, kazi aliyoifanya kwa weledi, ustadi na mafanikio tangu akiwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Usiku wa kuamkia Jumatano, hali ya taharuki ilitokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) jijini ...
11/09/2024

Usiku wa kuamkia Jumatano, hali ya taharuki ilitokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta (JKIA) jijini Nairobi baada ya wafanyakazi kuanza mgomo kupinga mpango wa Serikali wa kukabidhi usimamizi wa uwanja huo kwa kampuni ya India, Adani Group, Citizen Digital imeripoti.

Mgomo huo ulianza rasmi saa sita usiku, kwa mujibu wa taarifa kutoka Chama cha Wafanyakazi wa Usafiri wa Anga wa Kenya.

Taarifa za awali zilieleza kuwa shughuli za uwanja huo zilisimama kabisa, huku menejimenti ya uwanja huo ikijiandaa kutoa tamko rasmi kuhusu hali hiyo. Picha zilizotolewa kwenye mitandao ya kijamii zilionesha abiria wakihangaika kupata mizigo yao kutokana na mgomo huo.

Mpango wa kukodisha uwanja huo kwa miaka 30 kwa kampuni ya Adani Group ya India, kwa malipo ya uwekezaji wa dola bilioni 1.85, umeibua hasira kubwa nchini Kenya. Wapinzani wa mpango huo wanasema kuwa utafanya wafanyakazi wa ndani kupoteza ajira na kuwanyima Wakenya faida za kiuchumi za uwanja huo katika siku za usoni.

Kwa mujibu wa takwimu, uwanja wa JKIA unachangia zaidi ya asilimia tano ya Pato la Taifa (GDP) la Kenya kupitia ada za mizigo na abiria. Hata hivyo, serikali ya Kenya imejitetea ikisema kuwa mkataba huo ni muhimu ili kuboresha miundombinu ya uwanja huo, ikiwamo kuongeza njia ya pili ya kuruka na kuimarisha sehemu ya abiria.

Hivi karibuni, Jumuiya ya Mawakili wa Kenya na Tume ya Haki za Binadamu ya Kenya ziliwasilisha kesi mahakamani kupinga mpango huo, zikidai kuwa haufuati uwazi. Mahakama Kuu ilikubali kuzuia utekelezaji wa mkataba huo hadi kesi itakaposikilizwa.

Kipaza wamepewa wenye haki Yao isikilize Kyela FM Radio Maelezo ya Moja kwa Moja Timu ya Taifa ya Tanzania  Dhidi ya Gui...
10/09/2024

Kipaza wamepewa wenye haki Yao isikilize Kyela FM Radio Maelezo ya Moja kwa Moja Timu ya Taifa ya Tanzania Dhidi ya Guinea.

Tuambie utabiri Wako hapa hii Mechi inaishaje?

Address

Kyela
Mbeya
600

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kyela Fm Radio posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Kyela Fm Radio:

Videos

Share