16/05/2024
PART 1
Chimbuko/historia ya tahajudi:
Neno tahajudi limetokana na neno la kiingereza linaloitwa 'meditation' likiwa na maana ya kufikiri kwa uzingativu au kwa kujali. Neno meditation, nalo limetokana na neno la kilatini linaloitwa 'meditatio' likiwa na maana ya mazoezi ya mwili na akili.
Asili ya tahajudi ni dini za mashariki. Ilianzia huko Asia zaidi ya miaka 5,000 iliyopita. Kwa sasa tahajudi hufanywa zaidi huko magharibi (Ulaya na Marekani).
Tahajudi ya miaka hii (ya wakati huu), inazungumzia zaidi tahajudi ya kiyoga ambayo asili yake ni huko India.
Kwa ujumla, tahajudi inaelezwa k**a njia za uzingativu katika jambo ambalo mawazo yamelinuia. Lakini pia inaweza kuelezwa k**a ifuatavyo:
=> Ni hali ya uzingativu na utulivu katika hali halisi ya wakati wa sasa hivi.
=> Ni ile hali wakati mawazo yanapokuwa yameyeyushwa na kufikia mahali ambapo hakuna fikra yenye kuingia tena.
=> Ni ile hali ambayo, uzingativu, kwa makusudi kabisa umeachwa kuelekea kwenye nguvu kubwa zaidi ( Mungu? Nguvu kuu? ).
=> Ni ile hali ya kuweka mawazo na uzingativu katika kitu kimoja, mfano- sanamu ya kidini, pumzi au neno fulani unalotamka (mantra).
=> Wengine wanaielezea tahajudi kwamba, ni sala za usiku wa manane.
CouplePraying.jpg
Tahajudi na dini:
Kila dini ina aina yake ya uzingativu, ingawa ukiutazama kwa undani utagundua kwamba ni tahajudi halisi.
Dini ya kikristo wanatumia rozari, hii huwasaidia kujenga uzingativu. Waislamu wanatumia tasbihi ambayo huwasaidia kujenga uzingativu, lakini pia huwa wanakuwa na sala za usiku wa manane (tahajudi). Wabudha huwa wanafanya tahajudi kila siku kwani ndiyo nguzo yao kuu. Wabahai, hufanya tahajudi kila baada ya sala.
Faida za tahajudi:
Ili uweze kutambua faida za tahajudi, ni muhimu kuifanya kila siku, ikiwezekana asubuhi na jioni. Tahajudi ina faida nyingi sana, faida hizi utaziona tu k**a utafanya tahajudi kila siku. Hivyo, tahajudi inahitaji nguvu kubwa sana ya kujituma (wheel power). Ina faida kubwa sana, hivyo ni vizuri ukajenga mazoea ya kuifanya kila siku. Nakushauri, k**a huwezi kufanya tahajudi, basi ni afadhali ujifunze upendo ingawa, ni rahisi mara kumi kufanya tahajudi kuliko kuwa na upendo. baadhi ya faida hizo ni k**a ifuatavyo:
1. Husaidia kuongeza ubora wetu kiakili, kimwili pamoja na uwezo wetu kwa ujumla. Husaidia kuuburudisha mwili, pia husaidia kupumzisha akili na mwili.
2. Husaidia kujenga uzingativu na kukuwezesha kumudu kupata suluhu ya matatizo kirahisi.
3. Husaidia kuratibu msukumo wa damu pamoja na usafirishwaji wa damu mwilini.
4. Husaidia pumzi pamoja na kurahisisha usagwaji wa chakula mwilini.
5. Husaidia kuimarisha mfumo wa kinga mwilini.
6. Husaidia kuleta furaha ya nafsi.
7. Husaidia kuimarisha nguvu yako ya machale pamoja na nguvu zako za ziada.
8. Husaidia kutibu matatizo mengi ya kisaikolojia kwani hubadili hali ya mfumo wa fahamu na mawazo (endapo itafanywa kila siku).
9. tahajudi pia inaweza kutumika kuomba kitu unachohitaji, k**a vile kazi au mahitaji mbalimbali, ingawa inashauriwa uwe mwangalifu badala ya kufanya kazi unaweza ukawa mtegemezi wa tahajudi. Mfano, unaweza ukatumia tahajudi kuomba shilingi laki moja na ukapata bila kufanya kazi yoyote au kwa kufanya kazi kidogo sana ambayo hailingani na malipo ya laki moja.
Je, tahajudi huleta utajiri?
Ni swali gumu kwa sababu, utajiri ni dhana pana sana, inategemea tu unazungumzia utajiri upi, wa kitu gani na wapi. Hata ule utajiri wa kimazoea, nao bado ni mgumu kuuelezea. Mfano, tajiri wa kijijini, akihamia mjini anaonekana ni mtu wa kawaida kabisa kwani kuna matajiri wengi sana wanaomzidi.
Lakini, swali la kujiuliza ni hili, unataka utajiri ili iweje au upate nini? K**a unataka utajiri ili uwe maarufu kwa kuandikwa na magazeti, ukweli ni kwamba, kuna uwezekano mkubwa wa wewe kuandikwa na magazeti ingawa siyo kwa utajiri ila kwa kubaka mtoto. Lakini pia k**a unataka utajiri ili ukupe furaha na amani, ukweli utabaki palepale kwamba, hata k**a utaupata huo utajiri, furaha au amani haitapatikana kwani utakuwa umevunja kanuni ya maisha kwani hukuja duniani kutafuta utajiri, bali kuishi kwa kufanya kazi unayoipenda sana, inayokupa furaha na amani bila kujali maslahi, heshima au umaarufu kutoka kwenye kazi hiyo.
Kwakuwa kazi hii unaipenda, utaifanya kwa ufanisi mkubwa sana, na ndipo utajiri utakapokuja. Kanuni ya maisha kuhusu utajiri inaanza na kufanya kazi inayokupa furaha na amani na ndipo utajiri unafuata, haianzi na utajiri na ndipo furaha na amani vipatikane. K**a huamini, wachunguze matajiri unaowafahamu, ambao walipata utajiri ili uwape furaha na amani, utagundua kwamba, hawana furaha wala amani. Kwa upande wa pili wa shilingi, wale matajiri ambao, utajiri wao ulikuja kupitia kwa kufanya kazi inayowapa furaha na amani, utagundua kwamba wana furaha na amani kubwa sana.
Swali lililoulizwa hapo juu linasema, je, tahajudi huleta utajiri? K**a utajiri ni kupata furaha na amani ya nafsi, jibu ni ndiyo. Hii ni kwa sababu, tahajudi hukusaidia au kukufundisha namna bora kabisa ya kupumzisha akili na mwili na hivyo kuwa mtu mwenye furaha na amani. Kumbuka, ukishakuwa mwenye furaha na amani, wewe tayari ni tajiri wa mali pia.
Tahajudi ina madhara yoyote?
Kwa watu wenye matatizo ya kifafa, matatizo makubwa ya moyo au wenye matatizo ya akili, tahajudi inaweza kuwaumiza wasipokuwa waangalifu, ingawa kwa upande mwingine, tahajudi ni tiba/dawa kwao. Hivyo, wanashauriwa wachague tahajudi ambayo haitawaletea matatizo.
Ni vizuri wakajaribu aina tofauti tofauti ya tahajudi, halafu wakaangalia ni ipi inawasumbua na ni ipi inawapa nafuu. Wakishapata inayowapa nafuu, ni vizuri wakaendelea kuifanya mara kwa mara. Baada ya muda, watagundua kwamba, matatizo yao ya akili, moyo au kifafa yamepungua kwa kiwango kikubwa sana au yameisha kabisa.
meditation-techniques.jpg
Jinsi ya kufanya tahajudi:
Mbinu za kufanya tahajudi hutofautiana kutokana na kiwango cha uzingativu, uwezo wa kujenga taswira na namna mtu anavyoweza kukabili mawazo yanayomwingilia wakati anafanya tahajudi yake.
Baadhi ya mbinu hizi, humfanya mtu apotelee kwenye kile anachozingatia na kutoingiliwa kabisa na wazo lolote. Mbinu hizi ni rahisi mtu kujifunza mwenyewe, ingawa kuna baadhi zinahitaji awepo mwongozaji.
Hatua zinazotakiwa wakati unajiandaa kufanya tahajudi ni k**a ifuatavyo:
1. Tafuta sehemu iliyotulia, isiyo na makelele. Kaa kwenye kiti au chini, au lala kitandani. Hakikisha huumii mahali popote. Legeza mwili wako pamoja na misuli yote ya mwili wako kwa kadri utakavyoweza.
2. Sahau matatizo yako yaliyopita, yaliyopo na yajayo. Sahau matatizo yako ya kazini au nyumbani. Jitahidi usifikirie chochote. k**a kuna mawazo yataingia, usigombane nayo, usiyape muda na nafasi, wewe endelea na kile ulichoamua kukizingatia. Hakikisha uzingativu wako ni mkubwa. Pia kione hicho unachokizingatia kwa jicho lako la ndani, kijengee taswira kana kwamba unacho tayari au kana kwamba unakiona (unacho).
3. Ni muhimu sana kujali hisia zako wakati unafanya tahajudi. Kwa mfano, k**a unafanya tahajudi ya kujenga nyumba. Hakikisha hiyo nyumba unaiona ilivyo, ingia ndani ya hiyo nyumba, sebuleni, chumbani, chooni, stoo, jikoni na sehemu ya kulia chakula (dining). Kila unapoingia, onyesha hisia zako, jione una furaha ndani mwako na ikiwezekana tabasamu, pia jione una amani ndani mwako. Ukweli ni kwamba, utakapokuja kujenga hiyo nyumba, zile hisia ulizokuwa unazionyesha wakati unafanya tahajudi, zitajitokeza au utaziona. K**a tahajudi yako ulikuwa unaifanya ukiwa na huzuni, hali hiyo itajitokeza baada ya kumaliza kujenga nyumba yako. Inaweza ikatokea baada tu ya kujenga nyumba yako, ndugu zako au wa mkeo wakajaa pale nyumbani, wakawa wanafanya vurugu ambazo zitakuletea huzuni na hivyo kuanza kujuta ni kwa nini umejenga hiyo nyumba.
Ukweli ni kwamba, tatizo siyo ndugu, tatizo ni wewe mwenyewe, ni hisia zako ulizokuwa unazionyesha wakati unafanya tahajudi yako ya kujenga nyumba. Na k**a wakati unafanya tahajudi yako ulikuwa na hisia za furaha, hali hiyo pia itajitokeza baada ya kumaliza nyumba yako. Hata k**a ndugu wa mkeo au mumeo watajaa pale nyumbani, vicheko, tabasamu na mambo mengine ambayo yatakupa furaha yatatamalaki pale nyumbani. Kwa hiyo, hisia ni muhimu sana wakati unafanya tahajudi.
4. Pumua kwa kuingiza pumzi ya kutosha mapafuni, halafu toa pumzi yote na kufanya kifua kiwe k**a kitupu. Weka mawazo yako yote kwenye pumzi zako. Vuta pumzi kwa kina kiasi ili oksijeni iingie nyingi zaidi. Unapotoa pumzi unafanya msuli wa mapafu kujisafisha bila kukwazwa. Ni muhimu kuvuta na kutoa pumzi kwa kina angalau mara tatu kabla ya kuanza kufanya tahajudi yoyote.
5. Kila siku asubuhi baada tu ya kuamka na jioni au usiku baada ya watu wote kulala (au usiku wa manane), tenga dakika kumi na tano au zaidi kwa ajili ya kufanya tahajudi. Kuna wakati utakuta mwili hautaki, lakini jenga utashi mkubwa zaidi ya mwili hadi uzoee. Ukiahidiwa safari ya bure ya kwenda ulaya kutembea na ukaambiwa ndege itaondoka saa kumi usiku, nina uhakika ikifika saa saba utakuwa macho au yamkini unaweza usilale kabisa. Lakini pia ikitokea ukaahidiwa kutiwa au kumtia kila siku saa nane mchana na umpendaye sana, nina uhakika utafika kwenye eneo saa sita au saa saba mchana, hata chakula hutakumbuka. Ninakuomba ujenge utashi wa aina hii kwenye tahajudi.
6. Ukipata muda, k**a huna kazi ya kufanya, ukiwa peke yako, ofisini, nyumbani, kwenye basi/daladala, kituoni, jaribu kufanya tahajudi. Mazoezi ya tahajudi hufanyika mahali popote.
7. k**a ukifanya vizuri tahajudi, utahisi nafuu fulani kimwili au kiakili ama vyote. Utagundua kwamba, mwili hasa upande wa msukumo wa damu, utakuwa na mabadiliko.
INAENDELEA...