Meridian Sport

Meridian Sport Ukurasa wako namba moja wa habari za michezo Tanzania na kimataifa!

DROO YA CAF CL & CAFCL NI LEOKwa mujibu wa mfumo wa CAF kwenye klabu bingwa Afrika kupanga mechi za awali wana jumla ya ...
11/07/2024

DROO YA CAF CL & CAFCL NI LEO

Kwa mujibu wa mfumo wa CAF kwenye klabu bingwa Afrika kupanga mechi za awali wana jumla ya makundi matatu, ambapo kuna timu tano ambazo hazitocheza hatua ya awali ( Preliminary) timu hizo ni Al Ahly, Esperance, Mamelodi, Petro na TP Mazembe.

Kisha kuna timu nne (4) ambazo zinatambuliwa k**a HIGHEST RANKED yaani ziko na alama nyingi kwenye mfumo wa CAF ambazo timu hizo ni YANGA 🇹🇿, Pyramids, Raja na CR Belouzdad.

Kiufundi ukichukua hizo timu tano za juu kisha ukijumlisha na hizo nne basi unaenda kupata jibu ya timu bora Afrika kwa mujibu wa CAF kwenye klabu bingwa Afrika, Premier Club Competitions.

Lakini bado Yanga ataanzia hatua za awali sambamba na hao wenzake watatu, ni timu tano tu hazitoanzia hatua za awali.

Kwa upande wa Kombe la Shirikisho timu ambazo hazitaanzia hatua ya awali zipo 12 ambazo ni;

SIMBA SC- Tanzania
RS BERKANE- Morocco
FC LUPOPO- DR Congo
STADE MALIEN- Mali
ENYIMBA FC-Nigeria
ASEC MIMOSAS- Ivory Coast
ZAMALEK SC- Misri
USM Alger- Algeria
AS Vita- DR Congo
SHEKUKHUNE FC- Zambia
EL MASRY- Misri
CS Sfaxien- Tunisia

KMC FC wako mbele kwa bao dhidi ya Singida Big Star, bao limefungwa na Mao
16/05/2024

KMC FC wako mbele kwa bao dhidi ya Singida Big Star, bao limefungwa na Mao

06/04/2024

MOKOENA AUKUBALI MOTO WA AZIZI KI

Kiungo mshambuliaji wa Mamelodi Sundowns Teboho Mokoena akoshwa na uwezo aliouonesha Stephen Aziz Ki kwenye michezo yote miwili.

Katika mchezo wa pili wa robo fainali fainali Azizi Ki alikuwa ni mwiba mchungu kwa Masandawana, hadi kupelekea kufunga bao lililozua utata na kukataliwa na mwamuzi kwa kigezo cha kwamba mpira haukuingia wote langoni.

"Nafikiri wapo vizuri safu ya ulinzi hata kwenye kushambulia, yule namba kumi wao Azizi Ki alicheza vizuri sana leo"- Teboho Mokoena

Credit:

UZOEFU WAMYIMA KAZI ARTETA BARCARais wa Barcelona Joan Laporta ameweka wazi anatamani Xavi aendelee kuwa madarakani kwa ...
28/03/2024

UZOEFU WAMYIMA KAZI ARTETA BARCA

Rais wa Barcelona Joan Laporta ameweka wazi anatamani Xavi aendelee kuwa madarakani kwa msimu ujao.

"Nimemfanya iwe wazi kwake kwamba ningependa aendelee, lakini naelewa shinikizo alopata," Laporta aliiambia Mundo Deportivo wiki iliyopita.

"Niliuliza ikiwa kulikuwa na nafasi ya yeye kubadili mawazo yake, lakini niliona shinikizo usoni mwake. Nilimwambia aelewe na asijisikie kushinikizwa. Amesema atajiuzulu mwishoni mwa msimu k**a ilivyopangwa, lakini tutaona. Tusitie mkazo kwa sasa kwa sababu mambo yanakwenda vizuri."

Barcelona wamepunguza orodha yao fupi ya wagombea wa kumrithi Xavi kuwa ni pamoja na Luis Enrique, Hansi Flick, na Rafa Marquez.

Inadaiwa kwamba uongozi wa Barcelona una pingamizi dhidi ya kumchukua Arteta kwa sababu bado ana mkataba na Arsenal hadi 2025 na uzoefu wake mdogo unamwathiri.

Credit:

28/03/2024

Shabiki kindakindaki wa Yanga anayefahamika k**a Baba Rabiat na wakati mwingine hutumia jina la Shetani wa Yanga, ameteka hisia za mashabiki wengi wa na kwa namna yake ya uongeaji.

Amekuwa akitumia sana neno "Naweka Ahadi" yote kwa yote ni kuchaguza utani wa jadi kati ya mapacha hao wa Kariakoo kulwa na ndoto mmoja akitoka jangwani na mwingine anajiita mtoto wa mjini kutoka mitaa ya Msimbazi pale.

Kuelekea mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya utakaopigwa kesho tayari mwamba amekwisha toa ahadi ya kwamba endapo atamfunga Al Ahly basi mashabiki wa Simba wachukue pasi ya umeme kisha wamvue nguo na kumchoma na tena akasema "Serikali ya Jamhuri ya Muungani wa Tanzania chini ya Rais isiingile kati 😂 huu ni utani usiokera bali unafurahisha.

Tazama video KWENYE YouTube Yetu uone jinsi ambavyo mashabiki mbalimbali wa Simba walivyomfanyia baada ya kutoa ahadi hiyo.

Meridianbet ni sehemu sahihi ya kuweka pesa zako na ukazitumia kubashiri michezo k**a hii au kucheza na tembelea https://www.meridianbet.co.tz kuweka bashiri zako na kuvuna ushindi k**a mvua.🌧️🌧️🌧️🌧️

SIMBA WATOA TAMKO BAADA YA AL AHLY KUTUASeleman Matola, kocha msaidizi wa Simba amesema kuwa wanatambua makosa yalipo ja...
27/03/2024

SIMBA WATOA TAMKO BAADA YA AL AHLY KUTUA

Seleman Matola, kocha msaidizi wa Simba amesema kuwa wanatambua makosa yalipo jambo linalowafanya wafanye kazi kwa umakini kuelekea kwenye mechi zijazo ukiwemo wa Al Ahly kwa kuwaongezea wachezaji wao dozi nyingine.

“Unaona kwenye mechi ambazo tunacheza tunapata ushindi na wakati mwingine tunawapa ruhusa wapinzani kutufunga huwa tunaongea na wachezaji na tutaongeza dozi nyingine kwenye uwanja wa mazoezi.

“Kikubwa ni kuwa makini kwa kuwa mchezo wa mpira ni mchezo wa makosa, kuelekea kwenye mechi zetu zijazo tuna imani tutakuwa imara hilo linawezekana kutokana na wachezaji kujituma na kutimiza majukumu yao kwa ushirikiano,”.

Credit:

KANE & ERIC DIER WARUDISHWA SPURSHarry Kane na Eric Dier watakutana na klabu yao ya zamani ya Tottenham Hotspur, wakati ...
27/03/2024

KANE & ERIC DIER WARUDISHWA SPURS

Harry Kane na Eric Dier watakutana na klabu yao ya zamani ya Tottenham Hotspur, wakati Bayern Munich watakapocheza mechi ya kirafiki kwenye majira ya joto mnamo tarehe 10 Agosti mwaka huu huko Malta.

Credit:

LIONEL MESSI ATAJA KILICHOMUONDOA PSG NA BARCA, SAFARI YA ROSARIO ILIKUWA CHUNGU, PSG PAGUMU, SIKUWA TAYARI KUONDOKA"Mab...
27/03/2024

LIONEL MESSI ATAJA KILICHOMUONDOA PSG NA BARCA, SAFARI YA ROSARIO ILIKUWA CHUNGU, PSG PAGUMU, SIKUWA TAYARI KUONDOKA

"Mabadiliko yalikuwa magumu nilipoenda PSG, kwa sababu nilikuwa nafanya vizuri sana Barcelona na nilipanga kukaa hapo. Sikuwa tayari kuondoka, kila kitu kilitokea haraka sana, nililazimika kujenga upya maisha yangu kutoka siku moja hadi nyingine.

"Nikaanza kujua ligi nyingine, klabu nyingine, chumba cha kubadilishia nguo kipya. Ilikuwa mabadiliko ambayo hatukuwa tunayatafuta na ndio maana ilikuwa ngumu mwanzoni."

Vivyo hivyo, Messi alielezea safari yake ya kutoka Rosario kwenda Barcelona akiwa na umri wa miaka 13, na mara nyingi alilia kwa ajili ya Argentina pia.

"Ilikuwa ngumu kwangu nilipoanza Barcelona. Nilikuwa mtoto na nililazimika kuzoea marafiki wapya, nchi mpya, mji mpya, watu wapya, shule mpya.

"Ilikuwa ngumu kwangu mwanzoni, lakini nilidhani nilikuwa nafanya nilivyotaka, kucheza mpira wa miguu, katika timu kubwa k**a Barcelona na hilo lilinipa uwezo wa kusonga mbele, lilikuwa jambo la kustaajabisha na nilifurahia sana. Walinipatia sifa njema sana Barcelona, ​​nashukuru kwao."

Credit:

27/03/2024

SOUTHGATE AMPONGEZA KINDA MAINOO

"Anatupa aina tofauti ya mchezaji wa kiungo kuliko kitu kingine chochote tulichonacho na tunafurahishwa sana na kile alichofanya, hauwezi kuamini umri wake kwa kweli.

"Sifa zake zipo wazi kwa kila mtu kutazama, uwezo wake wa kupokea mpira chini ya shinikizo na kushinda changamoto, kudhibiti mpira katika maeneo yenye hatari." -Southgate kuhusu Kobbie Mainoo.

Credit:

Bayern wamethibitisha kwamba Kane ameanza mazoezi binafsi na miamba wa Bundesliga wanatumai kwamba hataweza kucheza dhid...
26/03/2024

Bayern wamethibitisha kwamba Kane ameanza mazoezi binafsi na miamba wa Bundesliga wanatumai kwamba hataweza kucheza dhidi ya Borussia Dortmund Jumamosi.

Arsenal watakutana na Bayern wakati Kane atarejea kucheza kaskazini mwa London kwa mara ya kwanza tangu aondoke Tottenham msimu uliopita.

Harry Kane Mwenye umri wa miaka 30 amekuwa katika fomu nzuri sana kwa Bayern, akifunga mabao 31 katika mechi 26 za Bundesliga msimu huu, na kurudi kwake ni msaada mkubwa kwa Wajerumani.

"Harry Kane alikamilisha mazoezi binafsi kwenye uwanja wa mazoezi wa FC Bayern Jumatatu asubuhi, alifanya mazoezi pamoja na kocha wa viungo Holger Broich." Walisema Bayern katika taarifa.

Credit:

ANGEL DI MARIA ATISHIWA KUUAWA NYUMBANI KWAKE ROSARIO.Mshambuliaji wa Argentina Angel Di Maria alipokea tishio nyumbani ...
26/03/2024

ANGEL DI MARIA ATISHIWA KUUAWA NYUMBANI KWAKE ROSARIO.

Mshambuliaji wa Argentina Angel Di Maria alipokea tishio nyumbani kwake na familia yake katika maeneo ya pembeni ya Mji wa Rosario alfajiri ya Jumatatu, vyombo vya habari vya eneo hilo viliripoti, ni katika mfululizo wa vurugu zinazohusiana na dawa za kulevya katika mji huo ambao Lionel Messi pia anatoka.

Ujumbe huo unakuja wiki moja baada ya Di Maria, ambaye sasa anacheza kwa mabingwa wa Ureno Benfica, kusema angependa kumalizia kazi yake katika klabu yake ya utotoni ya Rosario Central.

Ripoti za vyombo vya habari vya eneo hilo zilisema gari liliiacha ujumbe wa tishio mbele ya eneo la makazi ya siri ambayo Angel Di Maria (36) huishi na familia yake. Ujumbe huo uliwahusisha familia ya Di Maria na kusema hata gavana wa jimbo Maximiliano Pullaro hawezi kuhakikisha usalama wao ikiwa atarudi mjini.

“Mwambie mwanao Angel asirudi Rosario kwa sababu tutamuua. Hata Pullaro hatakusaidia. Hatuachi noti za karatasi. Tunaacha risasi na watu waliokufa nyuma,” ilisema taarifa hiyo, kulingana na tovuti ya habari ya Infobae, ikirejelea vyanzo vya polisi.

Mji wa Rosario, ni moja ya vituo vikubwa vya agro-port (Bandari) duniani, ambapo kumekuwa na ongezeko kubwa la vurugu na makundi ya biashara ya dawa za kulevya, kwani mji huo, kulingana na wataalamu, ni njia ya kutolea nje ya nchi madawa ya kulevya.

Nahodha wa Argentina na mwenye asili ya Rosario Lionel Messi pia alitishiwa kwa barua mwaka jana baada ya watu wasiojulikana kuwashambulia wafanyabiashara wa duka la vyakula la mke wake Antonela Roccuzzo.

Serikali ya Argentina ilisema wiki iliyopita itawasilisha muswada katika Bunge kuruhusu jeshi kuingilia kati katika operesheni za usalama ndani ya nchi ili kupambana na biashara ya dawa za kulevya na uhalifu huko Rosario.

Credit:

MMEMSIKIA HUKO MASHINE YA KUONGEA, SEMAJI LA KIMATAIFA?UONGOZI wa Simba SC umeweka wazi kuwa mpango mkubwa kuelekea mche...
25/03/2024

MMEMSIKIA HUKO MASHINE YA KUONGEA, SEMAJI LA KIMATAIFA?

UONGOZI wa Simba SC umeweka wazi kuwa mpango mkubwa kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ni kupata ushindi Kwa nguvu ya namna yoyote ile.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally amesema hesabu kubwa ni kupata matokeo chanya kwenye mchezo huo na ndiyo maana wakachagua kwenda Zanzibar kujifua.

"Hapa ni kupata ushindi tu dhidi ya Waarabu wa Misri huku mtego mkubwa ikiwa ni kubadilika kulingana na namna wapinzani watakavyokuja katika mchezo husika.

"Kwa namna yoyote Al Ahly Lazima apasuke Kwa Mkapa na hiyo ndiyo dhamira yetu tuliyonayo. Tuna Imani na timu yetu na tunajua ubora wa kikosi chetu na Lazima tushinde."

Aliongeza pia mechi hiyo wataimalizia nyumbani kwa Mkapa kisha wakienda Misri ni mwendo wa kushikilia bomba tu mpaka mwisho wa mchezo.

"Benchikha ni miongoni mwa silaha zetu muhimu kuelekea mchezo wetu wa Machi 29, 2024 Simba Vs Al Ahly, Benchikha ni kocha mkubwa mwenye wasifu mkubwa ambaye anaweza kucheza mechi k**a hizi.

"Ndio maana nasema, kwetu mechi hii ni ya mkondo mmoja tu! Tutahangaika kuhakikisha tunaimaliza hii mechi Dar es Salaam".

"Uwezo wa kushikilia bomba ‘kuzuia/kujilinda’ Simba tunao, tuliona hapa dhidi ya Wydad tulishinda 2-0 tukashikilia bomba mpaka mechi ikaisha".

"Kule nyumbani kwao (Wydad) tulishikilia bomba mpaka dakika ya 93, makosa madogo yakapelekea tukaadhibiwa. Simba hatuwezi kuzuiliwa na Al Ahly, wanasimba tumeamua jambo letu, Al Ahly anafia Benjamin Mkapa".

Credit:

PIGO KWA AL AL AHLY FURAHA KWA SIMBAMshambulajia wa klabu ya Al-Ahly Emam Ashour imebainika kwamba amateguka bega lake n...
23/03/2024

PIGO KWA AL AL AHLY FURAHA KWA SIMBA

Mshambulajia wa klabu ya Al-Ahly Emam Ashour imebainika kwamba amateguka bega lake na hivyo kumfanya kuwa nje kwa muda wa wiki sio chini ya tatu, kwa mujibu wa taarifa mbalimbali kutoka Misri.

Emam alipata majeraha hayo kwenye mchezo wa kirafiki kati ya Misri na New Zealand, na hivyo kumfanya kuwa hatiani kuikosa mechi ya Simba itakayopigwa Ijumaa Machi 29, katika dimba la Mkapa.

Taarifa hizi na zile za kukosekana kwa Hussein El Shahat huenda zikiwa nzuri kiasi kwa mashabiki wa Simba SC ambao wanaiombea timu yao ifuzu hatua ya nusu fainali Ligi ya Mabingwa Afrika.

Credit:

Kocha wa Klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti ameandaa mipango mitatu kujaribu kuiondoa Manchester City katika Ligi ya M...
22/03/2024

Kocha wa Klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti ameandaa mipango mitatu kujaribu kuiondoa Manchester City katika Ligi ya Mabingwa mwezi ujao mchezo wa kuwania kufuzu nusu fainali.

Gazeti moja nchini Hispania linasema kwamba Ancelotti kwa sasa anapendelea mfumo wa 4-4-2 ambao umefanya kazi vizuri hadi sasa ambapo unaifanya timu yake kuwa na tofauti ya pointi nane kileleni mwa La Liga.

Hata hivyo, akizingatia kipigo cha 4-0 msimu uliopita katika mchezo wa pili huko Etihad, anahitaji mfumo unaolinda viungo wake wa kati.

Carlo Ancelotti bado anaweza kwenda na wachezaji wanne wa kiungo katika timu yake, lakini anatafakari juu ya mfumo wa "double pivot" unaweka wachezaji wawili katikati Aurelien Tchouameni na Toni Kroos kuwa nyuma ya Jude Bellingham na Fede Valverde wakati viungo Vinicius Jr. na Rodrygo wanapangwa k**a washambuliaji.

Katika mfumo wa Diamond (almasi), Tchouameni anakuwa mwanajeshi pekee akitoa msaada kwa Kroos na Eduardo Camavinga huku Valverde akiwa upande wa kulia na Vinicius upande wa kushoto.

Hii ingemaanisha kwamba Rodrygo anakosa, na Bellingham anapangwa kati zaidi kuonekana k**a mshambuliaji kwenye karatasi.

Ikiwa Ancelotti atachagua kumtumia Kroos na Tchouameni kuunda "double pivot", anaweza pia kuwaweka Valverde na Vinicius mbele yao huku Brahim Diaz akiwa kiungo wa kati wa kushambulia na Jude Bellingham mshambuliaji wa kati.

Credit:

Mchezaji wa zamani wa Manchester City na Real Madrid, Robson de Souza maarufu k**a Robinho, amehukumiwa kifungo cha miak...
21/03/2024

Mchezaji wa zamani wa Manchester City na Real Madrid, Robson de Souza maarufu k**a Robinho, amehukumiwa kifungo cha miaka tisa (9) jela kwa kosa la ubakaji.

Mahak**a nchini Brazil iliamua kwamba mchezaji huyo wa miaka 40 atatumikia kifungo chake katika nchi yake licha ya kosa hilo kufanyika nchini Italia mwaka 2013.

Robinho alipatikana na hatia kwenye mahak**a ya Italia mwaka 2017 kwa kushiriki ukatili huo kwa mwanamke Malbanyani mwenye umri wa miaka 22.

Credit:

"Kibwana Shomary J3 ataanza mazoezi.Khalid Aucho yupo hatua ya pili ya utimamu na anaendelea vizuri.Zawadi Mauya anaende...
21/03/2024

"Kibwana Shomary J3 ataanza mazoezi.

Khalid Aucho yupo hatua ya pili ya utimamu na anaendelea vizuri.

Zawadi Mauya anaendelea vizuri.

Yao Kouassi ana majeraha ya nyama za paja mpaka sasa hivi kwa mujibu wa ripoti ya madaktari ni asilimia 50 kuivaa Mamelodi.

Pacome Zouzoua, ana shida ya goti lakini madaktari wa Ivory Coast walimuhitaji kuwa nae karibu zaidi hivyo taarifa za mchezaji huyo zitatoka baada ya mrejesho wa madaktari wetu na wa Ivory Coast.

Kwa mujibu wa Ali Kamwe.

Credit:

Mshambuliaji wa Man Utd Anthony Martial inasemekana ataondoka OT mwishoni mwa msimu huu k**a mchezaji huru baada ya mkat...
21/03/2024

Mshambuliaji wa Man Utd Anthony Martial inasemekana ataondoka OT mwishoni mwa msimu huu k**a mchezaji huru baada ya mkataba wake kutamatika.

Mfaransa huyo yuko karibu kuwa mchezaji huru baada ya kukipiga kwa muda mrefu Man Utd tangu akiwa kinda, lakini bado haijawekwa wazi atajiunga na timu gani.

Vilabu vingi vya Uturuki vilionesha nia ya kuwa nae lakini alikataa ofa hizo na sasa anahitaji muda zaidi wa kuchagua anakwenda wapi.

Credit:

Wachezaji wengi ambao wametoka Tanzania (Taifa Stars) ukiachilia mbali wale wachache wanaocheza nje ya Afrika, wamekiri ...
20/03/2024

Wachezaji wengi ambao wametoka Tanzania (Taifa Stars) ukiachilia mbali wale wachache wanaocheza nje ya Afrika, wamekiri kuteswa na baridi kali inayochapa Kwa kipindi hiki.

"Mazoezi ya huku yanaendelea vizuri, lakini changamoto pekee ni hali ya hewa. Baridi ni Kali sana huku kiasi ambacho tunafanya mazoezi tukiwa na Makoti makubwa," alisema Aishi Manula.

Mashindano hayo yanazikutanisha timu mbalimbali kutoka mataifa 20 kote duniani ambapo ukanda wa kusini kuna Tanzania (Taifa Stars) na Afrika Kusini mshindi wa tatu AFCON 2023 ambapo Tanzania tupo kundi moja na nchi k**a Bulgaria, Mongolia, na Azerbaijan.

Credit:

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Meridian Sport posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Meridian Sport:

Videos

Share