Mpili Sports News

Mpili Sports News Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Mpili Sports News, News & Media Website, Mbezi, Dar es Salaam.

28/12/2024
STARS YAMFUTA RAIS SAMIA, WATANZANIA  MACHOZI Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeweza kumfuta machozi, Rais Dkt. ...
20/11/2024

STARS YAMFUTA RAIS SAMIA, WATANZANIA MACHOZI



Timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeweza kumfuta machozi, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Watanzania kwa ujumla kutokana na ajali ya kuanguka kwa ghorofa, Kariakoo jijini Dar es Salaam baada ya kuipeleka Tanzania AFCON 2025 nchini Morocco.

Stars imelifanya hilo Novemba 19,2024 kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam, ambapo imefuzu kucheza fainali za AFCON 2025 zitakazochezwa nchini Morocco kwa kuichapa timu ya Taifa ya Guinea bao 1-0.

Stars ilihitaji ushindi wa aina yeyote kwenye mchezo huo ili kusonga mbele na ndicho ilichokifanya mbele ya Watanzania wengi ambao wamegubikwa na majonzi ya kupoteza Watanzania wenzao kwenye ajali ya kuanguka kwa ghorofa.


Vitambaa vyeusi kwenye mikono ya wachezaji wa Taifa Stars vikiashiria majonzi vilitosha kuwapa ari na nguvu wachezaji kuwafariji Watanzania wenzao.

K**a hiyo haitoshi Rais Samia ambae amekuwa kinara wa kufanikisha mafanikio ya Stars aliamua kununua tiketi zote za mchezo huo ili kutoa nafasi kwa Watanzania wengi kushuhudia mchezo huo na baada ya ushindi huo Rais Samia amewazawadia shilingi milioni 700 k**a pongezi kwa kufuzu kwenda
AFCON 2025.

Mbali na hayo Rais Samia pia amekuwa mstari wa mbele katika kununua magoli ya ushindi, akichagiza kampeni yake ya 'Bao la Mama'.

Ni Simon Msuva ndie aliyerejesha furaha kwa Watanzania baada ya kufunga bao zuri la kichwa.

Akizungumza baada ya mchezo kumalizika kocha wa Taifa Stars, Hemed Suleiman Morocco, amemshukuru Rais Samia na Watanzania kwa ujumla kutokana na sapoti yao kwa timu.

Shukurani hizo pia zimetolewa na Nahodha wa timu hiyo, Mbwana Samatta ambae amesema uamuzi wa Rais Samia wa kuruhusu watu kuingia bila kulipa kiingilio umesaidia kuwaongezea hamasa.

Pongezi zaidi kwa benchi la ufundi la Taifa Stars linaloongozwa na Kocha Hemed Suleiman Morocco akisaidiwa na Juma Mgunda na Jamhuri Kihwelu 'Julio'.

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameiona haja ya kuongeza muda zaidi wa uokoaji wa watu waliofukiwa na kifusi cha ghorofa ...
19/11/2024

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameiona haja ya kuongeza muda zaidi wa uokoaji wa watu waliofukiwa na kifusi cha ghorofa lililoanguka hivi karibuni Kariakoo jijini Dar es Salaam, kutoka saa 72 hadi saa 96.

Novemba 19,2024 Rais Samia amempigia simu Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na kumtaka kuongeza saa 24 zaidi kutoka zile 72 za awali ili kuwaokoa watu wanaodhaniwa kuwa bado wapo chini ya jengo hilo.

"Mheshimiwa Waziri Mkuu ninatambua utaratibu wa uokoaji una muda maalum wa saa 72 mpaka kusitisha zoezi hilo, binafsi nina matumaini kuwa Mwenyezi Mungu anaweza akatenda miujiza yake na kuweza kuwanusuru ndugu zetu wengine ambao bado wamenasa kwenye jengo hilo.

"Ninakupa maelekezo ya kutositisha zoezi la uokoaji na kuongeza muda wa saa 24 zaidi ili kuwapambania ndugu zetu ambao tunaamini bado wako hai."

Aidha Rais Samia ameonesha kutambua na kutathimini mchango mkubwa wa uokoaji unaofanywa na vikosi vyote na wananchi kwa ujumla ambao kwa pamoja wanashiriki katika zoezi hilo.

"Nina wathamini sana, wameonesha utu, uzalendo mkubwa na uchapakazi wa hali ya juu sana, hivyo nawatia moyo na kuwapa nguvu ya kuendelea kuwapambania ndugu zetu kwani ninyi ni mashujaa wa taifa letu."

Rais Samia amewasihi wananchi, ndugu na jamaa kuwa na subira na k**a taifa tuendelee kuwaombea ndugu zetu na wapiganaji wetu ili kufanikisha zoezi hilo kwa mafanikio makubwa.

SERIKALI YAENDELEA NA ZOEZI LA UOKOAJI KARIAKOO.*●Rais Dkt.Samia aagiza ukaguzi maghorofa yote*Wakati zoezi la uokoaji l...
18/11/2024

SERIKALI YAENDELEA NA ZOEZI LA UOKOAJI KARIAKOO.

*●Rais Dkt.Samia aagiza ukaguzi maghorofa yote*

Wakati zoezi la uokoaji likiendelea katika ghorofa lililoanguka Kariakoo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amezitaka mamlaka zinazohusika kuchukua hatuna stahiki ikiwemo ya kuyafanyia ukaguzi majengo ya ghorofa yaliyojengwa na yanayoendelea kujengwa ili kubaini uimara wake.

Dkt. Samia ametoa maagizo hayo katika taarifa yake kwa umma kuhusiana na ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salam hivi karibuni.

Alieleza kuwa hatuna hiyo itasaidia kubaini ubora wa majengo hayo na kuepusha madhara kwa watu na mbali zao.

Aidha alilitaka jeshi la polisi kumuhoji mmiliki wa jengo hilo ili kusaidia uchunguzi na kupata ukweli juu ya sababu za kuporomoka kwa jengo hilo.

Aidha Dkt. Samia amempongeza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na vyombo vya ulinzi, wadau mbali mbali na wananchi kwa kushiriki katika uokoaji na kuahidi serikali kugharamia matibabu pamoja na mazishi ya watu waliopoteza maisha.

Pia Dkt. Samia ametoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa watu waliofariki katika mkasa huo na kuwatakia ahueni ya haraka manusura wa tukio hilo ambao hadi Jumapili Novemba 17 jumla ya watu 13 walithibitishwa kufariki dunia.

RAIS DKT. SAMIA KUWAONDOLEA ADHA YA MAJI WANANCHI MKOANI TANGA.● *Mradi wa Chanzo cha Maji Mswaha Darajani kugharimu Bil...
17/11/2024

RAIS DKT. SAMIA KUWAONDOLEA ADHA YA MAJI WANANCHI MKOANI TANGA.

● *Mradi wa Chanzo cha Maji Mswaha Darajani kugharimu Bilioni 170*



Katika kipindi cha miaka mitatu tangu aingie madarakani, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea na mkakati wake kuhakikisha tatizo la uhaba wa maji katika maeneo mbalimbali nchini linatoweka kabisa, kwa kuanzisha miradi mbalimbali ya Maji ambayo imefanikiwa kwa kiasi kikubwa.

Mkakati huo wa Serikali ya awamu ya sita, umetekelezwa kupitia Sekta ya Maji ambapo kwa Mkoa wa Tanga, Rais Dkt. Samia amelekeza nguvu zake katika Mradi wa Maji wa Kata ya Mswaha
Darajani (Mswaha Darajani Water Intake), Wilayani Korogwe Mkoani Tanga.

Wakati Mradi huo unaendelea, Waziri wa Maji Jumaa Aweso, ametembelea mradi na kuwataka Wakandarasi wa Mradi huo wa Maji wa Mswaha Darajani, kuwatumia vijana wa eneo hilo kufanyakazi mbalimbali zenye kuhitaji ujuzi wa juu au chini katika ujenzi wa Mradi huo.

Amesema, kuna kazi nyingi katika mradi ambazo vijana wa maeneo hayo wanaweza kuzifanya ili kujipatia kipato, lakini pia amewasihi vijana hao kuwa waaminifu watakapopatiwa nafasi hizo za kazi.

Mradi huo wa Maji Mswaha Darajani, unaoendelea kutekelezwa kwa sasa, umeigharimu Serikali zaidi ya Shilingi Bilioni 170 ambao, unategemewa kusambaza maji katika maeneo ya Pangani, Handeni, Muheza na Korogwe Mkoani Tanga, na hivyo kupewa jina la Mradi wa Miji 28.

Waziri Aweso amewataka Wataalamu wa Sekta ya Maji kuhakikisha Wananchi wa Kata ya Mswaha, Wilayani Korogwe Mkoani humo, wananufaika vya kutosha na Chanzo cha Maji Mswaha Darajani (Mswaha Darajani Water Intake) kilichopo katika Kata yao.

Amesema, watu wa eneo hilo wapatiwe maji ya kutosha kwani Rais. Dkt. Samia anatambua kuwa, Wizara ya Maji inajenga miradi ya kimkakati ambapo anahitaji wananchi wa eneo la mradi husika kunufaika.

Aidha, amewataka wananchi wa Mswaha kuwa walinzi wakuu wa mradi huo katika kuujenga na kuutunza mradi kwa kutochafua mazingira yanayozunguka mradi huo.

RAIS SAMIA KUFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI*Umelenga kuibua fursa mpya kwa Watanzania* Mkutano...
17/11/2024

RAIS SAMIA KUFUNGUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA UWEKEZAJI SEKTA YA MADINI

*Umelenga kuibua fursa mpya kwa Watanzania*



Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini unatarajiwa kufanyika Novemba 16,2024 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo utaongeza fursa za uwekezaji katika Sekta ya Madini hapa nchini sambamba na kuweka msingi thabiti wa ushirikiano baina ya wadau, kuimarisha uzalishaji wa madini, na kuhakikisha kuwa rasilimali za madini zinawanufaisha watanzania kiuchumi na kijamii.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde Novemba 14, 2024 alipozungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya Mkutano wa sita wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini nchini Tanzania.

Waziri Mavunde amesema kuwa, Mkutano huo unaoongozwa na Kauli mbiu ya “Uongezaji Thamani Madini kwa Maendeleo ya Kiuchumi na Kijamii” unatarajiwa kuvutia washiriki muhimu zaidi ya 1,500 kutoka Tanzania na nchi mbalimbali duniani na kwamba ni jukwaa muhimu kwa wadau wa madini kubadilishana uzoefu, maarifa, na mikakati mbalimbali kwa lengo la kuongeza tija katika Sekta ya Madini, maendeleo ya taifa na uchumi kwa ujumla.

“Hilo litakuwa ni jukwaa la kujadili kwa pamoja mustakabali wa sekta ya madini, kushirikishana maarifa, ujuzi na kuangazia fursa mpya zinazojitokeza katika sekta hii inayokua kwa kasi. Pia, unatoa nafasi kwa washiriki kujifunza kuhusu Sera na mikakati mipya ya serikali, kujadili masuala ya kisheria na kiuchumi yanayohusiana na madini, na kushuhudia teknolojia mpya na ubunifu unaoweza kuleta thamani zaidi katika utafiti, uchimbaji na uongezaji thamani wa madini kupitia mawasilisho na maonesho kwenye mabanda yanayoenda sambamba na mkutano” amesema Mavunde

Kaulimbiu ya mwaka huu inalenga kuhamasisha uongezaji thamani wa madini k**a njia ya kuleta faida zaidi za kiuchumi na kijamii kwa Tanzania na dunia kwa ujumla na kusisitiza kuwa Serikali imejipanga kuhimiza uwe

TAIFA STARS YAMPA USHINDI RAIS SAMIA NA WATANZANIA Ndege iliyotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa timu ya taifa ...
17/11/2024

TAIFA STARS YAMPA USHINDI RAIS SAMIA NA WATANZANIA



Ndege iliyotolewa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imeleta tija baada ya kikosi cha timu hiyo kuibamiza timu ya taifa ya Ethiopia bao 2-0.

Ushindi huo umeelekezwa k**a zawadi kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kutokana na mchango wake mkubwa kwenye mchezo huo na kwa Watanzania kwa ujumla kutokana na sapoti yao kwa Stars.

Hivi karibuni Rais Samia ambaye ni mwanamichezo, ni mpenzi wa soka na tangu aingie madarakani ameleta mapinduzi makubwa kwenye michezo mbalimbali ukiwemo soka aliamua kutoa ndege maalum ya kukipeleka kikosi hicho ili kifike nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo bila bughudha.

Taifa Stars ilicheza Novemba 16,2024 dhidi ya timu ya Taifa ya Ethiopia katika mchezo wa kusaka tiketi ya fainali za AFCON 2025.

Awali Kocha wa Taifa Stars, Hemed Suleiman Ali maarufu k**a Hemedi Morocco alimshukuru Rais Samia kwa kutoa ndege ya Serikali kwa mara nyengine ili iwapeleke wachezaji wa Taifa Stars kwenda kulipigania taifa lao.

"Namshukuru mama yetu Rais Samia kwa kutupatia tena ndege ya kutupeleka DRC, tunaamini huu ni upendo wa hali ya juu ya Stars na kwa soka la Tanzania kwa ujumla.

"Ahadi yetu ilikuwa ni moja tu, nayo ni ushindi na tumeshinda, angalau tumejiweka katika mazingira mazuri ya kufuzu fainali za AFCON 2025 zitakazochezwa Morocco."

SERIKALI YA DKT. SAMIA YAFANIKIWA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA MAAMBUKIZI YA HIV Katika kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Uki...
16/11/2024

SERIKALI YA DKT. SAMIA YAFANIKIWA KATIKA MAPAMBANO DHIDI YA MAAMBUKIZI YA HIV



Katika kuelekea Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani kwa mwaka 2024, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, chini ya Uongozi Mahiri wa Dkt. Samia Suluhu Hassan, imefanikiwa katika mapambano dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huo, kutoka 1,700,000 mwaka 2017 hadi kufikia 1,540,000 mwaka 2023.

Mafanikio ya kupungua kwa maambukizi ya VVU yametokana na jitihada za Rais Dkt. Samia aliyewezesha kufikia mafanikio haya ikiwemo kuhakisha huduma bora za tiba na matunzo kwa WAVIU.

Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Ummy Nderianaga ameeleza kuwa, Tanzania imepiga hatua katika mapambano dhidi ya UKIMWI kufuatia kupungua kwa maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU), na hivyo kufikia idadi hiyo.

Maambukizi wa Virusi vya Ukimwi yameonekana kuathiri zaidi makundi kadhaa yakiwemo makundi ya vijana wenye umri wa miaka 15 hadi 24, madereva wa masafa marefu, wachimbaji wadogo wa madini na wavuvi kuchangia maambukizi mapya ya ugonjwa huo hapa nchini.

Nderianaga ameyasema hayo Jijini Dodoma, kuhusiana na Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani kwa mwaka 2024, ambayo Kitaifa yatafanyika Desemba 1, 2024 Mkoani Ruvuma.

Utafiti wa hali ya UKIMWI nchini (Tanzania HIV Impact Survey) kwa mwaka 2022/23, umeonyesha Mikoa mitatu yenye kiwango cha juu cha maambukizi ni Njombe asilimia 12.7, Iringa asilimia 11.1 na Mbeya asilimia 9.6, na Mikoa yenye maambukizi ya chini ni Kigoma asilimian 1.7, Manyara asilimia 1.8 na Lindi asilimia 2.6.

Tanzania imepiga hatua kubwa katika nyanja mbalimbali za mwitikio wa VVU ambapo kwa mujibu wa ripoti ya UNAIDS 2022, Tanzania imefikia Mkakati wa Kimataifa wa UKIMWI 2021 hadi 2026 kwa lengo la matibabu.

Mafanikio haya yamechangiwa na matokeo ya Utafiti wa Athari za VVU Tanzania Mwaka 2022-2023 ambao uliripoti kufikiwa kwa malengo ya UNAIDS 95-95-95 kwa asilimia 82.7, asilimia 97.9 na asilimia 94.3 (ngazi ya jamii).

RAIS DKT. SAMIA AFANIKISHA MATENGENEZO YA MABEHEWA 264 NCHINI CHINA● TRC kuanza kusafirisha mizigo kwa Reli ya SGR Febru...
16/11/2024

RAIS DKT. SAMIA AFANIKISHA MATENGENEZO YA MABEHEWA 264 NCHINI CHINA

● TRC kuanza kusafirisha mizigo kwa Reli ya SGR February, 2025



Jitihada zinazoendelea kufanywa tangu Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan aingie madarakani, zinaonekana ambapo Rais amepambana kuhakikisha miradi mbalimbali ya maendeleo inakamilika ili kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizokuwa zinalikabili Taifa kwa kipindi kirefu.

Pamoja na kuwepo miradi mingi mikubwa iliyoigharimu Serikali kiasi kikubwa cha fedha lakini pia, Mradi wa Treni za SGR umeonekana kuwa mkombozi kwa Watanzania katika sekta ya usafiri.

Katika kuhakikisha usafiri wa Treni ya SGR unafanikiwa ikiwa ni kwa kuwepo mabehewa ya kutosha ya abiria na ya mizigo, Serikali ya Tanzania inatarajia kupokea jumla ya shehena ya Mabehewa 264 ya mizigo kutoka nchini China, Desemba, 2024 yaliyokuwa yanafanyiwa matengenezo na Kampuni ya CRRC.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Shirika la Reli Tanzania (TRC) limesema, utengenezaji wa mabehewa hayo 264 ya mizigo umekamilika nchini China na kwamba, Meli iliyobeba mabehewa hayo imeng'oa nanga nchini humo Novemba 12, 2024 na inatarajiwa kufika Tanzania katikati ya mwezi Desemba 2024.

Katika mzigo huo kuna mabehewa 200 ya kubeba makasha (makontena) na mabehewa 64 ya kubeba mizigo isiyofungwa (loose cargoes).

Shehena hiyo ya mabehewa 264 ni sehemu ya jumla ya mabehewa 1,430 ambayo kwa mujibu wa mkataba kati ya Shirika la Reli Tanzania (TRC) na Kampuni ya Kimataifa ya China (CRRC) yatapelekwa kwenye Reli ya kisasa ya SGR.

TRC inategemea kuanza kusafirisha mizigo kwa reli ya SGR kati ya January au February mwakani.

Akizungumzia mafanikio ya mradi huo hasa katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa amesema, kuna mafanikio makubwa kupitia mradi huo ambao hadi sasa umetumia fedha nyingi katika utekelezaji wake.

Amesema, mradi huu utafungua uchumi wa nchi kwa kiasi kikubwa, kwa kutambu

SERIKALI YA SAMIA  YAAHIDI UCHAGUZI WA HAKI NA UWAZI SERIKALI ZA MITAA Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na ...
16/11/2024

SERIKALI YA SAMIA YAAHIDI UCHAGUZI WA HAKI NA UWAZI SERIKALI ZA MITAA



Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa ameeleza kuwa, Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27,2024 utakuwa wa haki na uwazi.

Pia, uchaguzi huo utazingatia misingi ya umoja na mshik**ano, pamoja na falsafa ya R4 za Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Waziri Mchengerwa amesema kuwa, Ofisi ya Rais TAMISEMI ilianzishwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa lengo la kusogeza maamuzi karibu kabisa na wananchi.

Amefafanua kwa kusema kwamba, uchaguzi wa serikali za mitaa ni tofauti na uchaguzi mkuu, kwani mfumo wake unalenga wakazi ambao wanatambuana katika maeneo yao.

Utambuzi huu wa wakazi unategemea wenyewe wakazi wa eneo husika.

Amesema hayo Novemba 12, 2024 jijini Dar es Salaam wakati akifungua semina ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini.

Waziri Mchengerwa ameendelea kusema kwamba Bunge halikufanya marekebisho ya Ibara ya 145 na 146 ya katiba, wala tafsiri ya sheria inayosimamia uchaguzi wa serikali za mitaa.

Hata hivyo, Bunge lilifanya marekebisho ya sheria inayosimamia mchakato wa chaguzi zinazoratibiwa na Tume Huru ya Uchaguzi.

Vilevile Waziri Mchengerwa ameeleza kwamba, kumekuwa na propaganda za kisiasa kuhusu hali ya uchaguzi wa serikali za mitaa, ambapo amedai zinatolewa na baadhi ya watu ambao hawakuwa wamejiandaa vyema.

Amesema kuwa, uchaguzi huo ni shirikishi, na maandalizi yamehusisha vyama vyote vya siasa kwa njia ya vikao na mashauriano ya mara kwa mara na wadau wa vyama vya siasa.

Kuhusu kutotumika kwa vitambulisho wakati wa uandikishaji, Waziri Mchengerwa amesema

"Tungeweza kunyima haki za Watanzania walio wengi endapo tungeamua kuwa lazima kila mtu awe na kitambulisho ili aandikishwe.

"Tunatambua kwamba wananchi wengi, hasa wanaoishi kwenye vitongoji na vijiji, hawana vitambulisho.

"Hivyo, hatua hii imezingatiwa ili kila Mtanzania apate fursa ya kush

RAIS SAMIA AMWAGIZA WAZIRI MKUU KUHARAKISHA UOKOAJI KARIAKOO Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na ajali ya kup...
16/11/2024

RAIS SAMIA AMWAGIZA WAZIRI MKUU KUHARAKISHA UOKOAJI KARIAKOO



Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amesikitishwa na ajali ya kuporomoka kwa ghorofa, Kariakoo Mtaa wa Mchikichi na Kongo jijini Dar es Salaam, ambapo amemwagiza Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kwa kushirikiana na timu za uokoaji kuhakikisha kazi hiyo inafanyika kwa haraka na ufanisi.

Kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii ikiwemo 'Instagram' na 'WhatsApp channel' Rais Samia ameandika: Hivi punde nimezungumza kwa kirefu na Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mbunge) kuhusiana na ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika Kata ya Kariakoo, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam, na kazi ya uokoaji inayoendelea.

Nimempa maelekezo kuhakikisha kazi hii inafanyika kwa haraka na ufanisi, na niendelee kupata taarifa ya kila hatua ya maendeleo yake.

Akionesha masikitiko yake Rais Samia amesema: Nimesikitika kupokea taarifa ya ajali ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa katika Kata ya Kariakoo, Wilaya ya Ilala, Mkoa wa Dar es Salaam.

Nimeuagiza Uongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Jeshi la Polisi, Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Uongozi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, na Idara ya Menejimenti ya Maafa kufanya kila linalowezekana kufanikisha zoezi la uokoaji na tiba kwa majeruhi.

Wakati hilo likiendelea na tukimuomba Mwenyezi Mungu awape pona ya haraka majeruhi, tuwaombee pia utulivu na subra ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wenzetu wanaotafuta riziki zao katika eneo hili muhimu kibiashara nchini ambao kwa namna mbalimbali wameathiriwa na ajali hii.

*RAIS SAMIA AALIKWA MKUTANO WA G20*Ndiye Rais wa kwanza Tanzania kushiriki mkutano huo    Mafanikio makubwa ya  Rais Dkt...
15/11/2024

*RAIS SAMIA AALIKWA MKUTANO WA G20*

Ndiye Rais wa kwanza Tanzania kushiriki mkutano huo



Mafanikio makubwa ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwenye uongozi wake yamewavutia viongozi wa nchi wanachama wa G20 na kuamua kumualika kushiriki mkutano wa viongozi wa G20 utakaofanyika Rio de Janeiro nchini Brazil kuanzia Novemba 18 hadi 19, 2024 ukiwa na kauli mbiu ya 'Kujenga ulimwengu wa haki na sayari endelevu'.

Mwaliko huo umetolewa na Rais Luiz Inacio Lula da Silva wa Brazil ambapo Rais Dkt. Samia atakuwa ndie Rais wa kwanza wa Tanzania kuhudhuria mkutano huo wa viongozi wa G20 tangu kupanuka kwa kundi hilo kutoka G8 hadi G20 mwaka 2009.

Ushiriki huo wa Rais Dkt Samia katika mkutano wa viongozi wa G20 unaashiria kuongezeka kwa ushawishi na mwonekano wa Tanzania katika jukwaa la kimataifa.

G20 inajumuisha nchi 19 ambazo ni Argentina, Australia, Brazil, Canada, China, Ufaransa, Ujerumani, India, Indonesia, Italia, Japan, Jamhuri ya Korea, Mexico, Urusi, Saudi Arabia, Afrika Kusini, Uturuki, Uingereza na Marekani pamoja na mashirika mawili ya kikanda ambayo ni Umoja wa Ulaya (EU) na Umoja wa Afrika (AU) hadi mwaka 2023.

Sifa mojawapo ya nchi wanachama wa G20 ni kwamba zinawakilisha takribani asilimia 85 ya Pato la kimataifa, zaidi ya asilimia 75 ya biashara za kimataifa na karibu theluthi mbili ya watu duniani.

*RAIS SAMIA AWAPA NDEGE TAIFA STARS* Ni mwanamichezo, ni mpenzi wa soka na tangu aingie madarakani ameleta mapinduzi mak...
15/11/2024

*RAIS SAMIA AWAPA NDEGE TAIFA STARS*



Ni mwanamichezo, ni mpenzi wa soka na tangu aingie madarakani ameleta mapinduzi makubwa kwenye michezo mbalimbali ukiwemo soka.

Rais Samia Suluhu Hassan, kipenzi cha wanamichezo na michezo kwa ujumla ameendeleza mapenzi yake kwenye soka baada ya kutoa ndege maalum kwa ajili ya kuwapeleka wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Taifa Stars tayari iko Kinshasa ikisubiri kuminyana na timu ya Taifa ya Ethiopia kesho Novemba 16,2024 katika mchezo wa kusaka tiketi ya fainali ya AFCON 2025.

Kocha wa Taifa Stars, Hemed Suleiman Ali maarufu k**a Hemedi Morocco amemshukuru Rais Samia kwa kutoa ndege ya Serikali kwa mara nyengine ili iwapeleke wachezaji wa Taifa Stars kwenda kulipigania taifa lao.

"Namshukuru mama yetu Rais Samia kwa kutupatia tena ndege ya kutupeleka DRC, tunaamini huu ni upendo wa hali ya juu kwa Stars na kwa soka la Tanzania kwa ujumla.

"Ahadi yetu ni moja tu, nayo ni ushindi, tutahakikisha tunashinda hiyo mechi ili kujitengenezea mazingira mazuri ya kufuzu fainali za AFCON 2025 zitakazochezwa nchini Morocco."

RAIS SAMIA AFANIKISHA UTALII TIBA TANZANIA  Ni mwanamke wa shoka, ni mama ni bibi na ni mlezi wa kweli wa Watanzania wot...
14/11/2024

RAIS SAMIA AFANIKISHA UTALII TIBA TANZANIA



Ni mwanamke wa shoka, ni mama ni bibi na ni mlezi wa kweli wa Watanzania wote bila kujali itikadi ama rangi zao, yeye ndie aliyebeba dira ya Mtanzania na Tanzania kwa ujumla.

Ni Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambae Askofu Dkt. Fredrick Shoo hivi karibuni alinukuliwa akikiri kuwa kiongozi huyu ni chaguo la Mungu anaestahili kuongoza sasa na hata baada ya sasa.

Rais Samia kiongozi mbeba maono amefanikiwa kuipaisha Tanzania kiutalii, uamuzi wake wa kushiriki filamu ya Royal Tour ulitosha kuonesha mwanamama huyo amedhamiria nini kwa nchi yake.

Royar Tour imelipa, watalii wanapishana huku na kule kutembelea vivutio vyetu vya utalii nchini.

Sasa amehamishia nguvu kwenye utalii wa Tiba, na serikali yake imezichagua hospitali maalum ambazo zitaendesha mpango wa utalii wa kimatibabu (Utalii tiba).

Hospitali hizo ni Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Saratani ya Ocean Road (ORCI), Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) na Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH).

Kwakuwa dhamira ni kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha utalii tiba kwa nchi za Afrika Mashariki na ikiwezekana Afrika kwa ujumla, uwekezaji katika utalii wa matibabu utakuwa endelevu na hospitali za rufaa zitajengwa katika kanda zote nchini na mipango iko tayari kuwa na kituo kingine kikubwa cha rufaa mkoani Kigoma kitakachotoa huduma za matibabu ikiwemo utalii wa matibabu.

Serikali imewekeza kwa kiasi kikubwa katika sekta ya afya kwa kuboresha miundombinu ya matibabu, kutoa mafunzo kwa wahudumu wa afya katika ngazi za madaktari bingwa.

MHE. BASHUNGWA ALINYOOSHEA KIDOLE BARAZA LA ARDHI KARAGWE, HAKI ITOLEWE  KWA WAKATI.Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo ...
13/11/2024

MHE. BASHUNGWA ALINYOOSHEA KIDOLE BARAZA LA ARDHI KARAGWE, HAKI ITOLEWE KWA WAKATI.

Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa ametoa wito kwa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kuboresha utaoji huduma wa Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya liweze kutenda haki kwa wakati katika usuluhishi wa migogoro na kupunguza malalamiko ya Wananchi ili kukomesha migogoro ya Ardhi Wilaya ya Karagwe.

Bashungwa ametoa rai hiyo leo Novemba 13, 2024 Wilayani Karagwe Mkoani Kagera katika Kikao cha Baraza la Madiwani cha kujadili taarifa za robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2024/25 kilichohusisha Watendaji wa Halmashauri na Kata.

“Mwenyekiti wa Halmashauri tutupie jicho na kuboresha Baraza la Ardhi ili kupunguza malalamiko ya wananchi, Mabaraza ya Ardhi yanapochelewesha haki kwa kumzungusha mwananchi ni gharama kubwa na yanatia umasikini”, amesema Bashungwa.

Ameitaka Halmashauri kufanya tathmini ya utoaji huduma wa Baraza hilo ili kujua changamoto zinazokwamisha utoaji wa haki kwa wakati na wanaohusika kukwamisha waweze kuchukuliwa hatua.

Bashungwa ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kujikita katika mipango miji na upimaji wa ardhi katika maeneo yanayoendelea kukua ili kuendana na uwekezaji unaofanywa na Serikali katika miundombinu ili kuepusha migogoro ya ardhi kwa wananchi.

Aidha, Bashungwa ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe kuweka mipango mahsusi na kufanya kampeni endelevu ya utunzaji wa mazingira kwa kupanda miti ya vivuli pamoja na matunda ili kusaidia utunzaji wa mazingira na vyanzo vya maji.

Kadhalika, Bashungwa ameeleza kuwa Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi ina mpango wa kupeleka Kivuko katika Ziwa Burigi kitakachotoa huduma ya usafiri kwa wananchi wa Mirilo na Ruita katika Kata ya Rugu ili kuondokana na matumizi ya mitumbwi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe, Wallace Mashanda amewasisitiza Waheshimiwa Madiwani kuendelea na mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi katika maeneo yanayowazungu

RAIS SAMIA ABORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NCHINI NA HIZI HAPA NI SABABU 10 ZA KWANINI UWEKEZE TANZANIA   Dhamira ya dha...
13/11/2024

RAIS SAMIA ABORESHA MAZINGIRA YA UWEKEZAJI NCHINI NA HIZI HAPA NI SABABU 10 ZA KWANINI UWEKEZE TANZANIA



Dhamira ya dhati ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kutaka kumwondoa Mtanzania kwenye umasikini sasa inaonekana kwa vitendo.

Ieleweke ndani ya miaka mitatu Rais Samia amefanikiwa kuboresha kwa kiasi kikubwa mazingira ya uwekezaji na sasa Tanzania inaibuka kwa kasi kuwa kivutio kikuu cha uwekezaji barani Afrika na kuvutia wawekezaji wa kikanda na kimataifa.

Zipo sababu za msingi zinazovutia uwekezaji nchini k**a vile:-

1. Mazingira Imara ya Kisiasa:- Tanzania ina rekodi kubwa ya utulivu wa kisiasa ikilinganishwa na nchi nyingi za ukanda huu.

2. Kujitolea kwa serikali kwa mabadiliko ya amani ya mamlaka, demokrasia na utawala bora hutoa mazingira salama kwa uwekezaji.

3. Utulivu katika uongozi wa kisiasa na kuzingatia sera rafiki za kibiashara na uwekezaji kunaifanya Tanzania kuwa tegemeo la kuvutia wawekezaji wanaotafuta usalama na mazingira wezeshi.

4. Uchumi Unaokua Haraka :-Uchumi wa Tanzania umekuwa ukikua kwa kasi, huku viwango vya ukuaji wa kila mwaka mara nyingi vikizidi wastani wa kikanda.

5. Nchi imepata maendeleo makubwa katika uchumi kupitia sekta za viwanda, kilimo na huduma za ujenzi.

6. Utajiri wa Maliasili:- Tanzania imebarikiwa kuwa na maliasili nyingi, zikiwemo madini k**a dhahabu, almasi, vito, pamoja na hifadhi kubwa ya gesi asilia.

Juhudi za serikali za kuboresha na kudhibiti sekta ya madini na nishati zimeunda fursa mpya kwa wawekezaji, kwani mahitaji ya rasilimali hizi yanaendelea kuwa juu.

7. Sera na Vivutio Vizuri vya Uwekezaji :- Serikali imeanzisha sera za kuboresha mazingira ya biashara na kutoa motisha kwa wawekezaji ikiwemo kufanya marekebisho ya sheria ya uwekezaji mwaka 2022

Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kina jukumu kubwa katika kukuza uwekezaji na hutoa huduma ya "onestop-centre" ili kurahisisha michakato.

8. Marekebisho ya kupunguza urasimu, kupambana na rushwa, na kuhakikisha u

Address

Mbezi
Dar Es Salaam

Telephone

+255755990645

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mpili Sports News posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Mpili Sports News:

Share