![AJALI YA NDEGE COMORO BADO KITENDAWILIBALOZI wa Tanzania nchini Comoro, Pereira Ame Silima, amethibitisha kutokea kwa aj...](https://img5.medioq.com/394/468/151810643944680.jpg)
27/02/2022
AJALI YA NDEGE COMORO BADO KITENDAWILI
BALOZI wa Tanzania nchini Comoro, Pereira Ame Silima, amethibitisha kutokea kwa ajali ya Ndege ya Fly Zanzibar na kusema juhudi za kuwatafuta abiria wa ndege hiyo na marubani wake wawili ambao ni raia wa Zanzibar zinaendelea.
Amesema vikosi vya uokozi kutwa nzima vimekuwa vikiendelea kuwatufata abiria hao waliokuwemo katika ndege hiyo huku yakionekana baadhi ya mabaki yakiwemo matairi.
Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano Usafirishaji na Uchukuzi, Amour Hamil Bakari, amesema wamepokea taarifa za tukio hilo na wanafuatilia kwa karibu kujua taarifa kamili kupitia ubalozi wa Tanzania nchini Comoro.
''Ndege imesajiliwa Zanzibar lakini imekuwa ikifanya kazi zake za kutoa huduma za usafiri wa abiria katika visiwa vya Comoro baada ya kukodiwa, " amesema
Aidha, Waziri wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Watoto, Nassor Ahmed Mazrui, amesema kijana wake aliyekuwa rubani wa pili katika ndege hiyo hajulikani alipo baada ya ajali hiyo.
''Familia tumekutana hapa huku tukitegemea zaidi kupata taarifa kutoka katika ubalozi wa Tanzania uliopo Comoro kuhusu ajali ambayo imehusisha mjukuu wetu'' amesema.
(Picha kwa hisani ya Millard Ayo)