Mecky TV

Mecky TV Huu ni ukurasa rasmi wa chaneli ya mtandao ya Mecky Tv Tanzania/Karibu kupata habari zote hapa.!

Finally💋
05/04/2023

Finally💋

Corazon 💙🤍
03/04/2023

Corazon 💙🤍

Chaga Queen 👑💋
02/04/2023

Chaga Queen 👑💋

Mi Amor❤️
01/04/2023

Mi Amor❤️

27/03/2023

Mambo💋

I have reached 400 followers! Thank you for your continued support. I could not have done it without each of you. 🙏🤗🎉
26/03/2023

I have reached 400 followers! Thank you for your continued support. I could not have done it without each of you. 🙏🤗🎉

Chris Ferdinand,Mzaliwa wa Afrika Kusini Mwenye Asili Ya Uingereza,Harakati za maisha zikamfanya ausake uraia wa Tanzani...
03/12/2021

Chris Ferdinand,Mzaliwa wa Afrika Kusini Mwenye Asili Ya Uingereza,Harakati za maisha zikamfanya ausake uraia wa Tanzania Na akaupata,Lakini baada ya kupata hela nyingi kupitia biashara ya Madini na Dhuluma kwa wenzake vikageuka kuwa mateso kwake..

Simulizi ya mkasa wa Fedy Tayari ipo Youtube .

Link hii hapa kutazama sehemu ya kwanza.
https://youtu.be/chtUf3TbMEg

NISAMEHE VANILLA-  Mwandishi : Mecky MchaneSEHEMU YA KWANZA (01)Kelele za kukonga nyoyo zilisika huku watumbuizaji wa mu...
20/08/2021

NISAMEHE VANILLA- Mwandishi : Mecky Mchane
SEHEMU YA KWANZA (01)

Kelele za kukonga nyoyo zilisika huku watumbuizaji wa muziki wa 'live band' wakiweka vionjo vya kufurahisha kundi kubwa la watu waliojumuika kusindikiza wikiendi ile.

Kwangu ilikuwa tofauti,sikuwa na furaha wala shangwe k**a wale watu waliokua katika ile 'Club'.

Akili yangu na moyo wangu vyote kwa pamoja vilishirikiana kutafakari juu ya mtu ambae ameniomba nikutane nae viwanja vile na nilikuwa sijawahi kuonana nae,nilikua na maswali mengi ambayo nilijiuliza,lakini baada ya maswali yote niliishia kujisemea 'aah maisha yenyewe ni haya haya', kauli hii ilinisaidia kuendelea kuwa na hali ya kujiamini na kuwa tayari kwa mazungumzo ambayo yalitarajiwa kufanyika na mtu ambaye nilifahamiana nae kupitia mtandao ambaye alijitambulisha kwa jina moja la Vanilla.

Masaa takribani mawili yalipita sikuona mtu atokee sehemu niliyokuwa nimeketi,ilikuwa ni saa 5 za usiku,nilianza kukata tamaa huenda miadi yetu isiende k**a tulivyopanga.

Wakati nikiendelee kuulazimisha moyo uendelee kupata radha safi ya kinywaji cha 'wine' hatimae mwanadada mrefu akiwa amevalia raba nyeupe,tight nzito ya rangi nyeusi,t-shirt la rangi mchanganyiko huku usoni akijinasisha miwani ya gharama mithili ya wadada wa kituruki aliingia sehemu ile.

Kila mtu alimuangalia yeye na kusubiri wajue anaenda kukaa meza gani,hata mimi sikuamini k**a angekuja upande wangu,alisimama kwa muda akitazama huku na kule,nilitaka kuita kwa sauti lakini nilihisi huenda akawa sio yeye.

Nikatoa simu yangu na kupiga namba yake,baada ya kuniona nimeweka simu sikioni hakuona haja ya kupokea,taratibu aliwapita watu kadhaa waliokuwa wakipata vinywaji na kufika meza niliyokuwa nimeketi.

'Aaah...bila shaka wewe ni Albert.. !' " naam ..hujakosea na wewe ni Vanilla sio..?" " ni mimi"

Baada ya majibizano yale Vanilla alinikumbatia kwa nguvu huku akishangalia,kwake ikikuwa furaha kubwa kuniona mimi,lakini bado nilikuwa na wasiwasi kwa nini aniamini kiasi kile.

Tulikaa na kuagiza vinywaji laini ili tuweze kuendelea na mazungumzo.

"Albert k**a tulivyokisha tambulishana,mimi majina yangu ni Vanilla Crispin...aaah nimehitimu shahada ya sheria chuo kikuu cha Dar es Salaam..vipi kuhusu wewe..?

Swali lake likawa gumu kidogo kwangu,mimi hata hizo shahada sizijui elimu yangu sio rasmi sana nilishindwa kujibu swali lake kwa wakati ule,upesi nikamuita mhudumu..

'Yes naam boss' "aah ebu tuletee maji,yasiwe ya baridi sanaa" " ok sawa usijali".

Baada ya mhudumu kutoka ilibidi nipotezee lile swali moja kwa moja na kuanzisha mazungumzo mengine.

Vanilla alionekana kuwa muwazi sana kwangu,alikuwa huru kujielezea kuliko vile mimi nlivyojielezea,mazungumzo yake yalionyesha kuwa ni mtu aliezama katika hisia nzito za kimapenzi juu yangu,lakini sikuwa haraka sana kutaka kwenda naye sawa kwani bado hatukuwa tumefahamiana sana.

"Albert..waonaje tuchukue kidogo pombe ....nahisi moyo wangu unahitaji kitu kizuri..." " kwanini pombe..? Leo ni mara yetu ya kwanza kuonana na mazungumzo yetu ni muhimu tukawa wazima wote" nilijaribu kumshawishi Vanilla asitumie kilevi lakini jitihada zangu hazikufua dafu,sauti nyororo ya Vanilla ilikata ubishi wote nikabaki kuwa mtumwa wa kila alichokisema.

Kadri muda ulivyozidi kwenda mazungumzo yetu yakatawaliwa na mada za mapenzi,kila mtu alionyesha hisia nzito kwa mwenzake na kabla ya kukutana Vanilla alionesha hisia fulani za kushawishika na mimi.

"Vanilla muda umeenda sasa,hii sehemu sio nzuri sana kukaa mpaka muda huu ,na pia kuondoka usiku sana sio vizuri kwako...naomba tuondoke"
Nilijaribu kumshawishi Vanilla tuweze kuondoka kwani mazungumzo yetu yalipoteza maana baada ya wote kuanza kuendeshwa na akili za pombe..

Haikuwa rahisi kumtoa Vanilla pale,alizidi kunishawishi tuendelee kubaki tofauti na hapo tuingie kupumzika 'gest house' mpaka kesho yake asubuhi,baada ya hapo tutafahamiana zaidi.
Akili yangu ilijawa na wasiwasi,kwa kiasi fulani sikuweza kumuamini Vanilla moja kwa moja,..nilijiuliza maswali mengi,...kwanini atake kulala na mimi na tumeonana kwa mara ya kwanza?? ...kwanini hataki kunifahamu zaidi..?? Lakini pia Vanilla alikuwa na kiasi kikubwa cha fedha kwenye ka mkoba kake alichoingia nacho pale club,nilishindwa kuelewa hela zote zile za nini na ana lengo hilo la kuwa karibu na mimi au kuna jambo jingine anataka kutoka kwangu.

Nilimwambia anyanyuke ili tukachukua chumba maana hali yake iliendelea kuwa mbaya zaidi na aliendelea kulewa.. "Albert ......naomba...naomba ...katafute chumba,..kiwe na shuka jekundu tu...." Vanilla aliongea kwa kusitasita akiwa taabani sasa,lakini kauli yake ilinishangaza kidogo,kwanini shuka jekundu?..yupo 'serious' au anaongea tu kwa sababu kalewa..kabla sijafanya kitu Vanilla alijaribu kusimama tayari kwa kuondoka pale lakini kwa bahati mbaya alianguka kwani alikuwa kalewa sana...

Watu kadhaa walisogea pale karibu na meza yetu na kuuliza nini kinaendelea, "Aah...hamna ...tatizo..nahisi amelewa sana ..."

Nilikuwa na wasiwasi kidogo na niliwataka watu watoke ili niweze kumpeleka chumbani.Upesi tulisaidiana na kijana mmoja aliekuwa jirani na pale na kumbeba Vanilla mpaka chumba kimoja cha guest pale.

Kimya kilitawala ndani ya chumba kile,Vanilla akiwa hajitambui,macho yangu hayakuta kufumba hata sekunde moja kwani bado niliyakumbuka maneno ya Vanilla aliyonitaka nitafute chumba chenye mashuka mekundu tu..na mle ndani ni mashuka meupe ndio yalitawala.
Nilijisogeza kitandani vizuri na kuuangusha mwili uliojawa na uchovu huku nikivuta shuka kwaajili ya kujipumzisha.

Haikuwa hali ya kawaida kwangu,nilianza kuhisi k**a sehemu ile inajaa hewa nzito ambayo haikuwa ya kawaida,nilijaribu kuugusa mwili wa Vanilla nilishtuka kwani ulikuwa ni wa baridi sana. Nilianza kushikwa na hofu nikiwa sijui nifanye nini..niliamua kunyanyuka na kwenda kufungua mlango ili nitoke nje kwanza kwa muda kwani hewa ya mle ndani haikuwa rafiki kwangu,lakini Vanilla wala hakuonesha dalili yoyote ya kuumizwa na ile hewa.

Punde tu baada ya kutoka nje ya chumba pale nikiwa nimesimama kwenye 'korido' ya ile nyumba ya wageni ghafla taa ya chumba chetu ilizima,sikuelewa nini kimetokea kwani swichi ilikuwa mbali na Vanilla alikuwa kalala fofofo,sasa imetokeaje taa imezima?..ni swali ambalo tuliulizana mimi na hewa tu pale kwani hakuna mtu ambaye angeweza kunijibu.

Kabla sijachukua hatua yoyote nilishangazwa na kilichoendelee kutokea,nikijihisi nipo ndotoni...." Aah hapana nini hiki.....!!!"

inaendelea .......

Simulizi hii imesimuliwa ipo youtube tayari ya "meckytv tz".

Kutazama mwendelezo ingia youtube andika "meckytv tz utakuta ipo kuanzia sehemu ya kwanza.

Au bonyeza link hii https://youtu.be/LJ6yddWB4aQ

Usisahau ku Like Page hii na pia Ku subscribe channel yetu ya "meckytv tz "

  Like Page Yetu kujifunza mengi zaidi.
16/04/2021



Like Page Yetu kujifunza mengi zaidi.

📌Alizaliwa miezi sita baada ya baba yake kuuwawa kwenye mapigano dhidi ya Utawala wa Kihispaniola.Mwamba akafanikiwa kus...
13/04/2021

📌Alizaliwa miezi sita baada ya baba yake kuuwawa kwenye mapigano dhidi ya Utawala wa Kihispaniola.Mwamba akafanikiwa kusoma sheria,kiongozi alietumikia nafasi nyingi muhimu serikalini, akawa gavana mdogo zaidi, akawa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Ufilipino, MANUEL ACUNA ROXAS...

Na Mecky Mchane

MANUEL ACUNA ROXAS, alizaliwa jimbo la Capiz huko Ufilipino mnamo Jan 1, 1892, miezi sita baada ya mauaji ya baba yake aliyeuwawa na utawala wa Hispania.

Mwamba akapata elimu ya msingi kwao Capiz na elimu ya juu aliipata katika jiji la Manila,na huko Hong Kong kwa muda mfupi.Mihogo ya chuo alianza kula akiwa na miaka 17 tu😊, ambako alienda kupata degree ya sheria (LL.B degree) katika chuo kikuu cha Ufilipino(The New University Of The Phillipines) mwaka 1913.

Baada ya hapo akaona haitoshi, Roxas akaendelea kusoma mpaka pale alipoona ameshika vizuri lugha tatu zilizokuwa zikichuana kwenye uwanja wa siasa kwa wakati huo huko Ufilipino(Kiingereza, Kihispaniola na Ki Tagalog ). Roxas alitumia muda wake pia kufundisha sheria National University (NU) pale Manila kuanzia mwaka 1915-1916.

Vyeo vilianza kumiminika kwa bwana Roxas ambapo mwaka 1919 akapata nafasi ya kuwa Gavana wa Capiz na akawa Gavana mdogo zaidi kwenye jimbo lake. Hakuishia hapo upepo ukamuendea sawia, mwaka 1921 akawa kwenye baraza la uwakilishi (Philippines house of representatives).

Neema za uongozi zikaendelea kumiminika zaidi mithili ya koki bovu, akaaminika zaidi na utawala uliokuwa madarakani,wakati huo Ufilipino ikiwa katika mfumo wa Commonwealth, 1922 Roxas akawa msemaji wa serikali akichukua nafasi ya Sergio Osmena aliehamishwa kuwa Seneta.

Miaka ya hapo kati bwana Roxas akatumikia vyeo vingi zaidi vya muhimu katika serikali ya Ufilipino kuliko mfilipino yeyote kabla yake.
Kumbukumbu nyingi za Roxas zikawa na utata.
Baadae akawa Luteni kanali (lieutenant colonel ) kwenye jeshi la akiba la Ufilipino.

Mambo yakabadilika mara Mjapan akatia mguu kufanya uvamizi, jamaa hakuchelewa, akaamua kuomba ushirika kwa Jenerali Douglas MacArthur wa US Forces. Baadae MacArthur na maofisa wa Ufilipino wakahamishiwa huko Australia Bwana Roxas akatimkia kisiwa cha Mindanao.

Baadae akawa panya kwenye mtego wa mjapani lakini hata hivyo alifanikiwa kutoka akiwa salama., MANUEL ROXAS akaja kuwania urais nchi ikiwa katika mfumo wa Commonwealth akafanya kampeni ya nguvu katika uchaguzi uliofanyika Aprili 23, 1946, Roxas akashinda.

Asubuhi moja ikabeba historia mpya tena katika maisha ya Manuel Acuna Roxas, ilikuwa ni July 4 ya mwaka 1946 USA akatangaza kuwa Phillipines iko huru, mizinga 21 ilipigwa, watu zaidi ya laki 2 warishuhudia tukio hilo viwanja vya Luneta Park katika jiji la Manila.

Manuel Acuna Roxas akawa rais wa mwisho wa utawala wa Commonwealth na akawa rais wa kwanza wa Jamhuri ya Ufilipino, sera za Roxas zikapata nguvu kubwa na kuungwa mkono na watu wake.

Haikuwa bahati kwa Roxas kumaliza miaka minne ya mhura wake, asubuhi ya tar 15 April, 1948 Roxas alitoa hotuba pale Cark Field karibu na Manila, punde tu baada ya kuhutubia alijihisi kuumwa, baadae usiku shambulio la moyo likazima mshumaa wa uhai wa bwana MANUEL ACUNA ROXAS.
Ilikuwa ni April 17, 1948 siku mbili baada ya kifo cha Roxas, makamu wa rais Elpidio Quirino akaapishwa kuwa rais wa Ufilipino.

Kumbukumbu nyingi zimewekwa kumuenzi Manuel Roxas ambapo kuna miji k**a Roxas city ilipewa jina lake pamoja na sura yake kuwekwa kwenye sarafu.

Ungana Nasi...

Facebook : Twitter : Instagram:

meckytv

Like PAGE YETU HAPA YA Meckytv  Kisha follow account zetu za INSTAGRAM PAMOJA NA TWITTER  Youtube: meckytv
13/04/2021

Like PAGE YETU HAPA YA Meckytv Kisha follow account zetu za INSTAGRAM PAMOJA NA TWITTER

Youtube: meckytv

10/04/2021

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255789102915

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Mecky TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share


Other News & Media Websites in Dar es Salaam

Show All