Mwananchi amependekeza siku ya Ijumaa iingizwe katika siku za mapumziko na Jumamosi iwe siku ya kazi ili kuweka urahisi kwa waumini wa dini ya Kiislamu kufanya ibada.
Mwananchi mmoja amependekeza kuwa, kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, bei ya kulipia ving'amuzi ipunguzwe au huduma ya ving'amuzi itolewe bure kwa wananchi.
Viongozi wa Serikali ya Wanafunzi kwenye vyuo vya kati na vyuo vikuu wameomba serikali kuwalipa mishahara kila mwezi pamoja na kuanzishwa kwa mfumo utakaowawezesha vijana kupata ajira baada ya kuhitimu vyuo.
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman amesema ni wakati wa vijana kutoa maoni na ushauri kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ili kuchangia ufanisi wa dira hiyo.
Mwananchi Hamis Mnubi amependekeza umeme usikatike tena nchini mpaka 2050 kwakuwa kuna miradi mingi ya maendeleo inayotegemea umeme.
Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Hemed Suleiman amesema ni wakati wa vijana kutoa maoni na ushauri kuhusu Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050 ili kuchangia ufanisi wa dira hiyo.
Wakili Jebra Kambole amesema Mahakama imesogeza mbele kusikiliza zuio la TAMISEMI kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka huu mpaka Septemba 02, 2024.
Wakili Peter Madeleka amesema hawajaridhishwa na maamuzi ya mahakama dhidi ya kesi ya viongozi wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) Wilaya ya Temeke ambao wanadaiwa kushikiliwa na jeshi la polisi, ambapo mahakama imesema hakuna ushahidi wa kutosha kuthibitisha tuhuma hizo.
Mahakama Kuu Dar es Salaam, imesema hakuna ushahidi unaoonesha kwamba viongozi wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) Wilaya ya Temeke wanashikiliwa na jeshi la polisi.
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amepiga marufuku kwa mamlaka zote za maji nchini kutoa huduma ya maji usiku wa manane wakati ambao wananchi wamelala.
Waziri wa Maji, Jumaa Aweso amesema wasoma mita za maji wanapaswa kuwafundisha wananchi jinsi ya kusoma mita zao ili kuepuka kutoa gharama zisizo sahihi.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Kenani Kihongosi amesema wananchi wa Mkoa huo hawatoi ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kuhusu taarifa za uhalifu pindi zinapohitajika badala yake wanalindana.
Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tamasha la Kizimkazi linalofanyika Visiwani Zanzibar ni tamasha la Kitaifa, hivyo litakuwa mikononi mwa Taifa.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi amemuagiza Mkurugenzi wa Tarafa ya Ngorongoro kufungua vituo vyote vilivyopangwa kwa ajili ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili viweze kufanya kazi yake.
Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza kurejeshwa kwa huduma za kijamii ikiwemo afya na shule zilizokuwa zimesitishwa na zingine kutotolewa kikamilifu katika Tarafa ya Ngorongoro.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri (Sera, Bunge na Uratibu), William Lukuvi wakati akisikilikiza wananchi hao waliokuwa wamekusanyika na kukesha kwa siku tano wakitaka kujua hatima ya malalamiko yao.
Rais Samia Suluhu Hassan amesema ameongea na wawekezaji wakubwa nchini kusaidia vilabu vya Yanga na Simba ili timu hizo zisonge mbele zaidi.
Rais Samia Suluhu ameagiza uwanja wa Suluhu Sports Academy kukamilika kwa wakati na kwa ubora ili uweze kutumika katika Mashindano ya Mataifa ya Afrika (CHAN).
Rais wa Yanga SC, Eng. Hersi Said amesema Ally Kamwe ndiye Afisa Habari wa Yanga SC, na Haji Manara ni mwanachama ambaye anatafutiwa nafasi atakayoweza kuhudumu klabuni hapo.
"Rais wa Klabu sio mfanyakazi wa klabu, wala haajiriwi na klabu, wala hapati shilingi 100 kutoka kwenye klabu." - Eng. Hersi Said, Rais wa Yanga SC
VIDEO: @wasafitv
Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa chama cha ACT- Wazalendo, Abdul Nondo ameshauri kuwa na Benki ya Maendeleo ya Vijana ambayo vijana watakuwa na uwezo wa kwenda kukopa kwa riba ndogo zaidi.