Tenda Radio Tz

Tenda Radio Tz New's /Entertaining /Music/ Sport's and Interviews News /Blog na Gilly Bonny

10/05/2024



Usiikose hii. Tusikilize upate fursa, ubadili maisha yako kiuchumi.

Mei 10, 2024 saa 2 Asubuhi hapa Jembe FM.

Tenda Radio imekita kambi jijini Arusha, kuzichambua fursa ya bajeti ya zaidi ya Sh. 104 Bilioni zilizowekwa kwenye Mfumo wa NeST na Halmashauri ya Jiji la Arusha, na jinsi wewe unavyoweza kupata sehemu ya bajeti hiyo. Tuko na Mkurugenzi wa Jiji hilo, Mhandisi Juma Hamsini na walioshinda tenda wanafunguka siri ya ushindi.

18/04/2024

Afisa Mtendaji Mkuu wa BRELA, Bw. Godfrey Nyaisa anaeleza uzoefu wake na Mfumo wa NeST, tunapataje fursa bila 'janja-janja'?

.matinyi

  Heri ya siku ya kuzaliwa (Happy Birthday) mtangazaji wa Tenda Radio na  Tunakutakia kila lenye heri, na kazi yako nzur...
16/04/2024


Heri ya siku ya kuzaliwa (Happy Birthday)
mtangazaji wa Tenda Radio na

Tunakutakia kila lenye heri, na kazi yako nzuri iendelee kuwapa watanzania njia ya kushiriki na kupata tenda za Serikali kupitia Mfumo wa NeST.

Serikali ya Tanzania imekanusha madai ya Mashirika ya Kitaifa na Kimataifa kwamba imewak**ata Watu watatu (Dkt. Slaa, Md...
16/08/2023

Serikali ya Tanzania imekanusha madai ya Mashirika ya Kitaifa na Kimataifa kwamba imewak**ata Watu watatu (Dkt. Slaa, Mdude na Wakili Mwabukusi) kwasababu ya kukosoa mkataba wa Uwekezaji wa Bandari ambapo imesema madai hayo sio ya kweli bali Watu hao wamek**atwa kwasababu za kuitisha maandamano ya kuiondoa Serikali madarakani.

Taarifa iliyochapishwa kwenye ukurasa wa mtandao wa X wa Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Nape Nnauye

imesema “Hakuna aliyek**atwa na hakuna ambaye atak**atwa Tanzania kwa kukosoa mkataba wa Bandari na mradi , mpango, programu au sera yoyote kuhusu mkataba huo”

“Watuhumiwa wamek**atwa kwa kutishia kufanya maandamano ya kuiondoa Serikali madarakani, pia kuhamasisha Wananchi kuwashambulia Polisi, wamek**atwa ili kufikisha ujumbe mzito kwa Wakosoaji wanaofikiria kufanya makosa yoyote ya kijinai”

“Kuk**atwa kwa Watu hao hakuzuii uhuru wa kutoa maoni Tanzania ila ni sehemu ya hatua za kisheria zinazolenga kuzuia maandamano yanayoweza kusababisha uasi dhidi ya Serikali iliyochaguliwa Kidemokrasia”

“Tangu imeingia madarakani March 2021 Serikali ya Rais Samia imekuza demokrasia kwa kuondoa vikwazo vya kisiasa kwa Vyama vya Siasa ikiwemo kuruhusu mikutano ya kisisasa, kuruhusu Online TV na magazeti yaliyofungiwa kufanya kazi na kuboresha uhuru wa kujieleza”

15/08/2023

MANENO YALIYOPELEKEA DKT SLAA NA WENZAKE KUSHIKILIWA NA POLISI

SEHEMU YA PILI."Kwa Mfano kwenye kata yetu kuna vikundi vinne vya vijana ambao wamenufaika na IITA, Vikundi Viwili vya w...
12/08/2023

SEHEMU YA PILI.

"Kwa Mfano kwenye kata yetu kuna vikundi vinne vya vijana ambao wamenufaika na IITA, Vikundi Viwili vya wanawake wamepata bahati ya kupata mafunzo ya namna ya usindikaji wa unga wa Miogo na hatmaye wameweza kutengeneza keki na Biscuti, wamejiajiri, wametengenezea watu wengine ajira na wengine wamepewa maeneo kwa ajili ya Ufugaji wa kuku, wamtupa sana ushirikiano, sisi tunafurahia pamoja na mambo mengine Nchi yetu ina tatizo la ajira kwa hiyo hii taasisi imeisaidia sana Serikali kupunguza tatizo la ajiria". Ameeleza Bw. Alen.

Kwa upande wake Afisa Uhusiano na Msaada, Mradi wa Enable TAAT kutoka IITA Augustin Deogratitus amesema miongoni mwa malengo ya taasisi hiyo ni kutoa mafunzo kwa vitendo bure, Kulea Vijana, ufugaji wa Samaki, kufuga Kuku, kuchakata Muogo kuanzia hatua ya kwanza hadi ya mwisho mpaka kuzalisha Wanga, kuwafikia Vijana na Wakulima kwa kuwapa mafunzo kwa njia ya Mtandao au ana kwa ana na kuwajengea uwezo wa kujiajiri kwa kuanzisha biashara zao ili waweze kuajiri watu wengine.

Aidha Wakizungumza kwa niaba ya wenzao, Wanufaika wa Mafunzo hayo Getrude Amon, Baraka Ayub na Husein Acta wameeleza kufurahishwa na Kile kinachofanywa na Taasisi ya IITA na kuahidi watachukua hatua za haraka kujiunga na utaratibu wa kupatiwa Mafunzo kwa vitendo ili waweze kuwa bora zaidi na kujipatia kipato katika shughuli za Uzalishaji huku wakitoa wito kwa Vijana wengine kuchangamkia fursa hiyo.

Mwisho.

Katika kuadhimisha siku ya Vijana Duniani, Taasisi ya Kimataifa Isiyo ya Kiserikali inayojishughulisha na Utafiti katika...
12/08/2023

Katika kuadhimisha siku ya Vijana Duniani, Taasisi ya Kimataifa Isiyo ya Kiserikali inayojishughulisha na Utafiti katika Mazao ukanda wa joto, International Institute of Tropical Agriculture (IITA) imewapatia mafunzo ya elimu ya ujasiriamali katika kilimo biashara ( Agribusiness) ili kujiajiri kupitia Kilimo zaidi ya Vijana 200 kutoka Wilaya ya Ubungo na Wilaya ya Kinondoni Jijini Dar-es Salaam.

Mafunzo hayo ambayo ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya vijana dunia yamefanyika tarehe 10 na11 Agosti, 2023 katika kata mkoa wa Dar-es Salaam kwa kushirikishiana na Halimashauri ya Ubungo, African -Asia Foundation na African Youth Transformation.

Mafunzo hayo yamewakutanisha vijana kwa lengo la kujadili changamoto mbalimbali zinazowakabili ikiwemo tatizo la ukosefu wa ajira na njia zipi za kuweza kuzitatua kupitia Kilimo biashara katika mnyororo wa thamani, Ufugaji na Ujasiriamali. ikiwa ni Sehemu ya kuadhimisha kilele cha siku ya Vijana Duniani ambayo hufanyika kila mwaka tarehe 12 Agost.

Mwaka huu 2023 maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani Kitaifa yamebebwa na kauli mbio Isemayo *"Kuelekea 2030, Tanzania ya Viwanda, BORESHA ELIMU kwa Vijana kwa Maendeo ya Taifa"*

Afisa Mtendaji wa kata ya Kwembe Bi. Rozina Kimario ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mafunzo hayo amewataka vijana kujiepusha na Makundi maovu na badala yake wajitambue na kuchangamkia fursa zinazotolewa na taasisi ya IITA ili waweze kupata Mafanikio kupitia kilimo, Ufugaji na Ujasiriamali kwa manufaa yao, familia wanazotoka, Jamii na Taifa kwa ujumla.

Naye Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Kwembe Bw. Alen Mhindo amesema Taasisi ya IITA imekuwa na mahusiano mazuri na Serikali, wamekuwa wakifanya kazi pamoja katika kuwawezesha vijana kwa zaidi ya miaka minne sasa, na imekuwa ikiwasaidia vijana ambao wamenufaika na fursa ya mikopo ya 10% ya Halmashauri kwa kuwapa maeneo kwa ajili ya Ufugaji, na kuwaruhusu kufanya shughuli na Uvuvi kwenye Mabwawa yao ya samaki yaliyopo katika kituo Chao cha mafunzo ( Youth Incubation Centre) Wilayani hapo.

INAENDELEA SEHEMU YA PILI.

Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Songwe imetekeleza kwa vitendo agizo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano T...
11/08/2023

Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Songwe imetekeleza kwa vitendo agizo la Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi la kuhakikisha barabara za lami zinajengwa na kuweka taa za barabarani katika maeneo yote yanayozunguka Miji yalipo Makao Makuu ya Ofisi za Serikali kote Nchini.

Hayo yamebainishwa hivi karibuni na Kaimu Meneja wa TANROADS mkoa wa Songwe Mhandisi Suleiman Bishanga alipozungumza katika Mahojiano Maalum na kipindi cha TANROADS mkoa kwa mkoa, Toleo Maalum la Mkoa wa Songwe la Miradi ya Barabara za Mikoa.

Amesema " Mkoa wetu wa Songwe tunafanya maboresho ya miji yetu ambalo ni agizo la Serikali kwamba mikoa yote lazima tuboreshe Maeneo ya miji ili magari na watu wetu waweze kupita kirahisi kwenda Makao Makuu ya Mkoa, hapa tunajenga barabara kwa kiwango cha lami na tutaendelea kuweka taa za barabarani hasa katika maeneo ambayo taa hazikuwekwa hapo awali".

"Hapa tuliposimama ni maingilio ya kwenda makao makuu ya mkoa wa wetu na pia ndipo zilipo Ofisi zetu za TANROADS mkoa, na Ofisi nyingi za Serikali zinaendelea kujengwa katika eneo hili, tunataka watu wanaopita hapa kwenda Mbeya na Tunduma waweze kusafiri na kupita katika maingilio haya vizuri kabisa" ameongeza Mhandisi Bishanga.

Amesisitiza kuwa TANROADS itaendelea kujenga na kuboresha Miundombinu katika maeneo mengine ya mkoa huo ikiwa ni pamoja na kuongeza taa za barabarani katika Miji ya Mlowo na Vvawa, Kuweka taa katika Barabara ya Mahenje, Kamsamba -Vvawa sehemu ya Kimondo na kwa Mwaka wa fedha unaokuja Serikali itaendelea kutekeleza miradi mingine ya maendeleo na maboresho ya barabara.

Mhandisi Bishanga ameongeza kuwa "katika Hospital yetu ya mkoa, tayari tumeshajenga kipande cha lami sasa tunakwenda kuweka taa za barabarani, tutaendelea kuboresha sehemu nyingine ambazo tayari zinaonekana kukua ili wananchi wanufaike na maendelezo ya barabara hizo".

Mashabiki na viongozi wa klabu ya Simba waliofika katika tamasha la Simba Day uwanja wa Mkapa Dar es Salaam wakiwa na ma...
06/08/2023

Mashabiki na viongozi wa klabu ya Simba waliofika katika tamasha la Simba Day uwanja wa Mkapa Dar es Salaam wakiwa na mabango ya kumpongeza Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa mazuri anayoyafanya haswa katika michezo.

Rais Samia Suluhu Hassan ndiye Mgeni rasmi katika tamasha hilo.

SEHEMU YA PILI.Naye Afisa Mtendaji wa kata ya Chitete yalipo Makao Makuu ya wilaya ya Momba Ruben Silvester Pazia amesem...
05/08/2023

SEHEMU YA PILI.

Naye Afisa Mtendaji wa kata ya Chitete yalipo Makao Makuu ya wilaya ya Momba Ruben Silvester Pazia amesema "tunampongeza sana, Rais wetu Dkt. Samia kwa kuweza kusaidia ujenzi wa kipande hiki cha barabara, pamoja na kazi kubwa anayofanya, tunamuomba atuongezee barabara nyingine za lami ili  Wananchi waweze kupata huduma ya usafiri wa uhakika na hivyo kusafirisha mazao ya chakula kwa urahisi, kupunguza gharama na muda wa safari.

Aidha Mchungaji Erasto  L Siwiti wa kanisani la FPCT Chetete ameishukukuru na kuipongeza Serikali kwa Jitihada mbalimbali inazofanya kusogeza huduma ya usafiri wa  barabara za lami karibu zaidi na Wananchi huku akitoa ombi kwa Rais Dkt Samia na Watendaji wake kuendelea na jitihada zaidi za ujenzi wa miundombinu hiyo hasa maeneo ya Vijiji ili Wananchi ambao ni wazalishaji wakubwa wa mazao ya chakula wapate urahisi wa kusafirisha na kuuza mazao yao kwenda kwa walaji na hivyo kujipatia kipato.

Wakizungumza kwa niaba ya Wananchi wenzao Bwana Stefano Simsimba, Fulgence Patrick, Enock Mwasanya,  Julius Mwasoso Mgogo na Filisian Johane wote wakazi wa wilaya ya Momba wametoa pongeza nyingi kwa Rais Dkt. Samia kwa kuwakumbuka na kuanza kuwapatia barabara za lami.

Wameongeza kuwa" tumepokea kipande hiki cha barabara ya lami kwa furaha kubwa sana, mwanzo hatukuwahi kuiona lakini kwenye utawala wa Rais Dkt. Samia ndio tumeona hii lami hapa, tunamuomba aendele kutuongeza barabara nyingi zaidi za lami katika Wilaya yetu ya Momba ili tuweze kuongeza kipato katika shughuli za uzalishaji hasa pale tunaposafisha mazao yetu kwa haraka kwenda sokoni kwa kuzingatia tupo jirani na Nchi ya Zambia kibiashara hii ni fursa kwetu"

MWISHO

SEHEMU YA KWANZA.Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Songwe imekamilisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha l...
05/08/2023

SEHEMU YA KWANZA.

Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) mkoa wa Songwe imekamilisha ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kipande cha mita 500 katika Mji wa Chitete Makao Makuu ya Wilaya ya Momba ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Serikali kila Makao Makuu ya wilaya lazima miundiombinu iboreshwe.

Msimamizi wa kitengo cha matengenezo ya barabara mkoa wa Songwe Mhandisi Silvan Henry Mloka amebainisha hayo Agosti 3, 2023 alipozungumza na kipindi cha TANROADS mkoa kwa Mkoa  kwa niaba ya Kaimu Meneja wa TANROADS mkoa wa Songwe Mhandisi Suleiman Bishanga.

Amesema katika mwaka wa fedha 2022/2023 kiasi cha fedha shilingi milioni 500 kilitengwa na Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami, kuweka taa za barabarani, pamoja kujenga Makalavati kwa ajili ya njia za Maingilio.

Mhandisi Mloka amesema mradi huo umetekelezwa na Mkandarasi mzawa wa kampuni ya GNMS CONTRACTORS CO LIMITED ya Iringa, ambapo barabara hiyo ya lami ni mwanzo wa kuendeleza na kuupendezesha mji kwa ujenzi wa miundombinu bora, na kwamba kila mwaka wa fedha Serikali itaendelea kutenga na kutoa fedha kwa ajili kujenga barabara za lami mpaka hapo Mji wote wa Chitete utakapozungukwa na lami hasa katika barabara zote ambazo zinahudumiwa na TANROADS.

"Tunaishukuru na kuipongeza Serikali ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutenga na kutoa fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa barabara pamoja na madaraja, vilevile tunamshukuru Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa ambaye mara zote anasisitiza na kutusimamia kwamba kazi zifanyike vizuri kwa ueledi, pia Mtendaji wetu Mkuu wa TANROADS Mhandisi Mohamed Besta ambaye naye anatusisitiza kuchapa kazi kwa bidii na kusimamia vema kiasi cha fedha kinachotolewa na Serikali ili kitumike vizuri k**a inavyopaswa kwa kuzingatia thamani ya fedha na miradi kujengwa kwa viwango vinavyokubalika kwa maslahi ya Umma" ameongeza Mhandisi Silvan Mloka.

INAENDELEA SEHEMU YA PILI >>

Katika kuendelea kuhakikisha bidhaa ya mafuta ya petroli inapatikana kwa uhakika maeneo yote nchini, Chama cha Waagizaji...
05/08/2023

Katika kuendelea kuhakikisha bidhaa ya mafuta ya petroli inapatikana kwa uhakika maeneo yote nchini, Chama cha Waagizaji na Wasambazaji Mafuta Tanzania (TAOMAC) wamekutana na Waziri wa Nishati, Mhe. January Makamba katika ofisi ndogo za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam tarehe 4 Agosti 2023.

Katika kikao hicho, TAOMAC walitoa taarifa ya mwenendo wa biashara ya mafuta duniani na hapa nchini pamoja na kuwasilisha changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya mafuta hususani suala la upatikanaji wa dola za Marekani. Chama hicho kilifafanua kuwa uhaba wa dola za marekani katika soko la fedha kunapelekea waagizaji kupunguza kiasi cha mafuta wanachoagiza kuepuka kuagiza mzigo na kushindwa kuulipia kwa wakati jambo ambalo linaongeza gharama za uendeshaji wa biashara na kuathiri bei ya mafuta kwa mteja wa mwisho.

Akizungumza katika kikao hicho, Makamu Mwenyekiti wa TAOMAC Ndg. Salim Baabde alisema “biashara yetu inafanyika kwa kutumia Dola za Marekani na inapotokea dola inakuwa adimu sokoni inaathiri moja kwa moja bei ya uagizaji ambayo mwisho wa siku inaathiri bei ya mafuta kwa mtumiaji wa mwisho”. Aidha walieleza kuwa hali inaweza kuzidi kuwa mbaya iwapo changamoto ya upatikanaji wa dola haitatuliwa kwa haraka, “Tunaiomba Serikali kuongeza nguvu katika kuhakikisha dola zinapatikana kwa kushirikisha benki za biashara ili kuepuka changamoto hii kukuwa zaidi na kuleta athari kubwa” aliongeza Ndugu Baabde.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TAOMAC, Ndg. Raphael Mgaya alimhakikishia Mhe. Waziri kuwa pamoja na changamoto hiyo, TAOMAC wataendelea kuagiza mafuta ingawa kwa gharama kubwa ili kuhakikisha nchi inaendelea kupata nishati hiyo muhimu katika hali ya uhakika na endelevu. “Tutaendelea kuhakikisha tunalinda dhamana tuliyopewa na Serikali ya kuhakikisha nchi inakuwa na mafuta wakati wote hata k**a ni kwa gharama kubwa” alifafanua Ndg. Mgaya.

Vile vile wamemshukuru Waziri na EWURA kwa ushirikiano ambao wamekuwa wanautoa kwa tasnia hasa katika vipindi vigumu na kuahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Serikali pamoja na kuelimisha umma kuhusu biashara ya mafuta ili kukabiliana na upotoshaji mkubwa hasa mitandaoni kuhusu biashara hii.

Kwa upande wake Waziri Makamba amewashukuru kwa ushirikiano waliutoa kuhakikisha kwamba nchi inapata mafuta muda wote. Waziri Makamba pia alieleza kwamba mlango wake uko wazi wakati wote kwa ajili ya mashauriano. “Sisi hapa Wizarani filosofia yetu ni ile ya open door ambapo yeyote anakaribishwa kwa ajili ya mashauriano na majadiliano”. Aidha, Waziri Makamba alisisitiza kuwa Serikali inaelewa changamoto ambazo sekta inakabiliana nazo kwa sasa na kuwa hatua madhubuti zimeendelea kuchukuliwa. Aidha Mhe. Makamba alisisitiza umuhimu wa wadau ikiwemo TAOMAC kuendelea kushik**ana na kushirikiana ili kuhakikisha upatikanaji wa mafuta kwa uhakika kwa ajili ya ustawi wa nchi na watu wake.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Stephen Byabato, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba, Kamishna wa Petroli na Mafuta Ndg. Michael Mjinja, Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Dr. James Andilile na wataalamu kutoka Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA).

TANROADS YAPOKEA TUZO MBILI  KATIKA KONGAMANO LA NANE LA WAHANDISI WANAWAKE TANZANIA (TAWECE). Rais wa Zanzibar na Mweny...
03/08/2023

TANROADS YAPOKEA TUZO MBILI  KATIKA KONGAMANO LA NANE LA WAHANDISI WANAWAKE TANZANIA (TAWECE).

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amemkabidhi tuzo mbili Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS), Mhandisi Mohamed Besta kwa kuwa Mfadhili namba Moja wa  Mkutano wa Kongamano la Nane la Wahandisi Wanawake Tanzania.

Tuzo ya pili ni kuwa Mwajiri aliyeongoza kwa kufadhili na kuwawezesha Wahandisi wengi Wanawake kutoka TANROADS kushiriki katika kongamano hilo ambalo limefanyika leo tarehe 03 Agosti 2023 katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Airport, Zanzibar.

Akizungumza na Wahandisi hao Rais Dkt. Husein Mwinyi amesema Serikali inatambua mchango wa taaluma ya uhandisi wa fani mbalimbali katika ukuaji wa uchumi wa Taifa kupitia huduma mbalimbali ikiwemo ujenzi wa viwanda, uboreshwaji wa miundombinu, utumiaji mzuri wa rasilimali na malighafi, usafiri na mawasiliano.

Ameeleza kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zinaendelea kuweka mipango madhubuti ya kuhakikisha wanaongeza idadi ya wahandisi hasa Wanawake na mafundi sanifu.

Rais Dkt. Mwinyi ameongeza kuwa  Serikali itahakikisha inawasaidia Wasichana wanaosoma masomo ya Sayansi katika elimu ya Sekondari, Vyuo vya mafunzo ya amali na Vyuo Vikuu katika hatua ambayo itasaidia kuongeza idadi ya Wahandisi Wanawake nchini.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi) Mhe. Atupele Mwakibete ameipongeza TANROADS  kwa namna  ambavyo  walivyo j...
02/08/2023

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Uchukuzi) Mhe. Atupele Mwakibete ameipongeza TANROADS kwa namna ambavyo walivyo jipanga kutoa elimu kwa Umma k**a vile elimu juu ya Usalama Barabarani, Hifadhi ya Barabara pamoja na Upimaji wa Magari yanayozidisha Uzito kwenye Mizani na huduma nyingine nyingi tunazozitoa.

Haya yamejiri alipotembelea Banda la TANROADS katika maonesho ya kimataifa ya Nane Nane yaliyoanza tarehe 01.08.2023 katika viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya.

02/08/2023

Kampuni ya Silverlands inayoshughulika na uzalishaji wa vifaranga na chakula cha kuku imesema inaanzisha mpango mahususi utakaoishirikiana na Programu ya BBT Mifugo kuunga mkono jitihada za Mheshimwa Rais Samia Suluhu Hassan kuwawezesha vijana na akinamama katika sekta ya ufugaji ili kukuza uchumi jumuishi na kupunguza mikopo kausha damu kwenye jamii.

Hayo yamesemwa leo na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akizinduzia mtambo wa kuangua Vifaranga vya kuku katika hafla iliyofanyika Mkoani Arusha Agosti 2, 2023.

“Mipango yetu katika tasnia ya kuku kwa sasa, ni kuibadilisha tasnia kutoka kwenye ufugaji wa kimazoea kwenda kwenye ufugaji wa kisasa na wenye tija kwa wafugaji. Nawataarifu Watanzania wote kwamba sasa Silverlands wako na BBT kwa upande wa ufugaji kuku. Kwa msingi huo nawakaribisha na wawekezaji wengine wanofanya kazi hii ya kuku na wao kuungana na serikali” Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega.

Waziri Ulega ameeleza kwamba BBT inafanya vizuri kwenye upande wa mazao, ufugaji wa ng’ombe na Samaki, na hivyo anawakaribisha wawekezaji waingie pia kwenye ufugaji wa kuku ambao unapendwa zaidi na vijana na kimanana wengi.

Serikali ya awamu ya sita kupitia Wakala ya barabara Tanzania (TANROADS) inatarajia kutumia zaidi ya shilingi Trilioni 1...
02/08/2023

Serikali ya awamu ya sita kupitia Wakala ya barabara Tanzania (TANROADS) inatarajia kutumia zaidi ya shilingi Trilioni 1.133 kwa ajili ya ujenzi na upanuzi wa barabara ya TANZAM mkoani Mbeya.

Kiasi hicho cha fedha ambacho kinatolewa na Serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mheshimiwa Dkt.Samia Suluhu Hassan kitahusisha ujenzi wa njia nne kuanzia Igawa - Mbeya hadi Tunduma na barabara ya mchepuo (bypass) kuanzia mlima Nyoka mpaka Songwe na kuendelea.

Hayo yameelezwa na Naibu Waziri Wizara  Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi) Mhandisi Geoffrey M Kasekenya alipozungumza na Wananchi hapo jana tarehe 01/08/ 2023 kwenye ziara ya Makamu wa Rais Dkt Phillip Isdor Mpango muda mfupi baada ya kukagua barabara ya mchepuo Inyala km 2.8 na Upanuzi wa Barabara ya TANZAM sehemu ya Inyala - Shamwengo km 3 pamoja na ukaguzi wa zahanati ya Shamwengo iliyopo eneo la Inyala mkoani Mbeya.

"Mheshimiwa Makamu wa Rais hivi tunavyongea sasa hivi kuanzia Uyole hadi Songwe km 29 zinajengwa njia nne; na njia iliyopo haitobomolewa, itatumika k**a Mchepuko (Diversion), tunavyoongea Mkandarasi yupo, anajenga kambi na tayari ameanza kusafisha njia kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara hiyo ambayo itapita katika Jiji la Mbeya, tunahakika ikikamilika changamoto ya msongamano wa magari itapungua" ameongeza Mhandisi Kasekenya.

Naye Mbunge wa Mbeya Mjini ambaye pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson amemshukuru Mheshimiwa Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutenga kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya upanuzi wa  barabara hiyo kutoka Igawa mpaka Tunduma ambayo sehemu kubwa inapita katika Jimbo la mbeya vijiji na Mbeya mjini.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Mbeya Vijiji Oran Manase Njeza amesema pamoja na jitihada kubwa zinazofanywa; anaiomba Serikali kuendelea kuboresha miundombinu mingine ikiwemo kuharakakisha ujenzi barabara ya Mbalizi - Shigamba km 52, inayotuunganisha na Nchi Jirani ya Malawi, barabara ya Isyonje- Kikondo km 22 inayotuunganisha na mkoa wa Njombe kupitia Makete pamoja na barabara ya Mbalizi - Chang'ombe hadi Makongolosi ambako kuna migodi mikubwa ya Madini.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amekagua barabara ya mchepuo wa Inyala yenye ...
01/08/2023

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango amekagua barabara ya mchepuo wa Inyala yenye kilometa 2.8 na Upanuzi wa Barabara ya TANZAM sehemu ya Inyala - Shamwengo yenye kilometa 3 mkoani Mbeya.

Akizungumza wakati wa ukaguzi wa barabara hiyo uliofanyika leo tarehe 1 Agosti 2023, Makamu wa Rais Dkt. Mpango ameipongeza Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) kwa kazi kubwa waliyofanya ya ujenzi wa barabara katika eneo hilo ambalo lilipoteza maisha ya watu wengi  ambao ni nguvu kazi ya Taifa kutokana na ajali za mara kwa mara.

Ametoa wito kwa madereva wa vyombo vya moto kote Nchini, kuendesha kwa uangalifu, kujenga utaratibu wa kukagua usalama wa magari yao wenyewe na kuzingatia sheria ili wanaowaendesha waendelee kuwa salama na kuepuka madhara yatokanayo na ajali zitokanazo na uzembe wa madereva barabarani.

Dkt. Mpango amewataka askari wa usalama barabarani kusimamia sheria kikamilifu lakini isiwe ndio kisingizio cha wao kutafuta fedha za mfukoni na badala yake wafanye kazi yao kwa uadilifu kulinda maisha ya binadamu wenzetu kwa Manufaa ya Taifa.

Akitoa taarifa fupi ya mradi huo, Meneja wa TANROADS mkoa wa Mbeya Mhandisi Masige Matari amesema ujenzi wa barabara hiyo ulitokana na agizo la Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango tarehe 12 September 2023; alipotembelea eneo hilo na kuiagiza Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kupitia TANROADS waimarishe barabara hiyo kwa kiwango cha lami, kupanua sehemu ya Mlima Inyala na pia kuweka taa sehemu za kukagulia magari kabla ya kuteremka na kupanda mlima.

Ameongeza kuwa kufuatia agizo hilo, Serikali iliidhinisha bajeti ya dharura kwa ajili ya kufanya ujenzi kwa kiwango cha lami, ambapo mradi huo umegharamiwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100 na umetekelezwa na Mkandarasi China Geo - Engineering Corporation kwa gharama ya shilingi bilioni 6.999 kwa kusimamiwa na TANROADS mkoa wa Mbeya.

Aidha Inyala ni eneo lenye mteremko mkali katika barabara kuu ya TANZAM mkoani Mbeya uliopelekea kutokea matukio ya mara kwa mara ya ajali za barabarani ambazo zilisababisha madhara mbalimbali ikiwemo vifo na majeruhi kwa watumiaji wa barabara hiyo.

01/08/2023

Lissu ngoma ngumu Geita"

Na Mwandishi Wetu, Geita

MAMBO yanaonekana kuwa magumu kwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), baada ya kuahirisha mkutano wake kutokana na kukosa watu katika Kijiji cha Ilolangula, wilayani Mbogwe mkoani Geita.

Mkutano wa Lissu ulipangwa kufanyika leo saa sita mchana katika Kijiji hicho k**a sehemu ya mwendelezo wa ajenda ya mikutano yao inayofanyika Kanda ya Ziwa.

Lissu aliingia kijijini hapo na timu yake kwa ajili ya mkutano huo, hata hivyo aliamua kuahirisha kuendelea na mkutano huo k**a njia ya kuepuka aibu anayokutana nayo kutoka katika mikutano yao inayoonekana kukosa mvuto.

Chadema wamezindua ziara za mikoani wakianzia na mikoa ya Kanda ya Ziwa, ambayo hata hivyo imekuwa ikikosa watu huku chanzo cha hali hiyo kikitafsiriwa k**a wananchi kuchukizwa na mwenendo wa Lissu kutoa lugha ya kuudhi anapokuwa anatoa hotuba yake.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Lissu alifika mbali baada ya kuamua kutumia muda mwingi kuwakashifu viongozi wa serikali, akiwemo Hayati Benjamin Mkapa kwa kumuita mwizi wakati wa utawala wake na kuzalisha chuki dhidi ya wananchi wastaraabu nchini.

01/08/2023

Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA bara Tundu Lissu amelazimika kuahirisha mkutano wa hadhara kwa kile kinachodaiwa ni kukosa watu katika kijiji cha Ilolangulu wilayani mbogwe mkoani Geita.

Mkutano huo ulikuwa unatakiwa kufanyika leo tarehe 01/08/2023 saa 6 mchana.

Lissu akiwa ameambatana na viongozi wengine wa CHADEMA akiwemo Mchungaji Peter Msigwa wakiwa wamejiandaa kufanya Mkutano k**a ilivyohada na mapema gari lao la matangazo lilitangaza toka asubuhi hali imekuwa tofauti baada ya kufika na kukosa watu, hivyo ikawalazimu Kuondoka eneo la tukio huku wakiwazomea na vijana, waliobainika kuwa hawaungi mkono baadhi ya mienendo ya Kiongozi huyo wa Upinzani.

Mkoa wa Morogoro unatarajia kunufaika na kilometa 435.8 kati ya kilometa 2035 za barabara zinajengwa sehemu mbalimbali N...
01/08/2023

Mkoa wa Morogoro unatarajia kunufaika na kilometa 435.8 kati ya kilometa 2035 za barabara zinajengwa sehemu mbalimbali Nchini na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutumia Utaratibu wa Engineering, Procurement, Construction and Financing (EPC + F).

Mwakilishi wa Meneja wa TANROADS mkoa wa Morogoro Mhandisi M***a Kaswahili amebainisha hayo hivi karibuni baada ya kutembelea na kujionea Maendeleo ya Ujenzi wa Mradi wa barabara ya Kidatu - Ifakara kwa niaba ya Meneja wa TANROADS wa mkoa huo Mhandisi Alinanuswe Lazeck Kyamba.

Amesema mwisho wa mradi wa Kidatu -Ifakara km 66.9 ukihusisha ujenzi wa daraja kubwa la mto Ruaha Mkuu ambao ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 87, ni mwanzo wa utekelezaji wa mradi mpya kwa uratatibu wa EPC + F kuanzia Ifakara – Lupiro – Mahenge – Kilosa Kwa Mpepo – utajumuisha kilometa 8 za kuingia Malinyi Mjini, barabara hiyo itaunganisha mkoa wa Morogoro kwa upande wa Ifakara, Mkoa wa Ruvuma upande wa Londo – Lumecha/Songea.

Mhandisi Kaswahili ameeleza kuwa kukamilika kwa Miundombinu ya mradi huo muhimu wa barabara kutaunganisha mkoa wa Morogoro na Ruvuma kupitia Ifakara - Lumecha, pia kutasaidia kuimarisha usafiri kwa kupunguza muda wa safari kwani wasafiri na wasafirishaji watalazimika kutumia barabara hiyo na hivyo watakuwa wamekoa zaidi ya Kilometa 200 ambazo wanazitumia sasa hivi kwa kuzunguka barabara ya mikumi - Iringa kwenda Ruvuma na maeneo ya Jirani.

Ametoa wito kwa Wananchi wa Morogoro kutumia barabara hizo kwa kuendelea kujikita katika shughuli za uzalishaji kwa sababu usafiri utakuwa wa uhakika na magari yatakuwa yakutosha, huku akiishukuru serikali ya awamu ya sita kwa kuhakikisha inasogeza huduma ya usafiri karibu na zaidi na Wananchi kwa kujenga miundombinu ya barabara ambayo ni kiungo muhimu katika Maendeleo ya mtu mmoja, mmoja, Jamii na Taifa kwa ujumla.

Aidha pamoja na mradi huo tarehe 16, Juni mwaka huu 2023, Serikali kupitia TANROADS ilisaini mikataba saba kwa ajili ya ujenzi wa barabara zenye jumla ya km 2,035 zitakazojengwa kwa wakati mmoja kwa utaratibu wa EPC + F.

31/07/2023

KATIKA hali ya kushangaza, mikutano ya Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu imezidi kukosa mvuto kutokana na wafuasi, wanachama na Watanzania kwa ujumla kuendelea na shughuli wakati kiongozi huyo akifanya mkutano wake.

Lissu yupo kwenye ziara zake za Kanda ya Ziwa kukutana na wanachama pamoja na Watanzania k**a njia ya kujenga chama chao sanjari na kuzungumzia mwelekeo wa Mkataba wa Bandari dhidi ya Dubai Ports World (DPW).

Katika mkutano uliofanyika leo wilayani Bukombe, mkoani Geita, Lissu alishindwa kabisa kuvutia watu wa kwenda kumsikiliza, jambo linaloonesha mwelekeo mbaya wa chama hicho katika ujenzi wa hoja zenye ushawishi.

Lissu anajitokeza hadharani kuzungumza na Watanzania kuhusu mchakato wa uwekezaji wa Bandari.

Hoja inayowatesa Chadema kwa sasa ni namna ya kuwaaminisha Watanzania kuhusu mchakato wa uwekezaji wa bandari huku wakitumia muda mwingi kukashifu viongozi wa serikali na wastaafu hali inayowapa wakati mgumu kuvutia watu kwenye mikutano yao.

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amemtaka Meneja wa Wakala Barabara Nchini (TANROADS) Mkoa wa Kigoma ...
31/07/2023

Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Profesa Makame Mbarawa amemtaka Meneja wa Wakala Barabara Nchini (TANROADS) Mkoa wa Kigoma kuhakikisha barabara ya Kasulu-Buhigwe- Manyovu yenye urefu wa kilomita 56 Sehemu ya Kasulu hadi Buhigwe KM 35 inakamilika kwa kiwango cha lami ifikapo oktoba mwaka huu.

Barabara hiyo ambayo ni sehemu ya Barabara ya Kabingo-Kasulu hadi Manyovu yenye urefu wa Kilomita 260. 6 inatarajiwa kuufungua na kuunganisha mkoa wa Kigoma na Kagera kwa barabara ya lami na hivyo kuchochea shughuli za kilimo, biashara na uwezekezaji katika ukanda wa magharibi mwa Tanzania.

“Hakikisheni TANROADS Kigoma na TANROADS Makao Makuu mnakagua miraid hii mara kwa mara ili kufahamu changamoto za wakandarasi na kuzipatia ufumbuzi wa haraka kabla ya msimu wa mvua kuanza’ amesema Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa ameelezea kuridhishwa kwake na kasi ya ujenzi wa barabara hiyo katika sehemu ya Kasulu hadi Manyovu yenye urefu wa Kilomita 56 na Mvugwe hadi Nduta Junction yenye urefu wa kilomita 59.35 na Nduta Junction-Kibondo Junction hadi Kabingo yenye urefu wa kilomita 62.5 ambayo kasi ya ujenzi wake inaridhisha na kumuonya Mkandarasi anayejenga sehemu ya Kanyani Junction hadi Mvungwe yenye urefu wa Kilomita 70.5 ambaye bado yuko nyuma ya muda.

“Serikali imedhamiria kuufungua mkoa wa Kigoma kwa barabara zake zote ili kuimarisha shughuli za biashara, kilimo na usalama hivyo haitamvumilia Mkandarasi anayefanya kazi nje ya mkataba kwa kuwa lengo la Serikali ni kuwahakikishia wananchi wake wanapata huduma bora kwa wakati ‘amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.

Prof. Mbarawa amewataka wakazi wa Kigoma na wa mwambao wa Ziwa Tanganyika kutumia uwekezaji wa miundombinu kuibua fursa za biashara na maendeleo ili kupunguza umasikini.

Katika hatua nyingine Prof. Mbarawa amekagua barabara ya Chankere hadi Mwamgongo katika Jimbo la Kigoma Kaskazini ambayo inapita kwenye mlima mkali na maeneo yenye uzalishaji wa mazao ya biashara na kuwataka wakazi wa maeneo hayo kuzingaia alama za barabarani na kujenga nje ya hifadhi ya barabara ili kuepuka usumbufu na kulinda usalama.

Ili kuharakisha shughuli za maendeleo na kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora na salama katika sekta ujenzi, usafir...
30/07/2023

Ili kuharakisha shughuli za maendeleo na kuhakikisha Wananchi wanapata huduma bora na salama katika sekta ujenzi, usafiri na usafirishaji sehemu mbalimbali Nchini, Serikali kupitia TANROADS inafanya matengenezo ya barabara ya TANZAM Highway KM 60 kwa kiwango cha lami katika eneo la Hifadhi ya Taifa Mikumi barabara kuu ya Morogoro- Iringa.

Mwakilishi wa Meneja wa TANROADS mkoa wa Morogoro Mhandisi M***a Kaswahili amesema hayo hivi Karibuni alipozungumza na Kipindi cha TANROADS Mkoa kwa Mkoa muda mfupi baada ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo kwa niaba ya Meneja wa TANROADS wa mkoa huo Mhandisi Alinanuswe L. Kyamba.

Amesema utekelezaji wa mradi huo umeanza kufanyika katika kipande cha barabara chenye urefu wa Kilometa 3.2 kwa kuondoa tabaka la zamani lililochoka na ambalo muda wake umekwisha na kusababisha eneo hilo kuwa na mashimo mengi, kufuatia hali hiyo Serikali imeamua kuijenga upya kwa kuweka tabaka jipya la lami kisha kubadilisha madaraja ya chuma ya zamani yaliyochoka na kuweka mapya ili kuongeza uimara katika barabara hiyo ambayo inaunganisha Tanzania na Nchi jirani za Zambia na Congo.

"Barabara hii imejengwa zaidi ya miaka 30 iliyopita na ilipangwa itadumu kwa miaka 25 ambapo sasa sehemu kubwa ya barabara hii imeanza kuchoka ndio maana tunaendelea kurekebisha, anayetekeleza mradi huu ni Mkandarasi mzawa kutoka kampuni ya Del Monte Building, Civil and Electrical Constructors Co.Ltd ya Jijini Dar-es Salaam ambaye ameanza mradi Februari 2023 na anatarajiwa kukabidhi kazi tarehe 30 mwezi wa tisa mwaka huu 2023" ameongeza Mhandisi Kaswahili.

Amesema kuwa Serikali inaendelea kuhudumia barabara hiyo na nyingine kwa kutenga kila mwaka wa bajeti kwa ajili ya ujenzi na matengenezo ya kuzilinda na kuepusha gharama ambazo zingetumia kuanza kujenga barabara upya, hivyo matengenezo yanayoendelea kufanyika yanaongeza muda wa matumizi ya barabara hiyo.

Mhandisi Kaswahili ametoa wito kwa Wananchi wanaotumia barabara hiyo na barabara nyingine za mkoa wa Morogoro kuendelea kutunza na kuzilinda alama za barabarani na miundombinu mbalimbali ya barabara ambayo inatoa taarifa kwa watumiaji wa barabara na madereva na kutokufanya uharibufu.

Address

Mwenge Bamaga
Dar Es Salaam

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tenda Radio Tz posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Tenda Radio Tz:

Videos

Share

Nearby media companies


Other News & Media Websites in Dar es Salaam

Show All

You may also like