28/06/2024
FAIDA ZA KUFUNGA NA KUOMBA KWA MKRISTO.
PASTOR SIMBEYE KINGS
HEALING WORSHIP CENTRE
MAOMBI NA KUFUNGA: SIKU YA PILI 28-JUN-2024
Kufunga na kuomba ni moja ya silaha muhimu kwa Mkristo.
Tunaendelea…………….
4. UKOMBOZI
Maombi yanaleta ukombozi wa nafsi,
Maombi yanaleta ukombozi wa familia,
Maombi yanaleta ukombozi wa Jamii na Taifa kwa ujumla.
Wakati Hamani alijaribu kuwaangamiza Wayahudi katika Ufalme wa Ashuru Esta alifunga kwa siku 3 pamoja na wajakazi wake.
Mungu aliingilia kati kwa nguvu na kuwaokoa na kuwaangamiza adui zao.
Esta 4:16 Uende ukawakusanye Wayahudi wote waliopo hapa Shushani, mkafunge kwa ajili yangu; msile wala kunywa muda wa siku tatu, usiku wala mchana, nami na wajakazi wangu tutafunga vile vile; kisha nitaingia kwa mfalme, kinyume cha sheria; nami nikiangamia, na niangamie. 17Basi Mordekai akaenda zake, akafanya yote k**a vile Esta alivyomwagiza.
5. KUFUNGA KUNANYENYEKESHA NA KUKUBADILISHA
Mojawapo ya njia zenye ufanisi zaidi za kunyenyekea ni kwa kufunga na kuomba.
Vyakula vinaweza kuwa sababu au mlango wa adui kutupiga katika maisha.
Kujizuia kula ni njia moja wapo ya kushuka na kunyenyekea kwa Mungu, hatufungi sababu hatuna bali hatuli sababu tunataka kuchukua muda na Mungu kwa ajili ya roho zetu.
Inashangaza kwamba tatizo katika bustani ya Adamu na Hawa lilianza na chakula k**a tunavyosoma kutoka Mwanzo 3.6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala.
Sio kila chakula ambacho Mungu amepitisha kwetu ni chetu, tujifunze kuona nafasi ya Mungu katika chakula.
Mungu anaweza kukupa milo yote lakini haimaanishi kuwa utumie vyote.
Kujizuia kupata raha ya mlo mmoja au zaidi kuna njia ya kimiujiza ya kukunyenyekesha na kusababisha baraka zaidi kwako.
I. Kufunga Hukusaidia Kumkaribia Mungu Zaidi. ...
II. Kufunga Hukusaidia Kujinyenyekeza Mbele za Mungu. ...
III. Kufunga Hukusaidia Kupinga Vishawishi na Kukua katika Kujidhibiti. ...
IV. Kufunga Hukusaidia Kuomba na Kutafuta Mwongozo wa Mungu. ...
V. Kufunga Hukusaidia Kuonyesha Mshik**ano na Wengine. ...
• KUFUNGA KUNAONYESHA KINA CHA HAMU YAKO WAKATI WA KUOMBEA JAMBO FULANI.
Ni kuonyesha kwamba uko makini vya kutosha kuhusu ombi lako, kulipa thamani ya kibinafsi. Mungu huheshimu hamu na kina, na kuomba kwa imani.
YOELI 1:14 Takaseni saumu, iteni kusanyiko la dini, Wazee na wakusanye wenyeji wote wa nchi; Waende nyumbani kwa Bwana, Mungu wenu, Na kumlilia Bwana,
YOELI 2:12 Lakini hata sasa, asema Bwana, nirudieni mimi kwa mioyo yenu yote, na kwa kufunga, na kwa kulia, na kwa kuombolea;
KUFUNGA KUNAACHILIA NGUVU YA KI-UNGU ISIYO YA KAWAIDA.
Kufunga na kuomba ni silaha ambayo tunaweza kutumia wakati wa upinzani dhidi ya mapenzi ya Mungu. Kazi ya Shetani ni kuleta mgawanyiko, kukata tamaa, kushindwa, huzuni, na mashaka miongoni mwetu.
Mungu amekuwa akitumia eneo la maombi kushughulikia na kuachilia pigo kuu kwa adui yetu!
Ezra 8:23 Basi tukafunga, tukamsihi Mungu wetu kwa ajili ya hayo; naye akatutakabali.
• MAOMBI HUKUTAYARISHA KWA BARAKA.
Mara nyingi katika Biblia, watu walioshinda walifunga kabla ya ushindi mkubwa walioupata.
Muujiza uliotokea, au jibu la maombi. Maombi yaliwatayarisha kwa baraka!
• MUSA ALIFUNGA KABLA HAJAPOKEA AMRI KUMI.
KUTOKA 34:28 Naye alikuwa huko pamoja na Bwana siku arobaini na masiku yake; hakula chakula, wala hakunywa maji. Naye akaandika katika hizo mbao, hayo maneno ya maagano, hizo amri kumi.
• WAISRAELI WALIFUNGA KABLA YA USHINDI WA KIMUUJIZA.
2 Mambo ya Nyakati 20:2 Wakaja watu waliomwambia Yehoshafati, wakisema, Wanakuja jamii kubwa juu yako watokao Shamu toka ng'ambo ya bahari; na tazama, wako katika Hasason-tamari (ndio En-gedi). 3 Yehoshafati akaogopa, akauelekeza uso wake amtafute Bwana; akatangaza mbiu ya watu kufunga katika Yuda yote.
• NEHEMIA ALIFUNGA KABLA YA KUANZA MRADI MKUBWA WA UJENZI.
NEHEMIA1:4 Hata ikawa niliposikia maneno hayo, nikaketi, nikalia, nikaomboleza siku kadha wa kadha; kisha nikafunga, nikaomba mbele za Mungu wa mbinguni;
Nehemia 1:4
• WAKRISTO WA KWANZA WALIFUNGA WAKATI WA KUFANYA MAAMUZI. Matendo 13:2-3
ZINGATIA HAYA MAWILI K**A USHAURI WANGU KWAKO
1. Kumbuka kwamba kufunga si "kupata" jibu la maombi. Mungu hawezi kuhujumiwa na juhudi za kibinadamu. Ikiwa Mungu anataka kujibu maombi yetu basi anajibu ndani ya mapenzi yake. Kufunga hututayarisha wewe tu kupokea jibu toka kwa Mungu.
2. Nakushauri; ikiwa afya yako inaruhusu kwa wakati huu. Ikiwa unaweza kufanya maombi na kufunga, basi fanya kwa imani na Mungu ataheshimu nia yako.
KARIBU UABUDU NASI KILA ALHAMISI NA JUMAPILI – 0754 665 775