12/03/2022
"Mwaka 2021/22, Serikali ilipanga kukopa shilingi bilioni 3,045.1 kutoka vyanzo vyenye masharti ya kibiashara, katika kipindi cha July 2021 hadi Januari 2022, Serikali imefanikiwa kukopa shilingi bilioni 1,639.7 sawa na asilimia 95.2 ya makadirio ya kipindi hicho" -Waziri wa Fedha Dk. Mwigulu Nchemba
"Tathmini ya uhimilivu wa deni iliyofanyika Novemba 2021 imeonesha kuwa deni la Serikali ni himilivu katika kipindi cha muda wa kati na mrefu kwa kuzingatia ukomo wa viashiria vyote vinavyokubalika kimataifa" —Waziri Nchemba
Kwa kipindi cha July 2021 hadi Jan 2022, mapato yaliyokusanywa na TRA (ya kodi na yasiyo ya kodi) yalifikia Tsh. Bil.12,046.1 sawa na 92.8% ya makadirio ya kipindi hicho, kati ya mapato hayo, mapato ya kodi yalikuwa Bil. 11,531.3 nayasiyo ya kodi ni Bil. 514.8"—Waziri Nchemba
"Katika kipindi cha July 2021 hadi Jan 2022, mapato yasiyo ya kodi yalifikia Tsh.Bil 1,492.8, sawa na 89.0% ya lengo la kukusanya Bil 1,678.1, kati ya hayo, Bil 1,016.6 zilitoka kwa Wizara na Idara zinazojitegemea na Bil. 476.1 ni mapato yatokanayo na na gawio" —Waziri Nchemba
-
-