Kasi Ya Awamu ya Sita.
#SamiaKazini
#kaziiendelee🔥🔥🇹🇿🇹🇿🇹🇿💪🏿💪🏿💪🏿💪🏿
#PumnzikaKwaAmaniMzeeWetu🙏 Unapoenda kupumnzika katika nyumba yako ya milele jua watanzania hatukudai katika utumishi wako, wewe ndiye mwanasiasa wa kwanza kuchangamsha siasa za vyama vingi. Tutakukumbuka kwa kuuishi utanzania wa kweli na uzalendo kwa Taifa.
#AsanteAgostino.
*Kama kijana nina Wivu Mkubwa sana na Uchu wa kuona Maendeleo ya Taifa langu, Umoja na Mshikamano wa Vijana Kupambana na Changamoto mbalimbali za taifa letu.*
Tamaa ya Mafanikio ni yangu na yako Tuungane kuitimiza.
*Vijana Tuungane Kuyatimiza…*
#SisiTanzania #WeTanzania🇹🇿
Umoja wa Vijana wa CCM ( UVCCM) umekitaka chama chao kumchukulia hatua Mbunge wa Kawe Josephat Gwajima kwa kitendo chake cha kuhamasisha watanzania wapuuze chanjo ya Covid-19.
Katibu Mkuu wa umoja huo Kenani Kihongosi ameyasema hayo leo Jumanne Julai 28 2021 mara baada kumalizika kwa kikao cha sektarieti ya UVCCM jijini Dodoma.
Amesema mbunge huyo ametoa maneno ya kichochezi na kwamba yanakwenda kuwagawa wananchi kwani Rais Samia Suluhu Hassan ameshatoa msimamo kwa wananchi wapate chanjo kwa hiari.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango, leo Julai 26, 2021 ametembelea Bandari ya Mtwara na kujionea ujenzi wa gati mpya uliofanywa bandari hapo kwa kugharimu shiling bilioni 157.
Akiwa bandarini hapo Mkamu wa Rais amesema Serikali ya awamu ya Sita imejipanga kuhakikisha kuwa Bandari ya Mtwara inatumika ipasavyo ili kuinua uchumi wa mkoa wa Mtwara na Taifa kwa ujumla. Ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Bandari kuendelea kutafuta masoko katika nchi jirani kama vile Msumbiji, Malawi na Comoro ili kuongeza wigo wa matumizi ya bandari ya Mtwara na kuliongezea taifa mapato.
Chama Cha Mapinduzi kinafutilia kwa makini mienendo ya baadhi viongozi wake ambao wamekuwa wakipotosha Umma na kwenda kinyume na maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu na maadili ya Chama.
CCM inawakikishia wanachama na watanzania kuwa hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wote ambao wanatumia nafasi hiyo kusukuma ajenda zao binafsi, kwa mujibu wa Katiba, kanuni za maadili na uongozi za CCM
Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmshauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi
26 Julai, 2021.
#Anews
Chama Cha Mapinduzi kinafutilia kwa makini mienendo ya baadhi viongozi wake ambao wamekuwa wakipotosha Umma na kwenda kinyume na maelekezo ya Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu na maadili ya Chama.
CCM inawakikishia wanachama na watanzania kuwa hatua kali za kinidhamu zitachukuliwa dhidi ya wote ambao wanatumia nafasi hiyo kusukuma ajenda zao binafsi, kwa mujibu wa Katiba, kanuni za maadili na uongozi za CCM
Shaka Hamdu Shaka
Katibu wa Halmshauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi
26 Julai, 2021
Hali ilivyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar.... Askari Polisi wameimarisha ulinzi... Huenda Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akafikishwa mahakamani hapo muda wowote.
#Anews
Mashabiki wa Simba na Yanga wamechezea virungu asubuhi ya leo wakiwa katika foleni ya kuingia uwanjani lake Tanganyika kwaajili ya mchezo.
#Asports
'Muha ni kikoko, kikoko ni Tambwe' - Huyu jamaa anadai alitembea kwa mguu kutoka Kigoma hadi Dar es Salaam kuishuhudia derby ya Julai 3 lakini hakupokelewa na viongozi.
Muda huu yupo hapa Lake Tanganyika Stadium, na anasema atatembea tena kwa mguu kutoka Kigoma kwenda Dar es Salaam kuelekea mechi ya Ngao ya Jamii.
#Asports
Taarifa ya askari kukatwa na kitu chenye ncha kali.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kamishina msaidizi wa Polisi ACP-JUSTINE MASEJO ametoa taarifa ya awali kuhusiana tukio la askari wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha ambae amefariki dunia baada ya kukatwa na kitu chenye ncha kali sehemu ya kichwani.
ACP-MASEJO amesema tukio hilo limetokea jana majira ya saa Tano usiku katika jitihada za kukamata mtuhumiwa ambaye taarifa yake ilifunguliwa katika kituo cha Polisi Mbuguni kijiji cha Makiba wilayani Arumeru Mkoa wa Arusha ndipo alitokea ghafla mtu mmoja jirani na nyumba alipokwenda askari huyo kukamata mtuhumiwa wa matukio mbali mbali ya yaliyolipotiwa kituoni hapo.
Kamanda Masejo amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linaendelea na Operesheni kali ya kumtafuta mtuhumiwa aliyefanya kitendo hicho.
@police_arusha
C.E.O wa @africanboy_brand kupitia ukurasa wake wa Instagram ame share video ikionyesha gari zake na Helicopter ikiwa ina shuka nakusindikiza na ujumbe ulio someka.
________________________________
✍✍ @juma_jux Deal done 💵💵💵 🚁🚁🚁
Baada ya ujumbe huo kutoka kwa Jux ume fanya mashabiki zake na watu wengine wabaki na maswali jee Jux kanunua Helicopter?....
#Aupdates