Jaribio la kutoroka katika gereza kuu la Congo limesababisha vifo vya watu 129, wakiwemo baadhi waliopigwa risasi na wengine walikufa katika mkanyagano kwenye gereza hilo lenye msongamano mkubwa, mamlaka ilisema Jumanne.
Wanaharakati walisema idadi ya vifo ni kubwa zaidi lakini hawakutoa takwimu kamili.
Tathmini ya awali ilionyesha kuwa wafungwa 24 waliuawa kwa "risasi za maonyo" zilizofyatuliwa na walinzi wakati wafungwa walipojaribu kutoroka kutoka Gereza Kuu la Makala katika mji mkuu wa Kinshasa mapema Jumatatu, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Congo, Jacquemin Shabani, alisema kwenye mtandao wa kijamii wa X.
Duniani Leo
Matangazo ya Duniani Leo kutoka idhaa ya kiswahili ya Sauti Amerika, Washington, D.C.
#habari
Duniani Leo
Matangazo ya Duniani Leo kutoka idhaa ya kiswahili ya Sauti Amerika, Washington, D.C.
#habari
MAISHA NA AFYA: Mapambo ya maua ndani ya nyumba na faida zake kwa afya ya binadamu.
Waandamanaji walaani mauaji yanayoendelea Gaza mbele ya Ubalozi wa Israel Amman
Waandamanaji walikusanyika karibu na ubalozi wa Israel huko Amman, Jordan leo Ijumaa kuwaunga mkono Wapalestina huko Gaza.
Takriban watu 250 walionekana kwenye maandamano hayo, wakibeba mabango na kuimba nyimbo.
Katika siku za hivi karibuni, Israel imetoa amri kadhaa zaidi za wakazi wa Gaza kuondoka tangu kuanza kwa vita vya miezi 10, na kusababisha malalamiko kutoka kwa Wapalestina, Umoja wa Mataifa na maafisa wa misaada juu ya kusitishwa kwa misaada ya biandamu kufikia maeneo ya kibinadamu na kutokuwepo kwa maeneo salama.
Shambulizi la hivi punde katika mzozo wa miongo kadhaa kati ya Israel na Palestina ulichochewa Oktoba 7 wakati kundi la Palestina la Hamas liliposhambulia Israel, na kuua 1,200 na kuchukua mateka wapatao 250, kulingana na idadi iliyotolewa na Israel.
Mashambulio yaliyofuata ya Israel dhidi ya eneo linalotawaliwa na Hamas tangu wakati huo yameua zaidi ya Wapalestina 40,000, kwa mujibu wa wizara ya afya ya eneo hilo, huku pia ikiwafukuza karibu watu wote milioni 2.3, na kusababisha baa la njaa na kusababisha madai ya mauaji ya kimbari katika Mahakama ya Dunia ambayo Israel inakanusha. - Reuters
Wapalestina kati yao watoto wakishiriki maziko ya waliofariki Israel iliposhambulia
Waombolezaji walisindikiza jeneza la mtu mmoja mwenye umri wa miaka 62 ambaye aliuwawa na majeshi ya Israeli nyumbani kwake wakati mashambulizi yalipofanyika huko katika mji wa Tulkarm eneo linalokaliwa kwa mabavu huko Ukingo wa Magharibi.
Kulingana na walioshuhudia mauaji hayo, Ayed abu Hija aliuwawa na mwanajeshi wa Israeli aliyemvizia na kumpiga risasi akiwa nyumbani kwake wakati mashambulizi yakiendelea.
Waombolezaji Wakipalestina pia walibeba mfano wa jeneza kwa kumuenzi Muhhamad Jabber, aliyekuwa maarufu kwa jina la Abu Shujaa, mkuu wa mitandao ya wapiganaji katika kambi jirani ya wakimbizi ya Nur Shams, ambaye aliuwawa na jeshi la Israeli Alhamisi (August 29) huko Tulkarm.
Jeshi la Israeli lilianzisha moja ya mashambulizi makubwa katika eneo linalokaliwa kwa mabavu na Israeli kwa miezi kadhaa sasa Jumatano (August 28), na kuuwa watu 19, wakiwemo makamanda wa Hamas na Islamic Jihad.
Israel imekuwa ikitekeleza kile imekitaja kama operesheni ya kijeshi karibu kila siku katika Ukingo wa Magharibi, tangu Oktoba 7, wanamgambo wa Hamas walipofanya shambulizi kutokea Gaza na kusababisha vita vikali vinavyoendelea.
Israel imesema kwamba operesheni yake ya kijeshi ina lengo la kuwamaliza nguvu wanamgambo wa Hamas na kuzuia mashambulizi dhidi ya raia wake
- Reuters
Duniani Leo
Matangazo ya Duniani Leo kutoka idhaa ya kiswahili ya Sauti Amerika, Washington, D.C.
#habari
Majeshi ya Israel yafanya operesheni kuondoa vilipuzi Ukingo wa Magharibi
Jeshi la Israel limesambaza kanda ya video Alhamisi ikionyesha majeshi yakifanya mashambulizi huko Ukingo wa Magharibi.
Katika taarifa yake jeshi lilisema vikosi vyake “vimefanikiwa kutegua vilipuzi kadhaa ambavyo vilikuwa vimechimbiwa barabarani lengo likiwa vitumike kushambulia majeshi yake.
Majeshi ya Israeli yamefanya mashambulizi makali na ya kiwango kikubwa Ukingo wa Magharibu.usiku kucha siku ya Jumanne.
Israel inasema mashambulizi hayo yaliyofanyika wakati mmoja kote eneo la kaskazini mwa Ukingo wa Magharibi – ambayo yamewauwa jumla ya watu 16, karibuni wote wanamgambo, tangu jioni Jumanne – yamelenga kuzuia mashambulizi dhidi ya jeshi hilo.
Israel imekuwa ikitekeleza kile imekitaja kama operesheni ya kijeshi karibu kila siku katika Ukingo wa Magharibi, tangu Oktoba 7, wanamgambo wa Hamas walipofanya shambulizi kutokea Gaza na kusababisha vita vikali vinavyoendelea.
Israel imesema kwamba operesheni yake ya kijeshi ina lengo la kuwamaliza nguvu wanamgambo wa Hamas na kuzuia mashambulizi dhidi ya raia wake.
-AP, Reuters
Wakaazi wakuta makazi na mahema yao yameangamizwa huko Deir al-Balah
Wakaazi wa Gaza walirejea majumbani mwao na katika mahema katika mji wa Deir al-Balah ulioko mashariki na kushuhudia uharibifu mkubwa katika eneo lao.
Jeshi la Israeli liliruhusu familia kurejea katika maeneo yaliyoko katikati ya mji huo wiki moja baada ya kuwalazimisha kuhama kuelekea upande wa magharibi.
Jeshi hilo lilidai kuwa Hamas walikuwa katika eneo hilo. Wale waliorejea walikuta nyumba na mahema yao yote yamebomolewa kabisa. - AP
#gaza #ukandawagaza #mateka #israeli #jeshi #voa #voaswahili #qaidfarhanalkadi #hamas #palestina #wapalestina
Duniani Leo
Matangazo ya Duniani Leo kutoka idhaa ya kiswahili ya Sauti Amerika, Washington, D.C.
#habari
Kupasuka kwa Bwawa la Arbaat Sudan kutokana na mvua kubwa 30 wafariki
Shirika moja la Umoja wa Mataifa, UN, linasema kuwa kupasuka kwa Bwawa la Arbaat huko mashariki ya jimbo la Red Sea, Sudan kipindi cha wikiendi imeleta mafuriko katika makazi yaliyoko karibu na kuua watu wasiopungua 30. Bwawa hilo lilikabiliwa na mvua kubwa. - (AP)
Video courtesy Alhurra Television.
#sudan #arbaatdam #climatechange #voa
Mashambulizi makali ya kiwango kikubwa yatekelezwa na Israel
Majeshi ya Israeli yamefanya mashambulizi makali na ya kiwango kikubwa Ukingo wa Magharibu.
Maafisa wa Palestina wamesema kwamba wanajeshi wa Israel wamewaua wapalestina tisa na kufunga njia zote za kuingia mji wa Jenin.
Israel imekuwa ikitekeleza kile imekitaja kama operesheni ya kijeshi karibu kila siku katika Ukingo wa Magharibi, tangu Oktoba 7, wanamgambo wa Hamas walipofanya shambulizi kutokea Gaza na kusababisha vita vikali vinavyoendelea.
Israel imesema kwamba operesheni yake ya kijeshi ina lengo la kuwamaliza nguvu wanamgambo wa Hamas na kuzuia mashambulizi dhidi ya raia wake.
#gaza #ukandawagaza #mateka #israeli #jeshi #voa #voaswahili #qaidfarhanalkadi #hamas #palestina #wapalestina #ukingowamagharibi
Qaid Farhan Alkadi, mateka wa Israeli ambaye hivi karibuni aliokolewa alipokuwa akishikiliwa na Hamas huko Gaza, alipokelewa kwa furaha katika Kituo cha Afya cha Soroka mjini Beersheba (Agosti 28). Kanda ya video iliyochukuliwa kutoka kituo hicho cha afya inaonyesha Alkadi akiwa amezungukwa na wanafamilia na maafisa wa jeshi, akitembea kutoka hospitalini.
Tafrija hiyo iliendelea karibu na Rahat, Israel, ambako Alkadi alionekana akiwa amekaa ndani ya hema katika kijiji ambako yako makazi yake Ubeduini.
When asked about his feelings post-rescue, Alkadi, speaking in Hebrew,
Alipoulizwa ulizwa kuhusu hisia zake baada ya kuokolewa, Alkadi, akizungumza kwa lugha ya kiebrania alisema ni faraja kubwa na kutaka hatua zichukuliwe kuwarejesha wale ambao bado wanashikiliwa.
#gaza #ukandawagaza #mateka #israeli #jeshi #voa #voaswahili #qaidfarhanalkadi #hamas #palestina #wapalestina
Duniani Leo
Matangazo ya Duniani Leo kutoka idhaa ya kiswahili ya Sauti Amerika, Washington, D.C.
#habari
Jeshi la Israeli lamuokoa mateka Qaid Farhan Alkadi aliyeshikiliwa Gaza
Vikosi maalum vya Israeli vimemuokoa mateka wa Israeli kutoka katika mahandaki eneo la kusini la Ukanda wa Gaza katika “operesheni nzito ya uokoaji”, jeshi limesema Jumanne (August 27), baada ya mtu huyo kutekwa na watu wenye silaha wa kikundi cha Hamas zaidi ya miezi 10 iliyopita mnamo Oktoba 7, 2023.
Jeshi lilisema Qaid Farhan Alkadi mwenye umri wa miaka 52, ni wa jamii ya Mabedui huko kusini mwa Israel, na alipelekwa hosptali na hali yake inaendelea kuimarika.
Reuters haikuweza kuthibitisha yenyewe sehemu ambapo video hiyo ya majeshi ya Israeli ilichukuliwa lakini Reuters waliweza kuthibitisha kwa kujitegemea, kuwa eneo hilo ni Hospitali ya Soroka, kutokana na majengo yalivyo na alama ambazo zinalingana na picha za majengo ya eneo hilo.
Wakati operesheni hiyo ilipothibitishwa, vituo vya televisheni vya Israeli vilionyesha helikopta ya jeshi ikitua katika hospitali wakati wahudumu wa afya na gari la wagonjwa lilikuwa likisubiri kumpokea Alkadi. - Reuters
#gaza #ukandawagaza #mateka #israeli #jeshi #voa #voaswahili #qaidfarhanalkadi #hamas #palestina #wapalestina
Jamii yazika miili ya waliofariki katika mafuriko jimbl la Red Sea nchini Sudan
Baadhi ya sehemu za mashariki mwa Sudan zimekumbwa na mafuriko baada ya bwawa kuvunjika na kuharibu vijiji 20 na kusababisha vifo vya watu 30.
Mvua kubwa zimesababisha mafuriko yaliyojaza bwawa la Arbaat mnamo Jumapili, kilomita 40 kaskazini mwa Port Sudan, mji ambao sasa unatumika kama makao makuu ya serikali, wanadiplomasia, mashirika ya misaada na watu waliokoseshwa makazi kutokana na vita vya miezi kadhaa kati ya jeshi na kikosi cha kijeshi cha RSF.
Umoja wa Mataifa umesema kwamba karibu watu 50,000 wameathiriwa na mafuriko, na kwamba huenda idadi hiyo inajumuisha tu watu waliokuwa wanaishi magharibi mwa bwawa hilo na kwamba si rahisi kuwafikia watu walio mashariki mwa bwawa. - Reuters
#sudan #mafuriko #vifo #maziko #uharibifu #vijiji #portsudan #rsf #jeshi #voa #voaswahili
Duniani Leo
Matangazo ya Duniani Leo kutoka idhaa ya kiswahili ya Sauti Amerika, Washington, D.C.
#habari
MAISHA NA AFYA: Ugonjwa wa MPOX unaendelea kuwa tishio la kimataifa
Duniani Leo
Matangazo ya Duniani Leo kutoka idhaa ya kiswahili ya Sauti Amerika, Washington, D.C.
#habari
Trump akosoa Harris anavyo shughulikia usalama mpakani kati ya Marekani na Mexico
“Alikuwa ni malkia wa mpakani. Mara ghafla anasema yeye siyo tena malkia wa mpakani,” alisema. “Kamwe hakujawahi kuwa na mpaka kokote duniani ambao unafurika watu kama mpaka huu.”
Harris alipewa jukumu mwezi Machi 2021 kukabiliana na “kiini” cha wahamiaji kutoka Guatemala, Honduras na El Salvador – Amerika ya Kati inayoitwa “Northern Triangle” – lakini haikupewa jina la “border czar” au kupewa jukumu la ulinzi wa mpaka.
Kwenye barabara chafu chini ya vilima vyenye vichaka vya Arizona, Donald Trump alitumia ukuta na rundo la vyuma kulinganisha jinsi yeye alivyoudhibiti mpaka huo na hatua za mpinzani wake Mdemokrat, Makamu wa Rais Kamala Harris.
Trump aliwaleta wanawake wenye huzuni, mkuu wa polisi wa Kaunti ya Cochise na mkuu wa umoja wa Doria ya Mpakani kupeleka ujumbe wake mzito juu ya ulinzi wa mpaka katika ziara yake Alhamisi, iliyopewa kauli mbiu “Make America Safe Again” (Ifanye Marekani Iwe Salama Tena.)
Kabla ya matamshi yake, Trump alianza kwa kukosoa rekodi ya Harris kuhusu uhamiaji na usalama wa mpakani, akimuita “makamu wa rais ovyo” alipokuwa anazunguka na kuzungumza na wakazi wa eneo karibu na uzio wa mpaka. - AP
#uselection #harris #trump #voa