Wito kutoka kwa Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Cuba, Mheshimiwa Humphrey Polepole.
VIDEO:Mbunge awageuzia kibao wenzake bungeni kuhusu suala la kulipa kodi kwa maendeleo ya Taifa.
#follow
#follower
#highlights
VIDEO:Kuelekea maboresho ya Daftari la Kudumu la Wapiga Kura nchini, walichokifanya vijana hawa baharini utabaki na mshangao. Kumbuka...“Kujiandikisha Kuwa Mpiga Kura Ni Msingi Wa Uchaguzi Bora”.
#follower
#highlights
VIDEO:Mhandisi Mramba atoboa siri unavyoweza kutumia umeme mdogo hadi raha nyumbani kwako
KATIBU Mkuu Wizara ya Nishati, Mhandisi Felchesmi Mramba akitoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya umeme.
Wizara Ya Nishati
Tanesco
Wakala wa Nishati Vijijini REA
#follower
#highlights
VITUO VYA TIBA SAIDIZI KWA WARAIBU KWA KUTUMIA DAWA (MEDICALLY ASSISTED THERAPY - MAT)
Vituo hivi husimamiwa na serikali na huhudumia waathirika wa dawa ya kulevya aina ya afyuni kama vile heroin na baadhi ya dawa tiba zenye asili ya kulevya. Waathirika wanaotibiwa kwenye vituo hivi hutibiwa kwa kutumia dawa mfano Methadone. Waathirika wanatakiwa kuhudhuria matibabu kila siku mpaka watakapomaliza matibabu. Huduma ya MAT hutolewa bure chini ya uangalizi wa wataalamu.
HUDUMA ZINAZOTOLEWA KATIKA VITUO VYA TIBA SAIDIZI KWA WARAIBU KWA KUTUMIA DAWA (MAT)
1.Kupatiwa dawa aina ya methadone
2.Kupatiwa Elimu juu ya UKIMWI na Kupima VVU
3.Kupatiwa dawa za kufubaza VVU (Antiretroviral therapy)
4.Kupatiwa elimu ya Kinga, Kupima na kutoa matibabu kwa wagonjwa wa Kifua kikuu.
5.Kupatiwa elimu ya Kinga na kutibu Magonjwa ya zinaa
6.Kupatiwa Ushauri nasaha
7.Kupatiwa matibabu ya magonjwa ya Akili
8.Kupatiwa Elimu juu ya maambukizi ya Homa ya ini B na C
dcea_tz
#follower
#insights
#highlight
#diramakininews24
VIDEO:Rais wa IPU, Spika Dkt.Tulia alivyotua na ulinzi mkali katika kanisa alilojificha Bikira Maria na Mtoto Yesu jijini Cairo
CAIRO-Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, leo tarehe 24 Mei 2024, ametembelea Kanisa la Mtakatifu Bikira Maria lililopo Cairo nchini Misri, eneo ambalo Bikira Maria alijificha na Mtoto Yesu kufuatia tishio la Mfalme Herode kutaka kumuua Mtoto Yesu. Ziara hii inasisitiza umuhimu wa kuenzi, kudumisha na kuendeleza amani, umoja na kuwa na uelewa wa pamoja katika imani na utamaduni wetu https://www.diramakini.co.tz/2024/05/videorais-wa-ipu-spika-dkttulia.html
Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Herbat Lucas, Lecture Parpay, Fahmi Abdallah
Thanks for being a top engager and making it on to my weekly engagement list! 🎉 Fildolin Tumbi, Hasheem Ommy, Lecture Parpay
Thanks for being a top engager and making it on to my weekly engagement list! 🎉 Munir Jaffer Jaffer, Mrisho Som
Thanks for being a top engager and making it on to my weekly engagement list! 🎉 Munir Jaffer Jaffer, Mrisho Som
MAWASILIANO KATI YA DAR NA MIKOA YA KUSINI YAKATIKA
LINDI-Mawasiliano kati ya Dar es Salaam na mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma yamekatika baada ya daraja la mto Mbwemkuru lililopo kati ya Kilwa na Lindi ambalo ni sehemu ya barabara Kuu ya Kibiti - Lindi, kukatika na kusombwa kabisa na maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.
Mabasi yanayoelekea mikoa ya Kusini ya nalazimika kuishia safari zao Kijiji cha Kiranjeraje huku yale yanayotokea Ruvuma, Mtwara na Lindi yakiishia umbali mfupi baada ya kupita Zahanati ya Kitomanga.
www.diramakini.co.tz
#MVUA
#Maafa
#majanga
TMA:Kimbunga Hidaya kimepoteza nguvu wakati kikiingia nchi kavu Kisiwa cha Mafia
DAR-"Aidha, mawingu ya mvua yaliyokuwa yakiambatana na kimbunga hicho yamesambaa katika maeneo ya Kusini mwa nchi hususani katika mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani na maeneo jirani na kuweza kusababisha vipindi vya mvua kubwa kwa baadhi ya maeneo.
"Kwa mafano hadi kufika saa 9 mchana, Kituo cha Hali ya Hewa cha Kilwa Masoko (Lindi) kimeripoti mvua ya jumla ya kiasi cha milimita 200.8 kwa kipindi cha masaa 6 yaliyopita.
"Kiwango hiki cha mvua ni kikubwa sana ukizingatia kuwa wastani wa mvua kwa mwezi Mei kwa kituo cha Kilwa Masoko ni milimita 96.6 tu https://www.diramakini.co.tz/2024/05/tmakimbunga-hidaya-kimepoteza-nguvu.html
TMA:Kimbunga Hidaya hadi saa tisa usiku leo kilikuwa kilomita 401 Mashariki mwa Pwani ya Mtwara
DAR-Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) imeendelea kutoa taarifa ya mwenendo wa kimbunga Hidaya kilichopo katika Bahari ya Hindi Mashariki mwa Pwani ya nchi yetu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Mei 3,2024 saa 3:00 asubuhi Kimbunga Hidaya kimeendelea kuimarika na kusogea kuelekea maeneo ya Pwani ya Tanzania.
"Hadi kufika saa tisa usiku wa tarehe 03 Mei 2024 kilikuwa kimeimarika zaidi na kufikia hadhi ya Kimbunga kamili kikiwa umbali wa takriban Kilomita 401 Mashariki mwa pwani ya Mtwara.
"Katika kipindi hiki kimbunga Hidaya kimeendelea kuimarika zaidi huku kasi ya upepo ikiongezeka hadi kufikia Kilomita 130 kwa saa.
"Mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa baharini bado inaonesha uwezekano mkubwa wa Kimbunga Hidaya kusalia katika hadhi ya Kimbunga kamili kwa saa 12 zijazo huku kikiimarika, na kendelea kusogea karibu kabisa na pwani ya Tanzania https://www.diramakini.co.tz/2024/05/tmakimbunga-hidaya-hadi-saa-tisa-usiku.html
"Nimefarijika kwa ujumbe wa video toka Shule ya Sekondari ya Misufini, Kijiji cha Misufini, Kata ya Ndungu, Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro wa wanafunzi Ibrahim na Mwanaulu pamoja na wazazi wao, kuhusu mabadiliko na uboreshaji wa elimu uliofanyika kwenye kata yao katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita.
"Tumepiga hatua kubwa za namna mbalimbali katika kila sekta kwenye kata zote 4,334 za nchi yetu, na ni jambo la kheri kuona hatua hizi zinatimiza kusudio lake la msingi ambalo ni kuboresha maisha ya wananchi wetu.
"Wito wangu kwa kila mmoja wetu ni kuendelea kufanya kazi kwa weledi, hasa wale tunaowapa dhamana kwenye utekelezaji wa mipango ya Serikali kwa wananchi,"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Ikulu Mawasiliano
Ofisi ya Rais - Tamisemi
Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
#diramakininews24
Thanks for being a top engager and making it on to my weekly engagement list! 🎉 Fresha Kinasa, Phinias Kitogoro, Eliamani Kivuyo, Prince Charles
VIDEO:Walimu wakuu wakabidhi hundi ya shilingi milioni 2 kwa Rais Dkt.Mwinyi kuchukua fomu ya urais 2025, atoa neno kupitia simu
ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameelezea kuridhishwa kwake na uungwaji mkono kutoka kwa jumuiya mbalimbali nchini katika uongozi wake.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo wakati akizungumza kwa njia ya simu na Mheshimiwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Lela Mohamed Mussa mara baada ya kupokea hundi yenye thamani ya shilingi 2,000,000 iliyotolewa na Jumuiya ya JUWASEZA kwa lengo la kumuunga mkono katika mbio za urais 2025.
Amesema,amefarijika kuona jumuiya hiyo inathamini jitihada zinazofanywa za kuwaletea maendeleo wananchi https://www.diramakini.co.tz/2023/12/videowalimu-wakuu-wakabidhi-hundi-ya.html
Dr. Hussein Ali Mwinyi
Ikulu habari Zanzibar