Bongo5.com

Bongo5.com The leading entertainment website in Tanzania, since 2006! Follow us on twitter http://twitter.com/bongofive and on YoutTube http://youtube.com/bongofive
(91)

Bringing you the latest scoops, gossip and news from Tanzania. You can send us your stories and photos to the email [email protected]

Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emanuella Kaganda amewaongoza Wananchi na Watumishi wa Wilaya ya Babati  kuadhimisha miaka...
09/12/2024

Mkuu wa Wilaya ya Babati Mhe. Emanuella Kaganda amewaongoza Wananchi na Watumishi wa Wilaya ya Babati kuadhimisha miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania kwa kupanda miti na kuwatembelea wagonjwa hospitali ya mji wa Babati (MRARA).

Maadhimisho hayo yamebeba kauli mbiu isemayo “Uongozi Madhubuti na Ushirikishwaji wa Wananchi ni Msingi wa Maendeleo yetu”

Katika hotuba yake Mhe. Kaganda amewaeleza Wananchi kuwa siku ya tarehe 9 Desemba ni siku muhimu kwa Taifa la Tanzania kwa kuwa Hayati Baba wa Taifa Mwl.Julius K. Nyerere na Viongozi wengine walifanya kazi kubwa kutufikisha katika Maendeleo ya sasa.

Aidha Kaganda amewataka Wananchi kuwaombea wapigania Uhuru na kufanya kazi kwa bidii ili kuijenga Tanzania ya kesho.

Shughuli mbalimbali zilizofanyika ni pamoja kufanya mazoezi kuimarisha afya kwa na kufanya matembezi (jogging), kupanda miti ya matunda na vivuli katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji Babati (Mrara)pamoja na kutoa zawadi kwa wazazi na wajawazito.

Sambamba na hilo katika mdahalo, Wananchi na Wazee wameeleza kuwa Tanzania imepata Maendeleo makubwa yakiwemo, uboreshwaji wa huduma za afya, uboreshwaji wa miundo mbinu ya Barabara, Maendeleo ya viwanda na Biashara , Maendeleo ya makazi, Maendeleo ya elimu Sayansi na Teknolojia pamoja na uwezeshwaji wa kiuchumi kwa Wananchi wakiwemo Vijana kupitia mikopo ya asilimia 10% ya halmashauri.

“Kwa kipindi Cha nyuma tulikuwa tunatumia siku tatu hadi tano kusafiri lakini kwa sasa Miundombinu imeboreshwa tunatumia siku moja” ameeleza Bi. Masiweta Sanka.

Sanka aliwahimiza vijana kuwa wazalendo kwa Nchi yao, kufanya kazi kwa bidii na kuwa mstari wa mbele kukemea vitendo vya rushwa.

Katika kuadhimisha miaka 63 ya uhuru wa Tanzania, vijana wa Generation Samia (Gen S) wameadhimisha siku ya uhuru kwa kuj...
09/12/2024

Katika kuadhimisha miaka 63 ya uhuru wa Tanzania, vijana wa Generation Samia (Gen S) wameadhimisha siku ya uhuru kwa kujitolea katika shughuli za mbalimbali za kijamii ikiwemo kufanya usafi wa mazingira katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Akizungumza katika tukio hilo, Msemaji wa Gen S, Sonata Nduka, amewashukuru waasisi wa taifa kwa kuijenga Tanzania huru, na kuipongeza serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuliletea taifa maendeleo na kudumisha mshik**ano.

“Miaka 63 ya uhuru siyo tu kusherehekea, bali ni kuchukua hatua za kusaidia jamii yetu. Kwa niaba ya vijana wa Gen S, tunampongeza na tunaahidi kuendelea kumuunga mkono Mheshimiwa Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika juhudi zake za kujenga taifa letu kwa mshik**ano, amani, na maendeleo endelevu,” alisema Nduka.

Ikumbukwe kuwa Disemba 07, Gen S walifanya tukio jingine kubwa la Gen S Jogging , ambapo zaidi ya vijana 2,000 walikshiriki mbio za pamoja, zilizolenga kuboresha mshik**ano wa kizazi cha mafanikio huku wakichangia damu kuokoa maisha ya wenye uhitaji wa damu.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma, kupitia mwakilishi wake Paul Mageni, amewashukuru Gen S kwa kufanya usafi, akisema kuwa hatua hiyo imewapa wagonjwa matumaini na furaha.

“Tunawashukuru sana Gen S kwa moyo wenu wa kujitoa. Kitendo hiki kimetoa mfano mzuri na mshik**ano kwa jamii,” alisema Paul Mageni kwa niaba ya uongozi wa hospitali.

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Peres Magiri, ameongoza viongozi wengine waandamizi wa wilaya hiyo, vikosi ya ulinzi na usalama...
09/12/2024

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa, Peres Magiri, ameongoza viongozi wengine waandamizi wa wilaya hiyo, vikosi ya ulinzi na usalama, watumishi na wananchi wilayani humo kufanya usafi katika hospitali ya Nangombo kuadhimisha miaka 63 ya uhuru wa iliyokuwa Tanganyika.

Mkuu huyo wa wilaya alisema uamuzi huo wa kusafisha hospitali hiyo ya wilaya ulikuja kufuatia maelekezo kutoka serikalini ya kuadhimisha siku hiyo kwa shughuli za kijamii na taasisi zilizotenga fedha kwa ajili ya shughuli hiyo zielekezwe katika kusaidia na kuhudumia mahitaji mbalimbali ya jamii husika.

Kutokana na maagizo hayo kutoka serikalini, Magiri alisema: “Kwa hiyo ndio sababu sisi wilaya ya Nyasa tuliamua tutashiriki kwenye maadhimisho haya kwa kufanya usafi hapa lakini pia kwa kile ambacho tumeweza kuwa tumepata, kwa ajili k**a matendo ya huruma, kuwasaidia wagonjwa waliolazwa hapa, ” alisema Magiri.

Magiri pia alitumia fursa hiyo kuwashukuru wote waliojitokeza kwenye usafi huo, hususan vikosi vya ulinzi na usalama, na kuwataka waendeleze moyo huo katika matukio mengine yatakayojitokeza siku zijazo.

Akizungumza baada ya shughuli hiyo ya usafi, Katibu wa Hospitali hiyo, Martin Ngore, alimshukuru mkuu huyo wa wilaya kwa uamuzi wake wa kuagiza siku ya uhuru wa Tanganyika iadhimishwe kwa shughuli ya usafi hospitalini hapo na akasema jambo hilo limesaidia mazingia ya utoaji tiba.

“Usafi uliofanyika unatengeneza mazingira mazuri ya kutolea huduma kwa hospitali lakini pia matendo ya huruma yaliyofanyika kwa wagonjwa wetu tunasema hii ni sehemu ya tiba,” alisema Ngore.

Katika hatua nyingine, Mkuu wa Wilaya Magiri ameshauri vyombo vya ulinzi na usalama wilayani Nyasa viwe na shughuli za pamoja ikiwemo mazoezi ya pamoja au hafla mbalimbali ikiwemo za kukaribisha mwaka.

Watoto Hassan na Hussein Amri Jummane (3) waliozaliwa wakiwa wameungana kwenye nyonga, kifua na wana miguu mitatu sasa w...
09/12/2024

Watoto Hassan na Hussein Amri Jummane (3) waliozaliwa wakiwa wameungana kwenye nyonga, kifua na wana miguu mitatu sasa wamereja nchini baada ya kufanyiwa upasuaji wa kutenganishwa huko nchini Saudi Arabia.

Akizungumza na vyombo vya habari kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) Dkt. Rachel Mhaville amesema watoto hao walipokelewa hospitalini hapo Agosti 2021 kutokea Igunga Tabora wakiwa na umri wa wiki mbili na kukaa hospitalini hapo miezi 11 wakipata matibabu mbalimbali na kuondoka kwenda nchini Saudi Arabia kwa ndege maalum Agosti 23, 2023 ili kufanyiwa upasuaji mkubwa wa kuwatenganisha.

Dkt. Mhaville amesema MNH ina uwezo wa kufanya upasuaji wa aina hiyo kutokana na wataalam na miundombinu iliyojitosheleza ila kutokana namna watoto hao walivyokuwa wameungana ilihitaji utaalam wa juu zaidi hivyo Serikali ya Saudi Arabia ilichukua jukumu ya kuwasafirisha ambapo tarehe 05 Oktoba, 2023 walifayiwa upasuaji huo uliodumu kwa saa 16.

Aidha Dkt. Mhaville ameishukuru Serikali ya Saudi Arabia kwa msaada huo ambao umewarejesha watoto hao katika maisha ya kawaida na kuongeza kuwa watoto hao wataendelea kuwepo eneo la Muhimbili kwani bado wanaendelea na matibabu ya awamu mbalimbali kuboresha ustawi wa maisha yao.

Katika hatua nyingine Dkt. Mhaville amewataka Watanzania kujitolea kumjengea makazi bora mama wa watoto hao ambaye anatoka katika mazingira duni huko Igunga Tabora ili aweze kuwalea vizuri kulingana na hali walizo nazo.

Kwa upande wake Mama wa Watoto hao Bi. Hadija Shabani ameishukuru Serikali ya Saudi Arabia kwa msaada wa matibabu ya kutenganisha watoto hao pamoja na Serikali ya Tanzania kwa jinsi ilivyoratibu zoezi la watoto hao kufanyiwa upasuaji wa kuwatenganisha.

Naye Daktari Bingwa Mbobezi wa Upasuaji Watoto wa MNH Dkt. Zaituni Bokhary amesema jopo la madaktari wabobezi upasuaji wa mishipa ya damu, mfumo wa mkojo wa watoto walishiriki upasuaji huo uliofanyika hospitali ya King Abdulaziz iyopo Riyadh Saudi Arabia

Written by

Mkuu wa Wilaya ya Babati, Emmanuela Kaganda, ameonyesha kutoridhishwa na baadhi ya taasisi kutokushiriki sherehe za miak...
09/12/2024

Mkuu wa Wilaya ya Babati, Emmanuela Kaganda, ameonyesha kutoridhishwa na baadhi ya taasisi kutokushiriki sherehe za miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania, zilizofanyika leo.

Katika hotuba yake akifungua mdahalo maalum kuhusu uhuru, Kaganda alieleza kuwa kitendo cha taasisi hizo kutoonekana katika sherehe hizo ni dhihirisho la ukosefu wa uzalendo na kushindwa kutambua umuhimu wa siku hiyo adhimu kwa Taifa.

Akizungumza kwa msisitizo, Kaganda aliagiza taasisi zote ambazo hazikuhudhuria sherehe hizo kuwasilisha maelezo ya maandishi yakieleza sababu za kutokushiriki.

Aliongeza kuwa hatua hiyo ni muhimu ili kuhakikisha kila taasisi inawajibika ipasavyo na inatoa mchango wake katika matukio ya kitaifa yanayojenga mshik**ano na heshima kwa nchi.

“Sherehe za Uhuru siyo tu siku ya kumbukumbu, bali ni fursa ya kuonyesha mshik**ano wetu k**a Taifa, Kutohudhuria ni sawa na kudharau historia ya nchi yetu na juhudi za waasisi wa Uhuru” alisema Kaganda

Tunahitaji kujua sababu za kushindwa kwenu kufika, ninaomba mdahalo huu urudiwe wakihusishwa Vijana, Wanafunzi na taasisi zote” alisema Kaganda

Aidha, Mkuu huyo wa Wilaya alisisitiza umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika matukio ya kitaifa k**a njia ya kudumisha mshik**ano wa kijamii na uzalendo miongoni mwa Watanzania.

Miaka 63 ya uhuru wa Tanzania unaadhimishwa leo kwa ngazi za mikoa na wilaya ili kuwakumbusha wananchi wapi nchi imetoka, ambapo katika mkoa wa Manyara imefanyika mjini Babati ikiongozwa na mkuu wa wilaya ya Babati kwa niaba ya mkuu wa mkoa Mheshimiwa Queen Sendiga.

Written by

Rufiji inajiandaa kwa tukio kubwa na adhimu linalofanyika kila mwaka la kumbukizi ya Mbunge wa kwanza wa Jimbo la Rufiji...
09/12/2024

Rufiji inajiandaa kwa tukio kubwa na adhimu linalofanyika kila mwaka la kumbukizi ya Mbunge wa kwanza wa Jimbo la Rufiji na mwana Umajumui wa Afrika Bibi T**i Mohamed.

Tanzania na Afrika inamkumbuka Bibi T**i Mohamed kwa mengi na mazuri ikiwemo kushiriki harakati za kupigania Uhuru wa nchi yetu, kupigania ustawi wa maisha ya wanarufiji na Pwani kwa Ujumla.

Kuanzia kwa Bibi T**i Mohamed akiwa ni Mbunge wa kwanza wa Jimbo la Rufiji sasa Jimbo hili lina Mbunge wa tisa ambae ni Mhe. Mohamed Mchengerwa.

Kupitia Mhe Mchengerwa akiwa Mbunge wa tisa kwenye Jimbo hili Rufiji imeshuhudia mengi makubwa na mazuri ya kimaendeleo kwa wanarufiji.

Sherehe hizi za kumuenzi Bibi T**i Mohamed zitaenda sambamba na uwasilishwaji wa Hali ya maendeleo ya Jimbo kwa wakati uliopita wakati wa sasa na Dira ya maendeleo. Mhe Mchengerwa amekwisha hudumu ngwe mbili 2015 - 2020 na 2020 - 2025 ni Mbunge aliyeingia katika historia ya kuongoza vipindi viwili mfululizo na Mwenyezi MUNGU akipenda 2025 kwenda 30 atavunja rekodi yake mwenyewe kwa kuendelea kuongoza kwa ngwe ya tatu mfululizo.

Wanarufiji wanalo la kujivunia kwa kijana wao hodari na mchapakazi Mohamed Mchengerwa kwa kuwaletea maendeleo.





*RUFIJI YA SASA*,
*MCHENGERWA MTUKAZI*

Simba nao wameshenentwa Algeria na Constantine kwa goli 2-1.Unahisi vilabu vya Tanzania vimekumbwa na tatizo gani ugenin...
08/12/2024

Simba nao wameshenentwa Algeria na Constantine kwa goli 2-1.

Unahisi vilabu vya Tanzania vimekumbwa na tatizo gani ugenini??

Simba wamewekwa cha pili huko, ndani ya dakika 4 magoli mawili
08/12/2024

Simba wamewekwa cha pili huko, ndani ya dakika 4 magoli mawili

Tayari goli lisharudi huko, dakika 46 Simba wamejiweka
08/12/2024

Tayari goli lisharudi huko, dakika 46 Simba wamejiweka

Mchezo mapumziko mpaka sasa Simba wapo mbele kwa goli moja.Kitu gani umekipenda mpaka sasa kutoka kwa Simba??
08/12/2024

Mchezo mapumziko mpaka sasa Simba wapo mbele kwa goli moja.

Kitu gani umekipenda mpaka sasa kutoka kwa Simba??

Dakika ya 30 mpaka sasa Simba wapo mbele kwa goli 1 likifungwa na beki wa kushoto Tshabalala
08/12/2024

Dakika ya 30 mpaka sasa Simba wapo mbele kwa goli 1 likifungwa na beki wa kushoto Tshabalala

Kupitia Instagram yake meneja wa   ameandika kuwa:-“Nadhani ifike mahali wasanii muwekezebidii kwenye kazi, kufeki story...
08/12/2024

Kupitia Instagram yake meneja wa ameandika kuwa:-

“Nadhani ifike mahali wasanii muwekeze
bidii kwenye kazi, kufeki story sababu ya fame ya kulazimisha bifu ili kutrend haisaidii, Msanii aitwae
W***y aseme ukweli alikuwa anabishana na mtoto wa k**e (Zuchu) aliblock njia Zuchu asipande kwenye
steji akisema alikuwepo tokea mwanzo hivyo anataka
apande yeye, ihali wakati zamu yake aliita apande kwenye stage aligoma na kusema hawezi kupanda yeye ni Headliner anataka Afunge show Mwisho, baada ya kuona wenzake wanapata shangwe akawa anforce kupanda kwenye Muda wa Zuchu na wala sio Diamond. Regarding why Diamond hajapanda is between us and organizer has nothing to do na msanii yoyote. Bless Up”

Written by

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na mabadiliko ya Viongozi mbalimb...
08/12/2024

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi na mabadiliko ya Viongozi mbalimbali. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, uteuzi na mabadiliko ya viongozi hao ni k**a ifuatavyo:-

Swipe kusoma Teusi zote

Address

Dar Es Salaam
23207

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Bongo5.com posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Bongo5.com:

Videos

Share