Tree Tv Online

Tree Tv Online Fuatana nasi kwa Habari za Uhakika

📍IKULU,Dar es SalaamRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Ra...
27/01/2025

📍IKULU,Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Rais wa Benki ya Dunia Bw. Ajay Banga,Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 27 Januari, 2025



📸:IKULU

📍Dar es Salaam🇹🇿🇲🇷▪️RAIS WA AWASILI TANZANIA KWA AJILI YA MKUTANO WA NISHATIRais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania, M...
27/01/2025

📍Dar es Salaam

🇹🇿🇲🇷

▪️RAIS WA AWASILI TANZANIA KWA AJILI YA MKUTANO WA NISHATI

Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania, Mheshimiwa Mohamed Ould Ghazouani, amewasili jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati.

Alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Mheshimiwa Mohamed Ould Ghazouani, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, alipokelewa na Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Festo Dugange,Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mheshimiwa Albert Chalamila pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati unafanyika jijini Dar es Salaam tarehe 27 na 28 Januari 2025 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere.

Mkutano huo unawaleta pamoja Wakuu wa Nchi za Afrika, wataalam wa nishati, viongozi wa sekta binafsi, na washirika wa maendeleo kwa ajili ya kujadili mikakati ya kukabiliana na changamoto za nishati na kuchangamkia fursa za bara hili. Kipengele muhimu cha mkutano huu kitakuwa kupitishwa kwa Azimio la Dar es Salaam, linalosisitiza dhamira ya pamoja ya viongozi wa Afrika kuhakikisha upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu kwa maendeleo ya bara la Afrika.

Tumejidhatiti kukuhudumia masaa 24, siku saba za wiki👌.   kuwasiliana na dawati la huduma kwa wateja la TCRA; piga simu ...
27/01/2025

Tumejidhatiti kukuhudumia masaa 24, siku saba za wiki👌. kuwasiliana na dawati la huduma kwa wateja la TCRA; piga simu bila malipo kupitia namba 0800008272, au tuma baruapepe kwenda [email protected].

📌Karibu Tukuhudumie📌

Makamu wa Rais wa Gambia awasili TanzaniaMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Gambia, Mhe. Muhammad Jallow amewasili jijini Dar ...
27/01/2025

Makamu wa Rais wa Gambia awasili Tanzania

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Gambia, Mhe. Muhammad Jallow amewasili jijini Dar es Salaam ambapo anamwakilisha Mheshimiwa Rais Adama Barrow katika Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika kuhusu Nishati, unaotarajiwa kuanza leo, Januari 27 na 28 2025 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere.
Mhe. Jallow amepokelewa na Waziri wa Maji nchini, Mhe. Jumaa Aweso.

Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika unawakutanisha viongozi wa nchi za Afrika, wadau wa Sekta ya Nishati na wadau wa maendeleo. Lengo ni kuimarisha juhudi za pamoja katika kukabiliana na changamoto za nishati barani Afrika, sambamba na kupitisha Azimio la Dar es Salaam, linalodhamiria kuimarisha juhudi za pamoja za Viongozi wa Nchi na Serikali za Afrika katika kuhakikisha Afrika inaondokana na changamoto za upatikanaji wa nishati ya uhakika, nafuu, na endelevu.

“Nimewaondolea Ulinzi wa Kiserikali kwasababu walifanya kazi serikalini na naamini walitengeneza fedha za kutosha sana h...
27/01/2025

“Nimewaondolea Ulinzi wa Kiserikali kwasababu walifanya kazi serikalini na naamini walitengeneza fedha za kutosha sana hivyo wanaweza kuajiri Walinzi wao binafsi, kufanya kazi serikalini haina maana ubaki na Walinzi maisha yako yote”

-Rais Donald Trump baada ya kuwaondolea Walinzi Viongozi mbalimbali wastaafu wa serikali ya Marekani.

📍Dar es Salaam▪️DKT. BITEKO AFUNGUA MKUTANO WA NISHATI WA VIONGOZI - AFRIKANaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. ...
27/01/2025

📍Dar es Salaam

▪️DKT. BITEKO AFUNGUA MKUTANO WA NISHATI WA VIONGOZI - AFRIKA

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akifungua Mkutano wa Nishati Barani Afrika (Africa Energy Summit, 2025) leo Januari 27, 2025 unaoendelea katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

The Deputy Prime Minister of the United Republic of Tanzania and Minister for Energy, Hon. Doto Biteko, giving his remarks in the official openning speech Africa Energy Summit 2025 in Dar es Salaam, held at the Julius Nyerere International Convention
Centre on January 27, 2025.



📸:W/Nishati

MATUKIO KATIKA PICHA.Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akifungua Mkutano wa Nishati wa Nchi ...
27/01/2025

MATUKIO KATIKA PICHA.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akifungua Mkutano wa Nishati wa Nchi za Afrika (Afrika Energy Summit) katika kituo Cha Mikutano Cha kimataifa Cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam, leo tarehe 27 Januari 2025.

27/01/2025

Sekta ya Utalii tupo tayari na tumenogesha jiji la Dar es Salaam kuelekea Mkutano wa Nishati Afrika 2025. Ukikutana na hawa jamaa wa porini usiogope wako powa na hawatakupopoa, we piga picha na sambaza🙏🏽🙏🏽🇹🇿🇹🇿

27/01/2025

Makumbusho ya Mawasiliano ni Hazina ya historia, elimu na burudani. Karibu utembelee makumbusho hii iliyopo katika ofisi za TCRA jijini Dar es Salaam.
📌HAKUNA KIINGILIO.
📞0800008272 kwa taarifa zaidi.

27/01/2025

Fahamu faida za kushiriki kwenye Tuzo za kimataifa za WSIS 2025. Kutazama kipindi kamili, tafadhali bofya link https://bit.ly/3Cm04Gy

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ( TCRA) inakutakia Heri ya siku ya kuzaliwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe...
27/01/2025

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ( TCRA) inakutakia Heri ya siku ya kuzaliwa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan


27/01/2025

kumtambua tapeli. K**a sio namba mia moja (100) potezea

Usikose Kufuatilia📻 “Kipindi Maalumu”, Living Water FM 103.3 FM📍 Mwanza📌Mada: NI RAHISI SANA🗓️ 27/1/2025, Jumatatu🕓 10:0...
27/01/2025

Usikose Kufuatilia

📻 “Kipindi Maalumu”, Living Water FM 103.3 FM
📍 Mwanza
📌Mada: NI RAHISI SANA
🗓️ 27/1/2025, Jumatatu
🕓 10:00 Jioni

WASIRA: UAMUZI WA MKUTANO MKUU UMEZINGATIA KATIBA YA CCM- Awapa darasa wanaodai sababu ya CCM kupitisha wagombea Urais- ...
27/01/2025

WASIRA: UAMUZI WA MKUTANO MKUU UMEZINGATIA KATIBA YA CCM

- Awapa darasa wanaodai sababu ya CCM kupitisha wagombea Urais

- Asema yupo tayari kuwapa somo waifahamu vyema katiba ya Chama

MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mainduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira, amesema uamuzi wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM, uliomchagua Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kugombea kiti cha Urais wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, umezingatia takwa la kikatiba na mamlaka ya Mkutano Mkuu.

Amesema baadhi ya watu wanaojiita wanaCCM wanaodai kwamba bado hawajaelewa sababu ya wajumbe wa Mkutano Mkuu Maalum wa CCM kupitisha uamuzi huo, atawasaidia kuelewesha kwani uwezo wa binadamu kufahamu jambo hauwezi kulingana.

Wasira aliyasema hayo jijini Dar es Salaam leo wakati viongozi, wanachama, wapenzi wa CCM na wananchi kutoka maeneo mbalimbali walipojitokeza kumpokea.

"Baada ya Mkutano Mkuu kutambua kazi kubwa zilizofanywa na serikali zote mbili, Serikali ya Muungano na Serikali ya Zanzibar, Mkutano Mkuu wa CCM ukasema k**a hali ni hii kuna sababu gani kuchelewesha kutangaza mgombea?.

"Sasa wapo watu wanaosema wao ni wanachama wa CCM, hawakuelewa. Hilo nalo siyo jambo la ajabu. Tutawasaidia kuelewa maana siyo watu wote wanaweza kuelewa sawa. lakini tunawaambia Mkutano Mkuu kwa mujibu wa Katiba ya CCM ndiyo kikao kikuu cha mwisho," amesema.

Wasira ameeleza kuwa Mkutano Mkuu wa Chama una mamlaka ya kubadili, kufuta na kurekebisha uamuzi wowote uliofanywa na kikao cha chini yake, kufuta maamuzi yaliyofanywa na kiongozi yeyote wa CCM.

Amesisitiza: "Sasa aliye na mashaka katika jambo hilo k**a wote hawawezi aje kwangu nitamsadia maana katiba ipo kichwani. Uamuzi tulioufanya umezingatia Katiba ya CCM ibara ya 101 inayotutaka tuchague jina moja la kuwa mgombea wa kiti cha Urais, tulitumia ibara hiyo na kwa mamlaka ya Mkutano Mkuu ameteuliwa Dk. Samia."
===

  kuwa salama mtandaoni.Ewe Mzazi/Mlezi, usalama wa mtoto wako mtandaoni unaanza nyumbani kwako. Tuwajenge katika mising...
25/01/2025

kuwa salama mtandaoni.

Ewe Mzazi/Mlezi, usalama wa mtoto wako mtandaoni unaanza nyumbani kwako. Tuwajenge katika misingi ya matumizi salama ya Teknolojia, ili wawe sehemu ya ujenzi wa uchumi wa kidijiti.

25/01/2025

Goodluck Gozbert muimbaji maarufu wa nyimbo za Injili amesema Nabii alimpa zawadi ya Gari aina ya Benz mwaka 2021. Sasa ameonesha video ya kuchoma moto gari hilo na kusema kwamba Chakula alichokula na ibada aliyoshiriki siku hiyo alipokabidhiwa gari hilo havikumpendeza MUNGU.

Nini maoni yako

Address

Tabata
Dar Es Salaam

Telephone

+255766660001

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Tree Tv Online posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Videos

Share