07/09/2024
MASOMO YA MISA, SEPTEMBA 08, 2024
DOMINIKA YA 23 YA MWAKA B WA KANISA
MWANZO:
Zab. 119:137, 124
Ee Bwana, wewe ndiwe mwenye haki, na hukumu zako ni za adili. K**a zilivyo rehema zako umtendee mtumishi wako.
SOMO 1
Isa. 35:4-7a
Waambieni walio na moyo wa hofu, Jipeni moyo, msiogope; tazama, Mungu wenu atakuja na kisasi, na malipo ya Mungu; atakuja na kuwaokoa ninyi. Ndipo macho ya vipofu yatafumbuliwa, na masikio ya viziwi yatazibuliwa. Ndipo mtu aliye kilema atarukaruka k**a kulungu, na ulimi wake aliye bubu utaimba; maana katika nyika maji yatabubujika; na vijito jangwani. Na mchanga ungโaao mfano wa maji utakuwa ziwa la maji, na nchi yenye kiu itakuwa chemchemi za maji.
Neno la Bwanaโฆ Tumshukuru Mungu.
WIMBO WA KATIKATI
Zab. 146:7-10 (K) 1
(K) Ee nafsi yangu, umsifu Bwana.
Bwana ndiye ashikaye kweli milele,
Huwafanyia hukumu walioonewa.
Huwapa wenye njaa chakula;
Bwana hufungua waliofungwa. (K)
Bwana huwafumbua macho waliopofuka,
Huwainua walioinama.
Bwana huwapenda wenye haki,
Huwahifadhi wageni. (K)
Bwana huwategemeza yatima na mjane,
Bali njia ya wasio haki huipotosha.
Bwana atamiliki milele,
Mungu wako, Ee Sayuni, kizazi hata kizazi. (K)
SOMO 2
Yak. 2:1-5
Ndugu zangu, imani ya Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wa utukufu, msiwe nayo kwa kupendelea watu. Maana akiingia katika sinagogi lenu mtu mwenye pete ya dhahabu na mavzi mazuri; kisha akiingia na maskini, mwenye mavzi mabovu; nanyi mkimstahi yule aliyevaa mavzi mazuri, na kumwambia, Keti wewe hapa mahali pazuri; na kumwambia yule maskini, Simama wewe pale, au keti miguuni pangu, je! Hamkufanya hitilafu mioyoni mwenu, mkawa waamuzi wenye mawazo mabovu? Ndugu zangu wapenzi, sikilizeni, Je! Mungu hakuwachagua maskini wa dunia wawe matajiri wa imani na warithi wa ufalme aliowaahidia wampendao?
Neno la Bwanaโฆ Tumshukuru Mungu.
SHANGILIO
Yn. 8:12
Aleluya, aleluya.
Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, asema Bwana; Yeye anifuataye atakuwa na nuru ya uzima.
Aleluya.
INJILI
Mk. 7:31-37
Yesu alitoka katika mipaka ya Tiro, akapita katikati ya Sidoni, akaenda mpaka bahari ya Galilaya, kati ya mipaka ya Deakapoli. Wakamletea kiziwi, naye ni mwenye utasi, wakamsihi amwekee mikono. Akamtenga na mkutano faraghani, akatia vidole vyake masikioni mwake, akatema mate, akamgusa ulimi, akamtazama juu mbinguni, akaugua, akamwambia, Efatha, maana yake, Funguka. Mara masikio yake yakafunguka, kifungo cha ulimi wake kikalegea, akasema vizuri. Akawaonya wasimwambie mtu; lakini kadiri ya alivyozidi kuwaagiza, ndivyo walivyozidi kutangaza habari; wakashangaa mno kupita kiasi, wakinena, Ametenda mambo yote vema; viziwi awafanya wasikie, na bubu waseme.
Neno la Bwanaโฆ Sifa kwako Ee Kristu.
DOMINIKA YA 23 YA MWAKA B WA KANISA
TAFAKARI
Karibuni ndugu zangu kwa adhimisho la misa takatifu asubuhi ya leo. Neno la Bwana leo tafakari yake inaongozwa na zaburi yetu ya wimbo wa katikati-Ee nafsi yangu umsifu Bwana. Hii ni zaburi ya shukrani na shangwe ya jinsi Bwana alivyomwema na mkuu. Yeye basi ameutendea makubwa moyo wa mwanadamu-yeye ndiye atoaye haki kwa anayeonewa, awapaye wenye njaa chakula, na awafunguao mateka. Yeye pia huwasaidia wageni, na kutoa nuru kwa vipofu, ni mume wa mjane na Baba wa yatima na nguvu zake na enzi yake ni kwa vizazi vyote.
Maneno yaliandikwa na kuhani mmoja baada ya ule uhamisho wa Babeli na baada ya wana wa Israeli kurudi nyumbani. Basi anakumbukia jinsi Mungu alivyosafiri nao akiwa kule utumwani, jinsi alivyokuwa Baba kwao kule ugenini ambako hawakuwa na mwenyeji, jinsi alivyoweza kuwapatia haki yao-basi waliishia kusema kwamba kweli ni lazima ee nafsi yangu umsifu Bwana, usiache kabisa kumsifu ee nafsi yangu. Na watoto wetu kumbukeni wema aliotutendea kule utumwani-kweli ni haki nafsi zetu zimsifu.
Maneno haya yanatumika kuelezea basi tena kwa msisitizo ujumbe wa nabii Isaya. Hapa tunakutana na wana wa Israeli wakiwa utumwani Babuloni nani wenye hofu kubwa. Wanawaogopa wababuloni, na pia wanaonewa. Leo basi anatoa matumaini kwa wale wenye moyo wa hofu na unyonge-anawaambia msiogope, Mungu Bwna wetu yupo, anatupenda, anakuja kutoa haki na hukumu. Na kwenye hukumu hii basi viziwi na vilema na bubu wasioweza kuona au kusikia watakuwa na sababu za kurukaruka na kushangilia kwani watatendewa kwa haki-wao hawajawahi kupata mtetezi lakini sasa basi watapata.
Maneno haya ya Isaya yalisemwa kwa baadhi ya wana wa Yuda na yalielekezwa kwa wale waliokuwa wamezoea kukosewa haki na kudhulumiwa. Sasa anawaambia kwamba Bwana atakuja kwenu na akija, kutakuwa na furaha. Palipozoea kudhulumiwa patakuwa na kila sababu ya kufurahi na kuchanua.
Ndugu zangu, ingawa basi unabii huu wa Isaya ulitimia kwa kiasi fulani baada ya wana wa Israeli kukombolewa utumwani Babeli, kwa mapana ulitimia kwa ujio wa Yesu. Huyu ndiye aliyekuwa sababu ya matumaini kwa wenye hofu, viziwi, bubu na wanaonewa na wageni. Na leo basi anawaponya viziwi na bubu tena kwa kutumia upendo mkubwa kabisa. Anamshika kwa kutumia mikono yake mitakatifu na baadaye kupona.
Ndugu zangu, Yesu alikuwa utimilifu mkuu kabisa wa unabii wa somo letu la kwanza. Yeye kweli alitangaza haya matumaini. Viziwi na bubu wa nyakati zetu ni wale wanaokosa maarifa katika jambo fulani-labda yule asiyejua kiingereza au asiyejua sheria fulani fulani.
Lazima tuwe k**a Yesu kwa watu hawa kwa kuwaletea matumaini. Usione mtu hajui kiingereza na wewe ukaamua kumtafsiria vitu vya uongo au asiyejua mahesabu na wewe ukamhesabia hesabu za uongo au asiyejua kuandika ukamdanganya. Au mgeni anayeulizia kutaka kujua eneo fulani wewe unamdanganya ili apotee au unampitisha njia ndefu ili basi labda u-uchukulie faida au unamuuzia kitu kibovu au unamuuzia kiwanja kilichoko kwenye maji, au gari bovu lililopigwa rangi au simu mbovu au bidhaa feki. Haya ni mambo tuliyokuwa tunayatenda maishani mwetu lakini kwa hapa kweli hatuwi k**a Yesu. Tunakuwa kinyume cha Yesu.
Jiulize kwa kudanganya wasiojua kiingereza au kuwauzia watu bidhaa fake kweli hapa umekuwa k**a Yesu? Sio vyema. Tusitese wageni. Yesu anafungua watu macho leo. Wewe wafungue macho.
Yesu amekwishakuja kuwapa viziwi na bubu na vipofu mwanga. Hivyo basi usivumilie giza leindelee kutawala. Wazuie wote wanaotaka kuziba macho na masikio ya wengine. Ukiona mtu akiuziwa kitu kibovu-mwambie, au ukiona mmoja anadanganya ili basi amzidi maarifa mwingine-mwambie Yesu amekwisha leta mwanga. Usiturudishe tena gizani. Acha tabia zako. Au hata ukimsikia mwanasheria anakuja na kudanganya na kuandaa uongo wake mpinge. Mwambie tumekwishaletewa mwanga na Kristo wetu.
Kingine ni kwamba Kristo leo ameonyesha kujali sana huyu bubu kiziwi. Amediriki hata kuugusa ulimi wake. Niambie ndugu zangu ni nani kati yetu aliye na utayari huu? Niambie jamani. Unafahamu kwamba hawa wasioweza kusema muda mwingi unakuta wanashusha udenda. Sasa yeye anaushika ule ulimi. Kweli hili ni tendo la ajabu. Sasa sisi tupo hivyo? Nikikuambia wewe kadada uliyevaa kana kwamba hujawahi kuchafuka, sasa nikikuambia uuguse ulimi wa bubu anayeshusha udenda utakubali? Au wa mwenye ukimwi au wa mwenye kansa. Kweli nasema ya kwamba Yesu ni mfano wetu wa kuigwa. Wengi kati yetu tunajitenga sana na wenzetu hasa kwa nyakati zetu. Hatuli na wagonjwa, tunawanyanyapaa. Wewe ndugu yanvu wewe-badilika. Tunza wazazi wako. Acha kujivuna na kujiona sana. Usijifanye kuona kinyaa.
Kingine ni kutambua kwamba kweli kuna watu wenye hofu kubwa. Kuna anayeishi kwa madeni kiasi kwamba anaogopa kupokea simu yoyote. Akiona simu anafikiri ni mtu anayetafuta deni lake anampigia na hivyo hapokei. Kuna asiyelipa kodi ya nyumba na hivyo basi hadhubutu kufika nyumbani mchana kwani anaogopa kudaiwa na mwenye nyumba. Akisikia hodi tu mara moja anamwambia mtoto usimwambie nipo. Kaa kimya. Kweli kuna wenye hofu nyingi sana. Mwingine ni mwoga uchawi au waganga au bundi akilia usiku hathubutu kulala. Atakwenda kuweka chumvi au akiingia ofisini na kukuta hata mjusi atamkemea. Mwingine ukimwalika ale chakula anafikiri labda utamloga au kumwekea sumu. Hivyo hali kabisa. Hivyo bado tunamhitaji Isaya mpya atutie matumaini. Wengi wetu bado tupo nyuma sana. Mwambie jamani Mungu yupo, sio kwamba ndani yahii dunia ni shetani ndiye aongozaye kila kitu. Yesu yupo pia nani wakutumainiwa sana. Acha woga wako hapa.
Unakuta hadi kiongozi wa jumuiya unaogopa uchawi; wewe?
Kingine ni kwamba watu ndio wanaoamua kumpeleka huyu mgonjwa na kilema kwa yesu na kweli anapona. Yule kilema hakuwa na uwezo wa kusema au kusikia yale mafundisho ya Yesu; ni Yesu ndiye aliyemfunulia tu. Ndivyo ilivyo na kwetu sisi ndugu zangu. Lazima jamii itusaidie, itupeleke kunakostahili, iwe k**a hii. K**a ni mgonjwa mumpeleke hospitali. Jamii mna mchango mkubwa sana. Sio vizuri mtu kuumwa na kuachwa k**a kwamba ni sisimizi aliyeshindwa na safari. Jamii lazima imsaidie na hili ni jukumu letu.
Kwenye somo la pili tunakutana na Paulo akikemea tabia za baadhi ya wakorintho kutokuwa watu wa kuwatilia wengine mataumaini. Walipoona maskini hawakuwapatia matumani-waliwafukuza na kuwastahi matajiri tu.
Sisi tuepukane na tabia hizi. Kwenye sherehe sio vizuri kuwafukuza maskini au kuwaalika tajiri tu. Maskini pia wapatiwe nafasi ndugu zangu. Kweli maskini tulikwishawadharau kwenye kanisa kiasi kwamba hadi leo kwenye kumchagua mwenyekiti wa halmashauri ya walei ni lazima uwe na pesa, maskini hapana jamani, tuwe watu wa kuwapatia maskini matumaini-baadhi ya hawa wenye viti hawana hekima yeyote-ni ujinga tu, watapigana hata na watu huko lakini ni pesa tu zinatufanya ati wachaguliwe. Hawa viongozi wasichaguliwe kwa kutazama fedha jamani. Wengine wanatumia dini k**a sehemu ya kufichia dhambi zao. Hekima yako ikuchague.
Tuwe Yesu leo. Watie watu matumaini. Amina.