World Sports Updates

World Sports Updates Ukurasa huu ni Kwa ajiri ya habari mbali mbali zinazotrend za Michezo Duniani

🚨| UPDATE: HENOCK INONGA- Mlinzi wa Simba, Henock Inonga ameuambia Uongozi kuwa anahitaji kuondoka klabuni hapo mwishoni...
10/05/2024

🚨| UPDATE: HENOCK INONGA

- Mlinzi wa Simba, Henock Inonga ameuambia Uongozi kuwa anahitaji kuondoka klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu na hataendelea kuitumikia klabu hiyo

- Menejiment ya Inonga imempa taarifa mteja wao kuwa walishapata timu mpya ya kwenda kusaini kuitumikia.

🚨AYOUB LYANGA 🔁 SIMBA SCHabari zilizonifikia mezanii ni kwamba Simba SC imemwekea ofa ya Tsh million 200 winga Ayoub Lya...
09/05/2024

🚨AYOUB LYANGA 🔁 SIMBA SC

Habari zilizonifikia mezanii ni kwamba Simba SC imemwekea ofa ya Tsh million 200 winga Ayoub Lyanga anaelekea kumaliza mkataba wake mwisho wa msimu huu.

Za ndaaaaani zinaeleza kuwa nyota huyo amegomea mkataba mpya huko Azam FC na Simba SC wamemwekea mezanii mshahara wa Tsh million 10 kwa mwezi.

🚨BREAKING NEWS: Klabu ya Yanga imekamilisha usajili wa beki wa kushoto wa FC Lupopo, Chadrac Boka mwenye miaka 24,ni mba...
09/05/2024

🚨BREAKING NEWS:

Klabu ya Yanga imekamilisha usajili wa beki wa kushoto wa FC Lupopo, Chadrac Boka mwenye miaka 24,ni mbadala wa Lomalisa Mutambala ambaye atatimka mwisho wa huu msimu, huyu beki huko DR Congo wanamuita Rais wa Maji au Marcelo wa DR Congo.

🚨| UPDATE: SAIDI NTIBAZONKIZA- Kiungo mshambuliaji wa Simba, Saidi Ntibazonkiza ameanza kuaga baadhi ya Wachezaji wenzak...
09/05/2024

🚨| UPDATE: SAIDI NTIBAZONKIZA

- Kiungo mshambuliaji wa Simba, Saidi Ntibazonkiza ameanza kuaga baadhi ya Wachezaji wenzake kwakuwa ameshapewa taarifa na klabu hiyo kuwa hayupo kwenye mipango kuelekea msimu ujao.

- Kutokana na hilo Saidi Ntibazonkiza atakuwa mchezaji huru ( Free agent ) mwishoni mwa msimu huu, klabu ya Simba haitamuongezea mkataba mpya mchezaji huyo baada ya msimu kumalizika.

- Ntibazonkiza is going to be a free agent as there are no talks to extend a new contract .

UPCOMING TRANSFER WINDOW 🪟 UPDATE 🔔📝💰🔔 🛜💻Simba SC inawatazama Mousa Camara na Kayode Bankole k**a wachezaji wanaoweza ku...
08/05/2024

UPCOMING TRANSFER WINDOW 🪟 UPDATE 🔔📝💰🔔

🛜💻Simba SC inawatazama Mousa Camara na Kayode Bankole k**a wachezaji wanaoweza kuchukua nafasi ya lakred k**a ataondoka Simba sc. Uchezaji wao umevutia sana upande wa nyumbani kwao nigeria ukionyesha tayari wanaweza kucheza soka la ushindani hasahasa la kimataifa .

NB;Kutana na Kayode Bankole wa Remo Stars. Mlinda lango huyo kwa sasa ndiye mwenye CLEAN SHEETS nyingi zaidi kwenye Ligi ya Mpira wa Miguu ya Nigeria.

Rekodi yake katika NPFL ni bora; Pia ndiye golikipa mwenye clean sheet nyingi zaidi katika misimu 2 iliyopita.

Kufikia hapa; kufikia sasa:

Ana clean sheets 42 katika mechi 78 za Ligi alizocheza🧤🥅

BADO MNA SHAKA NAYE 🛜💻

Kumbuka anamiaka 21 tu na amezaliwa 2002 ,mguu anaoupenda kuutumia ni wa kulia .amezaliwa tarehe 16/10/2002

Ni raia wa Nigeria na aliongeza mkataba 📝 tarehe 13/10/2021 na mkataba wake unafika ukingoni December 12/12/2024 ana urefu wa 1,85 m ni goalkeeper namba 1 wa REMO STARS ya Nigeria.

Kwangu MCB MICHEZO nampa KAYODE BANKOLE k**a mrithi sahihi 🫂 NI INCREDIBLE GOALKEEPER 🧤 🥅

🟡💎| UPDATE: CHADRACK BOKA- Klabu ya Yanga imeshafungua mazungumzo rasmi na klabu ya Saint Eloi Lupopo ili kupata saini y...
08/05/2024

🟡💎| UPDATE: CHADRACK BOKA

- Klabu ya Yanga imeshafungua mazungumzo rasmi na klabu ya Saint Eloi Lupopo ili kupata saini ya beki wao wa kushoto raia wa DR Congo, Chadrack Boka katika dirisha lijalo la uhamisho

- Mazungumzo yamefikia hatua nzuri sana kupata saini ya beki huyo.

⚫💎| UPDATE: LAMECK LAWI- Klabu ya Simba imekubali kutuma ofa Tsh Milioni 200 kwa Wamangushi ili kuinasa saini ya mlinzi ...
08/05/2024

⚫💎| UPDATE: LAMECK LAWI

- Klabu ya Simba imekubali kutuma ofa Tsh Milioni 200 kwa Wamangushi ili kuinasa saini ya mlinzi wa klabu ya Coastal Union, Lameck Lawi katika dirisha lijalo la uhamisho kuongeza nguvu kuelekea msimu ujao.

- Mwanzo klabu ya Simba walihitaji kulipa Tsh Milioni 170 lakini klabu ya Coastal Union walikataa ofa hiyo, ndipo Wekundu wa Msimbazi walikaa na kukubali matakwa ya Coastal Union kuhusu usajili wa Lameck Lawi.

- Inatajwa Azam na Ihefu zinajiandaa kutuma ofa rasmi ambazo ni serious kwa Coastal Union, Taarifa za kuaminika ni kuwa Lameck Lawi hajasaini karatasi zozote mpaka sasa za kimkataba katika klabu yoyote.

Kuna nini huko msimbazi🚀🚀🚀🚀
07/05/2024

Kuna nini huko msimbazi🚀🚀🚀🚀

Mabosi wa Simba wameshatuma mtu kwa beki wa kati wa ASEC Mimosas, Anthony Tra Bi Tra (25). Hesabu za vigogo hao wa Simba...
07/05/2024

Mabosi wa Simba wameshatuma mtu kwa beki wa kati wa ASEC Mimosas, Anthony Tra Bi Tra (25). Hesabu za vigogo hao wa Simba zinakuja baada ya kutokuwa na uhakika wa kubakia msimu ujao kwa beki wa kikosi hicho, Henock Inonga ambaye taarifa zinaeleza mwishoni mwa msimu huu anaweza kuondoka ili kutafuta changamoto mpya huku FAR Rabat ya Morocco ikimuhitaji.

Tra Bi Tra ameiongoza ASEC Mimosas kufika hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku akionyesha nia ya dhati ya kutaka kuondoka kutafuta changamoto mpya baada ya kuitumikia timu hiyo tangu mwaka 2021 akitokea FC Foix.

Tayari mabosi hao wameanza kujipanga mapema baada ya kuona ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu ni ngumu kuuchukua kwani watani zao Yanga wako kwenye nafasi nzuri ya kuuchukua kwa mara ya tatu mfululizo jambo ambalo hawataki litokea msimu ujao. Simba mpaka sasa ina asilimia kubwa ya kumpata beki mzawa wa Coastal Union, Lameck Lawi mwenye uwezo wa kucheza nafasi tatu tofauti kuanzia beki wa kati, beki wa kushoto na kiungo wa kati jambo linalowafanya kuhamishia nguvu kwa nyota wa kigeni.

05/05/2024

JUSTIN

Simba SC 🇹🇿has placed two midfielders from the Hafia SC 🇬🇳, Mohamed Damaro Camara 🇬🇳(21) and Ousmane Fernandez Drame (23) on the list of the first choice for signing in the club in case it parted with Fabrice🇨🇩 Ngoma and Sadio Kanoute🇲🇱.

Ousman Dembele alijiunga na Barcelona kutoka Dortmund kwa €105m 2017. Baada ya misimu sita huko, aliondoka na kujiunga n...
17/04/2024

Ousman Dembele alijiunga na Barcelona kutoka Dortmund kwa €105m 2017. Baada ya misimu sita huko, aliondoka na kujiunga na PSG msimu uliopita wa joto kwa €50m tu.

Wiki iliyopita, amefunga na kusherehekea dhidi ya Barça katika mechi yao ya kwanza ya robo fainali ya UCL. Jana amewafunga bao la pili na kutoa penati ya ushindi wa mchezo huko Barcelona na kushinda tuzo ya MOTM.

Klabu ya Barcelona imezikataa ofa za klabu kadhaa za Ligi kuu ya England, ambazo ziliwasilishwa klabuni hapo ili kuhitaj...
16/04/2024

Klabu ya Barcelona imezikataa ofa za klabu kadhaa za Ligi kuu ya England, ambazo ziliwasilishwa klabuni hapo ili kuhitaji huduma ya Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Brazil Raphael Dias Belloli ‘Raphinha’.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 27, anapigiwa upatu wa kurejea England, kufuatia kushindwa kuonyesha uwezo wake k**a ilivyotarajiwa, baada ya kusajiliwa FC Barcelona akitokea Leeds United mwaka 2022.

Hata hivyo FC Barcelona anapitia katika kipindi kigumu cha uchumi, hivyo inatajwa kuwa kwenye mpango wa kuwauza baadhi ya wachezaji wake ili kujinusuru na hali hiyo.

Address

Mwanza
Dar Es Salaam
16:00PM

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when World Sports Updates posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share


Other News & Media Websites in Dar es Salaam

Show All

You may also like