11/04/2024
WINNING WITH PEOPLE
Hapo chini ni cover ya kitabu mahususi kabisa kwaajili ya kuchechemua hisia za ushirikiano baina ya watu. Kitabu hiki ni chemistry ya vitabu viwili ndani ya kitabukimoja yani Volume 1 na Volume 2. Mwandishi ni John Maxwell mwalimu na mshauri wa mambo mbalimbali ya kijamii kiuchumi na kisiasa, na ndio maana jamaa ana kitabu kingine kinachoelezea namna ya kuwa kiongozi bora. Ukihitaji mwendo ni uleule tuma request kwa normal text kupitia nambari 061 2680 598 mimi nitakudondeshea bila kuchelewa.
Licha ya hayo yote kwa mtu ambaye ameshakisoma chote bila shaka aligundua kuwa mchanyiko wa vitabu hivi viwili amakwahikika vimwana vizuri Ani huwezi kujua kwamba hiki ni chakwanza na hiki ni cha pili. Kitabu cha kwanza ni THE 17 INDISPUTABLE LAW OF TEAM WORK cha mwaka 2001 chapili ni WINNING WITH PEOPLE Cha mwaka 2004.
Hii leo nitajikita kueleza juu ya kitabu cha pili cha WINNING WITH PEOPLE (2004).
Winning with people nikitabu kinachokazia sana suala la ushirikiano miongoni mwa watu katika jamii zaidi ikiwa ni kwa wale wenye common interests kwa mfano. Wafanyakazi wa kampuni moja, Team za mpira familia nakadhalika.
Na hapa ndipo utaweza kugundua changamoto inayo zisumbuaga team nyingi za mpira wa miguu Duniani,
Ndani ya kitabu hiki kimeunganishwa na sheria 17 zile za kitabu cha kwanza yani Volume 1 ya mwaka 2001 ili kuweza kuonyesha vile mambo yanapaswa kuwa ili kupata matokeo yanayo tegemewa na kampuni au taasisi yoyote ile hapa Duniani.
Hapa chini nitaeleza sheria ya kwanza ya kushinda na watu mpaka ya tatu lakini zingne nitakubembeleza kwa Lugha ya upendo ili na wewe ukafaidike k**a Mimi na hii ndiyo maana halisi ya WINNING WITH PEOPLE.
1.The law of significance, sheria hii ina sema kwamba "one is too small number to achieve greatness".kwa tafsiri rasmi ni kwamba, moja ni namba ndogo kabisa ili kuweza kufikia mafanikio.
Hiyo ina maana gani?, Ukweli ni kwamba watu wengi tunamjua christian Ronald, Lionel Messi, Zitto Zuberi kabwe, Mack Zuckerberg, Elon musk, Diamond platinumz na wengine wengi ambao hata sijawataja hapa kuwa watu walio fanikiwa zaidi katika taaluma zao si ndio....? Lakini ni lazima tukumbuke kwamba kidole kimoja hakivunji chawa kwahiyo hakuna mtu yeyote hapa duniani anaweza kusimama na kupambana mwenye kufikia malengo makubwa ni lazima kuwa kila mtu mwenye mafanikio makubwa nyuma yake kuna timu kubwa ya watu wanao msapoti na kuonekana mwenye mafanikio zaidi mbele ya watu.
2. Sheria ya pili ni, The law of a big picture, sheria hii inasema kuwa " The goal is more important than the role" sheria hii inanikumbusha simulizi ya maana riadha mmoja Raia wa Tanzania ambaye alikuwa na malengo makubwa ya kuwa mahindi katika mashindano ya riadha yaliyo fanyika nchini japani, ilistaajabisha sana siku kwanza hakuwa kipaumbele cha mwalimu hivyo alienda tu kwa kujaza nafasi ya ziada iliyo tangazwa na mamlaka hivyo hakuwa amejianda vilivyo katika mashindano yale.
Inshu nikujianda ! Siku zote mtu mwenye big picture ya kile anachokifanya huwa na malengo makubwa na matarajio makubwa zaidi kuliko kile anachokifanya, yani mkulima wa zao la Michikichi hupanga kuzalisha zaidi ya bidhaa moja ndani zao moja la mchikichi hapa ata pata mafuta ya kupikia (mawese), atapata mafuta ya mise kwaajili ya kuzalisha sabuni za mawingu, atapata kuni za kupikia maafa baada ya kuvuna zao lile, atapata pesa ya ada nk.
Hivyo vivyo, kwa mama mjamzito huwa na picha kubwa ya kumpata mtoto kuliko maumivu ya uchungu wakati wa kujifungua atafanya hivyo zaidi ya mara tano katika maisha yake. Swali kubwa ni kwamba Kwanini akubari kubeba mimba wakati kuna maumivu yanayo sadikika kuwa Makari zaidi kuwahi kutokea hapa Duniani?
Jibu ni The law of big picture.
Malengo ni makubwa zaidi kuliko mchakato wa kujifungua.
3. Sheria ya tatu ni, The law of the niche, sheria hii inasema kwamba " All player have a place where they add the most value"
Kiukweli sheria hii inagusa maisha yetu moja kwa moja katika jamii zetu kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa, awali ya yote kumbuka wakati upo mdogo katika familia yenu pengine ulikuwa mtu ambaye hukuwa unadhaniwa k**a ungekuwa hapo ulipo aliyekuwa anadhani wa May be ni kaka ako mkubwa au yule mdogo wako anaye kufuata hii yote ni kutokana na jamii zetu kufremiwa katika Angle moja ya dunia na kusahau kuwa unaweza kufanikiwa katika Angle nyingine kabisa labda kupitia Muziki, kucheza mpira, kudance au ujasiriamali.
Ninachotaka kusema ni kwamba, kila mtu anakipaji chake. Yani kila mtu kunakitu ambacho anaweza kukifanya zaidi kuliko mwenzake iwe katika kampuni, familia, baraza, bungeni, ikuru au hata kule kwenye idara za ulinzi na usalama, na ndio maana kuna vitengo tofauti tofauti katika maisha na siyo kila sehemu kila mtu anaweza kufiti No. Mfano mimi niko vizuri katika suala la mawasiliano katika kampuni na taasisi kuliko mtu mwingine yeyote , hivyo siwezi kufanya vizuri zaidi ikiwa nitafanya majukumu ya kufanya upelelezi wa masoko (market intelligence).
Hivyo ni bora kutambua kuwa hakuna mtu yeyote yule asiye kuwa na thamani ndani ya kampuni yako au katika taasisi yako na ndio maana teuzi nyingi za serikali huenda kwa connection, na kuishia kuibua taaruki ndani ya jamii wafu wengi wa kinung'unika kuto kuzingatiwa na kuonekana k**a wamesahaurika, shida ni kutokutamburika kwa thamani yako katika serikali.
Mwisho ingawa siyo kwa umuhimu ni kuombe sasa uchukue mda wako wa thamani kwa kufanya jambo la thamani zaidi, la kumalizia sheria hizi adhimu zilizo bakia kma unahitaji kuwa na thamani zaidi katika kazi yako na utakuja kunishukuru baadaye. Yapo mengi sana ndani ya kitabu hiki ambayo yataongeza thamani ya maisha.
Cha kufanya tuma ujumbe wa kuhitaji soft copy ya kitabu hiki na mimi ni takutumi bila kuchelewa, cha msingi fanya kunichek kwa 061 268 059 8 au kwa watsap namba 0624004071.
Insta Raymond Elgius.
All the Best.