26/04/2025
"Kwa niaba ya Marekani, namtakia heri Rais Samia Suluhu Hassan na Watanzania katika kuadhimisha miaka 61 ya kuundwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Marekani inathamini sana ushirikiano wetu wa kudumu na Tanzania, ambao unatokana na tamaa yetu ya pamoja ya ustawi na usalama. Katika mwaka ujao, tunatarajia kuimarisha ushirikiano wetu kwenye biashara na uwekezaji kwa manufaa ya pande zote mbili za watu wa Marekani na Tanzania.
Katika siku hii ya miaka 61 ya Muungano, tunaupongeza uongozi wa Tanzania katika Afrika Mashariki na kuthibitisha dhamira yetu ya kujenga dunia yenye amani na ustawi zaidi.
Kwa niaba ya Marekani, namtakia kila la heri Rais Samia Suluhu Hassan na Watanzania katika kuadhimisha miaka 61 ya kuundwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Marekani inathamini sana ushirikiano wetu wa kudumu na Tanzania, ambao unatokana na tamaa yetu ya pamoja ya ustawi na usalama. Katika mwaka ujao, tunatarajia kuimarisha ushirikiano wetu kwenye biashara na uwekezaji kwa manufaa ya pande zote mbili za watu wa Marekani na Tanzania.
Katika siku hii ya miaka 61 ya Muungano, tunaupongeza uongozi wa Tanzania katika Afrika Mashariki na kuthibitisha dhamira yetu ya kujenga dunia yenye amani na ustawi zaidi," Marco Rubio, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani.