Maguge Tv

Maguge Tv This page is describe product from Maguge Media and defferent product found on maguge media Maguge Media

"Nimezoea hamasa zake, hakuna anayemfikia,, Kwenye tasnia ya ushabiki wa soka itapoa sana""Mpira bila kelele za Manara h...
25/07/2022

"Nimezoea hamasa zake, hakuna anayemfikia,, Kwenye tasnia ya ushabiki wa soka itapoa sana"

"Mpira bila kelele za Manara haunogi, wengi tumeanza kuufatilia mpira sababu ya Manara,, Namshauri akate rufaa japo siingilii maamuzi" Diva Theebawse, Mtangazaji wa Wasafi FM.

Toa maoni yako

"Chanzo cha Yanga SC kucheza bila mashabiki dhidi ya Rivers Utd, ni (TFF)."Mchezo wetu na Rivers United (TFF) chini ya k...
25/07/2022

"Chanzo cha Yanga SC kucheza bila mashabiki dhidi ya Rivers Utd, ni (TFF).

"Mchezo wetu na Rivers United (TFF) chini ya katibu mkuu kidao na Rais wa (TFF) Wallace Karia, hawakuomba kwa maandishi (CAF) k**a sisi tulivyowaomba (TFF) tupate idhini ya kuingiza mashabiki kwenye mechi dhidi ya Rivers 🇳🇬, wakaandika barua nje ya muda"

"Kipindi hicho Karia kwa siku anapiga simu tatu, Kidao simu nne ili nipoze hilo jambo (Nisiseme) na nilifanikiwa"

"Hatukucheza tukiwa na mashabiki uwanjani dhidi ya Rivers kwa sababu ya (TFF)" - Haji Manara, Msemaji wa klabu ya Yanga SC.

Mbele ya Waandishi wa Habari Haji Manara toka afungiwe kujihusisha na soka kwa miaka miwili na kupigwa faini ya milioni ...
25/07/2022

Mbele ya Waandishi wa Habari Haji Manara toka afungiwe kujihusisha na soka kwa miaka miwili na kupigwa faini ya milioni 20 amefunguka baadhi ni haya yafuatayo👇

“Tulitangulia kufungwa na nilikuwa nimekaa eneo la Wageni Half Time mara nyingi mechi siangalii dakika tisini tena zile ambazo tumetangulia kufungwa ndio kabisa presha inakuwa juu"

"Half Time nikashuka jukwaani RC wa Arusha Mongella akaniita Haji njoo, hatujamaliza hata dakika moja ghafla bila kutarajia wala sikujua imetokea wapi mbele ya Viongozi, Rais wa TFF kwa ukali kabisa na kwa makelele mengi akawa ananifuata 'Wewe toka hapo, ondoka hapo wewe'”

“Nilikua naondoka na RC wa Arusha, wakati ananinyooshea kidole na kunipigia kelele huku anawaangalia Viongozi wa Coastal Union wamuangalie anachonifanyia, nikamwambia nimefanya nini? baadaye akasema hujui hapa kafa Mtu"

“kwa hiyo basi, Kutokana na ukiukwaji wa haki bila ya kanuni kusajiliwa na BMT tumepeleka malalamiko yetu, lakini tumeomba mara tatu nakala ya hukumu lakini hawataki kutupa nakala za hukumu wanaogopa ili sisi tusikate rufaa na mimi sijapewa namimi nitaendelea kuwa msemaji wa Yanga mpaka nipate nakala ya hukumu” Msemaji wa Yanga - Haji Manara

  ‘Barbershop,’ ambazo mbali na kuwanyoa nywele kichwani wateja, pia huwasinga sehemu mbalimbali za mwili (massage).Mwan...
25/07/2022

‘Barbershop,’ ambazo mbali na kuwanyoa nywele kichwani wateja, pia huwasinga sehemu mbalimbali za mwili (massage).

Mwandishi wa habari hii amefuatatilia huduma hiyo kwa siku kadhaa katika maeneo tofauti jijini Dar es Salaam.

Awali, akizungumza na mwandishi kuhusu yanayotendeka ndani ya saluni za kisasa, Israel Joachim anasema, “niliwahi kwenda saluni, lengo halikuwa kunyoa nywele, bali nifanyiwe ‘massage,’ kweli nilifanyiwa tena na msichana, haikuwa rahisi kuvumilia, kuna maeneo hatarishi nilikuwa nashikwa na huyo dada akaniambia k**a hali ni mbaya nijiongeze.”

Anasema baada ya kuingia kwenye saluni hizo kupata huduma, alichokutana nacho, hakimtoki kichwani kwa kuwa mbali na kulainisha misuli na kupunguza uchovu, vyumba vilivyomo saluni vina ushetani mwingi.

“Nilijiuliza nijiongeze na nini, kumbe alitaka (mtoa huduma mwanamke) nimpatie Sh30,000 anisaidie kuondoa hali niliyokuwa nayo, sikuwa na ujanja, nilitekeleza takwa lake sababu sikuwa na la kufanya kutokana na hali yangu,” anasema Joachim.

Hata hivyo, Mwandishi alibaini baadhi ya vyumba hivyo ni kichaka kipya cha biashara ya ngono na inaelezwa asilimia 80 hadi 90 ya wanaume wanaokwenda huko hufuata huduma hiyo ya ngono, ingawa huzuga kwa kuanza kwanza na huduma ya ‘massage.

“Wanaanza na huduma ya kwanza kwa sababu ile ya pili hawana uhakika k**a inatolewa pale, kwa baadhi ya watu niliowauliza kwa nini wanakwenda kule wanasema wale wanawake wanaotoa huduma hizo wana uwezo mkubwa wa kuwaandaa wanaume kushiriki ngono,” alisema Ramadhani Masenga, mtaalamu wa saikolojia kutoka Mental Health Hygiene Institute ya Dar es Salaam.

John Heche✍✍
24/07/2022

John Heche✍✍

"Hebu twambieni ukweli Manyonyo, Jana mmecheza na Team Gani? Al Hodood au Abuu Hamadi? Mbona mnatuchangaya kwa uongo wen...
24/07/2022

"Hebu twambieni ukweli Manyonyo, Jana mmecheza na Team Gani? Al Hodood au Abuu Hamadi? Mbona mnatuchangaya kwa uongo wenu?

Semaji la TADEA ahh tholi la CUF linasema mmecheza na Abuu Hamadi, Club inasema mmecheza na Al Hadood, mnaongopa Kwa faida ipi?

Mimi nafahamu Abuu Hamadi ni Jumuiya ya Wakata Kachumbari kwenye Sherehe nchini Misri, Wao kazi yao kukiwa na harusi na kuna Pilau huitwa Kwa ajili ya kukata Kachumbari.

Kundi hili maarufu hukodiwa hadi Morocco na nchi nyingine za kiarabu, Sasa sijui lini wameanza kucheza Mpira?

Nyieeee, Yaan waache Mikachumbari wahangaike na Soka?

Sasa twambieni ukweli Makolo, Mmecheza na Al Hodood au Abuu Hamadi ( Wakata Kachumbari) ?

Mkinuna natuma Bweni la Shule mliyofikia Ismailia.

Nb::Tumeomba Mechi na Manyonyo Siku ya Mwananchi tarehe 6/8/2022, Wakikubali Niiteni Nyau 🤪🤪

Byuti Byuti 🤪🤪🤪 "--Haji Manara✍

Taarifa Ya Serikali Kwa Wafanyakazi.
24/07/2022

Taarifa Ya Serikali Kwa Wafanyakazi.

Katika mahojiano na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema amegusia suala la “Tumbili” lilil...
23/07/2022

Katika mahojiano na aliyekuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Jaji Frederick Werema amegusia suala la “Tumbili” lililozua mvutano kati ya Jaji Warema na aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila Juni 2014.

Jaji Warema amesema kuwa alitumia msemo huo wa Kiganda kueleza kuwa ukiwa jikoni ndivyo unavyoweza kubaini mambo,

"Tumbili haamui mambo ya msituni" mimi ndio nilikuwa jikoni najua kilichokuwa kinaendelea, kwa hiyo kutumia neno tumbili ni Msemo ila watu walitafsili vibaya tu sikuwa na maana ya kumtukana binadam mwenzangu aliyeumbwa na Mungu.

✍️“Kuna vitu havipo sawa kwenye mpira kisa Usimba na Uyanga, kuna muda tunataka kubadili nyeupe kuwa nyeusi kisa Usimba ...
23/07/2022

✍️“Kuna vitu havipo sawa kwenye mpira kisa Usimba na Uyanga, kuna muda tunataka kubadili nyeupe kuwa nyeusi kisa Usimba na Uyanga, this is not fair.

“Nalitazama sakata la Haji Manara na hukumu ya miaka miwili namna watu wengi wanavyopinga hukumu na kuipa presha kubwa sana TFF, hiyo haipo sawa.”

“Mlikuwa wapi wakati Mbwana Makata anapigwa miaka mitano, Lwitiko wa Mbeya anachukua miaka 10, kuna yule Kiongozi wa Biashara United kafungiwa maisha na hata Mimi nimepigwa miaka mitano.”

“Haji sio exceptional ni Mwanafamilia ya mpira k**a ilivyo kwa wengine, anapopewa hukumu kwa mujibu wa kanuni haipaswi kuonekana ameonewa, kumbuka hata Mimi nilifungiwa kisa tu MAKALA tena ya mtandaoni, why not Haji dhidi ya Rais wa TFF?”

“Tunaupa taswira gani mpira wetu? Tunamaanisha kosa likifanywa na vigogo wa Kariakoo it means linapaswa kufumbiwa macho? Jibu ni HAPANA, binafsi ni muumini wa utawala wa sheria.”

“Kila kitu kipo wazi sana, k**a Haji hajaridhishwa na hukumu anapaswa kukata rufaa, ni haki yake! Sioni mantiki ya press na kusigana bila sababu, ni kuonesha mnataka kuwa juu ya mfumo.”

“Sioni sababu ya mvutano, Haji na Yanga wana vitu viwili tu vya kufanya kwasasa, kukata rufaa k**a hawajaridhika au kukaa kimya ili Haji atumikie adhabu yake, nje na hapo ni kuunajisi mpira wa miguu na kupoteza sifa nzuri tunayoanza kuijenga.”

“Nawaelewa nyote kuwa mnaamini kwenye haki na sheria, lakini kuna utaratibu wake, napenda sana kumuona Ndugu yangu Haji kwenye mpira ila kuna utaratibu wake nae anafahamu, basi muufuate”

“Tunapocodify na kuweka mifumo ituongoze ni kwakuwa tunafahamu sie ni Binadamu na huwa tunakosea, hatuwezi kwenda bila mfumo na sio kwa ubaya, inapokuja sheria haipaswi kuwa Simba wala Yanga bali SHERIA” Amesema Shaffih Dauda.

 : Maafisa watatu wa Jeshi la Magereza wakiongozwa na Mkuu wa Gereza la Liwale mkoani Lindi, SP Gilbert Sindani mapema h...
20/07/2022

: Maafisa watatu wa Jeshi la Magereza wakiongozwa na Mkuu wa Gereza la Liwale mkoani Lindi, SP Gilbert Sindani mapema hii leo majira ya saa 8:50 asubuhi wamefikishwa katika Mahak**a ya Makimu Mkazi Lindi kwa mara ya tatu kufuatia tuhuma zinazowakabili za mauwaji ya mfungwa kwenye Gereza la Liwale.

Taarifa za awali zinaeleza kwamba mfungwa alieuwawa ni Ally Abdallah.

Huko nchini Uingereza😲 Mapya yaibuka! Mwanadada kwa jina la Charlotte(23) amelazimika kununua mdoli wa mapenzi unaofanan...
20/07/2022

Huko nchini Uingereza😲 Mapya yaibuka! Mwanadada kwa jina la Charlotte(23) amelazimika kununua mdoli wa mapenzi unaofanana nae ili uweze kumsaidia katika mahusiano yake kwani bwana'ke huyo kwa jina la Callum(28) kiwango chake cha kufanya mapenzi kipo juu tofauti na yeye hapendi sana hivyo kushindwa kuhimili mechi za kibabe toka kwa bwana'ke huyo.

Charlotte amesema awali hakuafiki suala la kuruhusu mdada mwingine aingie katika mahusiano yao wawe katika mahusiano ya utatu sababu yeye angesikia wivu k**a ilivyo kwa watu wengi.

Hivyo, ilibidi aongee na bwana'ke huyo wanunue mdoli anayefanana nae awe anamsaidia 'kazi' pale anapokuwa hajisikii huku bwana'ke anataka. Ameongeza kwamba sababu ni mdoli wa plastiki hatosikia wivu tofauti ingekuwa ni mdada mwenzie kikwelikweli angejisikia wivu na kuleteana gubu.

Na ndio wakanunua hilo doli mwezi June mwaka huu kwa pesa ndefu, wanalivalisha nguo za kuvutia, pia wanalitoa out kwa gari doli hilo kwenda kutembea huku na huko ili lisijihisi upweke au kutengwa ndani na nje ya nyumba.

Charlotte anadai tangu hapo anahisi mahusiano yao yapo salama na yamenogeshwa na doli hilo.

Aliyewai kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii kwenye Serikali ya awamu ya tano, ambaye kwa sasa ni Mbunge, Dkt. Hamisi Kig...
19/07/2022

Aliyewai kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii kwenye Serikali ya awamu ya tano, ambaye kwa sasa ni Mbunge, Dkt. Hamisi Kigwangalla ameeleza msimamo wake kuhusu sakata la Loliondo na Ngorongoro.

‘’Msimamo wangu huko palepale kwamba pale kunatakiwa kuwepo chombo ambacho kitakuwa managed kwa pande zote wakiwemo watalii wakiwemo wanaoendesha shughuli za utalii, wanaondesha shughuli za uwindaji, Halmashauri kwa maana upande mmoja Madiwani na Mkurugenzi harafu Mbunge lakini pia viongozi wa Kimila lakini pia waifadhi, na pengine hicho chombo kinaweza kuwa kinakutana hata mala mbili kwa mwaka kinafanya maamuzi juu ya eneo lile la kilomita 1500.”

‘’Mimi maamuzi yangu sio kugawa kilomita 1500 kuzifanya pori tengefu au kuzifanya pori la akiba mimi hilo silisapoti, na msimamo wangu huko hapo na hupo wazi ‘’

‘’Huwezi kutangaza pori Tangefu kwenye aridhi ya Vijiji Sheria ilikataza mwaka 2009 kwahiyo kufanya hivyo ni kuvunja sheria, sasa Nchi yetu inaongozwa kwa sheria na misingi ya utawala bora na ukiwa kiongozi ni lazima uwe mfano wa kutekeleza sheria vile ambavyo zinataka, huwezi kutumia mabavu kwenye jambo ambalo liko wazi.’’-Mbunge, Dkt Hamisi Kigwangalla

‘’Sheria imeelekeza hivyo k**a ukienda tofauti na hivyo inamaana unavunja sheria na kusababisha migogoro, unataka sasa kufanya wananchi wabishe, wagome, walete vurugu jambo ambalo halitakiwi, kwanini ufanye hivyo solution ambayo ilitakiwa nikwamba wananchi waeleweshwe kwamba hili ni eneo potential.’’ -Mbunge, Dkt Hamisi Kigwangalla .

‘’Tunasema hakuna haja ya kulifungulia jini kwenye chupa k**a limetulia na chupa imetulia pale kwanini wewe ufungue kizibo?, we kiache vilevile waliokifungia mule ndani wanajua kwanini walifugia kile kizibo wakaweka jini mule ndani, kwahiyo wewe usikifungue kiache tu ndio maana hiyo chupa imewekwa pale na umeambiwa usifungue wewe unaenda kufungua ya nini.”-Mbunge, Dkt Hamisi Kigwangalla .

 : Yanga imethibitisha kuachana na wachezaji wake wawili, Chico Ushindi na Yacouba Sogne baada ya makubaliano ya pande z...
19/07/2022

: Yanga imethibitisha kuachana na wachezaji wake wawili, Chico Ushindi na Yacouba Sogne baada ya makubaliano ya pande zote mbili.

Hayo yamezungumzwa hii leo na Haji Manara, msemaji wa mabingwa hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara ametoa taarifa hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari.

Star Wa Muziki Africa SIMBA   Akiwa Kwenye Interview Na DW Africa Huko Ujerumani Amesema Kwamba "Tayari Nimeshanunua Nde...
19/07/2022

Star Wa Muziki Africa SIMBA Akiwa Kwenye Interview Na DW Africa Huko Ujerumani Amesema Kwamba "Tayari Nimeshanunua Ndege yake binafsi"

Alikuwa Akizungumzia Namna Msanii Unatakiwa Kuishi Au Kuwa Ili Kupata Ile Heshima Unayostahili Na Kuingiza Mkwanja Wa Kutosha

"Mfano Kwa Mtu K**a Mimi Ambaye Nimetokea Mtaani, Kwasasa Nanunua Gari La Kifahari Lenye Thamani Hadi TSH.BILIONI 2.3/Kwahiyo Itabidi Ufanye Hivyo Kwani Usipofanya Hivyo Hawatakuona Wewe Ni Wa Thamani (Watakuchukulia Poa)...Na Sasa Tayari Nimeshanunua Ndege Binfasi (Private Jet)" Diamond Platnumz

Hii Hapa List Ya Wasanii Wenye Wafuasi Wengi Zaidi Afrika Kwa Upande Wa Youtube 1.   - 6.84M Subscribers2.   - 3.91M Sub...
19/07/2022

Hii Hapa List Ya Wasanii Wenye Wafuasi Wengi Zaidi Afrika Kwa Upande Wa Youtube

1. - 6.84M Subscribers
2. - 3.91M Subscribers
3. - 3.39M Subscribers
4. - 3.30M Subscribers
5. - 3.07M Subscribers
6. - 2.94M Subscribers
7. - 2.78 Subscribers
8 . - 2.67M Subscribers
9. - 2.47M Subscribers
10. - 2.11 Subscribers

18/07/2022

Wasomi Wakumbushwa😆

 : Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema vipimo vya maabara vimeonesha kuwa ugonjwa ulioibuka mkoani Lindi ni Homa ya Mgu...
18/07/2022

: Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema vipimo vya maabara vimeonesha kuwa ugonjwa ulioibuka mkoani Lindi ni Homa ya Mgunda Leptospirosis, na kuwaomba wananchi kujihadharan na ugonjwa huo mpya.

Kufuatia taarifa za kuibuka kwa ugonjwa huo ulioibua hali ya sintofahamu, Wizara ya Afya kupitia kwa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu imetangaza rasmi kuwa ni mlipuko mpya wa ugonjwa wa Homa ya mgunnda unaosababisha wananchi kutoka damu puani na kuishiwa nguvu na hata kufariki.

Katika taarifa hiyo Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa ugonjwa huo wa Homa ya mgunnda unasababishwa na wanyama k**a vile panya, bweha na swala.

Ameeleza kuwa ugonjwa huu huambukizwa hupitia mkojo wa wanyama kwenye vyanzo vya maji ambapo tayari dawa imepatikana sanjari na namna ya kujikinga.

Hadi sasa wananchi 20 wameugua ugonjwa huo wilayani Ruangwa mkoani Lindi na wengine watatu kufariki, huku wawili wakiwa kwenye uangalizi maalumu.

Itakumbukwa Rais Samia Suluhu Hassan hivi karibuni alitoa taarifa ya uwepo wa ugonjwa huo ambao ulikuwa haujafamika jina, ambapo akieleza kuwa Serikali imepeleka wataalamu kwa ajili ya kufanya uchunguzi juu ya ugonjwa huo.

Soma ucheke🤣🤣👇🤦🙆Mwanamke wangu Alinipigia simu! Hello baby, nina njaa sana muda huu😭😭👉 samahani unaeza kuja kwangu muda ...
15/07/2022

Soma ucheke🤣🤣👇

🤦🙆Mwanamke wangu Alinipigia simu! Hello baby, nina njaa sana muda huu😭😭
👉 samahani unaeza kuja kwangu muda huu 🏠, na wakati unakuja naomba unijie na kuku🐓

👉Bila kupoteza muda 🤷 Nilianza kutafuta pahala wanauza kuku🐓 & Nilinunua mkubwa kabisa🐓 nikaenda nikenda kwa mpenzi wangu 🏠

👉 Alianza kumgawanyisha vipande, akatoa vipande viwili akawa anavichemsha na vingine akaviweka kwenye friji😲🙄🙆

👉 Wakati tumekaa zetu kuku anaendelea kuiva😁🙆.....

👉Ndani ya dk 10 wakati kuku anachemka jikoni, simu yake ikaita🥴🙄 akaingia chumbani kwenda kuongea na simu😲🥴🙆

👉 Baada ya kupokea simu, aliniambia kaka yake anakuja na hatofurahi akinikuta pale so nimpishe kidogo😲🤦🙆

👉Akanisisitiza niondoke haraka🚶🚶 atanipigia simu kaka yake akiondoka 😲🙆🤦😲😲
👉 Kwa amani kabisa nilielekea jikoni nikashusha sufuria chini nikatoa vile vipande viwili nikaacha mchuzi mtupu,😠, nikafungua friji nikachukua vipande vyote alivyokuwa ameviifadhi🙄, nikaanza safari ya kwenda kwangu🚶🚶🚶🚶
👉....Kuanzia jana nampigia simu kujua k**a kaka yake ameondoka ama laa wala hapokei simu zangu cha ajabu ananikatia kabisa😭😭😭.

👉 Watu wangu kwani kuna kosa nimefanya????😒😒😩😩

 : Mfanyabiashara mmoja mjini Tabora aliyefahamika kwa jina la Mohammed Mustafa, ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasi...
15/07/2022

: Mfanyabiashara mmoja mjini Tabora aliyefahamika kwa jina la Mohammed Mustafa, ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana ambao walimvizia wakati akitoka nyumbani kwake majira ya saa tatu asubuhi akielekea kwenye shughuli zake za kila siku.

K**anda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Richard Abwao, amsema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wa kina kuhakikisha linawatia nguvuni wahusika wote.

Ikiwa miamba wa soka nchini tanzania wakiendelea kuvunja bank na kufanya usajili, Mabingwa ya Tanzania wamefanya Uhamish...
15/07/2022

Ikiwa miamba wa soka nchini tanzania wakiendelea kuvunja bank na kufanya usajili, Mabingwa ya Tanzania wamefanya Uhamisho wa Stephanie Aziz Ki kwenda Yanga SC uliogharimu Euro 200,000 (takriban TSH milioni 468) k**a gharama za kusaini ambazo zitaenda kwa mchezaji na wawakilishi wake.

Katika uhamisho huo Ki (26) atalipwa mshahara wa Euro 10,000 (takriban TSH milioni 23) kwa mwezi.

Simba SC imeingia makubaliano ya kibiashara na M.BET Ikiwa imesaini mkataba wa udhamini wa miaka mitano na Kampuni hiyo ...
14/07/2022

Simba SC imeingia makubaliano ya kibiashara na M.BET Ikiwa imesaini mkataba wa udhamini wa miaka mitano na Kampuni hiyo ya michezo ya kubashiri ambayo sasa ni Mdhamini Mkuu wa Club hiyo kuanzia July 1 2022.

Taarifa ya Simba SC. imesema taarifa kamili juu ya udhamini huu zitatolewa na pande zote mbili siku ya Jumatatu August 1 2022.

 : "Ni miaka 6 sasa tangu tumeanza kufanya kazi pamoja my team my family WCB Wasafi. Upendo, umoja imekua nguzo kubwa sa...
12/07/2022

: "Ni miaka 6 sasa tangu tumeanza kufanya kazi pamoja my team my family WCB Wasafi. Upendo, umoja imekua nguzo kubwa sana kujifunza na tumefanikisha tukiwa pamoja k**a team.

"Shukrani za dhati kwa my family Wasafi, my Brother Diamond kwa kunipa nafasi dunia ione kipaji changu nilichobarikiwa na Mungu na kuweza kufika hapa nilipofika, nathamini sana mchango wako Mungu akusaidie.

"Mtoto anayekua ni yule anayetoka nyumbani kwenda kuanza maisha na kuipa heshima familia yake, Mmeniliea, mmenikuza sasa ni muda wangu kuondoka nyumbani na kuanza maisha mengine"--Rayvanny ukiongea alipokuwa akiaga WCB.

 : Shirikisho la Soka Duniani FIFA limeiagiza klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco kumlipa mchezaji Simon Msuva dola za ...
11/07/2022

: Shirikisho la Soka Duniani FIFA limeiagiza klabu ya Wydad Casablanca ya Morocco kumlipa mchezaji Simon Msuva dola za kimarekani 700,000 (zaidi ya bilioni 1.6 za kitanzania) baada ya mchezaji huyo kushinda kesi ya madai aliyoifungua dhidi ya Wydad.

-Msuva ambaye alikua amesaini mkataba wa miaka minne alilazimika kuusitisha mkataba wake Disemba mwaka 2021 kutokana na kuidai klabu hiyo malimbikizo ya mishahara pamoja na pesa za usajili (signing fee).

 : Msanii wa filamu mkongwe na mtangazaji, Chuma Suleiman almaarufu Bi Hindu, amefariki dunia asubuhi hii, nyumbani kwak...
09/07/2022

: Msanii wa filamu mkongwe na mtangazaji, Chuma Suleiman almaarufu Bi Hindu, amefariki dunia asubuhi hii, nyumbani kwake, Magomeni jijini Dar es Salaam.

Taarifa za kifo chake zimethibitishwa na ndugu wa karibu wa mkongwe huo huku sababu ya kifo chake ikitajwa kuwa ni maradhi ya muda mrefu.

 : Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amejiuzulu wadhifa wake. Akitoa hotuba yake:Johnson: Nina huzuni kuacha kazi b...
07/07/2022

: Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amejiuzulu wadhifa wake. Akitoa hotuba yake:

Johnson: Nina huzuni kuacha kazi bora zaidi duniani,

‘’Ninataka ujue jinsi ninavyohuzunishwa na kuacha kazi bora zaidi duniani,’’ waziri mkuu anasema.

"Nimekubaliana na Sir Graham Brady, mwenyekiti wa wabunge wetu wa viti maalum, kwamba mchakato wa kumchagua kiongozi mpya uanze sasa na ratiba itatangazwa wiki ijayo. Na leo nimeteua Baraza la Mawaziri kuhudumu, pia nitaendelea kuongoza hadi kiongozi mpya atakapochaguliwa.’’

''Inatia uchungu kutoona miradi yangu ikikamilika''

Johnson anasema ni upuuzi kubadilisha serikali – na kukataa wazo la uchaguzi mkuu - wakati ‘’tunatimiza majukumu mengi na makubwa hali ya kiuchumi ikiwa ngumu sana ndani na kimataifa’’.

‘’Najuta kutofanikiwa katika majadiliano na inatia uchungu kutoona mawazo na miradi mingi ikitimia.’’Amesema Boris

 : Katibu Mwenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka, amesema CCM haijawahi kuhofia kuondoka madarakani kwa sababu ya marekebisho...
05/07/2022

: Katibu Mwenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka, amesema CCM haijawahi kuhofia kuondoka madarakani kwa sababu ya marekebisho ya katiba na kusisitiza CCM itaendelea kushinda na kuongoza nchi.

“tunaamini jambo hilo haliwezi kutokea, sababu kazi tunayoifanya ni nzuri kwa wananchi na imani ya Watanzania kwa CCM ni kubwa sana”

 : Dooren Augustino Mrema ambaye ni mke wa mwanasiasa maarufu hapa nchini Agustino Mrema ameelezea kufurahia maisha ya n...
05/07/2022

: Dooren Augustino Mrema ambaye ni mke wa mwanasiasa maarufu hapa nchini Agustino Mrema ameelezea kufurahia maisha ya ndoa.

Akizungumza na vyombo vya habari, Doreen amesema anafurahia ndoa yake aliyofunga na Mzee Mrema kwa kuwa mzee huyo anamtimizia majukumu yote anayotakiwa na kumtosheleza ikiwemo tendo la ndoa tofauti na watu wanavyofikiria kwamba mumewe huyo hawezi kumtosheleza kinyumba

"Mimi sijadai talaka k**a habari za kwenye mitandao ya kijamii zinavyosema, mimi nipo kwenye ndoa na-enjoy sana penzi la mume wangu Mzee Mrema kwani anayejua utamu wa ndoa ni mimi niliyeko kwenye ndoa, sikiliza Mzee anaijua shughuli mpaka mimi nasema ni yeye au maana ananitosheleza vya kutosha, siwezi kumuacha Mrema yaani na-enjoy kupitiliza, amekuwa kijana na anafanya mazoezi ya kujiweka vizuri kiafya" amesema Doreen.

 : Sekretarieti ya TFF imefungua shauri mbele ya K**ati ya Maadili dhidi ya Haji Manara kutokana ukiukwaji wa maadiliMan...
03/07/2022

: Sekretarieti ya TFF imefungua shauri mbele ya K**ati ya Maadili dhidi ya Haji Manara kutokana ukiukwaji wa maadili

Manara alionekana akizozana na Rais wa TFF, Wallace Karia Julai 2, 2022

 : Tanzania na Ufaransa zimetia saini hati ya makubaliano ya usafiri wa anga ambapo ndege za Kampuni ya Ndege Tanzania (...
01/07/2022

: Tanzania na Ufaransa zimetia saini hati ya makubaliano ya usafiri wa anga ambapo ndege za Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) na Precision Air zitafanya safari za moja kwa moja kati ya Tanzania na Ufaransa. Safari hizo zinatarajiwa kuanza ndani ya kipindi cha miezi sita ijayo.

Address

Bugarika Pamba Nyamagana Mwanza
Mwanza
BUGARIKA,33214

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Maguge Tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Maguge Tv:

Videos

Share


Other Broadcasting & media production in Mwanza

Show All