MUST FM Radio - Mbeya

MUST FM Radio - Mbeya Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from MUST FM Radio - Mbeya, Media/News Company, Box 131, Mbeya.
(4)

Unadhani ni lazima mtoto kuwasaidia wazazi wake kila kitu mara baada ya kusomesha?Live kupitia Live Ladha ya leo ya 104....
21/02/2024

Unadhani ni lazima mtoto kuwasaidia wazazi wake kila kitu mara baada ya kusomesha?

Live kupitia Live Ladha ya leo ya 104.5 Must Fm.

01/06/2023

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amewataka Wakuu wa Shule pamoja na Wakurugenzi kuzingatia utaratibu uliotolewa na Kamishna wa Elimu kuhusu muongozo wa kufunga na kufungua shule ili kuwapatia nafasi wanafunzi kupumzika katika kipindi cha likizo.

"na mbaya zaidi kuna baadhi ya malalamiko tumeanza kupokea kwamba kuna shule zinazuia wanafunzi kwenda likizo bila hata kushauriana na wazazi na wengine wazazi wanatakiwa walipe kuwaweka wanafunzi mashuleni" alisema Prof. Mkenda.

Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kinapenda kukukumbusha uwepo wa Dawati la Malalamiko linalolenga kubor...
23/03/2023

Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kinapenda kukukumbusha uwepo wa Dawati la Malalamiko linalolenga kuboresha ubora wa huduma zake kwa kamili.
Hivyo katika kuhakikisha inafikia malengo ya kushughulikia malalamiko Afisa anayehusika na Dawati hili pia anakualika kufika ofisi nambari 18 Administrative Basement ili kutoa maoni yako.
"Kwa pamoja tunaweza kuimairisha ubora wa huduma zinazotolewa na Taasisi yetu"
104.5 MUST FM

08/03/2023

"Wanawake ni CHACHU ya mabadiliko"
Ujumbe kutoka kwa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), Utawala, Fedha na Mipango Dr. John P. John katika Kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani Mwaka 2023.

Dr. John pamoja na kuwapongeza Wafanyakazi Wanawake wa MUST, amewahimiza kuendelea kufanya kazi kwa juhudi na maarifa katika kulitumikia TAIFA lao.

01/08/2022

Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Dkt. Rashid Chuachua amesema msimu wa mavuno wa mwaka 2021 Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ilizalisha jumla ya tani takribani milioni 10 za mazao ya chakula na tani 636,000 ya mazao ya biashara.

Dkt. Chuachua ametoa kauli hiyo leo wakati akitoa salamu akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera kwenye ufunguzi wa Maonyesho ya Wakulima (Nanenane) Kitaifa, ambapo pia ameeleza kuwa katika kuhakikisha kuna usalama wa chakula, mikoa hiyo mwaka 2022, inatarajia kuzalisha mazao ya chakula kwa ziada ya tani 5,900,000.

01/08/2022

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Phillip Mpango amevitaka Vyombo vya Habari kuelimisha na kuhamasisha jamii masuala yanayohusu kilimo na ufugaji kwa ajili ya kuchochea maendeleo na uchumi nchini.

Dkt. Mpango ametoa wito huo leo wakati akitembelea mabanda katika ufunguzi wa Maonyesho ya Wakulima (Nanenane) Kitaifa Kanda ya Nyanda za Juu Kusini viwanja vya John Mwakangale, ambapo amesema lazima kuwepo na vipindi vya elimu kwa ajili ya wakulima pamoja na ufugaji wa aina zote ili kuwawezesha wananchi kufahamu kuhusu faida za sekta hizo.

28/05/2022

Leo ni Siku ya Hedhi Salama Duniani.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya Prof. Abel Makubi amesema ‘’hedhi salama ni afya na ni baraka za uumbaji wa Mwenyezi Mungu’’ hivyo ameitaka jamii kuachana na mila na desturi potofu kuhusu hedhi.

Unashiriki vipi kuhakikisha jamii yako inakuwa na mazingira ya Hedhi Salama? Pia unaweza kutuandikia maswali yako kuhusu mada hii, ndani ya kipindi chetu AFYA NA MAZINGIRA kuanzia saa 5 asubuhi mpaka saa 6 Adhuhuri hapa 104.5 MUST FM Dira ya Sayansi na Teknolojia.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania Mh. Kassim Majaliwa amewataka Viongozi na Watendaji wa mamlaka husika ku...
05/04/2022

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa amewataka Viongozi na Watendaji wa mamlaka husika kuwawezesha Maafisa Utamaduni na Michezo kushiriki katika vikao kazi vitakavyowawezesha kubadilishana uzoefu na kuimarisha stadi mbalimbali za kutekeleza majukumu yao.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo jijini Dodoma akiwa Mgeni Rasmi katika kikao kazi Cha Maafisa Utamaduni na Michezo Tanzania Bara.

Amesema sifa ya nchi yetu imetokana na umoja, utulivu na amani tuliyonayo hivyo ni vema kuulinda Utamaduni, Sanaa na Michezo.

28/03/2022
Wananchi wa Kata ya Iyela leo kwenye Uzinduzi wa Ulaji wa Vyakula mchanganyiko uliozinduliwa na Mstahiki Meya Dour Moham...
30/12/2021

Wananchi wa Kata ya Iyela leo kwenye Uzinduzi wa Ulaji wa Vyakula mchanganyiko uliozinduliwa na Mstahiki Meya Dour Mohamed Issa kwenye viwanja vya soko la Mwangonela Mtaa wa Ilembo.

30/12/2021

Afisa Lishe kutoka Halmashauri ya Jiji la Mbeya Bi. Fatuma Juma akitoa maelekezo kuhusu makundi ya chakula yanayokamilisha mlo kamili kwenye Uzinduzi wa Ulaji wa Vyakula mchanganyiko vinavyopatikana Mkoa wa Mbeya

Uzinduzi huo umefanyika viwanja vya soko la Mwangonela lililopo Mtaa wa Ilembo Kata ya Iyela.

02/12/2021

Jeshi la polisi mkoani Geita linamshikilia Veronica Gabriel (30) mkazi wa kijiji cha Mwabagaru, kata ya Buseresere, wilaya ya Chato kwa tuhuma za kusababisha vifo vya Watoto wake wawili, baada ya kuwanywesha sumu kisha na yeye kunywa kwa madai ya ugumu wa maisha.
K**anda wa Polisi wa mkoa huo Henry Mwaibambe amesema watoto wengine watatu wamelazwa katika kituo cha afya.
Una maoni yapi kutokana na kisa hiki, ungana nasi katika kipindi cha Rush Hour hapa 104.5 MUST FM ‘’Dira ya Sayansi na Teknolojia’’ kuanzia saa kumi kamili mpaka kumi na mbili kamili jioni.

24/11/2021

Mbunge wa Mbeya Vijijini Mh. Oran Njeza amesema atatoa msukumo kuhakikisha wabunifu wanapata nafasi ya kuziendeleza na kutangaza bunifu zao na pia kupata nafasi ya kushindana kimataifa.

Mh. Njeza ametoa kauli hiyo leo baada ya kutembelea maonesho ya bunifu katika Kongamano la Miaka 60 ya Uhuru katika Chuo Kikuu Cha Sayansi na Teknolojia likiongozwa na kauli mbiu "Miaka 60 ya Uhuru Mchango wa Sayansi na Teknolojia kwa Maendeleo Endelevu"

24/11/2021

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) Prof. Aloys Mvuma akizungumzia nafasi ya bunifu katika maendeleo, kufuatia uzinduzi wa Kongamano la Miaka 60 ya Uhuru likiongozwa na kauli mbiu "Miaka 60 ya Uhuru Mchango wa Sayansi na Teknolojia katika Maendeleo Endelevu"

Neema Kibonde kutoka Chuo Kikuu Cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST)  tunakupongeza kuendelea kuuwakilisha vizuri mkoa...
11/11/2021

Neema Kibonde kutoka Chuo Kikuu Cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) tunakupongeza kuendelea kuuwakilisha vizuri mkoa wetu wa Mbeya katika
Mashindano ya CRDB Taifa Cup, yanayoshirikisha mikoa yote Tanzania bara na Zanzibar.

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) Prof. Aloys Mvuma (kulia) leo amepokea vifaa vya kujiki...
02/08/2021

Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) Prof. Aloys Mvuma (kulia) leo amepokea vifaa vya kujikinga kwa ajili ya vijana wanapata Mafunzo ya Uanagenzi kutoka kwa Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Mbeya Bw. Cornelius Msigwa.

Benki ya CRDB tawi la Mbeya imetoa kofia ngumu 100 na gloves 100 ili kuwasaidia vijana katika kutekeleza majukumu yao.

Kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na MazingiraBado Siku 22"Ewe Mwananchi Ni Makosa kutumia Vifungashio vya Plastik...
17/03/2021

Kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira

Bado Siku 22

"Ewe Mwananchi Ni Makosa kutumia Vifungashio vya Plastiki visivyo na viwango vya ubora k**a Vibebeo
Mifuko ya Plastiki ilipigwa Marufuku tangu tarehe 1 Juni 2019.
USISUBIRI KUCHUKULIWA HATUA

Hongera sana Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Chuo Kikuu Cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) Bi. Devotha Sang...
09/03/2021

Hongera sana Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu Chuo Kikuu Cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) Bi. Devotha Sanga.

Siku ya Wanawake Duniani 2021

Kauli mbiu Siku ya Wanawake Duniani 2021 "Wanawake katika uongozi, Chachu katika kufikia Dunia yenye Usawa"Naomba tumpig...
05/03/2021

Kauli mbiu Siku ya Wanawake Duniani 2021

"Wanawake katika uongozi, Chachu katika kufikia Dunia yenye Usawa"

Naomba tumpigie kura Kiongozi huyu mahiri na mdau wa maendeleo ya Wanawake na Jamii kwa ujumla.

Naomba uifuate link hii inakuwezesha moja kwa moja katika kufanikisha kura yako.

https://www.instagram.com/p/CL4v4XRn_mO/?igshid=bym5vnmobr57

Leo ni siku ya kimataifa ya kupambana na matumizi na biashara ya Dawa za kulevya.Tumezungmza na Terry Fanani muhanga wa ...
26/06/2020

Leo ni siku ya kimataifa ya kupambana na matumizi na biashara ya Dawa za kulevya.

Tumezungmza na Terry Fanani muhanga wa matumizi ya Dawa za kulevya ambaye amefanikiwa kutoka kwenye matumizi hayo..Lakini pia Ni msanii mkongwe wa kundi la HARD BLASTERS kundi ambalo linajumuisha wasanii K**a Professor Jay na William shundi( Crazy one)

Fanani atazungumzia Zaid visababishi vinavyochangia watu kuingia kwenye matumizi ya Dawa za kulevya n.k

Tuandikie maoni yako upate kushirikiana nasi katika kipindi cha Hello Africa hapa 104.5 JUST FM "Dira ya Sayansi na Tekn...
21/06/2020

Tuandikie maoni yako upate kushirikiana nasi katika kipindi cha Hello Africa hapa 104.5 JUST FM "Dira ya Sayansi na Teknolojia" kuanzia saa 12 mpaka saa 4 kamili asubuhi.

Address

Box 131
Mbeya

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when MUST FM Radio - Mbeya posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to MUST FM Radio - Mbeya:

Videos

Share