TBConline

TBConline Ukurasa rasmi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC). Verified

FT' |  Taifa Stars wanamaliza mchezo kwa sare ya bila kufunganaTanzania 0-0 Ethiopia
04/09/2024

FT' |

Taifa Stars wanamaliza mchezo kwa sare ya bila kufungana

Tanzania 0-0 Ethiopia

76'|   Taifa Stars bado wanatafuta bado Tanzania 0-0 Ethiopia
04/09/2024

76'| Taifa Stars bado wanatafuta bado

Tanzania 0-0 Ethiopia

60’ |   Tanzania 0-0 Ethiopia Live   TBC Taifa na Mitandao ya kwa anwani ya TBConline
04/09/2024

60’ |

Tanzania 0-0 Ethiopia

Live TBC Taifa na Mitandao ya kwa anwani ya TBConline

MAPUMZIKO |  HT: Tanzania 0-0 Ethiopia
04/09/2024

MAPUMZIKO |

HT: Tanzania 0-0 Ethiopia

Matukio ya picha mbalimbali kutokea Uwanja wa Benjamin Mkapa utakakopigwa mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya...
04/09/2024

Matukio ya picha mbalimbali kutokea Uwanja wa Benjamin Mkapa utakakopigwa mchezo wa kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika (AFCON) 2025, Taifa Stars dhidi ya Ethiopia.

Fahamu maisha ya JK akiwa mwanafunzi UDSMSafari yake ya uongozi ilianza kung'aa wakati anasoma katika Chuo Kikuu cha Dar...
04/09/2024

Fahamu maisha ya JK akiwa mwanafunzi UDSM

Safari yake ya uongozi ilianza kung'aa wakati anasoma katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) pale alipochaguliwa kuwa Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa chuo hicho, chini ya umoja wao ambao kwa kipindi hicho uliofahamika k**a DUSO (Dar es Salaam University Student Organization) baadaye DARUSO.

Huyu hapa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete ambaye Jumapili hii ya Septemba 8, 2024, saa 11:00 jioni kupitia mtandao wa YouTube kwa anwani TBC Online kwenye exclusive ya "5 za JK akiwa Mwanafunzi UDSM" ambapo utapata kufahamu mengi kuhusu maisha yake wakati akiwa mwanafunzi wa UDSM.

Bunge limepokea na kukubali taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu uchambuzi wa sheria ndogo zilizo...
04/09/2024

Bunge limepokea na kukubali taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu uchambuzi wa sheria ndogo zilizowasilishwa bungeni kwenye mkutano wa 14 na wa 15 pamoja na taarifa za utekelezaji wa maazimio ya Bunge kuhusu sheria ndogo zilizowasilishwa bungeni kwenye mkutano wa 12 na wa 13.

Akiwasilisha taarifa hiyo bungeni Jijini Dodoma, Mwenyekiti wa k**ati hiyo Dkt. Jasson Rweikiza amesema lengo la uchambuzi wa sheria hizo ni kuhakikisha mamlaka zilizokabidhiwa madaraka ya kuweka sheria ndogo hazizidi mamlaka ya utungaji sheria yaliyotolewa na watu kwa wawakilishi wao, kuhakikisha madaraka ya kuweka sheria ndogo katika mfumo wa sheria za nchi yaliyokasimiwa na Bunge na mamlaka mbalimbali hayavunji haki za watu wala hayavuki mipaka pamoja na kuhakikisha sheria zinazotokana na Bunge zinaakisi maslahi ya umma.

Pia amebainisha dosari zilizojitokeza katika uchambuzi wa sheria hizo ambazo ni pamoja na sheria ndogo mbili kuwa na masharti yanayokinzana na Katiba, Sheria ndogo kumi kuwa na masharti yanayokinzana na Sheria Mama na sheria nyingine za nchi, Sheria ndogo 22 kuwa na masharti yasiyo na uhalisia, Sheria ndogo 13 kuwa na makosa ya kutoendana na misingi ya uandishi na sheria ndogo 13 kuwa na dosari katika Majedwali.

Bunge limeazimia mapendekezo ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo ya kuzielekeza mamlaka zilizotunga sheria ndogo zenye dosari ya kukinzana na uhalisia, masharti ya katiba ya nchi, sheria mama na sheria nyingine za nchi zifanyiwe marekebisho ya dosari hizo.

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Salum Haji Othuman ameishukuru Kamati ya...
04/09/2024

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Luteni Jenerali Salum Haji Othuman ameishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge, Ulinzi na Mambo ya Nje ya Kisiwa cha Ushelisheli kwa kuthamini mchango wa Jeshi hilo katika harakati za ukombozi barani Afrika.

Luteni Jenerali Othuman ameyasema hayo alipotembelewa na k**ati hiyo Makao Makuu ya JWTZ Msalato Jijini Dodoma.

Kwa upande wake
Mwenyekiti wa
Kamati hiyo ya Kudumu ya Bunge, Ulinzi na Mambo ya Nje ya Kisiwa cha Ushelisheli, Francois Adelaide amesema JWTZ imekuwa imekuwa msaada mkubwa kwa nchi nyingi za kusini mwa Afrika.

Amesema nchi yake itaendelea kukuza diplomasia ya ulinzi na Tanzania hasa kwenye mafunzo, mazoezi na kubadilishana ujuzi katika kukabiliana na uhalifu unaovuka mipaka pamoja na kukabiliana na majanga.

Upo mbali na unaisubiri mechi ya Taifa Stars dhidi ya Ethiopia kwa hamu!?Basi usijali… TBC inakujali na kukuletea matang...
04/09/2024

Upo mbali na unaisubiri mechi ya Taifa Stars dhidi ya Ethiopia kwa hamu!?

Basi usijali… TBC inakujali na kukuletea matangazo mbashara kwa redio na Televisheni buuure kabisa kuanzia saa 1:00 usiku!

Una kıla sababu ya kufurahia mbungi hii nyumbani kwako bila bugdha yoyote!

Tuiunge mkono Stars kinyumbanii…!

Kiputeee… Msererekooooo!

Mbungiiii Mwaaa Mwiii🔥🔥🔥

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema katika mwaka wa fedha wa 2024/2025 Serikali imetenga shilingi Bilioni 21...
04/09/2024

Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amesema katika mwaka wa fedha wa 2024/2025 Serikali imetenga shilingi Bilioni 21.1 kwa ajili ya kununua vifaa tiba vitakavyowezesha kuboresha huduma za uzazi kwa akina mama wakiwemo wenye ulemavu.

Amesema hayo bungeni Jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Stella Ikupa aliyeuliza kuhusu hospitali ngapi nchini zimetenga vyumba vya kujifungulia wanawake wenye ulemavu.

Dkt. Mollel amesema hospitali zote za rufaa za mikoa na hospitali za Kanda ambazo ni pamoja na CCBRT za Mtwara na Chato, KCMC, Meta Mbeya na hospitali 184 za halmashauri zina vyumba vya kujifungulia wanawake wakiwemo wenye ulemavu.

Naibu Waziri Mollel amefafanua kuwa Serikali itahakikisha fedha hizo zilizotengwa kwa ajili ya kuboresha huduma za uzazi kwa akina mama zinaboresha miundombinu ikatika vyumba vya kujifungulia ili kukidhi mahitaji ya akima mama wenye ulemavu.

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazima imeanza kupitia upya hali ya uzalishaji...
04/09/2024

Serikali kupitia Wizara ya Kilimo kwa kushirikiana na Ofisi ya Msajili wa Hazima imeanza kupitia upya hali ya uzalishaji wa viwanda vya Korosho vilivyobinafsishwa kikiwemo Kiwanda cha Tunduru kwa lengo la kuhakikisha wawekezaji wa viwanda hivyo wanavifufua.

Kauli hiyo imetolewa bungeni Jijini Dodoma na Waziri wa Kilimo Hussein Bashe wakati akijibu swali la Mbunge wa Tunduru Kaskazini Hassan Kungu aliyeuliza kuhusu sababu za kutofanya kazi kwa kiwanda cha kubangua korosho wilayani Tunduru mkoani Ruvuma kwa miaka saba sasa.

Waziri Bashe ameeleza kuwa kiwanda hicho cha Tunduru chenye uwezo wa kubangua korosho wastani wa tani 3,500 kilijengwa na Serikali mwaka 1981 lakini kutokana na mabadiliko ya kisera Serikali ilikibinafsisha kwa Kampuni ya Korosho African Limited mwaka 2001.

Kiwanda hicho kiliendelea na shuguhili za ubanguaji korosho mpaka mwaka 2019/2020 kilipositisha shughuli zake kutokana na kubangua korosho kwa hasara kinyume na matarajio.

Waziri Bashe amesema tatizo la wawekezaji kuchukua viwanda na kutoviendeleza lipo katika sekta mbalimbali na kwamba Wizara ya Kilimo na Ofisi ya Msajili wa Hazima wameshaanza mazungumzo ili kupitia upya mikataba ya ubinafsishaji kwa lengo la kuangalia masharti yalikuwaje na k**a wawekezaji hao wanakidhi masharti.

Rais Samia Suluhu Hassan ambaye yupo nchini China, akiwa na ujumbe wake amefanya kikao cha pamoja na Rais Xi Jinping wa ...
04/09/2024

Rais Samia Suluhu Hassan ambaye yupo nchini China, akiwa na ujumbe wake amefanya kikao cha pamoja na Rais Xi Jinping wa nchi hiyo na ujumbe wake.

Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa The Great Hall of The People Jijini Beijing leo Septemba 04, 2024.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaendelea na vikao vyake Jijini Dodoma ambapo miongoni mwa shughuli za leo ni...
04/09/2024

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linaendelea na vikao vyake Jijini Dodoma ambapo miongoni mwa shughuli za leo ni kupokea taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu uchambuzi wa sheria ndogo zilizowasilishwa bungeni kwenye mkutano wa 14 na 15.

Pia litapokea taarifa za Utekelezaji wa Maazimio ya Bunge kuhusu Sheria Ndogo zilizowasilishwa bungeni kwenye mkutano wa 12 na 13.

Leo ni kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Paul Alphonce, Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC). Tunamtakia ma...
04/09/2024

Leo ni kumbukizi ya siku ya kuzaliwa ya Paul Alphonce, Mtangazaji wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC).

Tunamtakia maisha marefu.

Unailinda vipi jamii dhidi ya ukatili?Maoni yako yatasomwa katika Kipindi cha Jambo Tanzania
04/09/2024

Unailinda vipi jamii dhidi ya ukatili?

Maoni yako yatasomwa katika Kipindi cha Jambo Tanzania

Unadhibiti vipi matumizi ya simu kwa mtoto?Maoni yako yatasomwa katika kipindi cha Jambo Tanzania
04/09/2024

Unadhibiti vipi matumizi ya simu kwa mtoto?

Maoni yako yatasomwa katika kipindi cha Jambo Tanzania

Unayafahamu majukumu ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa?Maoni yako yatasomwa katika Kipindi cha Jambo Tanzania
04/09/2024

Unayafahamu majukumu ya Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa?

Maoni yako yatasomwa katika Kipindi cha Jambo Tanzania

Yaliyomo katika kurasa za mbele za magazeti leo Septemba 04, 2024
04/09/2024

Yaliyomo katika kurasa za mbele za magazeti leo Septemba 04, 2024

Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 2) wa Mwaka 2024 umepitishwa na Bunge leo Septemba 3, 2024. M...
03/09/2024

Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 2) wa Mwaka 2024 umepitishwa na Bunge leo Septemba 3, 2024.
 
Miongoni mwa marekebisho yaliyopitishwa na Bunge ni pamoja sehemu ya saba ya muswada ambayo inapendekeza marekebisho katika Sheria ya Bohari ya Dawa, Sura ya 70 kifungu cha 16A ili kuondoa masharti ya lazima kwa Bohari ya Dawa (MSD) kuwekeza katika uwekezaji unaoruhusiwa katika Sheria ya Uwekezaji wa Wadhamini, Sura ya 53. Lengo ni kuongeza wigo wa uwekezaji wa MSD na kuiwezesha kujiendesha kibiashara k**a taasisi ya kimkakati kwa kuzingatia maelekezo yatakayokuwa yanatolewa na Msajili wa Hazina na mamlaka nyingine zozote zinazohusika.
 
Aidha kifungu cha 22 cha muswada huo pamoja na sehemu ya sita iliyokuwa ikipendekeza kufanya marekebisho katika Sheria ya Ardhi, Sura ya 113 vimefutwa.

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeridhia na kupitisha muswada wa  Marekebisho ya Sheria ya Ushindani wa Mwaka...
03/09/2024

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeridhia na kupitisha muswada wa  Marekebisho ya Sheria ya Ushindani wa Mwaka 2024 wenye lengo la kutatua changamoto mbalimbali zilizobainika katika utekelezaji wa masharti ya sheria hiyo.
 
Akitoa hoja mbele ya Bunge jijini Dodoma, Waziri wa Viwanda na Biashara, Selemani Jafo amesema kuwa marekebisho ya muswada huo yataleta manufaa makubwa kwa Watanzania na si kuwakandamiza.
 
Aidha, akitolea ufafanuzi kifungu cha 13 kilicholeta mjadala mzito bungeni kutokana na kifungu hicho kufuta kifungu cha 17 cha sheria mama kwa kuweka sharti la wauzaji wa bidhaa au huduma kuonesha bei ya kila bidhaa au huduma, Waziri Jafo amesema kifungu hicho hakitawahusu wafanyabishara wadogo huku akisema  kifungu hicho kitatungiwa kanuni hivi karibu kabla ya kuanza kutekelezwa.
 
Hata hivyo, Bunge liliamua kufuta kifungua hicho cha 13 ili kikafanyiwe marekebisho kutokana na kubainika kuwa na mapungufu ya kushindwa kutoa tafsiri ya “wafanyabishara wadogo” inaowalenga.
 
Aidha Waziri Jafo, amesema kuwa tayari ameielekeza Tume ya Ushindani (FCC) pindi sheria itakapoanza kutumika waanze kutoa elimu kupitia televisheni, mitandao ya kijamii na majukwaa mengine ili kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu utekelezaji wa sheria hiyo, huku akibainisha kuwa kutakuwa na usimamizi mzuri wa utekelezaji wa sheria hii na wala si kwa kutumia mabavu.

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro ameongeza adhabu ya faini aliyolimwa msanii Seif Kisauji maar...
03/09/2024

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro ameongeza adhabu ya faini aliyolimwa msanii Seif Kisauji maarufu Babu wa TikTok kutoka shilingi milioni 3 hadi milioni 5 akimtaka msanii huyo aombe radhi hadharani kutokana na kosa la kurusha mitandaoni maudhui ya sanaa yanayokiuka maadili.

Waziri Ndumbaro ametoa uamuzi huo leo Septemba 3, 2024 Mtumba Jijini Dodoma baada ya kusikiliza rufaa ya msani huyo ya kupinga adhabu aliyopewa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ya kufungiwa kujihusisha na shughuli za sanaa kwa miezi sita pamoja na kulipa faini ya shilingi milioni 3 kutokana na kurusha mtandaoni picha za video zinazokiuka maadili.

Aidha, kufuatia rufaa hiyo, msanii Seif Kisauji amekiri kosa la kusambaza maudhui hayo na kuomba apunguziwe adhabu hatua iliyomfanya Waziri Dkt. Damas Ndumbaro amuondolee adhabu ya kifungo cha cha miezi 6 cha kutojihusisha na shughuli za sanaa lakini akimwongezea kiwango cha faini kutoka milioni 3 hadi 5.

Sheria ya Basata iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019 kifungu cha 15 A inampa mamlaka Waziri mwenye dhamana ya masuala ya sanaa kusikiliza rufani na kutoa maamuzi.

"Kwa kushauriana na Naibu Waziri, Hamis Mwinjuma (MwanaFA) ambaye ndiye msimamizi wa sekta ya sanaa, nimefuta adhabu ya miezi sita aliyopewa kuanzia leo, lakini ninamtaka azingatie maadili katika kufanya kazi zake" amesisitiza Waziri Ndumbaro.

Awali katika kikao hicho Naibu Waziri Mwinjuma alimtaka msanii huyo, kurudi katika sanaa aliyokuwa akiifanya zamani ambayo ndiyo iliyomfanya jamii imtambue na kuelewa kuwa yeye ni kioo cha jamii hivyo anapaswa kufanya sanaa inayoelimisha na kuburushisha jamii bila kuharibu mila na desturi za Kitanzania.

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Xavier Daudi amewataka wakurugenzi wa...
03/09/2024

Kaimu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Xavier Daudi amewataka wakurugenzi wa utawala na usimamizi wa rasilimali watu wa wizara pamoja na waratibu wa jinsia, ngazi ya wizara, kuweka mbinu za kuimarisha mfumo wa utoaji haki, kudhibiti uonevu, dhuluma na unyanyasaji.

Naibu Katibu Mkuu amesema hayo leo wakati akifungua Semina Elekezi ya Mwongozo wa Jinsia (2023) kwa wakurugenzi wa utawala na usimamizi wa rasilimali watu wa wizara pamoja na waratibu wa jinsia ngazi ya wizara jijini Dodoma.

Amesema kumekuwepo kwa viashiria vinavyominya haki za watumishi k**a kutokupata stahiki zao kwa wakati, kutopewa nafasi za kujiendeleza, kukataliwa uhamisho, kutopewa likizo na nauli ya likizo kwamba ni mambo yanayo fedhehesha watumishi wa umma.

Amesema ujumuishwaji wa masuala ya jinsia ni muhimu sana maana ni chachu na huleta ufanisi na tija katika utendaji wa kazi. Aidha amesema hatua hiyo huwawezesha watumishi wanaume kwa wanawake kutumia ujuzi, vipaji na vipawa walivyonavyo kutekeleza majukumu yao na kuleta taswira njema katika taasisi zao.

Nyota wa Timu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia, Neymar Jr, ameendelea kujifua ili kujiweka sawa kwa ajili ya msimu mpya wa Li...
03/09/2024

Nyota wa Timu ya Al-Hilal ya Saudi Arabia, Neymar Jr, ameendelea kujifua ili kujiweka sawa kwa ajili ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya Roshn Saudi Arabia, baada ya kukaa nje kwa miezi 11.

Baada ya kujiunga na Al-Hilal, Neymar alipata majeraha ambayo yamemweka nje ya uwanja hadi sasa. Timu hiyo ya Al-Hilal, pamoja na mfungaji huyo bora wa muda wote wa Brazil, wamekuwa wakichapisha picha mbalimbali mitandaoni zinazoonyesha Neymar akifanya mazoezi ya utimamu wa mwili, akijiandaa kabla ya kuanza mazoezi ya pamoja na kikosi chake.

Neymar, ambaye ana mkataba wa miaka miwili na matajiri hao wa Jiji la Riyadh, amecheza mechi tano tu kabla ya kupata majeraha akiwa na Timu ya Taifa ya Brazil dhidi ya Uruguay mnamo Oktoba 2023.

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa Uruguay, Luis Suárez, ametangaza kustaafu soka la kimataifa.Akizungumza huku akitokwa mach...
03/09/2024

Mshambuliaji wa Timu ya Taifa Uruguay, Luis Suárez, ametangaza kustaafu soka la kimataifa.

Akizungumza huku akitokwa machozi wakati wa mkutano na waandishi wa habari mjini Montevideo, Uruguay, Suárez, mwenye umri wa miaka 37, amethibitisha kuwa mechi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Paraguay itakayochezwa Septemba 5, itakuwa ya mwisho kwake akiwa na timu yao ya taifa.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool na Barcelona ni mfungaji bora wa muda wote wa Uruguay akiwa na mabao 69 katika michezo 142, tangu aanze kuchezea timu ya taifa katika mechi dhidi ya Colombia mnamo Februari 2007.

"Nimekuwa nikifikiria na kuchambua hili. Ninaamini huu ndio wakati sahihi," amesema Suárez.

Suárez amecheza mashindano makubwa tisa ya kimataifa akiwa na Timu ya Taifa ya Uruguay.

Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ushindani wa mwaka 2024 umewasilishwa bungeni leo Septemba 03, 2024 kwa le...
03/09/2024

Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria ya Ushindani wa mwaka 2024 umewasilishwa bungeni leo Septemba 03, 2024 kwa lengo la kuufanyia marekebisho yanayopendekezwa, ili kutatua changamoto mbalimbali zilizobainika katika utekelezaji wa masharti ya sheria.
 
Akiwasilisha Muswada huo bungeni Jijini Dodoma Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. Selemani Jafo amesema vifungu vya 5 na 8 vya muswada huo vinapendekezwa kufanyiwa marekebisho kwa kuanzisha dhana ya "Hodhi ya Pamoja" na kuongeza kiwango cha hodhi ya soko kutoka asilimia 35 hadi 40 Ili kuweka vikwazo dhidi ya matumizi mabaya ya hodhi ya soko inayohusisha mtu zaidi ya mmoja na kuendana na mabadiliko ya kiuchumi na maendeleo yanayofanyika katika ngazi ya kitaifa, kikanda na kimataifa.
 
Aidha, kifungu cha 10A na 11A vinapendekeza kuongezwa ili kuweka masharti yanayozuia makubaliano baina ya watu walio katika ngazi tofauti katika mnyororo wa uuzaji wa bidhaa pamoja na Tume ya Ushindani kuidhinisha muungano wa kampuni wenye manufaa makubwa kwa umma huku kifungu cha 17 pamoja na Jedwali la Marekebisho katika aya B kikipendekezwa kufutwa na kuandikwa upya kwa kuweka sharti la wauzaji wa bidhaa au huduma kuonesha bei ya kila bidhaa au huduma.
 
Waziri Jafo amesema kuwa vifungu vya 61 na 84 vinapendekezwa kurekebishwa ili
mtu ambaye hajaridhika na maamuzi ya Baraza la Ushindani aweze kukata rufaa Mahak**a Kuu ambayo itasikilizwa na majaji watatu kwa lengo la kutoa fursa kwa mtu ambaye hajaridhika na maamuzi ya Baraza kuweza kutafuta haki kwenye chombo cha juu zaidi cha utoaji haki.
 
Bunge litaendelea kuujadili muswada huo na kisha kusomwa kwa mara ya tatu kabla ya kupitishwa.

Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC na Kocha Youssouph Dabo wamefikia makubaliano ya pande mbili ya kutoendelea kufanya kazi ...
03/09/2024

Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC na Kocha Youssouph Dabo wamefikia makubaliano ya pande mbili ya kutoendelea kufanya kazi pamoja kuanzia leo Septemba 03, 2024.

Dabo, aliyehudumu kwenye klabu hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja, anaondoka pamoja na wasaidizi wake wa benchi la ufundi aliokuja nao.

Hatua hiyo imekuja baada ya mwenendo mbaya wa klabu hiyo ya Azam tangu kuanza kwa msimu huu hasa baada ya kuondolewa
kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika kwa kufungwa jumla ya mabao 2-1 na Klabu ya APR ya Rwanda na kutoka sare katika mchezo wa kwanza wa Ligi Kuu ya NBC.

Dabo atakumbukwa kwa mafanikio yake ndani ya matajiri wa Chamazi, Azam FC, ambapo msimu uliopita wa 2023/2024 aliiwezesha timu hiyo kumaliza msimu katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 69, na kuisaidia kufuzu kucheza mashindano ya CAF Champions League (CFL).

03/09/2024

Mafunzo kwa Shirikisho la Askari wa K**e na wasimamizi wa sheria duniani yanaendelea katika Jiji la Chicago, Marekani kwa kushirikisha nchi mbalimbali ikiwemo Tanzania.

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo, Naibu Kamishna wa Uhamiaji kutoka Tanzania DCI Tatu Burhan amesema mafunzo waliyopatiwa yamejikita katika masuala ya ushirikiano wa kimataifa na utatuzi wa changamoto za wahamiaji wanaoingia katika mataifa mbalimbali na namna bora ya kutatua changamoto hizo.

Amesema mafunzo hayo yamewapa mwanga wa namna bora ya kukabiliana changamoto za wahamiaji ambao wamekuwa wakiingia katika nchi mbalimbali kwa lengo la makazi huku akiweka wazi kuwa suala la wahamiaji ni mtambuka.

Kwa upande wake
Ronald Vitiello ambaye ni
Mkufunzi Kutoka Wizara ya Huduma za Binadamu katika Jiji la Chicago akitoa mada kuhusu mipaka na wahamiaji amesema ni muhimu kwa washiriki wa mafunzo hayo kubadilishana uzoefu wa namna ya kukabiliana na wahamiaji.

Mafunzo hayo yanaendelea huku mada mbalimbali zikiwasilishwa ili kuwajengea uwezo wa kiutendaji washiriki hao ambao ni kutoka nchi 64 duniani.

Bunge kuendelea kujadili Miswada leoBaadhi ya wabunge wakiwasili bungeni Jijini Dodoma kushiriki kikao cha sita cha mkut...
03/09/2024

Bunge kuendelea kujadili Miswada leo

Baadhi ya wabunge wakiwasili bungeni Jijini Dodoma kushiriki kikao cha sita cha mkutano wa 16 wa Bunge hilo.

Shughuli za leo za Bunge ni pamoja na kujadiliwa kwa miswada miwili ambayo ni Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria
ya Ushindani wa mwaka 2024 na Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 2) wa mwaka 2024.

Aidha, Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo pamoja na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala, Katiba na Sheria zitawasilisha maoni kuhusu miswada hiyo.

Miswada hiyo itasomwa kwa mara ya pili na ya tatu kabla ya kupitishwa na Bunge.

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when TBConline posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to TBConline:

Videos

Share

Tanzanian Broadcasting Corporation

TBC is your news, entertainment, music fashion website. We provide you with the latest breaking news and videos straight from the entertainment industry.


Other Media/News Companies in Dar es Salaam

Show All

You may also like