Big Bros Media

Big Bros Media πŸ“» Welcome to Big Boss Radio, where the heartbeats of Tanzania unite! πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸŽ΅ No worries! And the best part?
(2)

"Welcome to Big Boss Radio (BBR), your vibrant community radio station and online TV hub, right here in the heart of Dar es Salaam! πŸ“»πŸ“ΊπŸŒ†

Since our inception in 2018, BBR has become the heartbeat of the youth, delivering a unique blend of news, information, sports, and lifestyle content that resonates with our dynamic audience. πŸŽ™οΈπŸ“°πŸ€πŸŒŸ

We're not just about music; we're your go-to source for staying

in the know. Our programming is enhanced with timely news reports, traffic updates, and weather forecasts, ensuring you're always ahead of the game. πŸš—πŸŒ¦οΈ

Can't be with us in person? We beam our broadcast to Dar es Salaam and beyond via live online streaming, making it easy for you to tune in from anywhere on the planet. You can catch up on all your favorite shows with our free podcasts available on our website. 🌍🎧

Our lineup of shows is designed to entertain, inform, and inspire. Dive into the sounds of 'Asubuhi Yetu,' experience the thrill of 'Sports Center,' explore the local scene with 'Tash*titi za Mtaa,' and savor 'Quality Time' on air. πŸŽΆπŸŽ€πŸŽ‰

Meet the friendly faces behind the microphone:
- Teddy Mzirai
- Fadhili Rashid
- Rashidi Hassan Mzee
- Flora Lugongo

BBR is more than just a radio station; it's a vibrant community that celebrates the spirit of Tanzania. Join us on this exciting journey, where every day is a new adventure in sound and stories! πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸŽ΅πŸ“» "

... 🚨 π—›π—œπ—¦π—§π—’π—₯π—œπ—” π—œπ— π—˜π—”π—‘π——π—œπ—žπ—ͺ𝗔Yanga imekuwa timu ya kwanza Duniani kupeleka kombe la ligi kuu kwenye kilele cha mlima Kiliman...
31/05/2024

... 🚨 π—›π—œπ—¦π—§π—’π—₯π—œπ—” π—œπ— π—˜π—”π—‘π——π—œπ—žπ—ͺ𝗔

Yanga imekuwa timu ya kwanza Duniani kupeleka kombe la ligi kuu kwenye kilele cha mlima Kilimanjaro πŸŒ‹

"Historia Imeandikwaβ€¦πŸ—»πŸ†
πŠπŽπŒππ„ 𝐋𝐀 πŒπ€ππˆππ†π–π€ 30x wa Kihistoria Kileleni Mlima Kilimanjaro"


TANZIA: Aliyekuwa Mtangazaji mahiri Nchini, Gardner G. Habash maarufu 'Captain' amefariki Dunia, leo Aprili 20, 2024Hadi...
20/04/2024

TANZIA: Aliyekuwa Mtangazaji mahiri Nchini, Gardner G. Habash maarufu 'Captain' amefariki Dunia, leo Aprili 20, 2024

Hadi umauti unamkuta alikuwa amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ( ) Jijini Dar es Salaam kutokana na changamoto ya Shinikizo la Damu

Kabla ya Kifo, Gadner alijipatia umaarufu kutokana aina ya utangazaji wake wa ucheshi kupitia vipindi vya jioni ambapo alianzia katika Kituo cha Redio cha Clouds FM baadaye Times FM, E-FM na kisha kurejea Clouds FM



Leo ni Eid El Fitr watakie heri ya Eid Ndugu Jamaa na Marafiki.
10/04/2024

Leo ni Eid El Fitr watakie heri ya Eid Ndugu Jamaa na Marafiki.


MWENGE WA UHURU SAME KUZINDUA MIRADI NANE YENYE THAMANI YA SH BIL3.6SAME,KILIMANJARO Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 umepokel...
08/04/2024

MWENGE WA UHURU SAME KUZINDUA MIRADI NANE YENYE THAMANI YA SH BIL3.6

SAME,KILIMANJARO

Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 umepokelewa wilayani Same , baada ya kumaliza mbio zake kwenye wilaya ya Mwanga makabidhiano yamefanyika viwanja vya shule ya Msingi Njoro halmashauri ya Wilaya ya Same.

Mkuu wa Wilaya ya Same Kasilda Mgeni amepokea mwenge huo kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Mwanga Abdallah Mwaipaya akisema ukiwa wilayani humo utakimbizwa umbali wa KM 138.4 kutembelea, kuweka Mawe ya Msingi na kuzindua jumla ya miradi Nane (8) yenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 3.6.

Wilaya ya Same inakua wilaya ya Saba kwenye mkoanwa Kilimanjaro na ndio itahitimisha mbio hizo kimkoa kwa mwaka huu 2024, kisha kukabidhi mkoa jirani wa Tanga hapo kesho Aprili 9,mwaka huu 2024.


Anaitwa Hadija Tindi  HADIJA TINDICHARITY AMBASSADORTASHTIITI ZA MTAA WATOTO NA MALEZI  Siku ya Alhamisi April 04, 2024 ...
03/04/2024

Anaitwa Hadija Tindi HADIJA TINDI
CHARITY AMBASSADOR
TASHTIITI ZA MTAA
WATOTO NA MALEZI Siku ya Alhamisi April 04, 2024 atakuwa ndani ya Studio zetu za Bigbros Radio Katika Kipindi Cha kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusu malezi

USIKOSE KUSIKILIZA TASHTITIZAMTAA KIJIWE CHA HABARI ZA MTAANI NA BURUDANI KUANZIA SAA 5:00 ASUBUHI MPAKA SAA 8:00 MCHANA JUMATATU - IJUMAA.
HOSTED BY

TUSIKILIZE KUPITIA LINK HII https://zeno.fm/radio/bigbros-radio-tz-eg0r/


Teuzi ccm
03/04/2024

Teuzi ccm

MASHABIKI WA SIMBA WAPATA AJALI VIGWAZABasi dogo aina ya Costa lililobeba mashabiki wa Klabu ya Simba limepata ajali map...
29/03/2024

MASHABIKI WA SIMBA WAPATA AJALI VIGWAZA

Basi dogo aina ya Costa lililobeba mashabiki wa Klabu ya Simba limepata ajali mapema alfajiri ya leo eneo la Vigwaza.

Taarifa za awali zinasema mashabiki hao walikuwa wakitokea Tunduma kuja Dar es Salaam ambapo leo klabu hiyo ina mchezo wa robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika dhidi ya Al Ahly ya Misri.

Tayari Kamanda wa Polisi Pwani anaelekea eneo la tukio, taarifa zaidi kuhusu majeruhi zitawajia baadaye.


Inaitwa "Sarco", kifupi cha sarcophagus, ni mashine iliyochapishwa kwa 3D iliyovumbuliwa na Mwanaharakati wa Euthanasia ...
28/03/2024

Inaitwa "Sarco", kifupi cha sarcophagus, ni mashine iliyochapishwa kwa 3D iliyovumbuliwa na Mwanaharakati wa Euthanasia wa Australia, Philip Nitschke na mbunifu wa Uholanzi, Alexander Bannink ikiundwa katika mfumo wa jeneza linaloweza kutenganishwa, lililowekwa kwenye stendi ambayo ina mtungi wa nitrojeni.

Sarco imetengenezwa maalumu kwa kuua mtu bila maumivu, ambapo mtu yeyote ambaye anataka kufa basi ataingia ndani ya mashine hiyo na kubofya kitufe na kapsuli itakayotoa nitrojeni na kisha atasikia kizunguzungu kidogo lakini atapoteza fahamu haraka na kufa.

Nitschke, ambaye amepewa jina la "Dr Death" kwa kazi yake hiyo ya kubuni mashine hiyo, anasema waliweka kielelezo cha kifaa kwenye onesho, pamoja na seti ya miwani ya uhalisia pepe, ili kuwapa wageni hali halisi ya maisha ya jinsi ingekuwaje watakapoketi kwenye mashine hiyo, kabla ya kubonyeza kitufe.

Alipoulizwa kuhusu utata unaozunguka euthanasia na vikwazo vya kisheria, Nitschke alisema: "Katika nchi nyingi kujiua si kinyume cha sheria, ni kusaidia tu mtu kujiua. Hii ni hali ambapo mtu mmoja anachagua kubonyeza kitufe na kufa bila maumivu badala ya ya kugongwa na treni au kujirusha ghorofani."

"Ninaamini ni haki ya msingi ya binadamu (kuchagua wakati wa kufa). Sio tu fursa ya matibabu kwa wagonjwa sana. Ikiwa una zawadi ya thamani ya maisha, unapaswa kuwa na uwezo wa kutoa zawadi hiyo wakati wa kuchagua kwako," alisema Nitschke

Inaarifiwa kuwa, ndani ya mashine hiyo, mtu akishaingia na kujilaza mfumo wa kielektroniki hutambua na kisha hutoa sauti kwa kutumia spika zilizofungwa humo kumuuliza muhusika yeye ni nani, wapi alipo na k**a anafahamu kitakachotokea, kisha baada ya majibu yote kwa usahihi mtu huyo hutakiwa kubonyeza kitufe kilichopo ndani ili kutimiza azma yake.

Kisha muziki mororo huanza kuimba na kumbembeleza muhusika ambaye husikia raha na kuchanganyikiwa kwa wakati mmoja kabla ya kupoteza uhai huku akisikia raha.

Hata hivyo, taarifa za awali zinaonesha kuwa mashine hiyo kwasasa inapatikana Nchini Uingereza na Ufaransa pekee kwani Mataifa hayo sheria zinaruhusu mtu kujiuwa na gharama za kulipia kifo ni Dola 1,000 kwa mtu mmoja na hulipwa kabla.

WASAFI  WAMPA POLE RAIS DK.MWINYIRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amepoke...
20/03/2024

WASAFI WAMPA POLE RAIS DK.MWINYI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amepokea salamu za pole kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Wasafi Nasibu Abdul Juma almaarufu Diamond Platinumz na ujumbe wake Ikulu Mnazi Mmoja tarehe 20 Machi 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi ameushukuru uongozi wa Wasafi kwa kuja kumfariji na kushiriki katika mazishi ya Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi pamoja na utayari wao kushiriki kutangaza mazuri yanayofanywa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Halikadhalika Mkurugenzi Mkuu wa Wasafi Nassib Abdul amempongeza Rais Dk.Mwinyi kwa kazi nzuri anayoifanya ya kuwaletea maendeleo Wazanzibari na kuvuka malengo ya ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 hususani katika sekta ya elimu.

Vilevile Wasafi wameahidi kuendelea kushirikiana na Rais Dk.Mwinyi na kumuunga mkono kuyatangaza mazuri yote anayotekeleza kwa wananchi wa Zanzibar, pia wamemkabidhi zawadi ya nyimbo maalum kwa ajili ya kazi nzuri alizofanya iliyotungwa na wasanii kutoka Wasafi.
Ikulu habari Zanzibar


Msanii wa vichekesho, Umar Iahbedi Issa maarufu β€˜Mzee wa Mjegeje’ amefariki dunia leo alfajiri katika Hospitali ya Rufaa...
20/03/2024

Msanii wa vichekesho, Umar Iahbedi Issa maarufu β€˜Mzee wa Mjegeje’ amefariki dunia leo alfajiri katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala, Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu.

Meneja wa msanii huyo, Real Jimmy amethibitisha taarifa hizo.

Kutoka Kwa Msanii Tuambie nawewe unatoka mkoa gani
13/03/2024

Kutoka Kwa Msanii

Tuambie nawewe unatoka mkoa gani

FEBRUARI 2024 YAVUNJA REKODI KWA KUWA MWEZI WENYE HALI JOTO ZAIDI... Mwezi Februari mwaka 2024, imekuwa Februari yenye j...
10/03/2024

FEBRUARI 2024 YAVUNJA REKODI KWA KUWA MWEZI WENYE HALI JOTO ZAIDI...

Mwezi Februari mwaka 2024, imekuwa Februari yenye joto zaidi kuwahi kurekodiwa duniani kote, k**a ilivyothibitishwa na Copernicus, taasisi ya Umoja wa Ulaya ya kuchunguza hali ya hewa, huku halijoto ikipanda juu ya vizingiti muhimu vya hali ya hewa angani na baharini.

Vipi kwako Joto la Februari maeneo uliyopo umelipata mwezi huo?


10/03/2024

BREAKNEWS

AJALI MBAYA,WATU KADHAA WAHOFIWA KUFA,COSTA NA LORI ZAGONGANA KILOMO-BAGAMOYO.

Ni ajali ambayo imetokea Jioni ya leo Jumapili Machi 10, 2024 ikihusisha magari mawili ambapo gari aina ya Costa iliyokuwa intokea Kilomo Bagamoyo kuelekea Jijini Dar es Salaam imegongana na Lori lenye Kokoto.

Ripota wetu Dear Mkasi anasema kwa hali ilivyo yaonekana kuna Vifo na Majeruhi.

Bado tunasubiri taarifa kutoka Jeshi la Polisi kujua undani Zaidi.

Tafadhali endelea kufuatilia Mitandao yetu ya Kijamii kwa Updates Zaidi kupata taarifa za kina zaidi.


POLISI MSTAAFU ALIYEJICHIMBIA KABURI ANUNUA JENEZA.Ofisa mstaafu wa Jeshi la Polisi, Saba Sita ameweka wazi jeneza ambal...
04/03/2024

POLISI MSTAAFU ALIYEJICHIMBIA KABURI ANUNUA JENEZA.

Ofisa mstaafu wa Jeshi la Polisi, Saba Sita ameweka wazi jeneza ambalo ndimo atazikwa, ambalo utengenezaji wake umechukua miezi sita kukamilika likiwa thamani ya Sh3,000,000.

Jeneza hilo limetengenezwa kwa mbao za mbunduki ambazo haziliwi na wadudu na hivyo lina uwezo wa kudumu kwa miaka 50.

Tukio hili ni nadra kwa mtu kujitengenezea jeneza lake akiwa hai kutokana na imani, mila na desturi za Watanzania, lakini Saba Sita ameenda mbali na kujitengenezea kaburi lake akisubiri siku ya kifo chake.


POLISI MANYARA WAWAONYA WAGANGA TIBA ASILI WASIOZINGATIA SHERIA.Mkuu wa Kamisheni ya Polisi Jamii Mkoa wa Manyara, Kamis...
04/03/2024

POLISI MANYARA WAWAONYA WAGANGA TIBA ASILI WASIOZINGATIA SHERIA.

Mkuu wa Kamisheni ya Polisi Jamii Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Kija Mkoyi amewataka Waganga na Wakunga wa Tiba Asili (UWAWATA) Mkoa wa Manyara kufanya kazi kwa kuzingatia Sheria na Vibali walivyopewa ili kulinda usalama na amani kwenye jamii.

Ameyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akifunga mafunzo maalumu kwa waganga na watoa tiba hao yaliyofanyika ukumbi wa River Nile Halmashauri ya Mji Babati.

Ameeleza kuwa tiba asili zinamchango mkubwa katika jamii k**a zitatumika vizuri na kuwataka watoa huduma hao kuacha ramli chonganisha kwani zinaweza kuhatarisha Amani.

Kwa upande wake Katibu wa Chama Cha Waganga na Wakunga wa Tiba Asili (UWAWATA) Mkoa wa Manyara, Adamu Issuya, amelipongeza Jeshi la Polisi kwa ushirikiano wanaoutoa katika kuhakikisha kazi zao zinafanyika Kwa uhuru na amani.

Amewataka waganga kuzingatia Sheria na kuachana na vitendo vya ukatili ikiwemo kutumia viungo vya binadamu katika kutoa tiba.

Jumla ya wanachama 51 wa UWAWATA Mkoa wa Manyara wamenufaika na Semina hii na kuahidi kwenda kuyafanyia kazi waliyojifunza.


RAIS DKT. SAMIA AMEDHAMIRIA KUENDELEA KUBORESHA SEKTA YA AFYA-MAJALIWA.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali inae...
28/02/2024

RAIS DKT. SAMIA AMEDHAMIRIA KUENDELEA KUBORESHA SEKTA YA AFYA-MAJALIWA.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali inaendelea na mkakati wa kuboresha sekta ya afya nchini ili kusogeza huduma bora za afya karibu na Wananchi.

Akizungumza baada ya kukagua maendeleo ya mradi wa hospitali ya wilaya ya Rorya, mkoani Mara, Mheshimiwa Majaliwa ameagiza kuendelea kukamilishwa kwa ujenzi wa hospitali hiyo pamoja na kununua vifaa tiba ili kuimarisha hali ya utoaji huduma kwa wananchi.

β€œKukamilika kwa hospitali hii kutasaidia kupunguza gharama kwa wakazi wa maeneo ya Karibu kutembea umbali mrefu hadi Tarime kufuata huduma za afya, hospitali hii ni suluhisho”.

Ujenzi wa hospitali hiyo ambayo inajengwa kwa njia ya force account umeshatumia kiasi cha shilingi bilioni 3.25 kutoka Serikali kuu zilizotoka kwa awamu tatu na mwaka 2020 ilianza kutoa huduma mbalimbali za wagonjwa wa nje ambapo inahudumia takribani watu 400 kwa mwezi.


RAIS DK.MWINYI AKUTANA NA UONGOZI WA KANISA LA KILUTHERI AFRIKA MASHARIKIRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Map...
28/02/2024

RAIS DK.MWINYI AKUTANA NA UONGOZI WA KANISA LA KILUTHERI AFRIKA MASHARIKI

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Makamu Askofu Mkuu wa Kanisa la Kilutheri Afrika Mashariki (KKAM), Askofu Dk.Philemon Mollel na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar kujitambulisha tarehe: 28 Februari 2024.

Aidha, Rais Dk.Mwinyi amesema Serikali inatambua mchango unaotolewa na Madhehebu ya Dini zote ikiwemo kuhubiri amani na utulivu katika kuleta umoja nchini.

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amelipongeza Kanisa hilo kwa utayari wao wa kushirikiana na Serikali katika kutoa huduma za kijamii nchini ikiwemo afya na elimu.

Naye Askofu Mollel amempongeza Rais Dk.Mwinyi kwa kuleta mabadiliko ya maendeleo na kuwaunganisha wananchi bila kujali itikadi za chama, kabila na Dini.


Ujumbe wa Mbunge wa Kigamboni faustine_ndugulile
28/02/2024

Ujumbe wa Mbunge wa Kigamboni faustine_ndugulile

14/09/2023

πŸ“» Welcome to Big Boss Radio, where the heartbeats of Tanzania unite! 🎢 We're your go-to destination for non-stop music all day, every day! πŸ‡ΉπŸ‡ΏπŸŽ΅

Catch  kutoka kundi la   akitambulisha wimbo wake mpya wa    live leo hii kwenye   kwanzia mida ya sa nane mpka kumi na ...
23/08/2023

Catch kutoka kundi la akitambulisha wimbo wake mpya wa live leo hii kwenye kwanzia mida ya sa nane mpka kumi na moja jioni Make sure una tune in hii si ya kukosa gurudumu hili litosongeshwa na 360 na Mjuzi wa mambo wa kumwita

Tusikilize kupitia
https://zeno.fm/radio/bigbros-radiowybm2d8z8p8uv/

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na  Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilut...
21/08/2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Maaskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) pamoja na Waumini wa Kanisa hilo, kwenye Maadhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) yaliyofanyika katika Ukumbi wa Viwanja vya Mfuko wa Wastaafu Mkoani Arusha tarehe 21 Agosti, 2023

Catch Sapologuano live leo hii kwenye   kwanzia mida ya sa nane mpka kumi na moja jioni.. Atafunguka kuhusu sakata lake ...
21/08/2023

Catch Sapologuano live leo hii kwenye kwanzia mida ya sa nane mpka kumi na moja jioni.. Atafunguka kuhusu sakata lake yeye na kuhusu mchongo mzima wa kushushwa na kurudishwa tena audio ya yakwake jux akimshirikisha make sure una tune in hii si ya kukosa gurudumu hili litosongeshwa na 360 Mollel na Mjuzi wa mambo wa kumwita

Tusikilize kupitia https://zeno.fm/radio/bigbros-radiowybm2d8z8p8uv/

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi wa kwan...
20/08/2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Majeshi wa kwanza Mstaafu Jenerali Mrisho S. Sarakikya na Familia yake wakati alipomtembelea kumjulia hali nyumbani kwake Mkoaranga Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha tarehe 20 Agosti, 2023.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Kampun...
20/08/2023

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye Picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Puma Energy na Mkurugenzi Mwenza wa Kampuni ya mafuta ya Trafigura Bw. Hadi Hallouche, mara baada ya mazungumzo yao Ikulu ndogo Jijini Arusha tarehe 19 Agosti, 2023. Miongoni mwa mambo waliojadili ni Biashara ya Hewa ukaa na gesi asilia kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.

HAPA LIPO LA KUJIFUNZA BARUA YA MAMA KWENDA KWA MWANAYE - SIKU TATU BAADA YA MAZISHI.Mpendwa mwanangu,Nataka ujue kwa ni...
20/08/2023

HAPA LIPO LA KUJIFUNZA

BARUA YA MAMA KWENDA KWA MWANAYE - SIKU TATU BAADA YA MAZISHI.

Mpendwa mwanangu,

Nataka ujue kwa nini nilikufa nikiwa masikini wakati nina mtoto k**a wewe.

Mwanangu, nilitaka kukupa baraka zangu kabla sijafa, lakini sasa nimeondoka na baraka zangu.

Chakula changu cha asubuhi, cha mchana na cha usiku kilikuwa miongoni mwa changamoto zangu nilipokuwa hai, lakini wewe umetumia pesa kupika kila aina ya vyakula, nyama na kununua aina mbalimbali za vinywaji siku ya mazishi yangu.

Mwanangu, ulichagua kuupaka mwili wangu uliokufa kwa kutumia mafuta mazuri na manukato yenye kunukia wakati nilipokuwa hai nilitumia mawese kujipaka kwa kukosa mafuta.

Umeivika maiti yangu kwa nguo ghali wakati ulishindwa kuninunulia hata khanga.

Maiti yangu ilipokuwa mochwari ulikuja kunitazama mara kwa mara, kwa nini umeijali maiti yangu wakati ulishindwa kunijali nilipokuwa hai?

Kitu kinachoniuma zaidi ni jeneza la bei kubwa ambalo umeuweka mwili wangu ilhali nilipokuwa hai The most painful niliishi katika nyumba mbovu ambayo haikumaliziwa kujengwa.

Ulipokuwa mdogo nilikaa na njaa ili wewe ule na kushiba, nilivaa nguo kuukuu ili upate nguo za kutosha. Nilidhani utanitunza nikizeeka.

Wakati wa mazishi yangu ulimalizia nyumba, ukaipaka rangi na kuusafisha uwanja ndani ya wiki moja ili tu upate kuadhimisha mauti yangu.

Sasa umeniandikia tanzia ukisema "Mama, nakupenda sana, pumzika kwa amani" - ilhali nimekufa nikiwa na maumivu moyoni.

Mwisho kabisa, mwanangu, nimekuandikia kukukumbusha kuwa hakuna mtu anayempenda mtoto k**a mama yake.

Mungu akusamehe.
____________________________

Tafadhali shea ujumbe huu uwafikie watu wengine ili waweze kuwajali watu wakiwa hai badala ya kuwajali wakiwa wamekufa.

Wajali sana wazazi wako wakati wakiwa hai.

Nawatakia siku njema.

UTEUZI
18/08/2023

UTEUZI

Mabondia wa Tanzania Bara πŸ‡ΉπŸ‡Ώ Ibrahim Class pamoja na Karim Mandoga wameelewa katika visiwa vya karafu Zanzibar kujiandaa...
18/08/2023

Mabondia wa Tanzania Bara πŸ‡ΉπŸ‡Ώ Ibrahim Class pamoja na Karim Mandoga wameelewa katika visiwa vya karafu Zanzibar kujiandaa na usiku wa vitasa Agosti 27 mwaka huu katika ukumbi wa Mao Tse Tung Zanzibar

Address

Namanga
Dar Es Salaam
14111

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Big Bros Media posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Big Bros Media:

Videos

Share


Other Media/News Companies in Dar es Salaam

Show All