08/05/2022
Wasanii na mashabiki tusikae tukajisahaulisha kuwa mziki ni kiwanda kikubwa cha sanaa inayohitaji system ya vitu vinne:
1. Ubunifu
2. Uhusiano wa mziki na maisha yetu (lifestyle)
3. Rythm/Vibe
4. Mapokeo (Delivery)
Msanii kufanikiwa kwa dunia ya sasa yenye utandawazi na ufahamu ulioongezeka, ni kucheza na hizo nyenzo 4.
Kuna wasanii wana sauti nzuri, wanarap na vina vikali, wana mionekano mizuri ya kiusanii lakini still ni undergroung.. kwa nini..
Sio afya sana kulaumu kuwa msanii wako pendwa hajawa mkubwa/hapewi ukubwa anaostahili.. Jibu ni moja... system imemkataa/hajaendana na system.
System haiwezi kukukubali ikiwa hujaendana nayo.
Imagine msanii unaimba/unarap vitu ambavyo jamii haiwezi kuvipokea na haina mahusiano navyo.
Mfano mdogo: Asilimia 90% ya wasikilizaji/wapenzi wa mziki ni vijana kati ya miaka 18-30.. hawana majukumu mengi.., umri wa mapokeo, umri ambao wengi wanakua energetic na wanataka ku-experience maisha,umri wa kujirusha, mapenzi nk.
Ukiimba siasa, harakati au misemo na nahau au ushauri nasaha wachache watakupokea basi at least uwe na vibe au uimbe kitu cha tofauti.
KWA NINI RAP NI KUBWA USA KULIKO KWETU:
Marekani rap ni kubwa kuliko kwetu sisi sababu moja tuh: Tuna lifestyle tofauti. Sisi hatuna hela tunaishi kiujamaa, tuna miiko na mila zetu.
USA jamii yao kila mtu na hustling zake na maisha yake.Wasanii wengi wa rap wanakulia kwenye gang members na wanaishi maisha hayo...
Kuuza madawa.., wizi, maisha ya kihuni nk coz almost ukahaba, ushoga, umeruhusiwa, bangi, ushoga, kumiliki silaha, pornigraphy, club za wavua nguo (strip club) nk ni kawaida wanajiona proud kwa hilo. So wakiimba kuhusu hustling, maisha ya club, madawa, uhuni inapokelewa coz hata jamii hiyo wanapitia mambo hayo.
TZ CASE STUDY
Huwezi toboa tz km mziki wako hauimbi
1.Mapenzi
2. Mishe mishe za uswahilini kwetu (Singeli wameweza)
3. Mziki hauna vibe au pengine mashairi yanayovuta hisia kwa jamii.
4. Hauna kitu cha ku-trend.
Tuache kulaumu mashabiki na vyombo vya habari...
Tutalalamika kila siku wasanii flani wanaimba matusi, wanaimba hovyo, wanakaa uchi, hawajui kuimba, mara wanabebwa nk but hao hao ndio utashangaa mziki wao unatrend, club unapgwa, wanalamba deals mbalimbali. Wanapiga pesa na miziki yao isiyoeleweka
MWISHO :TUSIISHI KM ZAMANI, DUNIA INABADILIKA ILA PIA SISI TUNAFELI KWA KUSHINDWA KU-APPRECIATE GOOD MUSIC