MwanaHabari Digital

MwanaHabari Digital PATA HABARI KWA HARAKA NA UHAKIKA KILA WAKATI KATIKA UKURASA HUU WA KIDIGITAL

Takriban watu 40 wameuawa kusini mwa Gaza na makumi ya wengine kujeruhiwa katika mashambulizi ya Israel kwenye eneo lili...
10/09/2024

Takriban watu 40 wameuawa kusini mwa Gaza na makumi ya wengine kujeruhiwa katika mashambulizi ya Israel kwenye eneo lililochaguliwa kuwa la kibinadamu, mamlaka ya Ulinzi wa Raia inayosimamiwa na Hamas ilisema.
Jeshi la Israel limesema ndege yake ilishambulia kitovu cha operesheni zilizofanywa Khan Younis eneo la wapiganaji wa Hamas, na kwamba imechukua hatua za kupunguza hatari ya kuwadhuru raia.

Wakaazi wa eneo hilo walisema mashambulizi matatu yalilenga mahema ya watu waliokimbia makazi yao katika eneo la kibinadamu la al-Mawasi, magharibi mwa jiji la Khan Younis, na kusababisha mashimo makubwa.
"Watu 40 waliuawa na zaidi ya 60 kujeruhiwa, huku wengi wakiwa bado chini ya vifusi," mkurugenzi wa operesheni wa mamlaka ya ulinzi wa raia wa Hamas aliambia BBC.
Walioshuhudia walisema milipuko mikubwa ilitikisa eneo la al-Mawasi muda mfupi baada ya saa sita usiku na miali ya moto ilionekana kupanda angani.

Khaled Mahmoud, mfanyakazi wa kujitolea wa shirika la kutoa misaada ambaye anaishi karibu na eneo la lililoshambuliwa, alisema yeye na watu wengine waliojitolea walikimbilia kusaidia lakini walishangazwa na ukubwa wa maafa.

"Mashambulizi hayo yalisababisha mashimo matatu yenye kina cha mita saba na kufukia mahema zaidi ya 20," Bw Mahmoud alisema.

Video ambazo hazijathibitishwa zilionyesha raia wakichimba mchanga huo kwa mikono wakijaribu kuwaokoa Wapalestina kutoka kwenye shimo refu lililosababishwa na mashambulizi hayo ya anga.

Akiweka ujumbe kwenye mtandao wa Telegram, msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) alisema limewashambulia "magaidi muhimu wa kundi la Hamas ambao walikuwa wakisimamia shughuli zao kwa kutoa amri na kudhibiti eneo lililotengwa kuwa la kibinadamu huko Khan Younis".

Maafisa wa Urusi wanasema kuwa walidungua ndege zisizo na rubani 144 za Ukraine kote nchini humo usiku kucha katika wimb...
10/09/2024

Maafisa wa Urusi wanasema kuwa walidungua ndege zisizo na rubani 144 za Ukraine kote nchini humo usiku kucha katika wimbi la mashambulizi yaliyosababisha kifo cha mwanamke mmoja, kuchoma moto majengo ya makazi na kusimamisha safari za ndege mjini Moscow.

Gavana wa Moscow, Andrei Vorobyov, alisema nyumba kadhaa katika eneo la majengo ya ghorofa ya juu huko Ramenskoye mkoa wa Moscow zilichomwa moto.
Bw Vorobyov alisema mwanamke mwenye umri wa miaka 46 alifariki na watu watatu kujeruhiwa huko Ramenskoye, huku watu 43 wakihamishwa hadi vituo vya makazi ya muda.

Ukraine hadi sasa haijazungumzia mashambulizi hayo.
Wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema Jumanne kwamba kati ya ndege 144 ambazo ulinzi wake wa anga zilinasa, nusu zilikuwa katika eneo la mpaka wa magharibi wa Bryansk, 20 ziko Moscow na 14 ziko katika eneo la Kursk.

Vyombo vya habari vya serikali viliripoti kuwa shambulizi hilo lilisababisha viwanja vinne vya ndege huko Moscow kufungwa na zaidi ya safari 30 za ndege za ndani na za kimataifa zinazohudumia mji mkuu wa Urusi kusitishwa.

Polisi kata kata ya ikungulyabasha bariadi Mkoani Simiyu CPL JEREMIAH LWAMIHETO ameamu kupita mtaa Kwa mtaa kuongea na w...
10/09/2024

Polisi kata kata ya ikungulyabasha bariadi Mkoani Simiyu CPL JEREMIAH LWAMIHETO ameamu kupita mtaa Kwa mtaa kuongea na watoto kupinga ukatili Kwa watoto na kuwasihi kutoa taarifa pale wanapofanyiwa ukatili Kwa Polisi kata.

Ameandika Rais Samia Suluhu Hassan Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya mauaji ya kiongozi waCHADEMA Bwana Mohame...
08/09/2024

Ameandika Rais Samia Suluhu Hassan Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa ya mauaji ya kiongozi wa
CHADEMA Bwana Mohamed Ali Kibao.

Natoa pole kwa viongozi wa chama hicho, familia ya Mzee Kibao, ndugu, jamaa na marafiki.

Nimeagiza vyombo vya uchunguzi kuniletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka. Nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana Haki ya kuishi. Serikali ninayoiongoza haivumilii vitendo vya
kikatili vya namna hii.

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema akizungumza na Mwananchi asubuhi ya leo Jumapi...
08/09/2024

Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema akizungumza na Mwananchi asubuhi ya leo Jumapili, Septemba 8, 2024 amesema familia ya Ali Kibao imejulishwa uwepo wa mwili unaofanana na Kibao katika Hospitali ya Rufaa ya Mwananyama, Kinondoni jijini Dar es Salaam.
"Polisi wameijulisha familia ya Ally Kibao kuwa kuna mwili unaofanana na wa Ali Kibao upo Hospitali ya Mwananyama. Sasa familia na viongozi wanakwenda kufuatilia nini kinaendelea na undani wake," amedai Mrema.

Kibao ambaye ni Mjumbe wa Sekretarieti ya Chadema anadaiwa jioni ya Septemba 6, 2024 maeneo ya Kibo Complex Tegeta jijini Dar es Salaam, akiwa safarini kutoka Dar es Salaam kuelekea Tanga na basi la Tashrif alishushwa kwenye basi hilo na kuchukuliwa na watu wasiojulikana majina yao wala walipotokea.

Jana Jumamosi, Msemaji wa Jeshi la Polisi, David Misime alisema wanafuatilia tukio hilo. Misime alisema hivyo saa chache kupita tangu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika kuzungumza na waandishi wa habari na kutoa wito kwa vyombo vya dola kufuatilia tukio hilo.

Mnyika alidai katika magari yaliyozuia basi hilo, inadaiwa watu wenye silaha walishuka na kupanda ndani ya basi hilo na kumk**ata kisha kumfunga pingu.

Viongozi wa Chadema, wakiongozwa na Freeman Mbowe kwa sasa wanaelekea Mwananyamala Hospitali.

*WAZIRI MKUU ASHIRIKI MBIO ZA HISANI ZA MAENDELEO BANK*Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 07, 2024 ameshiriki kati...
07/09/2024

*WAZIRI MKUU ASHIRIKI MBIO ZA HISANI ZA MAENDELEO BANK*

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Septemba 07, 2024 ameshiriki katika mbio za hisani za Maendeleo Bank Marathon 2024 zilizoanzia na kuishia katika viwanja vya Greenpark garden Oysterbay jijini Dar es Salaam.

Lengo la mbio hizo ni kukusanya zaidi ya shilingi milioni 200 kwa ajili ya kusaidia watoto wenye changamoto mbalimbali hapa nchini.

Kauli mbiu ya mbio hizo ni “Hatua ya Faraja- Msimu wa Pili”.

“Kuna mchungaji mmoja [Kiboko ya wachawi]  tulimuondosha nchini kutokana na kukiuka sheria ya kusajili, na nimeshuhudia ...
07/09/2024

“Kuna mchungaji mmoja [Kiboko ya wachawi] tulimuondosha nchini kutokana na kukiuka sheria ya kusajili, na nimeshuhudia huko alikokwenda amekuwa akisambaza clip za video kuthibitisha kuwa aliyokuwa akiyafanya yalikuwa ni kinyume kabisa na mafundisho ya kitabu cha dini ikiwemo masuala ya kutapeli watu, kuwatoza watu kinyume na taratibu, kuwaaminisha watu kwamba miujiza inaweza kuwafanya wao wawe matajiri mambo ambayo ni kinyume na mafundisho ya dini zetu.” - Hamad Masauni, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi

Picha: Wasanii na watu mbalimbali wamefika tayari Katika Viwanja Vya Leaders Leaders Kwa Pamoja Kuwaenzi na kuwa kumbuka...
07/09/2024

Picha: Wasanii na watu mbalimbali wamefika tayari Katika Viwanja Vya Leaders Leaders Kwa Pamoja Kuwaenzi na kuwa kumbuka Wasanii na Wadau ambao wametangulia mbele za haki, Wapendwa hao wanamchango mkubwa kwenye Tasnia Yetu Kwa Ujumla kwa kupitia Sanaa Yao na Vipaji vyako kwa Ujumla.


tanzania

Marekani imesema ina wasiwasi kuwa Urusi imetengeneza silaha mpya inayoweza kushambulia satelaiti.Lakini Urusi imekanush...
06/09/2024

Marekani imesema ina wasiwasi kuwa Urusi imetengeneza silaha mpya inayoweza kushambulia satelaiti.

Lakini Urusi imekanusha madai hayo ya Marekani, ikisema ni njama ya kutoa shutuma ili kulilazimisha Bunge la Marekani kutoa fedha za ziada kwa ajili ya Ukraine.

Katika mitandao ya habari ya New York Times, ABC na CBS - ripoti zilisema tishio hilo lilitokana na silaha za nyuklia zilizotengenezwa na Urusi. Kuna hofu kuwa zinaweza kutumika kushambulia satelaiti za Marekani angani.

Akizungumza na waaandishi wa habari hivi karibuni kuhusu silaha hii, msemaji wa usalama wa taifa katika Ikulu ya Marekani John Kirby, alisema hakuna tishio la moja kwa moja kwa watu wa Marekani.

John Kirby, amesema Rais Joe Biden amefahamishwa kuhusu suala hilo, alisema utawala wa Biden umelichukulia suala hilo 'kwa uzito mkubwa'.

Kadhalika alisema, Rais Biden ameamuru mawasiliano ya moja kwa moja ya kidiplomasia na Urusi juu ya suala hili.
John Kirby aliwaambia wanahabari hakuna ushahidi kwamba silaha hiyo imetumiwa.

Mbali na maoni ya John Kirby, maafisa wa serikali ya Marekani bado hawajatoa taarifa zozote kuhusu tishio hilo.
Mshauri wa Usalama wa Taifa, Jake Sullivan amedokeza kuwa serikali ya Marekani imekuwa kimya kwa makusudi

Pia aliwaambia waandishi wa habari kwamba mashirika ya kijasusi ya Marekani yatafanya kazi kukusanya taarifa kuhusu tishio hilo.

Burkina Faso yatangaza kupiga marufuku ndoa za jinsia Moja nakuweka sheria kali kwa yeyote atakayebainika kufanya hivyo....
06/09/2024

Burkina Faso yatangaza kupiga marufuku ndoa za jinsia Moja nakuweka sheria kali kwa yeyote atakayebainika kufanya hivyo.

Je, unamuunga mkono Kapteni Ibrahim Traore

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amempa siku tano aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEM...
06/09/2024

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amempa siku tano aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA Kanda ya Nyassa, Mchungaji Peter Msigwa, kuomba radhi na kulipa fidia ya shilingi bilioni 5 kutokana na madai ya kumkashifu na kuharibu chapa yake kutokana na matamshi ya Msigwa yaliyotolewa hadharani baada ya kuhamia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Katika barua (notisi ya madai) iliyotolewa Septemba 2, 2024 ikiwa na sahihi ya tarehe 4 Septemba, 2024, mawakili wa Mbowe ambao ni Hekima Mwasipu na wenzake kutoka Matwiga Law Chambers, Msigwa anadaiwa kutoa matamshi ya uongo na kumchafua Mbowe mbele ya umma.

“Msigwa alitumia majukwaa ya mikutano, vyombo vya habari, na hata mitandao ya kijamii kutoa madai ya kumkashifu mteja wetu,” ameleza Wakili Mwasipu.

Imeelezwa kuwa Msigwa alidai kuwa Mbowe ameanzisha "Mbowe Foundation," na anatumia chama cha CHADEMA kwa manufaa yake binafsi. Katika moja ya mikutano yake, Msigwa alinukuliwa akisema, "Mwenyekiti wa CHADEMA amegeuza chama kuwa SACCOS, fedha za chama zinaishia kwenye taasisi binafsi na si kwenye akaunti za chama.”

Mawakili wa Mbowe wameeleza kuwa matamshi hayo yameathiri sifa ya Mbowe ndani na nje ya Tanzania, hasa kutokana na nafasi zake mbalimbali kimataifa, ikiwa ni pamoja na kuwa Naibu Mwenyekiti wa Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia vya Afrika (DUA).

MACHINGA WAPO TAYARI KULIPA KODI KULIJENGA TAIFAKamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda pamoja n...
05/09/2024

MACHINGA WAPO TAYARI KULIPA KODI KULIJENGA TAIFA

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Yusuph Mwenda pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo Wamekutana Jijini Dar es Salaam leo 5 Septemba 2024 katika kikao cha pamoja na wafanya biashara ndogondogo(Machinga) ambapo wamejadili mambo mbalimbali yanayohusu kodi.

Katika kikao hicho kilicho fanyika katika ukumbi wa mikutano wa TRA jijini hapa Jumuiya ya wafanya biashara ndogondogo wakiongozwa na Mwenyekiti wa taifa wa jumuiya hiyo Stephen Lusinde walisema Wamachinga wapo tayari kulipa kodi ili kulijenga Taifa.

Marekani imewashtaki na kuwawekea vikwazo wasimamizi wa vyombo vya habari vya serikali ya Urusi na kuwawekea vikwazo wat...
05/09/2024

Marekani imewashtaki na kuwawekea vikwazo wasimamizi wa vyombo vya habari vya serikali ya Urusi na kuwawekea vikwazo watangazaji wanaohusishwa na Kremlin huku ikiishutumu Moscow kwa kampeni iliyoenea ya kuingilia uchaguzi wa rais.

Wizara ya sheria, serikali na hazina ilitangaza hatua zilizoratibiwa Jumatano "kukabiliana vikali" na shughuli zinazodaiwa.

Mwanasheria Mkuu Merrick Garland alishutumu shirika la utangazaji la RT, la Urusi, kwa kuilipa kampuni ya Tennessee $10m "kuunda na kusambaza maudhui kwa watazamaji wa Marekani kwa ujumbe fiche wa serikali ya Urusi".

Mkuu wa RT Margarita Simonyan alikuwa mmoja wa watu 10 walioidhinishwa kwa madai ya kujaribu kuharibu "imani ya umma kwa taasisi zetu". RT ilikanusha kuhusika.

Bw. Garland alisema kuwa Moscow ilitaka kupata "matokeo" katika kinyang'anyiro kati ya Donald Trump na Kamala Harris.

Msemaji wa usalama wa taifa wa White House John Kirby alisema kuwa mpango huo wa Urusi unalenga "kupunguza uungwaji mkono wa kimataifa kwa Ukraine, kuimarisha sera na maslahi yanayoiunga mkono Urusi, na kuathiri wapiga kura hapa Marekani".

Afisa wa Hazina wakati huo huo alisema kuwa RT na vyombo vingine vya habari vya serikali ya Urusi vilijihusisha na "kampeni mbaya ya kuajiri kwa siri washawishi wa Marekani bila kujua kuunga mkono shughuli zao mbaya".

Watafiti wawili wa Marekani wanadai kuwa Urusi inajiandaa kutumia kombora la masafa linalotumia nguvu ya nyukilia la 9M3...
05/09/2024

Watafiti wawili wa Marekani wanadai kuwa Urusi inajiandaa kutumia kombora la masafa linalotumia nguvu ya nyukilia la 9M370 Burevestnik, ambalo Vladimir Putin alilizungumzia katika hotuba yake kwa bunge mwezi Machi 2018.

Ripoti ya Reuters, pamoja na tweet kutoka kwa mchambuzi wa utafiti wa CNA Dekker Evelet, zilisema kuwa kwa ushirikiano na Hans Christensen kutoka Shirikisho la Wanasayansi wa Marekani , waligundua mabadiliko katika picha za satelaiti za kituo kilichopo katika eneo la Sheksninsky huko Vologda ambayo yanaonyesha kusafirishwa kwa makombora hayo.

Kituo hiki kinajulikana k**a kitengo cha kijeshi 25594, au hifadhi ya silaha ya Kurugenzi Kuu ya 12 ya Wizara ya Ulinzi ya Urusi, ambayo inasambaza silaha kwa Vikosi vya nyuklia vya kimkakati. Karibu na eneo hilo kuna mji wa Vologda-20, ambapo kitengo, kambi, na vifaa vyake vipo.

Kituo chenyewe kina maeneo matano na miundo ambayo watafiti huiita vifaa vya kuhifadhia ya kichwa cha nyuklia. Vifaa hivi ambavyo vimekuwepo mahali hapo kwa muda mrefu - vilionekana kwenye picha za satelaiti za Google Earth tangu mwaka 2003.

Watafiti wameona mabadiliko katika eneo hili kwenye picha mpya za satelaiti - lenye ujenzi na maeneo tisa tofauti.

Wachambuzi wa picha hizi wameona kitu ambacho wamekitaja k**a kifaa kinachoundwa kwa ajili ya ufyatuzi wa makombora Kimegawanyika katika makundi matatu.

Kwa mujibu wa chapisho la Reuters, eneo la ufyatuaji wa makombora lipo karibu na maeneo ya kuhifadhi kichwa cha nyuklia.

Kwa mujibu wa Evelet, maeneo haya " yanakusudiwa kutumiwa kwa ajili ya mfumo mkubwa wa makombora, na mfumo pekee mkubwa wa makombora ambao Urusi inauandaa ni Skyfall." SSC-X-9 Skyfall jina uliopewa mradi wa Burevestnik na NATO.

WADAU wa Utalii katika Hifadhi ya Taifa Serengeti wameiomba Serikali kupatia suluhisho la kudumu la ujenzi wa barabara k...
04/09/2024

WADAU wa Utalii katika Hifadhi ya Taifa Serengeti wameiomba Serikali kupatia suluhisho la kudumu la ujenzi wa barabara katika Hifadhi za Taifa hususani barabara ya Serengeti

Akizungumza leo na waandishi wa habari ambao wametembelea eneo hilo, ambapo Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Wolway Trekking Tanzania Limited, John Macha alipongeza hatua zinazochukuliwa na Serikali kupitia TANAPA katika kuboresha barabara hizo ambazo kwa kiasi kikubwa ziliathiriwa kwa kiasi kikubwa na mvua pamoja na wingi wa magari ya utalii yanayopita kwa siku pia yanachangia uharibifu wa barabara hiyo, takribani magari 300 mpaka 500 yaliyobeba watalii yanatumia barabara hiyo.

Macha aliyasema hayo mbele ya Kamishna ya Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Nassoro Juma Kuji, ambaye alifanya ziara ya kukagua matengenezo yanayoendelea kufanyika katika barabara ya Naabi hadi Seronera.

Kutokana na hali hiyo wadau hao wamependekeza kujengwa kwa barabara yenye tabaka gumu katika hifadhi hiyo ikiwa ni mwarobaini wa tatizo la barabara.

“Niipongeze Serikali kwa matengenezo haya ya barabara kutoka Seronera mpaka Golini tunafahamu hii ni kazi kubwa mnaifanya na tunaomba muendelee nayo lakini kwa ufumbuzi wa kudumu kuwe na jawabu la kudumu kwa sababu magari ni mengi mtakuwa mnafanya zoezi hili ndani ya wiki mbili mpaka tatu mnarudia zoezi hili.

“Kwa hiyo lile wazo Serikali kupitia Serengeti la kuwa na tabaka gumu la kudumu lingekuwa wazo zuri sana wakati huu tungesahau matengenezo haya ya mara kwa mara na hata kuongeza gharama ni bora tuingie gharama kutengeneza barabara itakayokaa muda mrefu hata k**a ni gharama kubwa,” alisema Macha

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mhe.Peres Magiri akiwa na k**ati ya Ulinzi na Usalama tarehe O3.09.2024 amemk**ata Mganga wa Kie...
04/09/2024

Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Mhe.Peres Magiri akiwa na k**ati ya Ulinzi na Usalama tarehe O3.09.2024 amemk**ata Mganga wa Kienyeji maarufu kwa jina la Askofu, katika Mhalo wa Mbamba bay Wilayani Nyasa, kwa upotoshaji wa kuwauzia dawa wavuvi wa Ziwa Nyasa na kuwaambia zinaosha nyota na wakifanya mapenzi ndani ya maji ya Ziwa Nyasa, hawatapata Virusi Vya Ukimwi.

Mhe. Magiri ametoa Elimu kwa Wavuvi wa Ziwa Nyasa na kuwataka waachane na uzushi wa Mganga huyo, ambaye ameingia katika Wilaya ya Nyasa,bila kufuata taratibu za kujisajili na kuwa na vibali kutoka kwa mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa.

Aidha ameliagiza jeshi la polisi Wilayani Nyasa kumuhoji mtuhumiwa na kumchukulia hatua za kisheria akipatikana na hatia.

Amefafanua kuwa Wavuvi wanatakiwa kuchukua Tahadhari juu ya Ugonjwa wa ukimwi ambao unaambukizwa kwa kufanya ngono bila kutumia kinga na kamwe hakuna mgamga ambaye anadawa za kutibu wala kuzuia ugonjwa wa UKIMWI.

Amewataka wavuvi kuzingatia maadili kwa kufanya kazi ya uvuvi kwa bidii na kamwe maneno ya mganga huyo ni ya kitapeli na hayanamashiko.

Hata hivyo baadhi ya wavuvi ya wamemshukuru na kumpongeza Mkuu wa wilaya ya Nyasa kwa kutoa ufafanuzi huo na kusema kuwa, hawamfahamu mganga huyo na hajawahi kuwapa dawa hizo na wanaelimu ya kutosha juu ya maambukizi ya virusi vya UKIMWI na wanaelewa umuhimu wa kufanya kazi kwa juhudi,wataendelea kuvua samaki na wataendelea kujikinga na gonjwa hatari la UKIMWI.

Mama mmoja na binti zake watatu walikuwa miongoni mwa watu saba waliouawa katika mji wa magharibi wa Ukraine wa Lviv, wa...
04/09/2024

Mama mmoja na binti zake watatu walikuwa miongoni mwa watu saba waliouawa katika mji wa magharibi wa Ukraine wa Lviv, wakati wa wimbi jipya la mashambulizi ya Urusi.
Mtoto mchanga na msichana mwingine pia waliuawa, maafisa walisema.

Meya wa Lviv Andriy Sadovy alisema Urusi iliishambulia kwa ndege zisizo na rubani na makombora ya hypersonic mapema Jumatano.

Shambulio hilo lilitokea wakati Ukraine ikijipata katika shambulio baya zaidi la Urusi mwaka huu - shambulizi dhidi ya taasisi ya kijeshi katika mji wa kati wa Poltava na kusababisha vifo vya watu 53.

Milipuko pia ilisikika siku ya Jumatano katika mji mkuu wa Kyiv huku ulinzi wa anga ukilenga makombora ya Urusi.
Watu watano walijeruhiwa huko Kryvyy Rih wakati hoteli iliposhambuliwa na vyumba vya karibu vya ghorofa kuharibiwa.

Shambulio la Lviv eneo la magharibi ya mbali ya Ukraine lilitokea wakati Ukraine yote ilikuwa chini ya tahadhari ya uvamizi wa anga.

Walioshuhudia walisema kuwa jiji hilo lililengwa takriban saa 05:40 kwa saa za eneo.

Wizara ya ulinzi ya Urusi ilisema kuwa ilifyatua makombora ya Kinzhal katika vituo vya ulinzi vya Ukraine huko Lviv na kwamba maeneo yote lengwa yalishambuliwa.

A Daytime Oasis with Gordon’s hosted by El-Casa: Sunsets, Sips, and Grooves at Livingstone’sAs the evening sun set, the ...
04/09/2024

A Daytime Oasis with Gordon’s hosted by El-Casa: Sunsets, Sips, and Grooves at Livingstone’s

As the evening sun set, the rooftop was curtained with a golden glow, which complimented the venue. There were twinkling blue lights and sunny yellow décor of photobooths and cocktail bars everywhere you looked, giving off major summer vibes and making everyone feel like they were living in a high-energy music video.

And don’t get me started on those cocktails! They were practically shouting “LOOK AT ME!”. The popsicle garnished green, yellow and red cocktails were so eye-catching! Whether you were in the mood for something sweet, tangy, or refreshingly cool, there was a cocktail that had your name on it.

Then the real magic happened as the sun set and the beats kicked in. The background music went from chill house vibes to a full-on summer soundtrack, with amapiano grooves that made your feet move whether you wanted them to or not. The DJ was on fire, spinning tracks that had everyone hitting the dance floor, and of course with your hosts being El-Casa, all the trendy socialites were there to show-off and looked the part.

It was one of those evenings where the vibe was so infectious, even the shyest of wallflowers couldn’t resist getting their groove on.

In short, the Gordon’s sundowners at Livingstone’s rooftop was a celebration of summer’s best—colorful, vibrant, and full of life. It was the kind of party that makes you forget about the world and just enjoy the moment. Here’s hoping for more nights like this one—where sunsets, sips, and summer beats come together to create the perfect evening, because, seriously, who wouldn’t want to do it all again?

If you weren’t at Livingstone’s rooftop for the Daytime Oasis last weekend, then you definitely missed out but YES you are in luck, because The El-Casa Boys are doing it all over again this month. YES! Let’s Bring BACK the DAY PARTIES with Gordon’s!

*TANZANIA KUJIIMARISHA ZAIDI KIDIPLOMASIA - MAJALIWA* WAZIRI MKUU  Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kujiimari...
04/09/2024

*TANZANIA KUJIIMARISHA ZAIDI KIDIPLOMASIA - MAJALIWA*

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itaendelea kujiimarisha kidiplomasia na itaongeza nguvu zaidi ili kuwawezesha Watanzania wengi kupata fursa mbalimbali katika jumuia za kimataifa.

Amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanikisha kuimarisha ushirikiano baina ya nchi washirika na sasa mafanikio yanaonekana.

"Rais wetu ameonesha nia njema katika kipindi chake cha miaka mitatu na nusu amefanya kazi kubwa ya kujenga diplomasia na mahusiano katika sekta mbalimbali na nchi nyingi duniani."

Ameyasema hayo leo (Jumatano, Agosti 4, 2024) alipokutana na Mkurugenzi Mkuu Mteule wa Shirika la Afya Duniani kanda ya Afrika (WHO) Dkt Faustine Ndungulie, Ofisini kwake Mlimwa Jijini Dodoma.

Jitihada hizo za Serikali ya awamu ya sita zimeiwezesha Tanzania kuendelea kupaa kidiplomasia kuiwezesha nchi kupata viongozi wakubwa ndani ya Taasisi za kimataifa.

"Tunaamini kazi kubwa tulizozifanya katika kipindi hiki cha miaka mitatu ya kumpata spika wa Umoja wa Mabunge duniani haikuwa kazi ndogo, na tena tumepata Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani kanda ya Afrika."

Aidha, Mheshimiwa Majaliwa amesema Serikali itaendelea kumuunga mkono Mkurugenzi huyo katika utekelezaji wa majukumu yake mapya.

"Wakati wote Waziri wa Afya atakuwa karibu nawe kuhakikisha kwamba sera zetu zinaenda sambamba na malengo ya WHO, kwa uwepo wako sisi lazima tuwe msitari wa mbele kuhakikisha kwamba tunakuunga mkono kwa mipango yetu ya afya ndani ya nchi."

Kwa upande wake Mkurugenzi huyo Mtarajiwa wa Shirika la Afya Duniani Kanda ya Afrika DKT. Faustine Ndungulile amemshukiru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumuunga mkono na kufanya ushawishi wa kidiplomasia ili kufanikisha ushindi huo.

"Kwa upekee sana ninamshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zake kubwa katika kufanikisha ushindi huu kwa ushawishi wake kwenye jumuia za kimataifa pia nawashukuru viongozi wengine wa Serikali, Bunge na wadau wote."

*Mwisho*

Rais Xi ameeleza kuwa "mwaka huu ni wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Chi...
04/09/2024

Rais Xi ameeleza kuwa

"mwaka huu ni wa maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya China na Tanzania, hivyo China inapenda kushirikiana na Tanzania katika kukuza na kuimarisha kwa kina ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili ili kuwanufaisha wananchi wa nchi mbili"

Rais Xi Jinping wa China leo amekutana na Rais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan huko Beijing kwa ajili ya kuhudhuria mkutano wa kilele wa mwaka 2024 wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC.

Takribani maafisa sita wa Ukraine, wakiwemo wajumbe wa baraza la mawaziri, wamejiuzulu nyadhifa zao kabla ya mabadiliko ...
04/09/2024

Takribani maafisa sita wa Ukraine, wakiwemo wajumbe wa baraza la mawaziri, wamejiuzulu nyadhifa zao kabla ya mabadiliko makubwa ya serikali yanayotarajiwa.

Kujiuzulu huku kunaacha baadhi ya nafasi za kazi serikalini zikiwa wazi, akiwemo waziri wa viwanda wa kimkakati anayehusika na utengenezaji wa silaha.

Mabadiliko hayo yanakuja huku kiongozi wa bunge wa chama tawala cha Servant of the People akisema nusu ya baraza la mawaziri litabadilishwa katika mabadiliko makubwa ya serikali wiki hii.

Mabadiliko hayo yanakuja wakati Ukraine inaendelea kukabiliana na mashambulizi ya kila siku ya Urusi katika miji yake, na inajitahidi kuzuia mafanikio ya Moscow katika eneo la mashariki.

Waliowasilisha kujiuzulu kwao siku ya Jumanne ni pamoja na waziri wa viwanda vya kimkakati Alexander Kamyshin, waziri wa sheria Denys Maliuska, waziri wa ulinzi wa mazingira Ruslan Strilets, naibu waziri mkuu Olha Stefanishyna na Iryna Vereshchuk.

Mmoja wa wasaidizi wakuu wa rais, Rostyslav Shurma, pia alifukuzwa kazi k**a kwa amri ya rais.

Wongel Zelalem anaripoti kuhusu rRais wa Burkina FasoIbraim Traore akisema haogopi kufa licha yakupokea vitishk vingi ku...
03/09/2024

Wongel Zelalem anaripoti kuhusu rRais wa Burkina Faso
Ibraim Traore akisema haogopi kufa licha yakupokea vitishk vingi kutoka kwa mataifa makubwa yenye Nguvu zakijeshi.

Iran Huenda Ikaanza kusambaza Makombora ya Balestiki kwa Urusi siku za usoni, Bloomberg inaripoti, ikinukuu vyanzo vya h...
03/09/2024

Iran Huenda Ikaanza kusambaza Makombora ya Balestiki kwa Urusi siku za usoni, Bloomberg inaripoti, ikinukuu vyanzo vya habari.

Iran tayari imeipatia Urusi mamia ya ndege zisizo na rubani za Shahed, ambazo hutumiwa kila siku na wanajeshi wa Urusi kushambulia miji ya Ukraine.

Mapema mwaka huu, shirika la habari la Reuters liliripoti kuwa Tehran huenda ilihamisha takribani makombora 400 ya balistiki hadi Moscow.

Vyanzo vya Bloomberg havikufichua muda , aina ya makombora au ukubwa wa usafirishaji, ingawa mmoja wao alisema kuwa usafirishaji unaweza kuanza ndani ya siku chache.

Marekani na washirika wa NATO wameionya mara kwa mara Tehran dhidi ya hatua hiyo na wamefanya juhudi za kidiplomasia kuizuia, shirika hilo linabainisha.

Baraza la Usalama la Kitaifa la White House halikujibu mara moja kuhusu hilo. Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran na ujumbe wake katika Umoja wa Mataifa pia haikusema chochote.

Marekani imek**ata ndege ya Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro, ikidai ilinunuliwa kinyume cha sheria kwa Dola milioni 13...
03/09/2024

Marekani imek**ata ndege ya Rais wa Venezuela, Nicolas Maduro, ikidai ilinunuliwa kinyume cha sheria kwa Dola milioni 13 [TZS bilioni 35.4] na kutoroshwa nje ya nchi.

Wizara ya Sheria ya Marekani imesema ndege hiyo aina ya Falcon 900EX ilik**atwa katika Jamhuri ya Dominika na kuhamishiwa jimbo la Florida nchini Marekani.

Hata hivyo, Venezuela imeshutumu unyakuzi huo, ikisema kitendo hicho ni sawa na uharamia.

Serikali Kupitia wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA imefanikiwa kuongeza mtandao wa Barabara za Wilaya kuto...
02/09/2024

Serikali Kupitia wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA imefanikiwa kuongeza mtandao wa Barabara za Wilaya kutoka kilomita 108,946,19 Hadi kilomita 144,429,77

Mtendaji mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff Ameyasema hayo Leo September 2,2024 jijini Dar es salaam Katika kikao kazi Cha wahariri na waandishi wa habari chini ya uratibu wa ofisi ya Msajili wa Hazina TR

Mhandisi Seff Amesema kuwa mtandao wa Barabara hizo zimegawanyika Katika makundi matatu ikiwemo za Lami, Changarawe, na Udongo

Amesema Hadi kufikia Juni,2024 barabara za Lami za Wilaya zilikuwa kilomita 3,337,66 sawa na Asilimia 2.31

Kati ya hizo Mhandisi Seff Amebainisha kuwa hali ya barabara hizo kilomita 2,743,81zipo Katika hali nzuri, kilomita 445,18 zipo Katika hali ya wastani huku kilomita 148,68 zikiwa Katika hali mbaya.

Kwa upande wa Barabara za Changarawe Mhandisi Seff Amesema kuwa ni jumla ya kilomita 42,059,17 sawa na Asilimia 29,12

Akizungumzia hali ya barabara hizo za Changarawe, Mhandisi Seff Amesema Kilomita 21,890,53 zipo Katika hali nzuri kilomita 15,792,23 zipo Katika hali ya wastani huku kilomita 4,426,41 zikiwa Katika hali mbaya.

Vilevile Kwa upande wa Barabara za Udongo Mhandisi Seff Amesema ni jumla ya kilomita 99,032,93 ni sawa na Asilimia 68,57

Amesema kati ya barabara hizo za Udongo kilomita 16,118,65 zipo Katika hali nzuri kilomita 34,739,20 zipo Katika hali ya wastani huku kilomita 48,175,09 zikiwa Katika hali mbaya.

Nyangumi aina ya ‘beluga’ anayeshukiwa kupewa mafunzo ya kijasusi na Urusi amepatikana amefariki katika pwani ya Norway....
02/09/2024

Nyangumi aina ya ‘beluga’ anayeshukiwa kupewa mafunzo ya kijasusi na Urusi amepatikana amefariki katika pwani ya Norway.

Mwili wa mnyama huyo - kwa jina la utani Hvaldimir - ulipatikana ukielea karibu na mji wa kusini-magharibi wa Risavika na kupelekwa kwenye bandari ya karibu kwa uchunguzi.

Nyangumi huyo alionekana kwa mara ya kwanza katika maji ya Norway miaka mitano iliyopita, akiwa na kamera ya GoPro iliyofungwa katika hatamu yenye maneno "Vifaa vya St Petersburg."

Mwili wa Hvaldimir uligunduliwa mwisho wa wiki na Marine Mind, shirika ambalo limefuatilia mienendo yake kwa miaka mingi.

Mwanzilishi wa Marine Mind, Sebastian Strand ameliambia shirika la habari la AFP, chanzo cha kifo hakijajulikana na mwili wa Hvaldimir haukuwa na majeraha yoyote.

Anakisiwa kuwa na umri wa miaka 15, Hvaldimir hakuwa mzee kwa nyangumi aina ya Beluga, ambao maisha yao yanaweza kufikia miaka 60.

Alikaribia boti za Norway kwa mara ya kwanza Aprili 2019 karibu na kisiwa cha Ingoya, karibu kilomita 415 (maili 260) kutoka Murmansk ambapo Meli ya Kaskazini ya Urusi iko.

Kuonekana kwake kulisababisha uchunguzi wa shirika la ujasusi la ndani la Norway, ambalo baadaye lilisema kuna uwezekano nyangumi huyo amefunzwa na jeshi la Urusi kwani alionekana kuwazoea wanadamu.

Urusi ina historia ya kutoa mafunzo kwa mamalia wa baharini k**a vile pomboo kwa madhumuni ya kijeshi. Lakini haijawahi kujibu rasmi madai kwamba Hvaldimir huenda alifunzwa na jeshi lake.

Wakati ajali hiyo inatokea, meli ya Titanic ilikuwa ikitoka Southampton, Uingereza kuelekea New York, Marekani, kwa mwen...
02/09/2024

Wakati ajali hiyo inatokea, meli ya Titanic ilikuwa ikitoka Southampton, Uingereza kuelekea New York, Marekani, kwa mwendo wa kilomita 41 kwa saa, na ndani ya saa tatu tu, Titanic ilizama katika bahari ya Atlantic usiku wa kuamkia Aprili 14. na 15, 1912.

Meli hiyo ambayo ilisemekana kuwa haijawahi kuzama ilizama. Takriban watu 1500 pia walikufa katika ajali hiyo. Inachukuliwa kuwa ajali kubwa zaidi ya baharini hata baada ya miaka 110.

Mabaki hayo yaliondolewa kwenye eneo la ajali mnamo Septemba 1985. Baada ya ajali hiyo, meli hiyo ilivunjika vipande viwili katika kina cha mita 3,843, kilomita 650 kutoka Canada, na sehemu hizo mbili zilikuwa umbali wa mita 800 kutoka kwa kila mmoja.

Ilisemekana kuhusu meli hii kubwa kwamba haiwezi kuzama, hata Mungu hawezi kuizamisha. Kulikuwa na sababu za imani hii pia.

Alexander de Pinho Alho, profesa na mhandisi katika Idara ya Uhandisi wa Majini na Bahari katika Chuo Kikuu cha Rio de Janeiro, alisema, "Katika suala la uhandisi, ilikuwa meli ya kwanza kutengenezwa kwa msingi wa muundo.

Sehemu kadhaa za kuzuia maji zilijengwa. ndani ya meli. Yaani ikiwa chumba kimoja cha meli kilijazwa maji, hakingeweza kuzamisha chumba kingine."

Kulikuwa na matatizo fulani wakati wa maandalizi ya meli hii, kulikuwa na mawazo mengi juu ya kiasi gani urefu wa meli unapaswa kuwekwa, ili waya za umeme na mabomba ya maji yaendelee kufanya kazi vizuri.

Urusi imerusha msururu wa makombora katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, saa chache kabla ya maelfu ya watoto kurejea shule...
02/09/2024

Urusi imerusha msururu wa makombora katika mji mkuu wa Ukraine, Kyiv, saa chache kabla ya maelfu ya watoto kurejea shuleni kwa siku ya kwanza ya mwaka wa masomo.

Meya, Vitali Klitschko, anasema kiwanda cha kutibu maji na mlango wa kituo cha metro kinachotumika k**a makazi vilipigwa. Shule mbili na chuo kikuu pia ziliharibiwa.

Kulingana na jeshi la Ukraine, makombora 22 ya baharini na ya anga yaliharibiwa na jeshi la anga.

Mamlaka ya eneo hilo inasema watu watatu walijeruhiwa na vifusi kutoka kwa makombora yaliyoharibiwa.

Kwa watoto wa shule katika mji mkuu, shambulio hilo la Jumatatu liliambatana na siku ya kwanza ya mwaka wa shule, siku ya sherehe nchini Ukraine.

Walimu na wazazi walijaribu kuweka hali ya kawaida, huku muziki ukicheza huku wanafunzi wakitabasamu walikaribishwa na bahari ya maua.

Mzazi mmoja, ambaye alijificha na bintiye nyumbani wakati wa shambulio la kombora kabla ya kumpeleka shuleni, alisema walikuwa wakionyesha kwa mara nyingine "kwamba taifa hili haliwezi kushindwa".

"Watoto wanatabasamu, lakini unaweza kuona mkazo katika nyuso za walimu wao [ambao] wanabeba mzigo huu", aliiambia BBC.

"Ninawashukuru sana kwa yote waliyofanya kuifanya kuwa likizo ya kweli kwa watoto."

Kwa Yevheniia mwenye umri wa miaka 33, ambaye alikuwa akimpeleka shuleni bintiye mwenye umri wa miaka sita kwa mara ya kwanza, siku hiyo ilitawaliwa na hofu.

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, ametoa wito kwa wataalamu wa tiba asili nchini kuachana na matumizi ya viungo ...
02/09/2024

Naibu Waziri wa Afya, Dkt. Godwin Mollel, ametoa wito kwa wataalamu wa tiba asili nchini kuachana na matumizi ya viungo vya binadamu na wanyama katika huduma zao, akisema kuwa dhana potofu zinazohusisha ngozi ya nyati, simba, na mkia wa nyumbu zinapaswa kukemewa kwa nguvu zote.

Kauli hiyo imetolewa wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Tiba Asili Kitaifa yaliyofanyika jijini Mwanza yaliyo ratibiwa na Wizara ya afya chini ya baraza la tiba asili na tiba mbadala.

“Tunahitaji kuondokana na imani hizi potofu ili kunusuru maisha ya wanyama pamoja na binadamu. Hakuna sababu ya kuendeleza matumizi haya ya viungo vya wanyama kwa kuwa ni hatari kwa mazingira na ustawi wa binadamu, Sisi sote tunapaswa kukemea vitendo hivi, kulinda mazingira, na kuhakikisha kwamba tunafichua wenye vitendo viovu”. Amesema Dkt. Mollel

Aidha, Dkt. Mollel ameitaka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kufanya tafiti za kina kwa wataalamu wa tiba asili kwani NIMR inapaswa kufanya tafiti za kina kuhusu vyanzo vya dawa zinazotumika na kuhakikisha kuwa zinatunzwa vizuri na kuendelea kuzalishwa kwa wingi

Kwa upande mwingine, Kaimu Mganga Mkuu, Dkt. Ahmad Makuwani, amekiri kuwa dawa zinazozalishwa na wataalamu wa tiba asili zimefanya maendeleo makubwa, huku mataifa mengine k**a Angola yakizisajili k**a dawa rasmi kwa matumizi ya binadamu.

Kilele cha maadhimisho haya kimewakutanisha waganga wa jadi na wataalamu wa tiba asili, huku kikiwa na lengo la kuboresha huduma za tiba asili na kutetea haki za wanyama katika utendaji wa tiba hizi.

Address

Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when MwanaHabari Digital posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to MwanaHabari Digital:

Videos

Share

Category


Other TV Channels in Dar es Salaam

Show All