13/07/2020
Dkt Hussein Ally Mwinyi ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa katika Serikali ya Awamu ya Tano Dkt Hussein pia ni mbunge wa jimbo la Kwahani huku Unguja Zanzibar.
:
Dk Hussein Mwinyi Alizaliwa Disemba 23, 1966 kwenye kisiwa cha Unguja, Zanzibar. Dk Mwinyi ni mtoto wa Mzee Ali Hassan Mwinyi (Rais wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) na mama Sitti Mwinyi ambaye amekuwa (First Lady) katika awamu ya pili.
:
elimu ya msingi amesoma jijini Dar es Salaam kati ya mwaka 1972 – 1976 akisoma katika Shule ya Msingi Oysterbay. Mwaka 1984 hadi 1985 wazazi wake walimhamishia Misri ambako aliendelea na masomo ya elimu ya msingi hadi kuhitimu katika Shule ya Msingi “Manor House Junior”.
:
Dkt Hussein Mwinyi alirejea Tanzania na kuendelea na masomo ya sekondari katika Shule ya Sekondari Azania ambako alisoma kidato cha kwanza hadi cha nne mwaka 1982 – 1984. Alipohitimu kidato cha nne alifaulu na kupangiwa Shule ya Sekondari Tambaza kusoma kidato cha tano na cha sita, hata hivyo aliishia kusoma kidato cha tano peke yake mwaka 1984/1985, mwaka huo huo 1985 alienda nchini Uturuki kusomea utabibu wa binadamu. Alianza masomo ya udaktari nchini Uturuki mwaka 1985 kwenye Shule ya Utabibu ya Chuo Kikuu cha Marmara na kuhitimu Shahada ya Utabibu wa Binadamu mwaka 1992.
:
Mwaka 1993, Mwinyi alikwenda nchini Uingereza kujiendeleza zaidi kielimu, aliendelea na masomo ya juu ya utabibu katika Hospitali ya Hammersmith ambako alihitimu shahada ya uzamili ya utabibu mwaka 1994 na kuunganisha shahada ya uzamivu ya udaktari hapohapo Hammersmith ambayo aliihitimu mwaka 1997.
:
Dkt Mwinyi amefanya kazi za kidaktari hapa Tanzania mwaka mmoja katika Hospitali ya Taifa Muhimbili na akafanya kazi katika hospitali ya Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Herbert Kairuki (HKMU) kwa miaka miwili hadi mwaka 1999.
:
Kwenye siasa aliingia mwaka 1999 akiliwania Jimbo la Mkuranga mkoani Pwani (Bara) na kushinda. Alipokuwa mbunge, Rais Benjamin Mkapa alimteua kuwa Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, alikaa katika wadhifa huo hadi mwaka 2005.
:
Kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 Dk Mwinyi akagombania jimbo la Kwahani, Zanzibar akashinda jimbo la Kwahani Zanzibar Baada ya kuwa mbunge kwa mara ya pili, Serikali ya Awamu ya Nne ilimteua kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais na alidumu hadi mwaka 2008 alipohamishiwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa alikokaa hadi mwaka 2010.
:
Mwinyi alirejea tena na kugombea ubunge katika jimbo la Kwahani mwaka 2010, akashindana tena Mara baada ya uchaguzi wa mwaka 2010 Rais Kikwete akamteua Mwinyi kuwa Waziri wa Ulinzi kabla ya kumrejesha Wizara ya Afya mwaka 2012 na miezi 19 baadaye (yaani Januari, 2014) kwa mara nyingine tena akamteua kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, nafasi aliyodumu hadi mwaka 2015.
:
Katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, Dk Mwinyi alirudi tena katika jimbo la Kwahani, hii ikiwa ni mara ya nne akashinda tena na kuchaguliwa kuwa mbunge kwa kipindi cha nne. Rais JPM amemteua Mwinyi kuwa Waziri wa Ulinzi na Kujenga Taifa na hivyo kumuongezea rekodi ya kuongoza wizara hiyo kwa kitambo cha kutosha.
:
Dk Mwinyi ni wawaziri mwenye rekodi za kuwa na shahada tatu za ubobezi wa taaluma na elimu ya juu katika fani moja. Amesoma kwa uhakika na ni mtu mwenye uwezo wa kutumia stadi za ubobezi wake kujenga weledi wa jumla unaomfanya atoe uongozi wa kudumu hadi hivi
:
Jambo la pili ni uzoefu wa kibunge wa miaka 20 unaoambatana na uzoefu wa uwaziri kwa miaka 15. Mwinyi ana rekodi nyingine tena, ni kati ya wabunge walioweza kukaa bungeni kwa vipindi vitatu mfululizo (2000 – 2020). Huyu ni mmoja kati ya viongozi wa zama za sasa waliokaa muda mrefu kwenye utumishi wa ngazi ya juu na ikumbukwe kwamba muda wote huo amekuwa kwenye nafasi za uwaziri. Uzoefu wake wa pamoja unamtofautisha na mawaziri wengine wengi wanaojifunza kazi na huwenda ukamjengea kujiamini zaidi na kufanya vizuri zaidi.