Nedy official Media

Nedy official Media Professional journalist📻📺
Mlimani Radio🎙️
Sports analysis⚽
UDSM Alumin🥇

_Ubora mkubwa wa Medeama ni usahihi wa matendo wakiwa na Mpira"Passing" pamoja na nguvu ya upambanaji "intensity" (Hapa ...
07/12/2023

_Ubora mkubwa wa Medeama ni usahihi wa matendo wakiwa na Mpira"Passing" pamoja na nguvu ya upambanaji "intensity" (Hapa naona nafasi ya Mudathir)

_hawana safu bora Sana ya ushambuliaji pia hawana safu bora Sana ya ulinzi, michezo mitano ya mwisho wamefunga mabao 3,wameruhusu mabao 6.

Nadhani ni mchezo sahihi kabisa Yanga kwenda kutafuta alama 3

Next;YangaSc vs MedeamaSimbaSc vs Wydad
06/12/2023

Next;
YangaSc vs Medeama
SimbaSc vs Wydad

Darasa huru 📌
05/12/2023

Darasa huru 📌

03/12/2023
Next gameMedeama vs YangaSc
02/12/2023

Next game
Medeama vs YangaSc

Pamoja na ubora wa mpango kazi wa Galaxy katikati eneo la uzuiaji (Compactness), lakini Simba walifanikiwa kutengeneza n...
02/12/2023

Pamoja na ubora wa mpango kazi wa Galaxy katikati eneo la uzuiaji (Compactness), lakini Simba walifanikiwa kutengeneza nafasi lakini wakakosa "Utulivu" Ili kutoa adhabu.

Yule fullback Mangolo 🔥

Bila shaka Simba wanahitaji kuwa Bora Sana eneo la ulinzi kuelekea mchezo wa kesho.
01/12/2023

Bila shaka Simba wanahitaji kuwa Bora Sana eneo la ulinzi kuelekea mchezo wa kesho.

You must tell your self, no matter how hard it gets, I will make it....Mafanikio yetu yamejificha kwenye juhudi na bidii...
30/11/2023

You must tell your self, no matter how hard it gets, I will make it....

Mafanikio yetu yamejificha kwenye juhudi na bidii sio kipaji Wala vyeti, KESHO TENA BILA KUCHOKA.

MUDA NA NAFASI:1.Asilimia kubwa ya Vilabu  vyenye mafanikio vinaishi kwenye muda na nafasi Kwa Makocha._Pep Guardiola (M...
29/11/2023

MUDA NA NAFASI:

1.Asilimia kubwa ya Vilabu vyenye mafanikio vinaishi kwenye muda na nafasi Kwa Makocha.

_Pep Guardiola (Man city)
_Carlo Ancelott (Real Madrid)
_jurgen Klopp (Liverpool)
_Pitso Mosimane (Al Ahly)
_Rhulan Mokwena (Mamelod)
_Patrice Carteron (TP Mazembe)

Hawa ni miongoni mwa makocha waliopewa nafasi na vilabu vyao na wakavipa mafanikio. Kila kocha hapo amekaa misimu mitatu na kuendelea!!.

Wenzetu wanaamini Kuna sehemu nyingi za kuboresha badala ya benchi la ufundi, wanaamini kuna maeneo mengi ya kuboresha kwenye taasisi kabla ya Kocha.

Mfano kwenye Miaka takribani saba ya Pep akiwa analitafuta taji la UEFA. Man City hawakuamini Pep Hana uwezo wa kucheza mashindano hayo ila waliendelea kumuboresheshe miundombini ya kazi ikiwemo wachezaji Bora Kila atakao wapendekeza Kwa Kila musimu, Hatimaye anatengeneza timu bora chini ya falsafa yake inaenda kubeba taji la UEFA (MUDA NA NAFASI).

Klopp wakati anatua pale Liverpool mwaka 2016 Alikuwa vipigo Sana lakini Liverpool waliamini kwenye (MUDA NA NAFASI) Hatimaye klopp anaenda kubeba UEFA champions league na taji la EPL mbele ya Pep.

Mokwena akiwa na kikosi Bora pale mamelod anatupwa nje ya mashindano msimu uliopita kwenye uwanja wake wa nyumbani lakini Mamelod waliamini kwenye (MUDA NA NAFASI) Hatimaye mokwena anaenda kushinda Africa Super League.

Kufanya vibaya Kwa klabu kunaweza kuwa na changamoto nyingi ndani ya taasisi, bahati mbaya tumeamua kuchagua kuwatoa makocha kafara na kuyaficha madhaifu mengine mengi. risk!!

Nadhani ni wakati Sasa timu ikifanya Vibaya kabla ya kocha basi inatakiwa kuwa na majibu ya maswali yafuatayo÷
_je taasisi imetimiza wajibu wake Kwa 100% ( Sajili bora, mazingira bora Kwa wachezaji - posho na mishahara n.k)!?
_je kocha amepewa miundombini yote anayo stahili (Wachezaji bora, Uhuru, Muda n.k)!?

Bahati mbaya tumechagua kwenda mbele kabla ya majibu. We need to change!!.

Concern
1. Viongozi watimize wajibu wao (Sajili bora, mazingira mazuri Kwa wachezaji, uhuru Kwa Mwalimu n.k)

2. Mwalimu ABDELHAK BENCHIKHA apewe MUDA NA NAFASI.

Football = Uwekezaji imara - Uongozi imara - Benchi la ufundi imara - wachezaji imara.

All the best Benchikha all the best SimbaSc.

Simba:Leo ni k**a Simba waliendelea waliposhia Kwa kuendelea kuonyesha madhaifu Yao zaidi.Udhaifu wa Simba kiwanjani1.In...
25/11/2023

Simba:
Leo ni k**a Simba waliendelea waliposhia Kwa kuendelea kuonyesha madhaifu Yao zaidi.

Udhaifu wa Simba kiwanjani
1.Intensity, Simba wamekuwa dhaifu Sana pale wanapokuwa hawana Mpira na hata wakiwa na Mpira.

Wakiwa hawana Mpira:
_ huoni nguvu au juhudi yoyote ya wachezaji kutaka kurudisha Mpira kwenye himaya Yao!! Mara nyingi hii inatoka na fitness level (wachezaji kuto kuwa sawa kimwili na kiakiri) au sababu za nje ya uwanjani.

Wakiwa na Mpira:
_mara nyingi passing Yao ni mbovu, wanapoteza Sana Mpira kitu ambacho ni hatari kwani unampa mpinzani nafasi ya kufanya quick transmission au turn over, hii mara nyingi inasababishwa na kukosa utulivu, kukosa kujiamini au quality ya mchezaji.
_wakiwa na Mpira pia huoni wakifanya movement za kutisha quick transition kuhakikisha wanamlazimisha mpinzani anafanya makosa kwenye eneo lake Ili watoe adhabu.

Leo intensity ya Simba kiwanjani ilikuwa chini Sana ( huwaoni wachezaji wakijituma kuutaka mchezo) ukiachana na changamoto ya tactics ni wachezaji wachache Sana ambao wamejituma na kutimiza majukumu Yao Kwa 100%.

2. Tactics
Bado Simba wanahitaji Sana kiungo halisi mkabaji (DM) mwenye game determination... Ambaye anaweza kuamua timu ichezeje hasa pale inapozidiwa. Nadhani Leo Mwalimu alilazimika kumtumia Che Malone kulingana na wale waliopo kuona hawatoshi kwenye eneo Hilo Kwa 100%

Asec Mimosas
Ubora
_walikuwa Bora Sana eneo la kiungo hasa uwezo wao wa ku posses Mpira na kupiga pasi zenye uhakika huenda hii ilitokana na udhaifu wa Simba eneo la kiungo.
_walikuwa Bora Sana pia kwenye utimamu wa mwili iliwapa ugumu Sana Simba kukabiliana kwenye physical bato.

Udhaifu:
_Walishindwa kuwa katili kwenye lango la mpinzani mara nyingi hii inatoka na pressure pia kukosa utulivu Kwa washambuliaji

Nadhani Asec walistahili kupata matokeo!!

Israel Mwenda + Kibu 🔥

NB: Nadhani Simba wadili na utimamu wa wachezaji kimwili na kiakiri Hali yao ya umbanaji Iko chini sana ndani ya kiwanja.

YANGA_Ubora1. Yanga walikuwa Bora Sana kwenye upande wa team work..., Kila mchezaji amemwaga jasho kadri ya uwezo wake. ...
24/11/2023

YANGA
_Ubora
1. Yanga walikuwa Bora Sana kwenye upande wa team work..., Kila mchezaji amemwaga jasho kadri ya uwezo wake. Well done!!

2. Yanga walikuwa Bora Sana wakati ambao hawakuwa na Mpira (pressing), ni siraha muhimu Sana kwenye Mpira Ili kumnyima mpinzani utulivu na nafasi ya kumiliki Mpira, Yanga Walifanya hivyo Kwa ubora mkubwa. Well done!!

3. Yanga walijaribu Sana kutengeneza nafasi lakini bahati na ubora wa safu ya ulinzi ya RC Blouizdad (Compactness+Concentration) uliwanyima nafasi ya kufunga mabao.

_Udhaifu
1. Concentration wakati wa uzuiaji, Kuna nyakati Yanga wakiwa wanashambulia Huwa wanajisahau kujilinda ... Kana kwamba mpinzani anapofanya transition au turn over anawakuta hawapo kwenye shape nzuri ya kujilinda. Risk!!!.
Bao la pili ilikuwa 2 against 2 walinzi wawili na washambuliaji wawili Kwa namna hiyo ni ngumu kuto adhibiwa unapokutana na wachezaji wenye quality kubwa. Bao la tatu piah Yanga wakiwa wanashambulia, inapigwa counter ya haraka kabla hawajarudi kwenye shape nzuri ya uzuiaji wanaadhibiwa.

2. Passing, Yanga asilimia kubwa walikuwa Bora sana kwenye passing, asilimia chache ya passing Yao mbovu inawaghalimu hasa kwenye maeneo ya hatari!!, wanahitaji uhakika zaidi wa pasi zao. nadhani hii Kuna muda unatokana na over Confidence!!.

Ni madhaifu ambayo ni muhimu kuendelea kuyafanyia kazi!!

RC Belouizdad
1.walikuwa Bora Sana kwenye usahihi na ufanisi kuanzia kuzui, ulikuwa huoni wakipoteza concentration hata wakati wa kushambulia Bado walibaki na idadi kubwa ya watu nyuma. Well done!!

2. Ufanisi eneo la ushambuliaji nafasi chache na udhaifu wa mpinzani walihakikisha wanatumia vizuri.

Nadhani RC Blouizdad walistahili kupata matokeo!!!

Bacca, Pacome + Aucho🔥🔥🔥

Mamadou Samake 🔥

CR Belouizdad 3_0 YangaSc

Nadhani Kuna sehemu tunajisahau !!1.Mpira ni taaluma k**a taaluma nyingine, ni k**a taaluma ya ualimu au taaluma ya udak...
07/11/2023

Nadhani Kuna sehemu tunajisahau !!

1.Mpira ni taaluma k**a taaluma nyingine, ni k**a taaluma ya ualimu au taaluma ya udaktari nk., Thus why Kuna Course nyingi About football!.

Bahati mbaya tumeamua kuchagua njia tofauti.... Ni rahisi tu mtu asiye na taaluma yoyote kuhusu Mpira wa miguu akapewa nafasi kwenye tasinia au taasisi ya Mpira wa miguu. We need to change!!, football is professional!!.

Ndiyo maana kwenye klabu inatakiwa kuchagua viongozi wachache wenye taaluma na weredi wa Mpira.

_Ni ajabu Sana kumpa dhamana ya kuongoza Mpira mtu ambaye Hana taaluma ya Mpira
_Ni ajabu Sana kumpa nafasi kwenye maamuzi mtu ambaye hana weredi wa Mpira.
Football is professional!!!...

2.Kwenye football Kuna vitu vingi Sana ... Football haianzi pale kiwanjani, have Alot of things kuanzia management.....

(sisi tumeamua kuchagua kuangalia kiwanjani tu) risk!!!!

Cristiano Ronaldo wakati anaondoka Man U alisema shida ya Man U haoni k**a wanaenda na ulimwengu wote wa kisasa (uendeshaji, chakula, technology nk) ilikuwa ngumu Kwa watu wengi kumwelewa kuliko k**a angesema tatizo ni Ten Hag!!!.

Ni ngumu kumuunga mkono Mo Dewji akilia kuhusu uendeshaji ni rahisi kuunga mkono bodi kumtimua Robertinho, hii ni mpaka pale tutakapo jua hatui!!.

Nadhani yanga kabla ya kucheza karata nzuri uwanjani walicheza karata nzuri kwenye ulimwengu wote wa kisasa.(uendeshaji, technology, Hali nk).

Dokta mmoja wa football analyst aliwahi kusema "football is game of intelligence people" akiwa na maana fupi Ya Mpira hakuna kukisia ni mchezo wa watu wanao uandika na kisoma.

Nadhani K**a Robertinho alikuja Kwa ajili ya kuifunga Yanga ni sahihi kuondoka k**a alikuja Kwa ajili ya kuipa timu matokeo mazuri hakustahili kuondoka.

Tangu atue Simba
Win 22
Loose 6
Draw 6

Robo fainali klabu Bingwa
Nusu fainali ASFC
Champion ngao ya jamii 🏆

Football is game of intelligence people!
Paul Mkaizthabith chumwi zakariaiGeorge AmbangileeGeoffrey LeaaGodlisten MurooPrisca kishambaa@simbasctanzania Tindwaa

.
06/11/2023

.

 ......
02/10/2023

......

Sjajua ni fitness level au ni aina ya uchezaji lakini Leo Simba Hali ya upambanaji ilikuwa chini Sana!!.Nadhani linataki...
01/10/2023

Sjajua ni fitness level au ni aina ya uchezaji lakini Leo Simba Hali ya upambanaji ilikuwa chini Sana!!.

Nadhani linatakiwa kufanyiwa kazi mapema, hata ukiwa na wachezaji wazuri lakini''intensity' ni muhimu Sana kwenye football......

Nadhani Singida Fountain Gate Fc Wana mchezo mgumu  Leo dhidi ya Future Fc, kuna nyakati Ili kukabiliana na mpinzani bor...
01/10/2023

Nadhani Singida Fountain Gate Fc Wana mchezo mgumu Leo dhidi ya Future Fc, kuna nyakati Ili kukabiliana na mpinzani bora unahitaji tu kufanya Kila kitu Kwa usahihi kiwanjani.

_kimbia KM nyingi kiwanjani, weka pressure kwenye Mpira kumnyima mpinzani utulivu na wepesi wa kutengeneza nafasi.

_win second bolls kupunguza risk ya kutengenezewa tukio(Shots/turn over).

_High concentration wakati wa uzuiaji(sharpness, fitness, mentally& physical fit).

_Epuka makosa yasiyo na ulazima (Faulos, kupoteza pasi, chenga zisizo na ulazima)

_Toa adhabu panapo stahili(skills, utulivu)

Kwenye football pia Kuna nyakati Haina ulazima wa kumiliki sana Mpira , utahitaji tu mkakati sahihi wa kupata matokeo (Counterattack, set pieces, Long bolls, shots)

All the best

Future Fc vs Singida Fountain Gate 🔥
12:00 jioni.

Power Dynamo michezo minne ya mwishoWamefunga bao 8Wamefungwa bao 5 Simba michezo minne ya mwishoWamefunga bao 11Wamefun...
01/10/2023

Power Dynamo michezo minne ya mwisho
Wamefunga bao 8
Wamefungwa bao 5

Simba michezo minne ya mwisho
Wamefunga bao 11
Wamefungwa 4

Ndiyo namba zinambeba Simba kuelekea mchezo wa kesho

Concern:
1.Power Dynamo michezo minne bao nane maana yake Wana wastani wa kufunga bao mbili kwenye Kila mchezo, zile bao mbili pale ndola hawakubahatisha Wana safu ya kufanya hivyo.

Kuelekea mchezo wa kesho Simba wanatakiwa kujua wanacheza na timu yenye wastani wa kufunga bao kwenye Kila mchezo, hivyo wanahitaji kuboresha safu ya ulinzi

ili kukabiliana na safu Bora ya ushambuliaji unahitaji kuzingatia principal of defending ÷

_Compactnes,unahitaji kuwa na watu wengi kwenye eneo lako na ukaribu baina ya mchezaji na mchezaji Ili kumnyima mpinzani wepesi wa kutengeneza nafasi za wazi na kumnyima Uhuru wa kufanya movement ambazo zinaweza kuwa na madhara.
Covering,wakati wa kuzuia unahitaji sharpness ya ku cover space inayoachwa na mchezaji mmoja, mfano kapombe amesogea juu inahitaji mmoja kati ya CB/DM kucover space yake Au mfano Malone ameenda ku offence inahitaji DM/FB ku cover nafasi yake.
Pressing,wakati wa kuzuia unahitaji kuweka pressure kubwa kwenye Mpira Ili kumnyima utulivu wa kufanya maamuzi sahihi mpinzani na kupoteza Mpira then kunirudisha kwenye himaya yako.

2.Power Dynamo Wana wastani wa kuruhusu goli kwenye Kila mchezo maana yake hata kesho Wanaweza kuruhu pia k**a Simba watakuwa Bora eneo la ushambuliaji.

Miongoni mwa principal za ushambuliaji ni÷
_Support,Mchezaji mmoja anapo move na Mpira anahitji support ya movement ya wachezaji wengine ambao watampa option nzuri ya wapi Mpira aupeleke.
JOHN CRUYFF aliwahi kusema "mchezaji asie na Mpira ndiye ataamua wapi Mpira uelekee!?.

_Create Space (width, length and depth) unahitaji kutanua uwanja Ili ku separate safu ya ulinzi ya mpinzani na kupata space za kushambulia

Simba Wana wastani mzuri wa kufunga hivyo kesho Wana nafasi ya kufunga pia wanahitaji kuwa Bora eneo la ushambuliaji

Simba Wana wastani wa kuruhu bao, hivyo kesho pia wanaweza kuruhusu, wahitaji kuzingatia Sana principal za uzuiaji!.

Simba vs Power Dynamo 🔥.


Yanga vs El Merrikh 🔥🔥🔥19:00 usiku.
29/09/2023

Yanga vs El Merrikh 🔥🔥🔥
19:00 usiku.

Future is bright....
24/09/2023

Future is bright....

Man City kwenye premier league msimu huu 2023_2024.🔵 Game: 6✅ Win: 6⚽ Goals: 16❌ Conceded: 3💎 Point: 18/18Miongoni mwa v...
23/09/2023

Man City kwenye premier league msimu huu 2023_2024.
🔵 Game: 6
✅ Win: 6
⚽ Goals: 16
❌ Conceded: 3
💎 Point: 18/18

Miongoni mwa vitu ambavyo Pep Guardiola amekuwa aki win ni jinsi ambavyo amekuwa akifanya sajili.

Kuna nyakati huhitaji mchezaji bora ila unahitaji mchezaji kulingana na uhitaji wa timu na falsafa ya timu.

Kuna nyakati huhitaji kuingia kwenye soko la ushindani kutafuta wachezaji Bora, unahitaji kuwa na Jicho la kuona wachezaji ambao watafiti kwenye falsafa yako.

Thus why Wachezaji wengi wa City wanaonekana kuwa bora Sana kulingana na pep kuwajenga kwenye falsafa yake na sio kutegemea brilliant yao tu.

Nadhani ni Darasa huru anatoa Kwa vilabu vingine na notes unaondoka nazo bure!!

NB: Kuna watu wamefurahi kadi ya Rodri!!, Nafasi yake atacheza hata Walker na kipigo kitatembea k**a kawaida 😅.

Pep Effect..... 🙌.

Dakika chache alizopewa aliwafanya Singida waone Kila rangi uwanjani!!!Mwalimu Dabo, nadhani hana haja ya kufikiri mara ...
22/09/2023

Dakika chache alizopewa aliwafanya Singida waone Kila rangi uwanjani!!!

Mwalimu Dabo, nadhani hana haja ya kufikiri mara mbili Dimba la chini.

First half ÷Simba  walikuja na high pressure (pressing) na kuwalazimisha Costal union kufanya makosa Goli la kwanza Lawi...
21/09/2023

First half ÷
Simba walikuja na high pressure (pressing) na kuwalazimisha Costal union kufanya makosa

Goli la kwanza Lawi anafanyiwa pressing anapoteza Mpira, inapigwa Turn over Simba wanapata bao.

Goli la pili lack of concentration Kwa walinzi wa Cost Saido anashuti golikeeper anaokoa hakuna Beki wa kuosha, Mpira unarudishwa mara ya pili Bado unamkuta Baleke akiwa free(walinzi wa Cost hawakuwa na Concentration eneo la tukio).

Goli la tatu movement ya Miqusson anafanyiwa madhambi kwenye box (pen).

Baada ya red Card hapo ndipo ugumu wa mechi ulipokuja Kwa Nini
_Costal union walibaki na option ya kupunguza magoli, hivyo kilichobaki ulikuwa ni mpango sahihi wa kuzuia.

Second half
Pep Guardiola aliwahi kusema njia nzuri ya kuzui ni kumiliki Mpira.

_Costal walirudi uwanjani wakiwa tayali na mentality ya kuzui Kwa kuuweka Mpira kwenye himaya Yao(possession)

_idadi kubwa ya wachezaji kwenye eneo lao na uwingi wa wachezaji wenye uzoefu(confidence) ikarahisishia mpango wao.

Simba wakajikuta kwenye wakati mgumu wa kupata nafasi ya kuweka Mpira wavuni, bahati mbaya Robertinho hakujibu maswali aliyo ulizwa na Zahera akabaki kwenye approach Ile Ile ya kufanya high pressing bila mafanikio.

Huenda Mwalimu hakuwa na haja ya kutafuta plan Kwa sababu tayali alikuwa na uhakika wa alama tatu na goli tatu.

Opinion:
K**a Mwalimu Robertinho angehitaji magoli zaidi Nilidhani ingekuwa Bora k**a angebadili approach Kwa kupunguza high pressing na kuwasubili Costal wasoge kwenye eneo lake Ili idadi ya wachezaji ipungue kwenye eneo lao alafu watumie Counterattack au space zitakazopatikana.

Zahera baada ya kuwa pungufu na quality ya Simba hakuwa na chakupoteza zaidi ya kupunguza idadi ya magoli akafanikiwa kwenye mpango wake, well done👏.

Lawi 🔥🔥
Ajibu, Chama, Ngoma 🔥🔥🔥
Simba 3_0 Costal union

Jose Mourinho aliwahi kusema ukishindwa kufunga zuia.Kaze kwenye muundo wa 3_5_2 lengo kubwa ilikuwa ni kuzui na watu we...
20/09/2023

Jose Mourinho aliwahi kusema ukishindwa kufunga zuia.

Kaze kwenye muundo wa 3_5_2 lengo kubwa ilikuwa ni kuzui na watu wengi kwenye eneo lake.

Principal of defending
_ Compactness (ukaribu), lengo ikiwa ni kumnyima mpinzani wepesi wa kutengeneza nafasi, Namungo walikuwa compact Sana kwenye eneo lao na kuwafanya Yanga kupata ugumu wa kutengeneza nafasi za wazi.

_Press (pressure), Ili kuzui vizuri inatakiwa ku apply pressure Kwa mpinzani Ili kumnyima utulivu na kumlazimisha afanye makosa, Namungo walikuwa wanafanya low pressing na kuwafanya Yanga mara nyingi kupoteza pasi na kuwanyima utulivu eneo lao la ushambuliaji!!.

Delay (punguza kasi), hakikisha unapunguza Kasi ya mpinzani Kwa kumiliki Mpira, Namungo walipokuwa wanapata Mpira hawakuwa na pressure zaidi ya kuhakikisha wanaweka Mpira kwenye himaya Yao ikawasaidia kupunguza Kasi ya mashambulizi.

Bahati mbaya Namungo walipata tabu kufanikiwa kwenye Counterattack kutokana na Shape ya uzuiaji ya Yanga CB wanatanuka pembeni DM ana Cover space ya kati.

Gamondi kwenye 4_1_3_3 lengo ikiwa ni kushambulia kupitia katikati na Viungo watatu (Pacome, Nzegeli+Azizi Ki) Ambao wote ni attacking midfielders chini akiwa Aucho peke ake k**a DM. eneo la Juu akiwa Musonda na Mzize

Ugumu ukawa kwenye vitu viwili÷
_kufungua ukuta wa Namungo, kwa sababu Namungo walikuwa Compact Sana.
_Aucho kwenye eneo la chini alikosa support ya CM, hivyo timu kukosa balance eneo la kiungo kutoka na uwingi wa viungo wa Namungo.

Nadhani Mwalimu alimhitaji mapema Sana Moloko, Ili kutanua uwanja na kudistribute ukuta wa Namungo ambao ulikuwa compact Kwa ajili ya kupata space.

Kaze alikuwa vizuri Sana kwenye mpango kazi wake 👏.

Azizi ki 🔥
Yanga Sc 1_0 NamunDominick SalambabGeorge AmbangilelMaster TindwawGodlisten MurorAlly KamwewDickson Mpilipili 🇹🇿 🇹🇿li

Binafsi Kwa haraka eneo la kiungo Simba linaathiri eneo la ulinzi kimfumo ...1.kwenye falsafa ya Simba na approach ya Ro...
18/09/2023

Binafsi Kwa haraka eneo la kiungo Simba linaathiri eneo la ulinzi kimfumo ...

1.kwenye falsafa ya Simba na approach ya Robertinho inategemeana Sana Fullbacks ambao wanatumika zaidi kushambulia!!

_kwa namna hiyo unaposhambulia, space ya Fullbacks inabaki wazi, hivyo unapofanyiwa turnover au counterattack Ile space inatumika k**a uchochoro.

_Hivyo Ili kutengeneza muundo mzuri wa uzuiaji kwenye falsafa/ mfumo huu

_inatakiwa kuwa na DM ambaye atakuwa Defensive zaidi kuliko offensive Kwa lengo la kutengeneza shape ya walinzi watatu/wanne (CB,CB,DM)

_ambao kwenye majukumu DM anaweza sogea Pembeni Moja Kwa moja Ili kucover Ile space iliyo achwa na fullback au anaweza kukaa katikati alafu CB akawa anatanuka pembeni.

Reference: Mechi ya mtimbwa

_ Jukumu la kumkimbiza Mateo halikuwa la Shabalala tena, Kwa Sababu Mpira ulidondoka nyuma yake na sio alipitwa...., Jukumu lilikuwa la CB ambaye ilikuwa rahisi ku cut out kumfwata Mateo alafu DM angefwata Box kuziba space ya CB Aliye Cut out, ingekuwa rahisi zaidi kuliko run Walizofanya kufwata box na kuacha Shabalala amkimbize Mateo.

_Au wakati Shabalala amepanda DM angezogea upande ule Ili kucover space yake maana yake hata k**a CB wangekimbia kumfwata box isingekuwa na madhara.

Hiki kitu kilimkuta TAA msimu uliopita pale Liverpool na akaitwa uchochoro lakini brain ya kllop aliona shida ni eneo la kiungo na hakujiuliza mara mbili zaidi ya kuongeza viungo 4.

Tatizo Simba!?!?:
1. Hakuna pure Defensive midfielders
_Mzamiru na kanoute box to box
_Ngoma ni defensive lakini yuko more offensive kuliko defensive..
Wote timu inaposhambulia ni rahisi kuwaona juu ya mstari wa katikati risk!!, Walinzi hawatepuka lawama!!

2. Kuna muda safu ya ulinzi inapoteza shape ya V, CB wote wawili wanakuwa kwenye mstari mmoja kosa linapofanyika hakuna wa kufuta kosa la mwezake.

Nadhani dirisha dogo Simba wanahitaji Pure Defensive midfielder na backup nzuri ya kapombe na Shabalala... Duchu na mwenda sidhani k**a kunakitu kikubwa wanaweza kukupa zaidi ya hiki wachotoa kapombe na Shabalala.

Note: Nadhani k**a konoute/ Ngoma mmoja atapewa majukumu ya kucheza chini ya Fullbacks (CB,CB,DM)itapunguza makosa eneo la ulinzi.

JICHO LANGU 👁️.

Binafsi Robertinho ni Coach Mzuri ni Bahati mbaya tu ndiye mwenye jukumu la kubeba lawama hata k**a Baleke ndiye aliyeko...
18/09/2023

Binafsi Robertinho ni Coach Mzuri ni Bahati mbaya tu ndiye mwenye jukumu la kubeba lawama hata k**a Baleke ndiye aliyekosa bao la wazi.

Lakini nadhani he is good Coach kwenye Game approaching,.

rejea game ya Wydad Ali win kwenye Approach lakini individual mistake ya wachezaji kushindwa kutumia nafasi uwanja wa taifa na individual mistake ya Golikeeper kule ugenini inawafanya wanatolewa.

Rejea Daby baada ya Miaka kadhaa Simba kushindwa kumfunga yanga kwenye michuano ya ligi Robertinho anafanya homework nzuri anakuja kushinda bao 2_0 mbele ya Yanga Bora Sana ya Nabi.

Robertinho ameshinda ngao ya jamii mbele ya Yanga hii tuyoimba Bora Sana Kwa Sasa!!

Mchezo wa juzi dhidi ya Power Dynamo, Simba wanaonekana kuzidiwa first half, Mwalimu anausoma mchezo anarejea akiwa Bora (Coach ability), bahati mbaya mistake ya Golikeeper inamnyima matokeo ya ushindi.

Msimu wake wa kwanza
_Robo fainali klabu Bingwa Barani Afrika
_Unbeaten Ligi kuu
_Nusu fainali ASFC
_Champion ngao ya jamii.

Binafsi k**a nitaulizwa mara 100, Robertinho anatosha Simba jibu kitakuwa jepesi tu BIG YES

Uongozi usiingie kwenye mtego wa pressure ya mashabiki!!.

Note: Wachezaji wa Simba wanahitaji kwenda more than Talent, (Kuna muda fighting spirit inakuwa chini Sana Kwa baadhi ya wachezaji) yaani hawajitumi, risk!!.
5fm @kishambamedia

Do Good and Good Will come to you..!!Backstrong... 7 .5fm
16/09/2023

Do Good and Good Will come to you..!!

Backstrong...
7 .5fm

Binafsi mchezo wa Jana nadhani ilikuwa vita ya Robertinho na Hans!! Kwa Nini!?Robertinho hakubadilika kwenye approach ya...
11/08/2023

Binafsi mchezo wa Jana nadhani ilikuwa vita ya Robertinho na Hans!! Kwa Nini!?

Robertinho hakubadilika kwenye approach yake ya direct football... Kwenye 4_2_3_1 Silaha yake kubwa ikiwa ni Fullbacks, (Kapombe+Shabalala) ambao wakisogea juu Onana+Kibu Wanaingia ndani k**a isolated winga na kuongeza idadi ya watu eneo la katikati.

Mtego unakuwa hapo Kwa sababu Wanakuwa na idadi kubwa kwenye eneo la mpinzani!!

Kwa Nini Hans!!
1.Hans ni k**a alifanya Homework yake vizuri!! SFG wakiwa wanashambuliwa/hawana Mpira basi wanakabia chini Ili kuwa na idadi kubwa ya watu kwenye eneo lao, Kwa lengo la kuweka pressure kwenye Mpira na kuwafanya Simba washindwe kutengeneza nafasi Kwa urahisi.

2.Carno+ Mangalo mipira ya juu kwao k**a chakula, Kwa hiyo Singida walizuia na watu wengi Ili Simba abaki na Option ya kutumia mipira mirefu Kwa sababu walikuwa na uhakika wa kushinda Mipira hiyo.

3. SFG wakipata Mpira wanashambulia Kwa Kasi kupitia pembeni, hivyo hawakuwapa nafasi kubwa Kapombe+Shabalala kushambulia.

Simba wakapata wakati mgumu bahati mbaya hawakubadilika wakabaki kwenye mdudo wa singida, bahati mbaya zaidi wakawa wanakosa mtu special anaeweza kuamua mechi kwenye mazingira magumu(Chama).

Opinion!!
Nilitegemea Robertinho abadili approach, Kwa sababu SFG wanakuwa wengi kwenye eneo lao basi asinge fanya pressing. angewasubili kwenye eneo lake Ili apate space then atumie Countattack!! Kwa sababu wachezaji wa kucheza Countattack anao!!.

So far ulikuwa mchezo mzuri Kwa timu zote mbili naamini Kila mtu aliona!!

_SFGconcetration eneo la ulinzi!!🔥🔥🔥

_yule kagoma +kijili 🙌

_Inonga+marone 🔥

_Ngoma👏, ila natamani kumwona zaidi kwenye tafu game

JICHO LANGU 👁️.

Inashangaza Azam changamoto yao ni Ile Ile kulingana na msimu uliopita!!Azam waliruhusu magoli goli 29Yanga waliruhusu m...
10/08/2023

Inashangaza Azam changamoto yao ni Ile Ile kulingana na msimu uliopita!!

Azam waliruhusu magoli goli 29
Yanga waliruhusu magoli 18
Simba waliruhusu magoli 17

Ukiangalia takwimwi hizo maana yake Azam walikuwa na shida kwenye safu ya Ulinzi!! , Na hakuna asiye jua kawa Moja ya changamoto kubwa ilikuwa GOLIKEEPER!!

Changamoto ya pili ilikuwa Centerback walikuwa wanakosa Beki kiongozi na mwenye uzoefu ndiyo maana Kuna nyakati Mwalimu alikuwa anamtumia manyama k**a centerback kitu ambachokilikuwa kinaonyesha Kuna shida!!

Kwa hiyo nilitegemea wafanyie kazi maeneo hayo kuliko eneo lingine lolote!! Badala yake hakuna kilichofanyika!!, nawaona Azam waki struggle Sana msimu kwenye eneo la ulinzi.

Yani Viungo wanalazimika kufanya kazi kubwa ya kusaidia safu ya ulinzi kuliko ushambuliaji, poor!!!

Yanga hawakufanya vizuri msimu uliopita Kwa Sababu ya Mayele tu, ni Kwa sababu kulikuwa na mtu Bora golini.

Magoli aliyofungwa Foba jana hayana shida, lakini makosa aliyofanya inasikitisha, Kuna timu zinahitaji kosa Moja/mawili tu k**a Yale zikutupe nje ya michuano!!.

Binafsi Azam nafasi Yao itabaki Ile Ile hawajatibu tatizo!!.

Wajitathimini hasa eneo la golikeeping nadhani ni eneo nyeti Sana linalo waua mara zote, inashangaza Sana!!.

Azam wanahitaji Sana uhakika wa Golikeeper na Beki kiongozi!!


Address

Ahadi. Mgogo@gmail. Com
Dar Es Salaam

Telephone

+255622704140

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Nedy official Media posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Nedy official Media:

Videos

Share



You may also like