MUCHI TZ

MUCHI TZ Bring about News, sports & comedy videos
(1)

Tayari keshakuwa Mwananchi!! Okrah magic🔰🔰🔰🔰💚💚💚
31/12/2023

Tayari keshakuwa Mwananchi!! Okrah magic🔰🔰🔰🔰💚💚💚

Usajili Bora mpaka Sasa kwa mwaka huu 📝
31/12/2023

Usajili Bora mpaka Sasa kwa mwaka huu 📝

Tulishawahi kukosa pale tulipotegemea tutapata, tukawa na matumaini juu ya mambo mazuri lakini yakatokea mabaya kinyume ...
29/12/2023

Tulishawahi kukosa pale tulipotegemea tutapata, tukawa na matumaini juu ya mambo mazuri lakini yakatokea mabaya kinyume na mategemeo yetu.

Maisha hayakwenda vile tulivyodhani kuwa yataenda, njia zile nyepesi ambazo tulipita kwa kujiamini ndio ziliishia kuacha makovu kwenye miili yetu sababu vikwazo vilizidi na kuwa vingi.

Kuna baadhi ya siku kwetu hatuwezi ku*isahau sababu zimeacha vilio vingi mioyoni mwetu, maisha yamejaa habari nyingi za huzuni na masikitiko kuliko mategemeo yetu ya furaha na amani.

Ndoto nyingi nzuri zenye kheri ziliishia kupepea tu mithili ya bendera katikati ya mategemeo yetu ya mafanikio na fanaka, tukaishia kuvuna shari na mambo ambayo tulishindwa kustahimili.

Angalau tungalikuwa na uwezo wa kuchagua maisha, basi mimi ningechagua kuwa mtoto milele. Ningetamani kuwa mtoto sababu maisha ya utotoni ni matamu sana kuliko ya ukubwa na majukumu.

Ukubwa ni jalala, naaam ukubwa ni mzigo. Nje ya elimu ya darasani ambayo tuliipata kwa shida sana lakini bado binadamu wamekuwa ni funzo tosha kwetu sababu wametufundisha vingi ambavyo hatukupata bahati ya kujifunza pindi tulipokuwa shuleni.

Ni mara ngapi tumepokea usaliti k**a malipo ya uaminifu wetu mbele ya wale watu ambao tulitegemea watadumu maishani mwetu milele.

Ni mara ngapi tumevuna dharau, kejeli, masimango, dhihaka, fedhuli, matusi na aibu kutoka kwa watu ambao tuliwafanya ni ndugu katika maisha yetu.

Ukweli ni kwamba maisha yanamhitaji mpambanaji anaeweza kuendana na wakati. Ambae atamudu machungu na shida za za sayari hii.

Eeh! Mwenyezi Mungu tujaalie moyo wa uvumilivu juu ya kuishi na viumbe hivi ambavyo havina jema wala fadhila kabisa.

Tujaalie pia uwezo wa kumudu machungu ya maisha, uwezo wa kukubali kila taarifa ya huzuni kisha kufuta machozi na kuinuka kuendelea na safari. Tujaalie Mungu wetu, tujaalie

(Ipo siku nasi majina yetu yataitwa kwa heshima mbele ya wale waliotudharau. Tuendelee kuwa na imani)

Muandishi nia AMANI DIMILE ✍🏼

Shida yetu tunapenda kuongopewa, tena tunapenda ule uongo ambao huwa unatutia matumaini.Ukweli Simba haipo kwenye ubora,...
24/12/2023

Shida yetu tunapenda kuongopewa, tena tunapenda ule uongo ambao huwa unatutia matumaini.

Ukweli Simba haipo kwenye ubora, k**a Ahmed Ally mtu ambae amekuwa akiitetea timu kwenye nyakati mbaya zaidi amefikia hatua ya kutoa kauli ile basi jua hali ni mbaya.

Jana kuna muda ilipigwa Shot na Azam TV ikimuonyesha Ahmed akilalamika kutopendezwa na kile anachokiona uwanjani.

Na yeye kafika mwisho kaona hawezi kuendelea kuwaongopea wanasimba kuwa wana timu bora. Amewaambia ukweli ili wajue uhalisia wa timu yao.

Good Afternoon

YANGA hawaeleweki ni k**a wana utaratibu wao, Premier League anauwasha Aziz Ki na CAF anauwasha Pacome Zouzoua! Yanga ha...
23/12/2023

YANGA hawaeleweki ni k**a wana utaratibu wao, Premier League anauwasha Aziz Ki na CAF anauwasha Pacome Zouzoua!

Yanga hawaeleweki nani Staa wa timu, mara Maxi Nzengeli, mara Aziz Ki, mara Pacome, mara Aucho, mara Bacca, mara Dickson Job mara Kibwana ama Kibabage, mara Mudathir ama Nondo, ama Diarra! Yanga hawaeleweki kabisa😀

Wananchii mpo tayari kuwapokea wazambia Hawa?? Lolote linaweza kutokea
23/12/2023

Wananchii mpo tayari kuwapokea wazambia Hawa?? Lolote linaweza kutokea

K**a kuna mtu mgeni kwamba yule aliyecheza beki 3 kwenye hizi game sio beki chaguo la kwanza, atashangaaaa! Atatamani am...
20/12/2023

K**a kuna mtu mgeni kwamba yule aliyecheza beki 3 kwenye hizi game sio beki chaguo la kwanza, atashangaaaa! Atatamani amuone huyo chaguo la kwanza ni Marcelo aliyekuwa Madrid au Ashley cole.

Nickson hakujiandaa sana kiakili kucheza hizi games, zilimjia baada ya Lomalisa kuumia, Lakini amezipokea k**a challenge na ameonesha kiwango kizuri sana, nina hakika Lomalisa amefurahia.

Uwezo wake wa kukokota mpira kwa kasi na kuwapita wapinzani hadi kufika kwenye box ni mzuri, uwezo wa kurudi ku-cover eneo lake kwa kasi ni mzuri tena kwenye 1v1 situation ana win mipira.

Lakini kelele zilizopigwa na mashabiki, wanachama na hata baadhi ya wachambu*i baada ya Lomalisa Kuumia zilikuwa zimejikita tu kuongelea mazuri ya Lomalisa na wala sio atafanya nini.

Leo dogo amechukua challenge na ameubonda, walimbeza wanabali wanajifichia kwa Paccome na zile brilliant goals zake na kubaki midomo wazi juu ya Nickson, Bongo hatujui mpira sisi! Tujifunzee.

Tumezoea kuona mmoja tu akiwa juu na wala sio wawili wakiwa juu. Nina uhakika Kocha Miguel Gamondi hatapata mawazo kabisa Joyce Lomalisa akiumia (Simuombei) au akikosekana kwa sababu yeyote.

Namkubali Lomalisa ni beki mzuri sana kwenye kushambulia na ball control, Lakini hatupaswi kutotambua kuna wengine wana uzuri sehemu nyingine k**a Nickson anakaba zaidi na anashambulia pia.

Bongo tunapenda mmoja awe juu tu, Bongo hatujui mpira sisi. Tujifunze. Hatujui!

CHAMBUA 🗣 Maoni kila mtu ana yake✍️

USTADH KHALID AUCHO ana dharau sana na mpira, kwenu inaweza kuwa mechi ngumu sana ama mchezo mgumu sana ila kwake ni kit...
20/12/2023

USTADH KHALID AUCHO ana dharau sana na mpira, kwenu inaweza kuwa mechi ngumu sana ama mchezo mgumu sana ila kwake ni kitu rahisi sana, k**a Yanga ni Logarithms basi yeye ndio Four Figure, k**a Yanga ni Biology basi yeye ndio BS yenyewe!

Hii picha ilipigwa mechi dhidi ya Al Ahly, wakati hao ‘Madogo’ wanahangaika hapo yeye kasimama tu na mali pembeni, ni ngumu sana kuwaaminisha Wajukuu zetu kuwa hapo walikuwa kwenye mechi, kifupi yeye ndie Mwamu*i anaamua Yanga icheze kwa namna gani, huwezi kumwona Aucho ukiitazama Yanga ila ukimwona Aucho umeiona Yanga nzima.

Leo karudia ‘dharau’ zake zile zile! Tunaweza waimba sana wakina Pacome na Aziz Ki ila yeye amechagua kuwa jiwe kuu kwenye ujenzi wa kasri lao! Ana dharau sana, anaujua sana mpira! Top top Midfielder!

NIMEMALIZA😀

VISIT MOROGORO🇹🇿

TOTAL DOMINANCE ✍🏻Yani k**a ingekuwa mchezo wa Boxing basi tungesema Medeama hata punch moja haikufika kwenye uso wa Yan...
20/12/2023

TOTAL DOMINANCE

✍🏻Yani k**a ingekuwa mchezo wa Boxing basi tungesema Medeama hata punch moja haikufika kwenye uso wa Yanga. Yanga walikuwa bora kuanzia dakika ya kwanza mpaka ya mwisho na kwa aina ya nafasi ambazo walitengeneza 3-0 ni matokeo yanayodanganya

✍🏻Msingi mkubwa wa Yanga ulikuwa hapa kwenye positions za hawa wachezaji wawili pale Yanga wakiwa na mali : Kibabage na Mudathir . Maeneo ambayo walikuwa wanasimama/ wanakuwa hayo maeneo ndio msingi mkubwa .

1: Kibabage anasogea juu zaidi ya uwanja k**a winga na Mudthir anatoka ndani na kwenda pembeni kuwa k**a winga wa kulia . Ilikuwa na faida gani ?

2: Ni kuruhusu viungo watatu washambuliaji kucheza katikati ya mstari wa kiungo na ulinzi wa Medeama tunaita " between the lines " ( Aziz , Maxi na Pacome ) ndio sehemu ambazo walikuwa wanapokelea mipira na ilikuwa hatari sana kwa Medeama na ngumu kwao kukabiliana nayo .... faida yake ?

3: Kuwa na wachezaji wako hatari katika maeneo hatari na magumu kuzuia , maana yake wana options hizi : Kupiga golini na kupiga pasi za mwisho kwa Kibabage Musonda Mudathir na pia kwao wao wenyewe kwa wenyewe

4: Lakini wao kuwa eneo hilo kitu kimoja na kupata pasi sahihi kwa wakati sahihi ni kitu kingine . Hapo ndio anaingia kiungo mwenye kazi hiyo : Aucho . Anajua sana kupiga pasi za mbele tena za chini chini ambazo zinavunja mstari wa kiungo wa timu pinzani ( Line breaking passes )

✍🏻Nafikiri Medeama ni k**a vile walikosa imani kwamba wanaweza kuonesha mamlaka uwanjani na haiba ya kuutaka mchezo , walikuwa slow sana , mipira wanapoteza kirahisi ( k**a kwenye goli la tatu la Yanga ) wanachelewa kufika kwenye mpira , recovery runs zilikuwa za chini sana na ukicheza dhidi ya wachezaji wazuri watakupa shida sana .

NOTE

1: Gamondi alikochi ushindi wa 6-0 lakini wachezaji wameamua kumpa 3-0 .

2: Yao Yao , Mr. Reliable . Performance zake ni nzuri kila ukimuona uwanjani

3: Job na Bakari walifanya homework yao dhidi ya Sowah , leo walikuwa vizuri tofauti na Ghana

4: Pasi za mbele za Aucho ndio msingi kwa Maxi Pacome na Aziz

5: PACOME .. what a player . He is so good 🔥🔥

FT: Yanga SC 3-0 Medeama

George ambangile ✍️✍️

Wananchii dondosha likes 🔰🔥
20/12/2023

Wananchii dondosha likes 🔰🔥

𝐇𝐀𝐋𝐅 𝐓𝐈𝐌𝐄⏱️ |   Young Africans SC 1-0 Medeama SC
20/12/2023

𝐇𝐀𝐋𝐅 𝐓𝐈𝐌𝐄⏱️ |

Young Africans SC 1-0 Medeama SC


Wananchii hapo vipi??
20/12/2023

Wananchii hapo vipi??

CAF CHAMPIONS LEAGUE 🤩🇹🇿 YANGA SC 🆚 MEDEAMA 🇬🇭 ⏰ 16:00🏟️ MkapaMchezo huu ni wa kufa ama kupona kwa Yanga kwani inahitaji...
20/12/2023

CAF CHAMPIONS LEAGUE 🤩
🇹🇿 YANGA SC 🆚 MEDEAMA 🇬🇭
⏰ 16:00
🏟️ Mkapa
Mchezo huu ni wa kufa ama kupona kwa Yanga kwani inahitaji ushindi ili kurejesha matumaini ya kumaliza nafasi mbili za juu kundi D ili kujihakikishia kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa mara ya kwanza katika historia. Kila la kheri 🇹🇿

SIUUUUU .! 🔥✍🏻Kwenye mechi k**a hizi za kimataifa unapaswa kutoa adhabu pale makosa yanapotokea . Simba walifanya makosa...
19/12/2023

SIUUUUU .! 🔥

✍🏻Kwenye mechi k**a hizi za kimataifa unapaswa kutoa adhabu pale makosa yanapotokea . Simba walifanya makosa Wydad hawakutoa adhabu lakini , wao Wydad walivyofanya makosa Simba wakatoa adhabu stahiki .

✍🏻Simba kwenye build up ya 2-3 ( Inonga na Malone nyuma ) huku mbele yao kwenye mstari mmoja Zimbwe Ngoma na Kapombe ilikuwa na dhumuni la kuwapa njia mbili za kupita

1: Kupita katikati ya uwanja , kivipi ? Kwasababu Mzamiru alikuwa anasogea juu kuungana na Chama hivyo kutengeneza namba 8 wawili dhidi ya kiungo wa ulinzi wa Wydad

2: Kupita pembeni ya uwanja kwa kutumia wingers wao ( Onana na Kibu ) kwenye 1v1 dhidi ya fullbacks wa Wydad

Njia ya kwanza ilipata ugumu kwasababu Wydad ndani ya uwanja walizuia vizuri , njia ya Simba ikawa pembeni ya uwanja na walifanikiwa vipi ?

1: Kwasababu winga wa kulia wa Wydad alikuwa harudi nyumu kuzuia .. hapo Simba wakatumia faida hiyo kwa Onana na Chama kumshambulia beki wa kulia wa Wydad ambaye alikuwa peke yake ... spaces zikaanza kupatikana

2: Njia nyingine ya Simba ilikuwa ni turnovers : magoli yote mawili yametokana na Wydad kuporwa mpira na Simba kushambulia .

✍🏻Kipindi cha kwanza Wydad walikosa ufanisi na maamu*i sahihi katika nyakati sahihi ndio ambazo ziliwaangusha pamoja na ubora wa Ayoub Lakred golini kwa Simba .

✍🏻Baada ya hapo Benchikha ni k**a akawaambia Wydad " Hold my beer " ngoja niwape Haram Football sasa . Mabeki wa kutosha nyuma , wanapaki Bus halafu kuvizia counter attacks .

NOTE

1: Ayoub Lakred perfect match kwake , Saves na hata kuk**ata crosses : confidence imerudi.

2: Inonga Malone Kapombe Zimbwe 🔥 uzuiaji

3: Ngoma passing game 🔥

4: Kibu D , kuzuia anasaidia kusogeza timu juu anafanya vizuri

5: Boly alipata nafasi mbili bora na zote alikosa

6: W***y Onana , k**alizia vizuri sana nafasi zote mbili 🔥🔥 muda wa kujenga confidence huu.

FT: Simba 2-0 Wydad

Credit: George ambangile✍️

🇲🇼 PETER BANDA 🔜 SINGIDA FOUNTAIN GATE Peter Banda atajiunga na Singida Fountain Gate k**a mchezaji mpya mwezi huu. 🇲🇼Ad...
19/12/2023

🇲🇼 PETER BANDA 🔜 SINGIDA FOUNTAIN GATE
Peter Banda atajiunga na Singida Fountain Gate k**a mchezaji mpya mwezi huu. 🇲🇼
Ada ya usajili itakuwa USD $80,000 (Sh 200milioni) lakini italipwa kwa awamu mbili.
Singida inatarajiwa kukamilisha sehemu yao ya makubaliano leo lakini Banda tayari amesaini na anarejea Tanzania.
Credit: Micky Jr ✍️

18/12/2023

daktari anachomesha 😂

18/12/2023

SHEMEJI part 2

BENCHIKHA kuhusu mchezo wa kesho✍️
18/12/2023

BENCHIKHA kuhusu mchezo wa kesho✍️

Kiungo wa zamani wa Yanga anayekipiga kwa sasa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amekiri kiungo mpya aliyetua kwenye timu...
18/12/2023

Kiungo wa zamani wa Yanga anayekipiga kwa sasa Azam FC, Feisal Salum ‘Fei Toto’ amekiri kiungo mpya aliyetua kwenye timu hiyo, Shekhan Ibrahim Khamis ni bonge la mchezaji mwenye kipaji na uwezo mkubwa, lakini akamuonya mapema kwa kumtaka ajipange kwelikweli kwa vile ametua katika timu yenye presha kubwa.
“Shekhan ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa na ana kipaji namuona mbali, natarajia atafanya vizuri akipewa nafasi na atapata mafanikio makubwa ndani yake,” alisema Fei Toto na kuongeza;
“Najua amekuja timu kubwa, anatakiwa kupambana na kuonyesha kile alichonacho bila kujali anaenda kupambana na mastaa gani. Ni mchezaji ambaye nimemshuhudia ni mdogo wangu ameanza kujulikana sasa, lakini ni mchezaji ambaye amekuzwa na kufanywa bora chini ya JKU amepita kwenye misingi ya soka hivyo naamini atakuwa bora.”

Duniani kote hakuna Tajiri ama Mfanyabiashara aliyeingia kwenye mpira kizembe bila kuwa na hesabu zake, Matajiri wanafah...
18/12/2023

Duniani kote hakuna Tajiri ama Mfanyabiashara aliyeingia kwenye mpira kizembe bila kuwa na hesabu zake, Matajiri wanafahamu dunia ya mpira bado ipo kwenye Ujamaa na sio Ubepari, Matajiri wanajitahidi kuwabadili Mashabiki kuwa Wateja wa klabu, wanawekeza ila sio kwamba uwekezaji uathiri biashara zao, hakuna Tajiri wa namna hiyo.

GSM amenunua tiketi zote za mzunguko na sherti lake ni Mashabiki wa Yanga wavae u*i alioutengeneza yeye kwa maana GSM nembo yake ionekane, niliposema kuwa Tajiri na Yanga wamepiga hesabu nzuri na ina faida kubwa sana kwao (GSM & YANGA) wamekuja kukosoa kwa maswali.

Kuna hoja kuwa Mashabiki hawatonunua jezi mpya kwakuwa tayari wanazo, nataka nimkumbushe Juma kwa kauli ya CEO Marina aliyekuwa Chelsea wakati anaongea na NIKE kupandisha thamani ya mkataba alisema “Bidhaa ya mpira wa miguu sio dawa kuwa mpaka mtu aumwe, ama sio dhana za kilimo mpaka wakati wa kilimo” yes jezi inanunuliwa wakati wowote.

Hata k**a Shabiki akija na jezi ya GSM msimu uliopita bado majibu yake ni kuwa Tajiri alishaingiza pesa kupitia hiyo jezi na ni sehemu ya faida ya yeye kuwa Shabiki wa Yanga, bado hupaswi kusahau kuwa Yanga hawashindwi kuuza angalau jezi mpya hata piece 500 wiki hii, fanya 500 zidisha kwa 30,000 ni 15,000,000/= Tshs sio haba! Leo hii tunasahau kwenye mpira kuna Vintage Retro Kits?

Kupitia kwa hii activation ya Tajiri k**a Mashabiki watajaa maana yake full house inasukuma agenda kubwa ya thamani ya Yanga, kupitia jezi za Mashabiki wa mzunguko ambapo picha nyingi hupigwa, mmewaza Wadhamini watapata MILEAGE kiasi gani? Hatutazami GSM pamoja na Wadhamini wengine watau*ika vyema barani Afrika na duniani?

Tajiri katoa pesa, toa pesa upate pesa! Ikitokea Yanga kafuzu Robo fainali Klabu inaingiza kiasi gani? Ni mara 10 ya pesa ya mzunguko, hivi ndivyo Wafanyabiashara duniani huwaza kwakuwa wanajua Mashabiki wengi hawajiona Wateja wa klabu! Ndio maana Roman Abramovich alikuwa anaikopesha Chelsea na akasamehe mpaka madeni.

Hongera sana GSM, akili k**a hizi Matajiri wengine Patrice Motsepe, Moise Katumbi wamezitumia sana Afrika, k**a ambavyo Tajiri MO pale Simba anavyoikopesha klabu, ndivyo inapaswa kuwa.

VISIT MOROGORO🇹🇿

Credit: Jr_farhanjr

🗣️ “Hakuna timu isiyofungika, tuondoe mawazo hasi kichwani kwetu tutaingia uwanjani tukiwa kifua mbele na lengo likiwa n...
18/12/2023

🗣️ “Hakuna timu isiyofungika, tuondoe mawazo hasi kichwani kwetu tutaingia uwanjani tukiwa kifua mbele na lengo likiwa ni kushinda. Tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi kuipa nguvu timu yao naamini baada ya mechi tutafurahi kwa pamoja,” - Kocha Abdelhak Benchikha.

✍🏻Man United sidhani k**a walienda Anfield wakiamini wanavuna alama tatu , bali ilikuwa kufanya kazi kuwa ngumu kwa Live...
17/12/2023

✍🏻Man United sidhani k**a walienda Anfield wakiamini wanavuna alama tatu , bali ilikuwa kufanya kazi kuwa ngumu kwa Liverpool na pengine wakipata nafasi ya counter attack basi watumie hiyo

✍🏻K**a timu yako inapiga mashuti 34 dhidi ya 6 ya mpinzani wako basi haya ndio maana yake

1: Hukutengeneza nafasi bora sana

2: Wachezaji wako hawakuwa wafanisi mbele ya goli ( lango )

3: Mpinzani wako alizuia vizuri katika nyakati sahihi

Kwa Liverpool leo , hayo yote yalitokea leo : kuna nyakati ilipaswa nafasi bora zaidi itengenezwe lakini wanapoteza mipira kirahisi , kuna nyakati umaliziaji mbovu na kuna nyakati United walizuia vizuri pale walipohitajika .

✍🏻Nafikiri leo bila mpira kwa Man United k**a wangepoteza basi isingekuwa kwasababu ya uvivu uwanjani bali ubora wa mpinzani , YES kwenda mbele United hawakuwa vizuri kabisa lakini bila mpira waliamua kujituma sana na ukiwa Anfield unatakiwa kufanya hivyo , vinginevyo unakutana na hali mbaya

✍🏻Liverpool walikuwa wanataka kutengeneza idadi kubwa ya wachezaji hasa pembeni ya uwanja kwa " combination play " lakini Garnacho na Antony licha ya kutokuwa sawa wakiwa na mali hawakuwaacha mafullbacks wao kuwa peke yao na hiyo iliwanyima njia Liverpool pembeni ndani hakukuwa na space ya kutosha kwao ( Scott Amrabat na Mainoo walijitahidi )

✍🏻Ukicheza k**a United walivyocheza basi kwenye counter atfacks kwenda mbele unahitaji

1: Upigaji pasi sahihi kwenda mbele pale wakipata mpira

2: Wachezaji wa pembeni ambao wapo wafanisi wakiwa na mali , dribbling and Passing

3: Kiungo mshambuliaji kuwa karibu sana na straika pale ikipigwa mipira mirefu .

Lakini United hawakufanya hayo mambo kwa ufanisi hata kidogo ndio maana ilikuwa uwanja umeinama tu kwao

NOTE

1: TAA kwenye passing , technique yake ya hali ya juu sana

2: Konate na VVD walikuwa na kazi rahisi sana dhidi ya Hojlund , moja wana nguvu mbili Hojlund hana msaada

3: Szobo hii ni mechi yake ya kuisahau haraka sana , mambo hayakuwa sawa kwake

4: Varane : uzuiaji wake 🔥

5: Onana good game kacheza 🔥

6: Mainoo anacheza k**a ana miaka 27 , mtulivu , hapaniki akiwa na mali.

FT: Liverpool 0-0 Man United

✍️ George ambagile #

ASERNAL TUJUANE KWA LIKES😂❤️
17/12/2023

ASERNAL TUJUANE KWA LIKES😂❤️

SIMBA WAMEAMUA KUJA NA HII:Mgeni rasmi wa MNYAMA TUESDAY - HALF DAY, General Abdelhak Benchikha.Sio siku ya kukosa.
17/12/2023

SIMBA WAMEAMUA KUJA NA HII:

Mgeni rasmi wa MNYAMA TUESDAY - HALF DAY, General Abdelhak Benchikha.

Sio siku ya kukosa.

Thank you for 26K followers! 🙏❤️✊     sana kwa support yenu🙏💚✊ Let's go my fans
17/12/2023

Thank you for 26K followers! 🙏❤️✊ sana kwa support yenu🙏💚✊ Let's go my fans

Wengine walitambulishwa mchana, lakini Stephane Aziz Ki alitambulishwa Yanga SC, usiku wa manane akitokea Asec Mimosas m...
17/12/2023

Wengine walitambulishwa mchana, lakini Stephane Aziz Ki alitambulishwa Yanga SC, usiku wa manane akitokea Asec Mimosas mwezi Julai 2022.

Msimu wake wa kwanza kwenye NBC Premier League akiwa na Yanga, Aziz Ki alifunga magoli tisa (9) huku kiwango chake kikionekana kutokuwa katika ule ubora ambao Wananchi waliutarajia.

Magoli mawili aliyoyafunga jana dhidi ya Mtibwa Sugar, yamemfanya Stephane kucheka na nyavu mara tisa (9) kwenye mechi 10 ambazo Yanga imecheza kwenye NBC Premier League msimu huu.

Yeye ndiye kinara wa mabao kwenye NBC Premier League kwa sasa akifuatiwa na Maxi Nzengeli, Jean Baleke wa Simba Feisal Salum wa Azam FC ambao wote wamecheka na nyavu mara saba.

Kwa namna unavyouona mwenendo wa Aziz Ki msimu huu, unafikiri nyota huyo atamaliza na magoli mangapi mwishoni mwa msimu?

(Imeandikwa na )

Finally the long wait is over Skudu kafunga goli lake la kwanza Akiwa na Yanga…lilikuwa ni goli Zuri kuanzia kwenye move...
17/12/2023

Finally the long wait is over Skudu kafunga goli lake la kwanza Akiwa na Yanga…lilikuwa ni goli Zuri kuanzia kwenye movement,jinsi alivyo-scan nafasi upande wa kushoto na curving yenyewe ilikuwa superb 🔥

Kwa kifupi ni goli la kuombea mkopo Bank😄

To be honest miguu ya Skudu ina magoli na Assist kadhaa endapo atapewa dakika za kutosha…Kila mwanadamu anahitaji malaika wa Amani ili afanye vizuri malaika mwenyweni ni self-confidence na hiyo confidence haiji K**a huaminiwi so Kila mchezaji anahitaji Imani ya kocha ili afanye vizuri.

ni dribbler mzuri Ana uwezo wa kuwachua walinzi watatu mpaka wanne na kufanya mambo yatokee Ila Jana kuna wakati alijaribu kufanya utundu ukashindikana kwasababu Hana confidence ya kutosha…kwa kifupi aliogopa kuzomewa na jukwaa hivyo alikuwa limited kwenye baadhi ya mambo.

Skudu apewe dakika za kutosha ana kitu.

Anaandika_@Hansrafael✍️✍️

Kile kiporo cha Simba na Azam kilichotarajiwa kupigwa Januari Mosi hakitapigwa tena sambamba na mechi nyingine za viporo...
17/12/2023

Kile kiporo cha Simba na Azam kilichotarajiwa kupigwa Januari Mosi hakitapigwa tena sambamba na mechi nyingine za viporo kutokana na Bodi ya Ligi (TPLB) kuweka bayana kuwa ni ngumu kucheza kwa kubanwa na kalenda ya michuano tofauti ikiwamo fainali za AFCON 2023.
Michuano hiyo itapigwa kati ya Januari 13 hadi Februari 11, 2024 nchini Ivory Coast, na Tanzania ni miongoni mwa timu shiriki, hivyo kufanya baadhi ya mechi za Ligi Kuu kuvurugwa kwa sasa ikiwamo hiyo ya Simba na Azam na ile ya Januari 4 kati ya Simba dhidi ya Geita Gold, sambamba na kiporo cha Yanga na Dodoma Jiji.
Simba na Yanga kwa sasa zinacheza mechi za viporo, Simba ikianza dhidi ya Kagera Sugar ju*i kwenye Uwanja wa Uhuru, KMC utachezwa Desemba 23, Mashujaa umepangwa kuchezwa Desemba 26 ugenini Uwanja wa Lake Tanganyika na Tabora United kwenye Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ni Desemba 29. Hata hivyo, mechi na Tabora United nayo haina uhakika k**a itachezwa kwani tayari mashindano ya Kombe la Mapindu*i yatakuwa yameanza na Simba inashiriki. Mashindano hayo yanaanza Desemba 28 Unguja, Zanzibar.
Kwa upande wa Yanga, mechi ya Desemba 29 dhidi ya Mashujaa nayo iko kwenye hatihati kwani Kombe la Mapindu*i litakuwa limeanza. Yanga baada ya mechi ya jana dhidi ya Mtibwa, itakuwa na mechi nyingine dhidi ya Tabora United itakayochezwa Desemba 22 na ya Kagera Sugar itakuwa Desemba 26 zote zikichezwa ugenini.
Kutokana na kuwepo kwa mwingiliano wa ratiba ya Ligi Kuu na Kombe la Mapindu*i, TPLB imesogeza mbele mechi zote za Januari na sasa zitachezwa baada ya michuano ya Afcon kumalizika Februari.

K**a kawa Rotation imelipa Wananchi wamerudi kwenye njia za ushindi,soka Joga Bonito limerejea, mnara wa 4G umesoma,Mtib...
16/12/2023

K**a kawa Rotation imelipa Wananchi wamerudi kwenye njia za ushindi,soka Joga Bonito limerejea, mnara wa 4G umesoma,Mtibwa Sugar hawajui kulicho waua.

Gamondi leo alifanya mabadiliko (Rotation) ya wachezaji watano ukilinganisha na kikosi kilichocheza na Medeama na matunda yake yameonekana.

Yanga kwenye 4-3-3 Sureboy alisimama k**a namba #6 huku mbele yake wakicheza namba #10 wawili Maxi na Aziz ki ambao walikuwa na jukumu la kuwafungua Mtibwa na kufunga magoli.

Mtibwa leo walikuja kujilinda zaidi kwenye Mid-block na kusubiri Counter-attack lakini Yanga walikuwa Superb kwenye pressing hivyo Mwamnyeto na Bacca hawakuwa na kazi kubwa ya kuzuia.

You know what?

Kwa mwendo huu Aziz ki anakwenda kuwa top Scorer wa ligi....kijana ana nguvu,utashi,uju*i na uwezo.... tazama goli lake la pili halafu utaelewa kila kitu🔥🔥

Skudu anatakiwa kupewa dakika za kutosha maana kijana ana kipaji kikubwa sema kwasasa anakosa confidence kutokana na ufinyu wa dakika za kucheza.

FT Yanga 4-1 Mtibwa Sugar.
Hansrafael✍️✍️✍️

Address

Dar Es Salaam
Dar Es Salaam

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when MUCHI TZ posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Videos

Share



You may also like