09/12/2024
Sherehe ya ubarikio iliyokuwa ikifanyika katika mtaa wa Ngusero kata ya Osunyai Jijini Arusha, imekatishwa ghafla wakati ikiwa inaendelea ikidaiwa ni baada ya kundi la watu tisa kuvamia eneo hilo huku wakiwa na mapanga na kumkata mtu mmoja sehemu ya mkono na sikio jijini humo.
Mashuhuda wa tukio hilo wakizungumza na mwandishi wetu, wameeleza kuwa chanzo cha tukio hilo ni dereva bodaboda kuponea chupuchupu kumgonga mtoto aliyekuwa eneo la nje ya shereha hiyo na alipokaripiwa na watu waliokuwepo karibu yake aliondoka na baadae kurejea akiwa wenzake huku wakiwa na mapanga na kutenda tukio hilo.
Kwa taarifa zaidi ingia YouTube tafuta GADI TV.