Ufunuo TV

Ufunuo TV TV maalumu kwa Neno la Mungu kwa Watu wote Ulimwenguni

07/07/2024

Bwana Yesu apewe Sifa.

Karibuni Wana wa Ufalme.

Send a message to learn more

Bwana Yesu asifiwe Wapendwa. Kwasasa mutapata mafundisho Kila siku ya neno la MUNGU, kutoka kwa Mwalimu wa Neno la MUNGU...
07/07/2024

Bwana Yesu asifiwe Wapendwa.

Kwasasa mutapata mafundisho Kila siku ya neno la MUNGU, kutoka kwa Mwalimu wa Neno la MUNGU Mwl. "FIDELIS TEGEMEO JOHN"

Swali la Leo linajibiwa hivi, si kweli kwamba Wana wa Esrael hawakuwaoa Waafrica.

1. Yusufu mwana wa yakobo alioa mmisiri akiwa kwa farao.

2. Ibrahimu babu wa Imani alizaa na Hajri mjakazi wa sara. Hajri alikuwa anatoka misiri.

3. Suremani alizaa na malikia wa sheba. Leo hii sheba ni nchi ya Ethiopia.

4. Musa. Mke wa pili wa Musa alikuwa Mwafrica kutoka Kushi. Kushi Leo hii ni nchi ya Sudani. Tena baada ya kumuoa mtu mweusi kutoka Kushi, Miliamu akaanza kueneza uongo Musa amepotoka kuoa mtu mweusi, lakini maneno hayo MUNGU alikasirika na kumpiga ukoma Miliamu.

HESABU 12:1-15.

1 Kisha Miriamu na Haruni wakamnenea Musa kwa sababu ya mwanamke Mkushi aliyekuwa amemwoa; maana, alikuwa amemwoa mwanamke Mkushi.

2 Wakasema, Je! Ni kweli Bwana amenena na Musa tu? Hakunena na sisi pia? Bwana akasikia maneno yao.

3 Basi huyo mtu, huyo Musa, alikuwa mpole sana zaidi ya wanadamu wote waliokuwa juu ya uso wa nchi.

4 Bwana akanena ghafula na Musa, na Haruni na Miriamu, na kuwaambia, Tokeni nje ninyi watatu, mwende hemani mwa kukutania. Basi hao watatu wakatoka nje.

5 Bwana akashuka katika nguzo ya wingu akasimama pale mlangoni pa Hema, akawaita Haruni na Miriamu, nao wakatoka nje wote wawili.

6 Kisha akawaambia,Sikizeni basi maneno yangu;Akiwapo nabii kati yenu,Mimi,Bwana,nitajifunua kwake katika maono,Nitasema naye katika ndoto.

7 Sivyo ilivyo kwa mtumishi wangu, Musa; Yeye ni mwaminifu katika nyumba yangu yote;

8 Kwake nitanena mdomo kwa mdomo, Maana, waziwazi wala si kwa mafumbo; Na umbo la Bwana yeye ataliona. Mbona basi ninyi hamkuogopa Kumnenea mtumishi wangu, huyo Musa?

9 Hasira za Bwana zikawaka juu yao; naye akaenda zake.

10 Kisha hilo wingu likaondoka kutoka pale juu ya hema; na tazama, Miriamu akawa mwenye ukoma, mweupe k**a theluji; Haruni akamwangalia Miriamu, na tazama, yu mwenye ukoma.

11 Kisha Haruni akamwambia Musa, Ee bwana wangu nakusihi sana usituwekee dhambi juu yetu, kwa kuwa tumefanya ya upumbavu, na kufanya dhambi.

12 Nakusihi, asiwe k**a mmoja aliyekufa, ambaye nyama ya mwili wake nusu imelika hapo atokapo tumbo la mama yake.

13 Musa akamlilia Bwana, akasema, Mpoze, Ee Mungu, nakusihi sana.

14 Bwana akamwambia Musa, Je! K**a baba yake angalimtemea mate usoni tu, hangaliona aibu muda wa siku saba? Na afungwe nje ya kambi muda wa siku saba, kisha baada ya hayo ataletwa ndani tena.

15 Basi Miriamu alifungwa nje ya kambi muda wa siku saba; wala watu hawakusafiri hata Miriamu alipoletwa ndani tena.

MUHIMU: Hao ni baadhi tu wapo wengi sana, lakini wayahudi walizaa na waafrica na tena uzao huo ulitoa manabii wakubwa ambao walikuwa chotara waafrica na uyahudi.

Kwa Maswali wasiliana nami.

Simu & Whatsapp: 0785043326.

MUBARIKIWE SANA WANA WA UFALME:

21/12/2021

HAPO MWANZO NDOA YA WAKE WENGI HAIKUWA DHAMBI:

Mwanzo 30:1-13
[1]Naye Raheli alipoona ya kuwa hamzalii Yakobo mwana, Raheli alimwonea ndugu yake wivu. Akamwambia Yakobo, Nipe wana; k**a sivyo, nitakufa mimi.
And when Rachel saw that she bare Jacob no children, Rachel envied her sister; and said unto Jacob, Give me children, or else I die.
[2]Yakobo akamghadhibikia Raheli, akasema, Je! Mimi ni badala ya Mungu, aliyekuzuilia uzao wa mimba?
And Jacob's anger was kindled against Rachel: and he said, Am I in God's stead, who hath withheld from thee the fruit of the womb?
[3]Akasema, Yuko mjakazi wangu, Bilha, uingie kwake ili kwamba azae juu ya magoti yangu, nami nipate uzao kwa yeye.
And she said, Behold my maid Bilhah, go in unto her; and she shall bear upon my knees, that I may also have children by her.
[4]Basi akampa Bilha mjakazi wake kuwa mkewe. Yakobo akaingia kwake.
And she gave him Bilhah her handmaid to wife: and Jacob went in unto her.
[5]Naye Bilha akapata mimba, akamzalia Yakobo mwana.
And Bilhah conceived, and bare Jacob a son.
[6]Raheli akasema, Mungu amenipa haki yangu, naye amesikia sauti yangu, akanipa mwana. Kwa hiyo akamwita jina lake Dani.
And Rachel said, God hath judged me, and hath also heard my voice, and hath given me a son: therefore called she his name Dan.
[7]Bilha, mjakazi wa Raheli, akapata mimba tena, akamzalia Yakobo mwana wa pili.
And Bilhah Rachel's maid conceived again, and bare Jacob a second son.
[8]Raheli akasema, Kwa mashindano makuu nimeshindana na ndugu yangu, nikashinda. Akamwita jina lake Naftali.
And Rachel said, With great wrestlings have I wrestled with my sister, and I have prevailed: and she called his name Naphtali.
[9]Lea alipoona ya kuwa ameacha kuzaa, alimtwaa Zilpa, mjakazi wake, akampa Yakobo kuwa mkewe.
When Leah saw that she had left bearing, she took Zilpah her maid, and gave her Jacob to wife.
[10]Zilpa, mjakazi wa Lea, akamzalia Yakobo mwana.
And Zilpah Leah's maid bare Jacob a son.
[11]Lea akasema, Bahati njema! Akamwita jina lake Gadi.
And Leah

20/12/2021

Yohana 1:34-42
[34]Wanafunzi wa kwanza wa Yesu
[35]Tena siku ya pili yake Yohana alikuwa amesimama pamoja na wawili katika wanafunzi wake.
Again the next day after John stood, and two of his disciples;
[36]Akamtazama Yesu akitembea, akasema, Tazama, Mwana-kondoo wa Mungu!
And looking upon Jesus as he walked, he saith, Behold the Lamb of God!
[37]Wale wanafunzi wawili wakamsikia akinena, wakamfuata Yesu.
And the two disciples heard him speak, and they followed Jesus.
[38]Yesu aligeuka, akawaona wakimfuata, akawaambia, Mnatafuta nini? Wakamwambia, Rabi, (maana yake, Mwalimu), unakaa wapi?
Then Jesus turned, and saw them following, and saith unto them, What seek ye? They said unto him, Rabbi, (which is to say, being interpreted, Master,) where dwellest thou?
[39]Akawaambia, Njoni, nanyi mtaona. Wakaenda, wakaona akaapo, wakakaa kwake siku ile. Nayo ilikuwa yapata saa kumi.
He saith unto them, Come and see. They came and saw where he dwelt, and abode with him that day: for it was about the tenth hour.
[40]Andrea, nduguye Simoni Petro, alikuwa mmoja wa wale wawili waliomsikia Yohana na kumfuata Yesu.
One of the two which heard John speak, and followed him, was Andrew, Simon Peter's brother.
[41]Huyo akamwona kwanza Simoni, ndugu yake mwenyewe, akamwambia, Tumemwona Masihi (maana yake, Kristo).
He first findeth his own brother Simon, and saith unto him, We have found the Messias, which is, being interpreted, the Christ.
[42]Akampeleka kwa Yesu. Naye Yesu akamtazama, akasema, Wewe u Simoni, mwana wa Yohana; nawe utaitwa Kefa (tafsiri yake Petro, au Jiwe).
And he brought him to Jesus. And when Jesus beheld him, he said, Thou art Simon the son of Jona: thou shalt be called Cephas, which is by interpretation, A stone.

Address

Nyegezi

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Ufunuo TV posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share