"ACHENI KUTOA TAARIFA ZENU BINAFSI MITANDAONI" ENG. MAHUNDI
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Maryprisca Mahundi ametoa wito kwa wananchi kuacha kutoa taarifa zao binafsi kwenye mitandao kwa sababu za kiusalama.
@wizarahmth
@maryprisca_mahundi
@marypriscawomenempowerment
@tzcuom @cuom.family @tzcuom @cuom_gallerytz
Kuelekea Siku Ya Wanawake Duniani
@utpc_tz @sidasweden @swedenintz @usembassytz @jamiiforums @imsforfreemedia @twaweza.nisisi @unesco @misatanzania @tamwa_ @maendeleoyajamii @gwajimad
Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Dkt. Tulia Ackson kesho Novemba 11, anatarajiwa kuwasili Mkoani Mbeya kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kushika wadhifa huo.
Tulia Trust
Polisi mkoani Mbeya inawashikiria watu sita kwa tuhuma za kuvamia na kupora magari yanayosafirisha mizigo kwenda nchi za jirani.
WANANCHI MBEYA WALIA NAULI KUPANDA KIHOLELA.
Wananchi Mkoani Mbeya wamelalamikia kitendo cha wamiliki wa magari ya kusafirisha abiria kupanda kiholela kwa kisingizio cha kupanda kwa mafuta.
MBARONI KWA KUJIFANYA MAAFISA WA JESHI LA POLISI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wawili Juma Mapunda (47) na Said Wanyika (27) wote wakazi Songea Mkoa wa Ruvuma kwa tuhuma za kujifanya maafisa wa Jeshi la Polisi.
WAZIRI PROF. NDALICHAKO AZIAGIZA TAASISI KUAJILI WATAALAMU WA LUGHA ZA ALAMA
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof. Joyce Ndalichako amewaagiza wakuu wa taasisi mbalimbali kuboresha mfumo wa kuwasiliana na viziwi ili wafikapo ili kupata huduma kwa kuajiri wataalam wa lugha.
Ofisi ya Waziri Mkuu
Tazama kwaya ya Viziwi ikitumbuiza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Viziwi Duniani.
WANANCHI WATAKIWA KUSHIRIKIANA NA WATU WENYE ULEMAVU.
Katika kuelekea kuadhimisha kilele cha wiki ya Viziwi duniani wananchi wameshauriwa kushirikiana na viziwi ili kuhakikisha wanapata huduma stahiki kutokana na kundi hili kusahaulika wakati wa utoaji huduma za kijamii.
WAZAZI WATAKIWA KUWA KARIBU NA WATOTO WAO ILI KUPUNGUZA VITENDO VYA UKATILI.
Wazazi na walezi wametakiwa kuwa karibu na watoto wao ili kupunguza vitendo vya ukatili na mmomonyoko wa maadili vinavyoendelea kutokea kwenye familia na jamii.
Afisa Taaluma Msingi Jiji la Mbeya Neema Njavike amesema hayo kwenye mahafari ya pili ya Shule ya awali na msingi ya Paradise Mission iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya Mbeya.
Mwili wa mtu mmoja anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 35, umekutwa kwenye mto Ayanga, mtaa wa Rift Valley, Jamatini Jijini Mbeya.
MADIWANI WATAKIWA KUWA MAKINI KATIKA MATUMIZI YA FEDHA ZA UMMA.
Madiwani wametakiwa kusoma kwa makini nyaraka za manunuzi pamoja na mikataba mbalimbali kutokana na baadhi ya watumishi kutokuwa waaminifu.
WANASAYANSI 250 KUTOKA MATAIFA MBALIMBALI KUFANYA KONGAMANO LA TAFITI ZA UKIMWI NA KIFUA KIKUU, JIJINI MBEYA.
Zaidi ya wanasayansi 250 wa kada mbalimbali za afya kutoka mataifa mbalimbali duniani wanatarajia kushiriki kwenye kongamano la kisayansi lenye lengo la kushirikishana matokeo ya tafiti zilizofanyika kwenye magonjwa ya kuambukiza hususani UKIMWI na Kifua kikuu.
Kongamano hilo ambalo litafanyika kwa siku mbili Jijini Mbeya kuanzia Septemba 21, 2023.
Mbeya Zonal Referral Hospital
MWANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE ATIWA MBARONI KWA TUHUMA ZA KUCHOMA MOTO VYUMBA VYA MADARASA.
Jeshi la Polisi Mkoani Mbeya linamshikilia mwanafunzi wa kidato cha nne wa shule ya Sekondari Iyela Yese Charles mwenye umri wa miaka 17 kwa tuhuma za kuchoma vyumba viwili vya madarasa katika shule hiyo.
MOTO WATEKETEZA MADARASA MAWILI SHULE YA SEKONDARI IYELA.
Watu wasiojulikana wamechoma moto vyumba viwili vya madarasa katika shule ya Sekondari Iyela, Jijini Mbeya.
Kamanda wa Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mbeya, Malumbo Mgata amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema chanzo cha moto huo bado hakijafahamika.
Waandishi wa Habari Mkoa wa Mbeya walipotembelea ofisi za UTPC, Dodoma mwishoni mwa wiki iliyopita.
MBARONI KWA TUHUMA ZA KUMUUA BABA YAKE MZAZI.
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya inamshikilia Humphrey Kihali [25] mkazi wa Ilemi Jijini Mbeya kwa tuhuma za mauaji ya baba yake mzazi aitwaye Francis Kihali [50] Mkazi wa Ilemi Jijini Mbeya.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya ACP Anthony Mkwawa amesema Septemba 10, 2023 majira ya saa 10:45 jioni katika eneo la Ilemi mtuhumiwa alimvizia baba yake mzazi akiwa chumbani kwake na kisha kumpiga kwa kutumia ubao ambapo alikimbizwa Hospitali ya Rufaa Kanda ya Mbeya na kufariki dunia leo Septemba 11, 2023 majira ya saa 1:30 asubuhi.
Ameongeza kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtuhumiwa ana tatizo la akili. Uchunguzi unakamilishwa ili hatua zingine za kisheria zifuate.
#HABARI Wanafunzi na walimu wa shule ya msingi Uhuru, iliyopo katika Kata ya Mwakibete Jijini Mbeya wamemuomba Mbunge wa jimbo hilo na ambae pia ni Spika wa Bunge la Jamhuri yaMuunganowaTanzania Dk. Tulia Ackson awasaidie kuboresha madarasa, matundu ya choo na madawati.
WAKULIMA WAITWA KUPATA ELIMU YA KILIMO CHA KISASA
Wananchi wameshauriwa kufika katika ofisi za Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora. pindi wanapopata changamoto za haki zao.