16/05/2024
*UCHUMBA NINI ?*
โuchumba ni kipindi cha makubaliano kati ya watu wawili wenye jinsia mbili tofauti, waliofikia hatua ya ukomavu wanapokubaliana kuanza safari ya mahusiano kwa lengo la kuingia kwenye ndoa.
โโUchumba ni hatua ya awali inayohusisha watu wenye jinsia mbili tofauti kuwa na mahusiano ya ukaribu yanayolenga kuzaa ndoa nzuri, yaani kuja kuwa mke na mume baadae.
Lengo la uchumba ni kuchunguzana kwa nia ya kufahamiana na kujengana kuwa bora zaidi.
Lengo la uchumba sio kuchunguzana ili ujue madhaifu yake kisha umuache. Hayo huwa tunafanya kwenye urafiki.
Kwenye uchumba tunalenga kumtengeneza mtu kufaa kwenye maono yako, kuendana, kuhabarishana kwa undani wewe ni nani unapenda nini! Nk
Kabla ya uchumba huwa kuna hatua ya *urafiki*
hatua ya urafiki ndiyo inayokuwezesha kumfahamu mtu, kabla haujamtamkia neno lolote, changamoto kubwa watu wengi tumeingia kwenye hatua ya uchumba kabla ya kuanza na urafiki, matokeo yake unakuta mambo ya kufanya kwenye urafiki unayafanya kwenye uchumba, hii ni sababu pia watu wanaumizana hovyo.
Kabla haujamtamkia au kumkubalia mtu kuwa mchumba wako, tenga muda wakumjua kwanza, k**a mko maeno ya karibu, Jenga urafiki kwanza, na k**a yuko mbali fanya tafiti za wanaomjua kwanzaa.
Hatua ya urafiki inaweza kurukwa tu, endapo kumetokea Divine connection,, kuna wakati mahusiano yanaanza na Mungu mwenyewe moja kwa moja, unakuta Dada amekaa na Mungu yuko tayari, na kaka amekaa na Mungu na yuko tayari hapa inaweza kutokea Divine connection gafla mkajikuta mmekuwa connected,, nje na hapo jenga urafiki wekeza kwenye kumjua kwanza.
Unapoingia kwenye uchumba kimsingi, ili mtu awe mchumba unapaswa kuhakikisha uchumba wenu unafahamika kwa wazazi wako wa kimwili au wakiroho, aidha kuna mlezi yeyote kati yenu anayewashinda, nje ya hapo nyie ni marafiki tuu mlioamua kujadili mambo ya ndoa๐คฃ
Na baadaye uchumba huidhinishwa kwa kijana kutoa taarifa kwao na kuja kwenu kutoa kishika uchumba (posa) hapa ndipo uchumba wenu unarasimishwa sasa.