#funkyfriday iko powered by Mr Dj @kidaog_tz ndani ya #thevoltage⚡ ya @mainfmtanzania 🔥🔥🔥
#HABARI: Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itasimamia na kutekeleza masuala yote yaliyoainishwa kwenye taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Afya kwa wote na Utayari wa Kukabiliana na Dharura.
Ameyasema hayo leo (Alhamisi, Novemba 21, 2024) alipofungua mkutano wa pamoja na Mawaziri na viongozi wa Juu wa Shirika la Afya Duniani kuhusu hali ya utekelezaji wa afya kwa wote na utayari wa kukabiliana na dharura nchini. Katika Mkutano huo Mheshimiwa Majaliwa alizindua taarifa ya Tathmini ya Utekelezaji wa Afya kwa wote na Utayari wa Kukabiliana na Dharura.
#Mainfmcup2024
#vijiwevimeitika
#sokalikohuku
#HABARI: Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mhe. Thobias Andengenye amevitaka vyama vya Siasa mkoani Kigoma kuendesha Kampeni zenye utulivu na amani kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika nchini Novemba 27, 2024.
Andengenye ametoa wito huo kufuatia kuanza rasmi kwa Kampeni za uchaguzi huo leo Novemba 20, 2024 ambapo amesisitiza kuwa lengo ni kuhakikisha wakazi wanapata fursa ya kusikiliza sera za vyama mbalimbali vya Siasa kupitia wagombea wanaoviwakilisha ili waweze kuchagua viongozi watakaowataka.
Katika hatua nyingine Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimezindua rasmi Kampeni zake mkoani Kigoma ambapo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Christopher Gachuma amemwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) kwenye uzinduzi huo kimkoa.
Akizungumza na wanachama wa CCM waliojitokeza kushiriki uzinduzi huo uliofanyika katika uwanja wa Kiganamo mjini Kasulu, Gachuma amewataka wananchi kushiriki katika kampeni hizo na kufanya maamuzi ya kuchagua viongozi ambao watamsaidia Mhe. Rais. Dkt. Samia katika kutekeleza miradi ya maendeleo sambamba na kuendelea kutunza amani ya nchi.
#Mainfmcup2024
#vijiwevimeitika
#KARIAKOO:Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan amesema kuwa tukio la kuporomoka kwa ghorofa katika eneo la Kariakoo kumetoa ujumbe mkubwa wa kuangalia usalama wa majengo katika eneo hilo na kuongeza kuwa jengo hilo halikusimamiwa vizuri.
Rais Samia ameyasema hayo leo 20 Novemba,2024 Kariakoo Jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na Wananchi na Wafanyabiashara wa eneo hilo huku akisema kuwa kazi iliyofanywa na watu mbalimbali katika eneo hilo imefanywa kwa ushirikiano na kwa weledi mkubwa huku akiwashukuru Watu wote walioshiriki kwenye uokozi.
#MICHEZO:Shabiki wa Taifa Stars maarufu kwa jina la Mzaramo amewataka mashabiki kuacha kile alichokiita siasa za mpira huku pia akiwataka kuwaheshimu makocha Wazawa.
Kauli hiyo ni baada ya Timu hiyo kuibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Guinea ambapo imefuzu kushiriki mashindano ya AFCON 2025 nchini Morocco.
#MICHEZO:Baada ya mchezo wa Taifa Stars Mwenyekiti wa Klabu ya Simba SC Multaza Mangungu ameipongeza timu hiyo kwa Ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Guinea ambalo limepelekea kufuzu mashindano ya AFCON 2025.
#VIDEO: Shuhudia furaha ya Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo, Dkt. Damas Ndumbaro baada ya timu ya taifa ya Tanzania @taifastars_ kufuzu kushiriki Afcon 2025.
#Mainfmcup2024
#vijiwevimeitika
#Michezo
#HABARI:Katika kusherehekea kumbukizi ya siku ya kuzaliwa kwa Ghalib Said Mohamed ambaye ni mdhamini na mfadhili wa Klabu ya Yanga, Afisa habari wa timu hiyo Ally Kamwe amesema kuwa siku hii GSM ataitumia kufanya matukio mbalimbali, ikiwemo kusaidia jamii yenye uhitaji Kibaigwa mkoani Dodoma.
#MICHEZO: Mshikaji wako Ndorobo anasema mchezo wa leo kati ya Taifa Stars Vs Guinea, ni sare au Stars anafungwa.
Unakubaliana naye kwenye hili?
#Mainfmcup2024
#vijiwevimeitika
#Michezo
#MICHEZO: Slim Suma anasema kwa upande wake anaiona Taifa Stars ikishinda mchezo wa leo dhidi ya Guinea, unakubaliana nae kwenye hili?
#Mainfmcup2024
#vijiwevimeitika
#Michezo
Mapambano dhidi ya Rushwa ni jukumu la kila mmoja kwenye jamii, timiza jukumu lako la kutoa taarifa ya vitendo vyote vya Rushwa na viashiria, vishawishi na kila aina ya ukiukwaji wa taratibu unaohusisha Rushwa kuelekea Uchaguzi wa Serikali za mitaa. @takukuru.tz
@mainstreammedia_tz
#uchaguziserikalizamitaa2024
#rushwa
#takukuru
#UOKOAJI:Bondia Hassan Mwakinyo amefika katika eneo la Kariakoo Jijini Dar es Salaam eneo ilipotokea ajali ya kuporomoka kwa ghorofa kwaajili ya kushiriki katika zoezi la uokozi.
Mwakinyo amesema kuwa zoezi hilo siyo rahisi kama linavyozungumzwa na baadhi ya watu katika mitandao ya kijamii huku akivipongeza vikosi vya jeshi na waokoaji wengine kwa kazi kubwa wanayoendelea kuifanya hadi sasa.