03/07/2024
MAUMIVU YA KIUNO NA MGONGO NA SULUHISHO LAKE
Maumivu ya mgongo ni ile hali ya kuhisi maumivu au kutojiskia vizuri/kawaida katika misuli au mifupa ya mgongo wako (eneo lililopo kati ya kiuno na shingo).
Maumivu haya yanatofautiana baina ya mtu na mtu na pia yanategemea sana wapi ilipo shida katika mgongo wako; nini kisababishi na kiungo kilichoathiriwa (kilichoumizwa/jeruhiwa).
Vivyo hivyo dalili nazo hutegemea na kisababishi na hivyo baadhi ya watu huwa na dalili zinazofanana huku wengine wakiwa na dalili za aina mbali mbali kuanzia mamivu ya mgongo, kushindwa kufanya shughuli za kawaida za kila siku kutokana na maumivu, homa na kutetemeka, kupungua uzito (hasa baada ya ajali/magonjwa ya mifupa), kupungua nguvu katika misuli ya miguu, miguu kuwaka moto/kuchomwa chomwa mithili ya sindano au miiba, ganzi kwenye miguu hadi kushindwa kumudu kuzuia haja ndogo na/au kubwa.
Aina kuu za maumivu ya mgongo:
Mara nyingi, maumivu ya mgongo hujitokeza katika aina kuu mbili ambayo ni:
(Maumivu yanayosambaa)
1. Maumivu yasiyohama (yapo katika eneo la mgongo husika hajalishi unafanya nini – localized pain). Mara nyingi maumivu ya namna hii ni yale yanayokuwa yametokana na kujeruhiwa kwa misuli/mifupa ya mgongo kwa ajali au kupigwa eneo la mgongoni. Au, ni yale yanoyotokanana mkao mbaya usiozingatia afya ya mgongo [anagalia mako mzuri katika somo “post” iliyopita –MKAO MZURI (NI UPI)?] hivyo kusababisha kuchanika kwa misuli ya ndani ya mgongo na kusababisha maumivu!!
2. Mamivu yanayosambaaa na kuangazia maeneo mengine ya mwili wako mbali na mgongo k**a vile miguu. Maumivu haya hutokana na mgandamizo katika mfumo wa fahamu/neva kutoka kwenye mifupa, uvimbe au kuumizwa kwa uti wa mgongo/neva zinazochomozea mgongoni baada ya ajali au kujeruhiwa mgongo wako kwa kupigwa/kuanguka. Mfano: shida ipo mgongoni ila unahisi ganzi kwenye m(i)guu au m(i)guu kuwaka moto).
Visababishi vya maumivu ya mgongo:
(Ubebaji wa mizigo)
Moja ya visababishi vikuu vya maumivu ya mgongo ni
▪️Aina ya kazi unayofanya.
▪️Mkao
▪️ Ubebaji wa mizigo mizito
▪️Kulalia godoro laini na lililobonyea/linalobonyea katikati wakati wa kulala.
▪️Kujeruhiwa mgongo wako kunakotokana na ajali, michezo, kuanguka, kupigwa, n.k au uvimbe (kansa) katika uti wa mgongo.
▪️Ujauzito/uzito wa kupita kiasi (kitambi)
▪️Msongo wa mawazo (stress)
▪️Magonjwa yanayoathiri mifupa (pingili) za mgongo k**a vile TB ya mifupa ya mgongo
▪️Kuvunjika au kuhama kwa mifupa ya mgogo kutoka nafasi yake.
MAUMIVU YA KIUNO:
Haya ni maumivu ya yanayotokea maeneo ya kiuno.
Maumivu haya ni moja ya mambo ambayo yanasababisha idadi kubwa ya watu katika nchi zilizoendelea kuwa waumini wazuri wa mahospitali eidha kulazwa au kuhudhuria klinik mara kwa mara. Maumivu ya mgongo yanauhusiano mkubwa sana na misuli,kano na mifupa.
VYANZO
Kwenye vertebral disc
Maumivu yanatokea pale ambapo kutakuwa na kupasuka au kulika kwa gegedu zinazounda pingili za kiuno. Misuli dhaifu na tindikali nyingi inayoingia kwenye damu pamoja na upungufu wa madini ya chokaa hali huwa mbaya zaidi.
-Kuharibika kwa misuli eneo husika.
-Mifupa na kano{ligament}
-Figo na kibofu cha mkojo.
-Matatizo ya tezi dume au kizazi kwa akina mama.
-Kula kupita kiasi au kunywa.
-Kukosa choo kwa muda mrefu.
-Misuli iliojishikiza kwenye kiuno huadhiriwa na tabia mbaya ya ulaji na uvaaji usiozingatia kanuni za afya bila kusahau magonjwa ya mifupa{arthriti}.
Mvutaji wa sigara usababisha mtu kukohoa kutokana na ni****ne. Hali hiyo husababisha mzunguko wa damu kuwa mdogo huku misuli ikipoteza ulaini elasticity na hapo ndipo maumivu huongezeka sana.
Kukosa choo kwa muda mrefu zaidi usababisha kiuno kuuma kutona na utumbo mpana kuchafuka huku gesi ikizalishwa kwa wingi.
Matatizo ya uzazi kwa jinsia zote mbili, pamoja na kuongezeka kwa lactic acid kwenye misuli.
SULUHISHO
Andika neno SULUHISHO kwenda What's App au nipigie +255756395091 nikupe mwongozo vizuri