27/10/2024
Msanii maarufu wa Bongo Fleva, Marioo, amesheherehekea mafanikio makubwa ya wimbo wake mpya, "Unanchekesha," ambao umefanikiwa kushika nafasi ya kwanza kwenye chati ya Apple Music Tanzania. Akiandika kwenye ukurasa wake wa Instagram, Marioo alifichua kuwa alichukua dakika 9 pekee kuandika verse na chorus ya wimbo huo, huku mtayarishaji akitumia dakika 10 kuunda mdundo.
Marioo alisisitiza umuhimu wa ushirikiano na S2kizzy katika kufanikisha wimbo huo, akisema, "Ninajivunia sana kazi yetu ya pamoja. Tumefanya kazi kwa bidii na Mungu ametujalia matokeo mazuri." Wimbo huo umeendelea kuwa gumzo, na hivi sasa jina la Marioo linaonekana kwenye nyimbo 15 kwenye chati ya Apple Music, akionyesha nguvu ya kazi yake.
Ushindi huu unamfanya Marioo kuwa moja ya wasanii wanaoongoza katika tasnia ya mu*iki nchini, huku akitoa mfano wa jinsi ubora wa kazi unavyoweza kuleta mafanikio. Tunatarajia kuona nini kingine atakachokileta katika siku zijazo!