![KANUNI 5 ZA KUBORESHA MAISHA YAKO♦️Maisha ya kipekee katika hii dunia huishi wale wenye kuishi kwa kanuni na misingi bor...](https://img5.medioq.com/933/124/500651519331243.jpg)
23/08/2024
KANUNI 5 ZA KUBORESHA MAISHA YAKO♦️
Maisha ya kipekee katika hii dunia huishi wale wenye kuishi kwa kanuni na misingi bora ya maisha. katika maisha kuna kanuni ukiziishi hakika utaishi maisha ya kitajiri na maisha ya mafanikio, na mafanikio hayo sio tu pesa, k**a wengi vile wanaamini.
bali ni kuishi kwa kuwa na shauku ya maisha, kujawa na amani ya moyo, kuishi kwa uhuru, na kuishi kwa furaha ambayo inatokana mja kumshukuru ALLAH Katika kila kitu, jambo ambalo ALLAH huzidi kumzidishia baraka mja wake katika maisha yake.
Hizi Apa kanuni tano Ambazo k**a utaamua kuziishi hakika utaona mabadiliko makubwa katika maisha yako kwa Uwezo wa ALLAH:
1. FANYA KAZI KWA BIDII, LAKINI KAMWE USIWEKE PESA MBELE.
Mafanikio ya kweli hayapatikani kwa mtu kumiliki pesa nyingi, pesa Kazi yake ni matumizi tu, usije ukauza utu wako kwa sababu ya pesa, fanya kazi kwa bidii, ishi kwa malengo, ishi kwa makusudio, ishi kwa shauku katika haya maisha.
Hayo ndio yatakufanya uishi kwa maisha ya furaha na mafanikio na sio pesa, kwani unaweza miliki pesa zote duniani lakini k**a huishi maisha ya makusudio hakika utaishi maisha ya kuteseka, unawezaje furahia maisha yako wakati unachukia kile unakifanya.
Hii haina maana pesa ni uovu hapana, pesa ni kitu kizuri k**a utakitumia kwa nia nzuri, pesa inaweza tumika kununa vitu vya thamani, unaweza saidia watu wengi kupitia pesa, lakini ishi kwa kujua pesa huishia mkononi na sio moyoni.
Fanya unachokipenda na pesa itakuja tu yenyewe, jenga mahusiano mazuri na watu wenye manufaa kwako, mshukuru sana mola wako, ishi kwa huruma na daima sambaza upendo kwako na kwa wengine, na kamwe usiweke pesa mbele, tanguliza utu, tanguliza thamani za watu na sio pesa.
2. KUWA NA KAWAIDA YA KUTOA BILA KUWEKA MATARAJIO KWA WATU AU VITU.
Huwezi kuipata ile baraka inayopatikana katika kutoa wakati unatoa lengo upate kitu, toa kwa upendo, toa kwa huruma toa kwa lengo la kusaidia, hakika utajikuta baraka zinakuenea katika maisha yako na furaha halisi utaihisi moyoni.
Kwani imeshuhudiwa leo hii watu wengi hutoa baada ya kuona kuna maslahi yao binafsi, hutoa kwa lengo la kuonekana, ili apate sifa, ili nae aje apewe siku inafuata jambo ambalo huwapelekea kuvunjwa moyo sana katika maisha yao.
Usiweke matarajio kwa watu, unaweza kutoa lakini sio kila mtu anamoyo k**a wako, toa bila kuweka matarajio kwa watu, utaishi kwa amani sana ya moyo, utaishi maisha ya kipekee sana, na ALLAH Hupenda wale wanatoa kwa ajili yake na sio vyenginevyo.
Toa Upendo na ALLAH atakupa watu sahihi kukupenda katika maisha yako, Toa Huruma kwa watu na ALLAH atakupa watu watakaokujali sana katika maisha yako, wallah kuna mambo ukitoa ALLAH atakulipa bora zaidi, pale tu ukiondoa matarajio kwa watu.
3. ISHI SASA NA IISHI LEO YAKO.
Kuna watu kutafakari sana yaliyopita imekuwa ni kawaida yao, jambo ambalo matokeo yake ni kuishia muda mwingi kutokuwa na furaha, iishi leo yako, ikumbatie leo yako iishi kwa shauku na matumaini makubwa, jambo hili litakufanya uishi maisha bora kabisa.
ALLAH ﷻ anasema: "Na bila ya shaka wakati ujao utakuwa bora kwako kuliko ulio tangulia."{A-Dhuha: 4}.
Unapofikiria na kuhuzunika kuhusu maamuzi uliyoyafanya jana hakika unajitesa, jana imeshapita na huwezi irudisha, usihuzunike kwa yaliyopita ndio yamepita, kumbuka mafunzo tu na sio maumivu utazidi kuikosa ladha ya leo yako.
Fanya mambo yanayokuboreshea maisha yako na sio yanakuharibia maisha yako, wacha kuihofia kesho yako, wacha kuihofia future yako, future yako imeshikiliwa na kipi unakifanya leo, yupi unatumia muda mwingi nae leo.
Bali nini unakisikiliza leo, nini unakiangalia leo, na nini unajifunza leo, hayo ndio yatakayojenga maisha yako ya baadae, kubwa zaidi kumbuka ALLAH ndio Mwenye mamlaka na kesho yako na ALLAH Hakutakii ila kheri, hivyo Kuwa na matumaini makubwa ndani yake.
Hivyo itumie leo yako katika mambo yanayoboresha maisha yako, fikiria zaidi kile unapenda na sio kile hupendi. tumia muda wako kujali wale wanakujali, ongea kile unapenda kuongea, fanya vitu kwa ajili yako na kwa wegine na iishi leo yako kwa shauku kubwa.
4. ISHI KWA UADILIFU.
Maisha yanataka uadilifu, daima angalia kipi sahihi na sio nani yupo sahihi, epuka kuangalia kipi rahisi bali angalia kipi kina manufaa kwako, utaishi kwa mafanikio na furaha ya kipekee k**a utakuwa muadilifu katika kila kitu.
Ishi maisha ya kuwaweka watu wote sawa, wote jua ni k**a wewe, usijione bora kuliko yoyote yule, muheshimu kila mtu, mtendee kila mtu vile unapenda kutendewa wewe, mfanye kila mtu ajihisi wa kipekee kwa kumjali hisia zake.
Moja ya watu wanapendeza zaidi kwa ALLAH Ni watu wenye uadilifu, mtu mwenye uadilifu anaweza akavumilia maumivu lakini ahakikishe unapata haki yako, mtu mwenye uadilifu hawezi ongea uongo kwa manufaa yake binafsi.
Kuwa sahihi kuwa muadilifu, onyesha tabasamu kwa kila mtu na usiishi kwa kumchukia yoyote yule, anaetumia muda kwa ajili yako ni juu yako nawe kutumia muda wako kwa ajili yake, hili huboresha mahusiano yetu na kuwa IMARA kabisa.
5. TABASAMU NA CHEKA KIASI.
Kutabasamu ni moja ya tiba bora ya magonjwa ya moyo, chuki, visasi, vinyongo na hata wivu kupita kiasi, tabasamu huleta faraja pale unapolilazimisha wakati wa maumivu, hakuna mtu asiepitia machungu katika maisha ila tabasamu hupunguza maumivu.
haijalishi unapitia nini katika maisha yako Tabasamu na maisha, kumbuka ALLAH anakupitisha humo lengo akufunze mambo, ili akubariki maisha yako, tabasamu na maisha bila kujali moyo uko hali gani, tabasamu hurejesha matumaini.
Na Daima kuwa na kawaida ya kucheka kiasi, kwani kucheka kupita kiasi ni hatari kwa imani yako, kicheko huuwa imani yako, kicheko kingi mara kwa mara huondosha nuru ya uso. Cheka penye haja cheka kiasi ambacho ujihisi vizuri tu.
Kwani muda mwengine hatucheki kwa sababu tuna furaha bali tunakuwa na furaha kwa sababu tunacheka. hivyo furaha yetu ndio kipaumbele chetu katika maisha yetu ili ALLAH Aone shukrani zetu juu ya haya maisha na atuzidishiye.
Na sio muda wote mtu unakuwa Serious kupitiliza, utatisha, utakimbiza watoto kukusogelea na watu wengine, kwani uso wenye tabasamu huvutia zaidi kuliko uso uliokunjwa, Onyesha tabasamu juu ya maisha na wengine watatabasamu juu yako.
Tunamuomba ALLAH Atufanyie wepesi kuziishi hizi kanuni bora kabisa ambazo zimeboresha maisha ya wengi na kuishi maisha ya mafanikio na maisha yaliyojaa Furaha🤲