24/09/2021
Hofu ya ujasusi yazua hamu ya teknolojia salama zaidi
"Watu wanaonekana hawaelewi kwamba usalama na simu za mkononi k**a kitu kimoja ni jambo ambalo halipo," anasema Pim Donkers.
Bwana Donkers ni mwanzilishi mwenza na mtendaji mkuu wa kampuni ya teknolojia ya Vifaa vya ARMA Uswisi, ambayo inatengeneza vifaa salama vya mawasiliano.
Kwa hiyo, zaidi, ana nia ya kuonya watu juu ya uwezekano wa udhaifu uliopo katika suala la usalama na simu za smartphone.
Analinganisha simu za mkononi na mzinga wa nyuki ambapo "watu wengine ndio huingia na kutoka ndani ya mfumo, kufanya biashara na kutumia data yako vibaya iliyokusanywa kupitia ving'amuzi vyote."
"Smartphone k**a kianzio katika suala la mawasiliano salama bila shaka yoyote ni jambo ambalo halipo tena. Haitatokea kamwe," anaonya.
Wasiwasi wake mkubwa juu ya mapungufu ya faragha ya simu za mkononi kumeungwa mkono na simulizi nyingi tu za hivi karibuni, haswa kuhusu kubainika kwa programu ya kijasusi inayojulikana k**a Pegasus, ambayo chanzo chake ni kampuni ya NSO Group ya Israeli.
Mnamo mwezi Julai, iligundulika kuwa programu ya Pegasus inaweza kukuwekwa kwenye simu za iPhones na Android, na kuruhusu waendeshaji kutoa ujumbe, picha na barua pepe, kurekodi simu na hata kuamsha kipaza sauti au maikrofoni na kamera kuanza kufanya kazi yake kwa siri.
Uwezo wa kufikia simu ya mtu na kufanya unachotaka licha ya kwamba yenye iko mbali na mtumiaji halali kuna wakati ilizingatiwa k**a nchi chache tu ndio zenye uwezo wa kufanya hivyo.
Lakini teknolojia imeendelea haraka sana na nguvu za upelelezi na uchunguzi sasa hivi ziko mikononi mwa nchi nyingi na hata watu binafsi na makundi madogo madogo.
Kuwa na wasiwasi k**a huo akilini, mahitaji ya watumiaji yameongezeka katika hulo huku usalama ikiwa k**a sehemu yao kuu ya wakati wanauza bidhaa yao - kuanzia simu za kisasa zenye namba za siri yaani zilizofichwa kimaksudi k**a njia mbadala ya kupata faragha kwakatika injini za utafutaji habari na ramani.
Takwimu zingine zinaonyesha kuwa vifaa vya simu ya mkononi husumbua watu wengi.
Uchunguzi wa Kituo cha Utafiti cha Pew unaonyesha kuwa Wamarekani 72% waliripoti kuhisi kuwa wanachofanya katika simu zao kinafuatiliwa na watangazaji wa matangazo ya biashara, kampuni za teknolojia au kampuni zingine.
Karibu nusu ya watu walioulizwa na kituo cha Pew walisema waliamini kuwa shughuli zao nyingi mtandaoni zinafuatiliwa na serikali.
"Tumezungukwa na vichwa vya habari vinavyozungumzia ukiukwaji wa data, uvamizi na uingiliaji wa aina nyingine," anasema Larry Pang, mkuu wa maendeleo ya biashara katika kampuni ya IoTex ambayo hutengeneza kamera za usalama zilizoundwa kutunza data ya kibinafsi.
"Kila wakati tunasoma kwamba mashirika na serikali ambayo yameahidi kutulinda, ukweli ni kwamba, hufanya mambo nyuma ya migongo yetu kwa faida yao," anasema.
Bidhaa zingine kwenye soko la faragha sio zinazoweza kushikika.
Programu ya Xayn, kwa mfano, ni bidhaa iliyoelezwa k**a "inayolinda faragha ya mtu" anapokuwa mtandaoni.
Kampuni hiyo inasema Xayn inaruhusu watumiaji kutumia kifaa cha utaftaji cha Google bila kutambuliwa na mtu mwingine au kuweza kuhifadhiwa data zao.
Hadi sasa, imepakuliwa na watumiaji takriban 215,000, na wengi wao wanatoka Marekani, ikifuatiwa na Uingereza, Ujerumani, Uholanzi na Urusi.
"Njia zilizopo kimsingi hufuatilia kila kitu ambacho mtumiaji hufanya anapotafuta kitu mtandaoni," anaelezea Dk Michael Huth, mkuu wa idara ya kompyuta katika Chuo cha Imperial London na mwanzilishi mwenza wa na afisa mkuu wa utafiti wa kampuni ya Xayn.
"Hii ni dhahiri haswa na bidhaa k**a vile TikTok, ambapo kuzungumza mara moja au mbili tu kunatosha kumjua mtumiaji vizuri na kuanza kumpendekezea video wanazopenda," Dk Huth anaongeza.
"Kiwango hiki cha ufuatiliaji, uchambuzi wa utabiri na kufuatilia mwenendo wa mtu sio tu ni changamoto kwa udhibiti wa hisia zetu na uhuru, bali hata uhuru wetu halisi pia."
Mwanzilishi mwenza na mtendaji mkuu wa kampuni ya Xayn, Leif-Nissen Lundb忙k anasema kwamba mahitaji ya faragha yanageuka kwa haraka sana kuwa "harakati za ulimweng
"Majadiliano juu ya faragha katika digitali mara nyingi hulenga kile kisichowezekana na wakati mwingine huwa na bahati mbaya," anasema.
"Sasa hivi kinachojitokeza ni faragha na teknolojia k**a maadui - lakini sio lazima iwe hivi. Teknolojia ya hali ya juu inaweza kulinda faragha yetu katika njia za kidijitali na kuturejeshea uhuru wetu."